MAPENZI YA CHUO 1


"Naitwa Omary Rashidi, nilijiunga na chuo kikuu cha Dar( UDSM) maarufu kama Mlimani mwaka 2015. Kama kawaida ukiwa mwaka wa kwanza unakuwa na mihemko na kila kitu"

"Nilipewa mkopo 80% Kwahy ada nilikuwa nalipa 20% tu. Tulipopewa bumu ya kwanza niliona kama nimekuwa Billgate pale chuoni. Kumbuka ndio ilikuwa mara ya kwanza kumiliki ATM kadi kila dakika nilikuwa natamani kwenda kutoa pesa ilimradi tu niwe nazo nifurahie na nisikie zinavyohesabika na kutoka kwny mlaongo wa ATM Machine"

"Kuna mdada mmoja alinivutia pale chuoni basi nikaona hakuna haja ya kuumia nimfate tu nimwelezee, kumbe dada alikuwa mwaka wa 2 na alishazoea maisha ya chuo, mie nikaingia kichwa kichwa mtegoni. Dada yule aliniambia kama ninahitaji kuongea nae nipange siku twende mlimani City kuna maeneo mazuri ya kupumzika ili tuongee vzr"

"Siku ilipofika nilijipanga na nikaenda kutoa laki 3.5 kwnye ATM, hizo ndo pesa zilizokuwa zimesalia maana zingine nilikuwa nazo mfukoni pmj na pesa nilizotoka nazo nyumbani, tulipofika mlimani pale tukachil sehemu tukapata vichwaji, hapo tuliacha kama 30 hv tu kwa vichwaji laini na snacks, dada akaniambia yeye anapenda vitu vizuri sasa kama nampenda na ninaweza kumhudumia nimfanyie shopping hahahahahaha jamani nilijiroga kumkubalia"

"Nilimwambia we ingia unapoona kuna unachotaka nitalipa, si nina kiburi kwsbb nimetokea shinyanga nadhania vitu vya mule ni kama kwetu tu hlf nimepewa pesa za ng'ombe kama laki 9 hv za kuanzia maisha kwahy nina milioni na ushee mfukoni pmj na za chuo"

"Dada alichagua nguo na vitu vingine vingi ambavyo mengine nilikuwa sijui hata yana kazi gani, si unajua ushamba tena wa mjini, gharama iliyokuja pale ni laki 7 jumla, nililipia lkn sikuamini macho yangu kama ndio pesa zangu zinaisha vile maana mie nilipokuwa nahesabu pesa zangu zinazidi milioni basi nilijua hata akichagua hvyo vinguo hakuna shida nitalipa labda elfu 50 tu hv, asikwambie mtu siku hy sitokuja kuisahau kabisa"

"Mdada baada ya kumaliza na mie kulipia,tulitoka mle ndani akasema sasa tuchukue bajaji turudi chuoni akaita najaji na tukarudi, kwnz kipindi chote tuko kwny bajaji nilikuwa sijielewi kabisa,nlikuwa naona kama nimeibiwa na mwizi ninae na sina cha kufanya.

Post a Comment

Previous Post Next Post