MAPENZI YA CHUO 2

"Mdada baada ya kumaliza na mie kulipia,tulitoka mle ndani akasema sasa tuchukue bajaji turudi chuoni akaita najaji na tukarudi, kwnz kipindi chote tuko kwny bajaji nilikuwa sijielewi kabisa,nlikuwa naona kama nimeibiwa na mwizi ninae na sina cha kufanya"

"Tulipofika geti la chuo aliniambia nilipie bajaji nikalipia, akaniaga palepale kwa kuniambia tutaonana baadaye yeye anapeleka vitu ndani ya hostel, nilimwangalia anavyoondoka kwa mwendo wa madaha nikajisemea moyoni hii ndio Dar nishaibiwa kwanza sijui ht km ni mwanafunzi japo namwaona chuo, ilipofika saa 2 usiku akanipigia akaniambia tukale nikaenda, aliniambia mle ndani chuoni vyakula ni vibaya kwhy tutafute chakula nje kdg"

"Tulichukia tena bajaji hadi River side, hapo ilinitoka kama 50 za chakula na vinywaji na aliondoka na chips mishikaji na juice kabeba alisema kuna rafiki yake anaumwa anamperekea, ukijumlisha na bajaji kwenda na kurudi basi ni kama 60 hv ilitoka pale, tulipofika getini kama kawaida aliniambia ngoja nimpelekee mgonjwa chakula 'bye baby kesho', kwa kweli siku ile niliumia na nilichanganyikiwa,sikuweza kusoma wala kulala"

"Nilijaribu kumtumia ujumbe hakujibu licha ya kumwona online whtap na status akawa anapost picha za vyakula nlivyonunua pale river side lkn picha yangu ni km ilikatwa hv sikuonekana, kesho asbh niliwahi chuoni ili nimwone tu hahaha aisee wanaume tuna maisha magumu sn, bado nilikuwa na matumaini licha ya ujambazi huo"

"Nilienda kwake nikamsalimia, aliitika na kudakia halafu nilitaka nikupigie simu uje tukanywe chai,pale pale alinidaka na kunipeleka cafteria, tulikunywa chai kali na baada ya hapo aliniambia anataka kwenda kutengeza nywele ko nimsaidie kiasi chcht, nikastuka nikamwambia kwss sina labda hadi kesho jioni hv"

"Hapo mie nilikuwa namtega labda nimwombe aje geto nipate penzi, kumbe niliyekuwa namtega ni msoma ramani za penzi yeye alikuwa ananisoma tu, jioni nilimtumia meseji kumwalika ninapokaa,akanijibu yeye huwa haendi kwa watu kama nataka kutana nae nitafute eneo zuri yaani akanitajia hoteli na lodge anazotaka, sasa mie kipindi hicho basi najua hata hoteli basi,mie msukuma najua hoteli za kwetu ndo hizo mnazoita kwa mamantilie Dar, siku hy ilipita hvyo"

Post a Comment

Previous Post Next Post