MREMBO KUTOKA JALALANI 01-----05

SEHEMU YA 01
Ni majira ya tano nikiwa natoka zangu misele na washkaji zangu nikiwa na gari yangu ndogo aina ya spasho tukiwa tungi( tumelewa) tulifika mitaa ya gheto kwangu washkaji zangu walinitaka niwashushe waendelee na Safari ya kwenda ghetoni kwao 

Niliwashusha nami nilishuka nikatoa wallet yangu noti zilinona nilichomoa noti kazaa bila hata kuhesabu kwa jeuri ya pesa niliyokuwa nayo niliwapa 
" Oyaa mtapata supu asubuhi au vipi?" 
" Poa mwanangu"
" Harrison eeh, mwanangu mi ghetto kwangu siendi"aliniambia Peter
" Kwanini"
 " Mama mwenye nyumba jamaa yangu kuanzia majuzi kaniganda kinoma nimpe chechi zake"
" Kwani anakudai shingapi?"
" Laki na nusu mwanangu"
" Kwahiyo?"
" Twenzetu kwako tukalale" 
" Usiwaze zama kwenye gari tuondoke"

Peter alizama kwenye gari niliendesha gari ghetto nikiwa nimewasha mziki na kuweka sauti ya juu yani fulu makelele hapo mtaani watu walikoma Mana hakuna kulala

Nilipaki spasho yangu sehemu ya maegesho na kuingia ndani na jamaa yangu Peter hata geti sikufunga 

Huko ndani kuligeuka club mziki mnene fulu kiyoyozi 
Kwenye maisha yangu sikuwaza kitu maendeleo nyumba niliyoishi ni ya urithi baba na mama waliacha Mali nyingi wao walishatangulia mbele za haki

Sikuwaza kuhusu kesho nilichojua Mimi ni kutumia pesa zinizoee watoto wazuri kwangu walikula na kunywa walivyotaka niliwagharamikia kwa gharama yoyote ilimradi niwapate 

Nilifikia hatua hata nilipomtamani mke wa mtu haikuwa rahisi kumkosa sikuongea kwa mdomo pesa ilizungumza 

Tabia yangu ilikuwa mbaya mno hata wenyekiti wa mitaa waliongea mpaka walichoka walipolalamikia kuhusu suala la kuwasha mziki sauti ya juu iliyokosesha watu usingizi

Watu walinichukia kwa majivuno yangu ya kutambia pesa 

Hata nilipofanya vurugu hakuna aliye sema juu yangu na hata walipochukua hatua ya kunipeleka polisi hawakupata haki zao nilitumia pesa kukandamiza jasho lao 

Ulikuwa utaratibu wangu naagiza ndafu nakula upande na jamaa zangu na kitakachobaki natupa Tena kwenye milango ya watu

Wenye hali duni walinitazama na kunilaumu wakiniambia nafanya kufuru lakini sikuwa na muda wa kusikiliza kelele zao

Sikiwaza biashara Wala kazi nilitumia nilizokuwa nazo 

Nikiingia club utaskia
" Harrisoooon" sauti za wadada warembo kila mtu akitaka kuwa na Mimi na kwa jinsi nilivyojaaliwa u handsome Basi niliona kilakitu kwangu ni chepesi sio pesa wala marembo

Usiku mmoja nikiwa nimelewa Sana nilifika ghetto nikiwa peke yangu nilifungua mlango wa gari lakini nilishindwa hata kushusha mguu kwa jinsi pombe zilivyo nizidi nililala hapohapo nikiwa nimekaa

Nilikuja kuamka baada ya mwanga mkali kunipiga usoni kumbe palisha kucha muda Sana nilitazama saa yangu ilikuwa tayari ni saa tatu asubuhi

Viungo vyote vilikuwa vinauma kwa kulala kwa kujikunja kwenye gari

Nilishuka ili niingie ndani lakini alitokea kichaa mmoja mwanamke alisimama mbele yangu
" We chizi hebu toka" nilimwambia lakini hakutoka alinyoosha mkono Kama kuomba kitu
Nilijua hakuna anachohitaji kingine zaidi ya chakula

Nilirudi kwenye gari na kuchukua mabaki ya nyama na kumpa
" Santeee" aliniambia
" Haya nimeshakupa sepa!!" Nilimfokea alikuwa akichekacheka tu hata hakujali ukali wangu
" Machizi mengine bwana sijui wanajuaje mahali penye kula Sasa si nimempa hataki kuondoka" niliwaza namna ya kumtoa

Nilimnyang'aya ule mfuko wa nyama na kwenda kuutupa nje ya geti alichukia na kutoka 

