baada ya warda kukaa katika usukani sheby alizunguka upande wa pili na kuingia ndani ya gari.. “Haya funga mkanda tuendelee na safari” alizungumza sheby akimuambia warda ambae muda huo alikua hajaelewa kwanini Sheby alimuachia yeye usukani.. “Kwanini unaniachia nikuendeshe honey?” aliuliza Warda “Amna nimependa niendeshwe na mpenzi wangu na pia niwe na wasaa mzuri wa kukuangalia jinsi ulivyopendeza” alizungumza Sheby jambo ambalo lilipelekea Warda atabasamu na kufurahi “Mmmmh sawa bana mi sina neno tena hapo” alizungumza warda huku akiingiza gari barabarani na safari ya kwenda beach ilianza… Mida ya saa kumi na mbili kasoro, sheby na mpenzi wake walikua maeneo ya Coco beach wakicheza michezo mbalimbali kama wapenzi wafanyavyo pindi wanapokuwa beach, lakini wakati wakiendelea na michezo hiyo sheby machale yalimcheza huku mwili ukimsisimka, kwakua sheby alipitia mafunzo mbalimbali kipindi alipokuwa nchini China alishaelewa nini maana yahali hiyo kutokea, kwamba chochote kibaya kinaweza kutokea kuanzia muda huo, hapo alimchukua mpenzi wake na kwa mwendo wa haraka alianza kutembea nae kwa hatua fupi fupi lakini za haraka akielekea sehemu aliyopaki gari, alifika na kufungua mlango wa gari na kumwambia warda atulie ndani ya gari mpaka atakaporudi kwani pale kuna kitu amekisahau maeneo yale waliyokuwa wakicheza, alirushia mlango wa gari na baada ya hapo alirudi kule alipokuwa akicheza na mpenzi wake…
******* ******** ********
John kitendo alichofanyiwa na sheby kwa kupigwa na kusababisha jino lake moja kung’ooka alihesabu ni kama kitendo cha kinyama sana ambacho hakuwahi kufanyiwa tangu azaliwe na ndiyo maana akaamua kupanga kuwa lazima amfanyie sheby kitu kibaya ambacho hatokuja kukisahau katika maisha, siku hiyo ya Jumamosi wakati Sheby akitoka nyumbani na gari lake akiwa amempakia mpenzi wake Warda kwa safari ya kuelekea beach John alibahatika kuliona gari hilo, hivyo aliamua kulifuatilia kwa ukaribu zaidi na mpaka Sheby muda ambao anaingiza gari lake katika maegesho ya Coco beach John alikua akimfatilia bila ya yeye sheby kujua kuwa anafuatiliwa
#itaendelea
Sheby muda ambao anaingiza gari lake katika maegesho ya Coco beach John alikua akimfatilia bila ya yeye sheby kujua kuwa anafuatiliwa, alipohakikisha sheby ameshuka na mpenzi wake na kuelekea beach kwaajili ya kuogelea, hapo John alitoa simu yake na kubonyeza namba kadhaa ambapo baada ya sekunde chache simu upande wa pili ilipokelewa…
“Hello, njooni maeneo ya Coco beach sasa hivi ili tumalize kazi yetu, hakikisha mnakuja na silaha za kutosha na zana za kutosha za kufanyia kazi” alizungumza John na baad ya hapo akakata simu, hazikupita dakika kumi gari aina ya noa ilipaki karibu na gari la sheby huku kukionekana vijana wapatao wanne wakiwa ndani ya gari hiyo huku wakiwa na bastola katika viuno vyao… Wakati sheby akiwa katika harakati za kuondoka eneo lile la Coco beach, John pamoja na vijana wake walikuwa wakimtazama na kumfuatilia kwa kila hatua, kipindi ambacho sheby alimleta warda katika gari na yeye kurudi kule beach hicho ndicho kipindi ambacho