Nusu saa baada ya sheby kutoweka eneo, wanakijiji walikuwa wamefurika eneo la tukio na hazikupita dakika tano, ambulance tano pamoja na defender nne za polisi ziliwasili eneo la tukio, miili ilipakiwa na kwenda kuzikwa na halmashauri kutokana na ndugu wa marehemu kukosekana licha ya kutangazwa zaidi ya wiki nzima katika vyombo vya habari ************ Zilikatika siku,wiki na hatimae mwaka kupita huku sheby akiendelea vizuri na kazi zake katika TRA tawi la posta, Warda nae alizidi kunawiri na kunekana mpya mbele ya mboni za sheby kila siku, baada ya miaka mwaka kupita sheby alipandishwa mkurugenzi mkuu wa TRA kufutia kustaafu kwa Mr Yusufu ambae umri ulikua umeenda, ilifanyika tafrija fupi na hapo ndipo sheby aliamua kumvisha mpenzi wake warda pete ya uchumba huku zoezi zima likisimamiwa na Mr Yusufu ambae alimchukulia Sheby kama mwanae. Ilikua imepita miezi miwili tangu sheby amvishe pete ya uchumba mpenzi wake warda, hatimae waliamua kufunga ndoa, baada ya zoezi la kufunga ndoa kukamilika ambalo lilikua chini ya Mr Yusufu, Sheby alikabidhiwa kipaza sauti ili aweze kuongea neno la mwisho…
“Ndugu zangu wote, napenda niwashukuru kwa wote mliohudhuria katika sherehe hii na kuhakikisha kijana wenu nakamilisha zoezi hili la kufunga ndoa, shukrani za dhati ziende kwa baba yangu mlezi Mr Yusufu kwa kuwa na mimi katika kila hatua ya maisha yangu, sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea kwa Mungu kila la heri, shukrani zangu zingine ziende kwa mke wangu mpenzi kwa kuwa nami na kuhakikisha nasimama imara katika misukosuko yote na changamoto zote nilizokumbana nazo katika maisha, hakika “You’re my Heart Ur my world” sheby alizungumza kwa hisia na ukumbi wote ulikafurika kwa shangwe huku wakisema “YES SHE DESERVES TO BE YOU’RE WORLD”. SHEBY alimchukua mke wake na kuelekea nyumbani kwake Kigamboni ambapo waliendelea na maisha yao kama kawaida na baada ya mwaka mmoja kupita walibahatika kupata mtoto wa kiume na walikubaliana kumuita “ZAWADI” wakiwa na imani kuwa ni Baraka kutoka kwa Mungu, kwapamoja walipiga magoti na kumshukuru Mungu kwa kuwapigania mpaka hapo walipofikia.
MWISHO MWISHOOOO
Tags:
CHOMBEZO