Wakati anaufata ule mfuko wa nyama Mimi nilifunga geti aliokota mtuko wake na kurudi getini

Niliingia zangu ndani kumalizia usingizi wangu nililala

Niamshwa na kelele zilizotokea getini geti liligongwa mfululizo Kama mtu mwenye Shari

" Hivi Nani nagonga geti langu kwa nguvu hivyo nikimkuta na kata kichwa" niliongea kwa jazba

Kitu nilikuwa sijali ni kumuumiza mtu nilitafuta panga langu nilipoweka na kutoka

Geti liliendelea kugongwa nilifika getini na kufungua sikutaka kuangalia ni Nani aliyekuwa akigonga  

Nilishusha panga kwa aliyekuwa akigonga
" Aaaaah" alipiga ukelele ndipo nilimtazama dah alikuwa ni yule kichaa

" MUNGU wangu!" Nilishtuka maskini nilimkata mguuni yani nyama ya mguu ilining'inia kwa mara ya kwanza niliingiwa na roho ya huruma

Niliangalia pande zote hakukuwa na mtu zaidi yetu nilimvuta mkono na kuingia nae ndani nilifunga geti

Hakuweza kutembea kwasababu ya maumivu
Lakini nilishindwa kumbeba alikuwa mchafu mno hata alikuwa akitoa harufu ya jalala nguo zake hazikujulikana rangi yake zilichafuka Sana
" Sasa nafanyaje na huyu chizi hata nikimpeleka hospitali watasema asafishwe mmh" nilipata wazo kuna mdada alikuwa akinifulia nguo zangu nampa pesa

Nilimwacha yule chizi na kutoka nilienda kumtafuta Asia kwenye nyumba aliyopanga

Nilifika kila aliyeniona alikimbia wengine walibadili njia waliona ni ajabu mtu Kama Mimi kufika maeneo Yale pili waliniogopa kutokana matukio yangu 

Nilifika na kukakuta katoto kadogo Kama wa Mika nane hivi
" Totoo" nako kaliogopa
Mfukoni nilikuwa sikosi bigG nilitoa moja na kumpa hapo kalitulia
"Eti mtoto Asia yuko wapi?"
" Yupo ndani anakula" kalinijibu
" Kamwite" aliingia ndani na kutoka akiwa na Asia,, Asia alishtuka kwa ujio wangu Mana hata yeye nilikuwa nampiga nikikuta nguo hazijatakata
" Ha..hari." alibabaika
" Nifate" nilimwambia nikiondoka kwa jinsi alivyokuwa akiniogopa hakunawa hata mikono 

Tulienda mpaka nyumbani getini
" Harrison umeua au mbona damu getini"
Aliniuliza alipoona damu 
" We acha undezi ingia ndani" nilimwambia

Tuliingia na kumkuta yule kichaa bado akiwa analia

" Harrison usiniambie wewe ndo umefanya hii kazi" 

" Huu si muda wa maswali tuongee biashara"
" Biashara gani unataka uniuzie kesi?"
" Alafu wewe nitakuzibua Sasa hivi,, Sasa ni hivi muogeshe huyu kichaa nataka nimpeleke hospitali"
" Mimi" 
" Sasa Nani naongea nae" 
" Sawa nisaidie kumbeba"
" Mimi nimbebe?"
" Ndio Sasa nitamuogeshaje"
" Hapana we muogeshe hapahapa kwani kichaa anaaibu?"
" Hari..Sasa hapa namuogeshaje" 
" Nakufungia mpira mrefu unamuogesha ukimaliza unafanya usafi nitakuongezea hela"
" Mmh sawa lakini hata Kama ni kichaa huyu bado ni mwanamke ondoka Basi nimvue nguo" aliniambia Asia

Nilitoka nakufunga mpira mrefu nilimtupia na sabuni 

Niliingia chumbani kwangu na kutafuta gauni Mana mademu zangu walikuwa waliacha nguo zao

MREMBO KUTOKA JALALANI

SEHEMU YA 02
Niliingia chumbani kwangu na kutafuta gauni Mana mademu zangu walikuwa wakiacha nguo zao
*********************

Nilipata gauni japo niliona kwake lingepwaya ni gauni ambalo aliacha demu wangu mwamnvita yeye alikuwa kajazia 

Nilitoka mpaka mlangoni niliweka gauni chini 
" Harrisoon" Asia aliniita
" Lete mafuta" aliniambia
" Wewe mwache hapo uje uchukue"
" We Harrison wewe mbona upo hivyo Sasa Mimi namwachaje hapa?"
" Kwani ni mtoto mchanga huyo si anakaa?" Asia ilibidi amwache aje kuchukua gauni na mafuta