John pamoja na vijana wake walikuwa wakikisubiri kwa hamu, kitendo cha sheby kuondoka eneo lile, vijana wawili wa John walisogea mpaka eneo lilipokua gari la sheby na walipofika walizunguka upande ambao warda ndipo alipokuwa amekaa na kugonga kioo cha upande huo, Warda alifungua kioo ili kutaka kumsikiliza aliyekua akigonga kioo hicho alikua anashida gani, hilo likawa kosa kubwa kwani kitendo cha kufungua kioo alikutana na mdomo wa bastola ukimtazama usoni, warda alishtuka sana na almanusura ajikojolee…. “Toa lock za mlango wa nyuma” mmoja kati ya jamaa wale aliongea kwa sauti nzito na ya kukwaruza.. warda kwakua alikua katika hali ya uoga alijikuta akitoa lock za mlango huo wa nyuma, hilo nalo likawa kosa jingine, kwani yule jamaa wa pili aliingia katika mlango huo na hapo warda alistuka akiwekewa kitambaa puani na hazikupita hata sekunde tano warda alipoteza fahamu kutokana na ukali wa madawa ambayo yaliwekwa katika kitambaa kile, wale jamaa walimbeba warda na kumuingiza katika noah waliyokuja nayo na baada ya hapo waliliondoa gari hilo kwa kasi na safari ya kuelekea Bagamoyo ilianza
#itaendelea
jamaa walimbeba warda na kumuingiza katika noah waliyokuja nayo na baada ya hapo waliliondoa gari hilo kwa kasi na safari ya kuelekea Bagamoyo ilianza, lakini wakati gari hilo likiondoka kwa kasi eneo hilo sheby nae alikuwa ndo anafika eneo hilo ambapo kwa haraka alipatwa na hofu na kuhisi kuna jambo baya limefanyika hivyo aliliangalia gari hilo kwa umakini wa hali ya juu…
T 850 BWK, hizo ndizo namba ambazo alizinukuu sheby katika diary yake ndogo ambayo muda wote alikua akitembea nayo, baada ya kumaliza kunakili namba hizo sheby aligeuka na kuelekea sehemu ambayo alikua amepaki gari lake, kabla ya kulifikia aliona milango miwili ikiwa wazi ilihali wakati anatoka alikua ameifunga na alikua amemuacha mpenzi wake mle ndani, sheby alianza kutembea kwa tahadhari kubwa kuelekea eneo lile ambalo ndipo alipokua amepaki gari lake, sheby alipigwa na butwaa baada ya kutokumuona mpenzi wake warda na wakati anaondoka alimuacha kwenye gari, hakika alipagawa, alivuta pumzi kwa nguvu na kuzitoa taratibu jambo ambalo lilifanya arudi katika hali yake lakini bado alikua na kitete, alivyoangalia vizuri katika siti aliyokua amekaa warda hapo alikiona kitambaa, alikichukua na kukikagua na kutokana na ujuzi aliokua nao aliweza kutambua kuwa kitambaa hicho kilikuwa kimewekwa dawa ya usingizi, hapo alishusha pumzi ndefu na baada ya hapo alibonyeza kitufe kidogo kilichopo katika dash body ya gari na baada ya sekunde kadhaa kiscreen kidogo mfano wa tv kilitokea kwa upande wa dereva, hapa alibonyeza kitufe ambacho kiliandikwa play na baada ya muda kile screen kikaanza kuonyesha matukio yaliyotokea…. “Oooh shiit!!” alizungumza sheby baada ya kuona tukio la kutekwa kwa warda lilivyokuwa, alitoa ili diary na kuangalia ile namba ya gari aliyoinakili, sheby alipoinua macho yake na kutazama mbele aliona kuna kijana ambae alikua akimuangali kwa kuibia ibia huku akibonyeza bonyeza simu yake, sheby alimtilia wasiwasi
#itaendelea
Tags:
CHOMBEZO