Baada ya muda aliniita
" Harrison tayari njoo na tenge"
" Sasa tenge natoa wapi Mana hakuna demu aliyeacha tenge hapa zaidi ya magauni na suruali"
" Basi ngoja nimfunike na langu uje Basi huku tayari"

Nilitoka hata sikumwangalia yule kichaa
Niliingia kwenye gari na kukaa siti yangu ya dereva
" Mbona umeingia "
" Unataka nifanyaje?"
" Ujue Harrison wewe husaidiki Mimi nitampakizaje mwenyewe"
" Mkokote huyo bwana alafu chukua hii pafyupu mpulizie asije akaacha harufu kwenye gari yangu" Asia alimpakiza japo kishida sikutaka hata kumgusa nikihofia kubaki na harufu mbaya aliyokuwa nayo

Alichukua pafyumu na kumpulizia

" Sasa Hari Mimi naondoka?"
" Unaondokaje?"
" Kazi si nimemaliza kazi yako?"
" Unafikiri nani atamshusha kwenye gari"
" Jamani hivi angekuwa ndugu yako usinge msaidia?"
" Aah achana na hayo bwana panda gari twende hospitali"
" Utaongeza pesa"
" Pesa kitu gani bwana?"

Asia aliingia tulifika hospitali tulipokelewa Asia alisaidia kumshusha 

Tulipelekwa mapokezi hakuna aliyethubutu kuuliza nini kilimpata wakiogopa shoo zangu yani jicho moja dokta aliongoza wodini mwenyewe 

Kidonda chake kilikuwa kikubwa Sana kwanza alisafishwa na dawa ambayo ilimsababishia maumivu makali alilia Sana
" Kumbe vichaa nao wanaliaga hivyo" 
" Ujue Harrison unamatatizo?"
" Matatizo yangu ni yapi?"
" Sasa kichaa si mtu Kama wewe"
" Haya nimeuliza tu?"

Tulisubiri mpaka dokta alipomaliza kumshona alitoka
" Nani ndugu wa mgonjwa" aliuliza
Asia alinitazama
" Unaniangalia nini?"
" Nakuangalia wewe mbona huitiki"

Ilibidi niende kumsikiliza dokta
" Huyu ni mkeo?"
" We jiangalie Mimi naweza kuwa na mke kichaa?"
" Kumbe ni kichaa?"
" Kwani we huoni"
" Sijajua mbona yupo Safi tu Kama wanawake wengine"
" Achana na hayo ongea ulichoniitia"
" Mmh samahani ila nikitaka nikuambie tu kuwa uwe makini na kidonda kisiingie maji Wala uchafu utamrudisha hapa baada ya siku tano tutoe nyuzi"
" Niondoke nae sio kwamba atabaki hapa niwe nakuja kumwangalia tu?"
" Kama ulivyosema huyu ni kichaa anatakiwa kuwa na mtu anayemfahamu ili asilete shida"
" Sasa kwani Mimi namfahamu?"
" Wewe si ndo umemleta hapa?"
" Mimi nimemwokota tu huko"
" Kumsaidia mtu sio mpaka awe ndugu au mtu unaye mfahamu huwezi jua ipo siku ukasaidiwa na mtu usiye mfahamu kwakuwa umeamua kumsaidia wee msaidie tu mpaka pale atakapopona "
" Huo ni mtihani nawezaje ishi na kichaa ndani ya nyumba yangu?"
Ilikuwa ni ngumu kwakweli 
" Fanya Kama Dada yako ndo kapatwa na tatizo Kama hili"
" Hata Dada mwenyewe sina labda ningevuta taswira huenda ningekuwa na moyo wa kumsaidia"
" Harrison!!" Asia alihamaki
" Jina langu kwani vipi?"
" Unakuwaje Kama sio mwanadamu wewe?"
" Kwani nimefanyaje?"
" Mungu wangu! Hivi unafikiri hizo pesa zitakufanya usipate shida milele si ndio?"
"We Nani apate shida?"
" Haya bwana ila hasara roho pesa makaratasi tu hayo ipo siku utakumbuka maneno yangu"
" Alafu we Asia naona sikuhizi huna adabu"
" Ni samehe ila naomba usimwache huyo Dada hapa"
" Ni Dada ako huyu"
 " Hapana"
" Sasa mbona unachonga Sana Domo lako haya Basi kasaidianeni mleteni kwenye gari" nilikubali lakini moyoni niliwaza yangu

Asia na yule daktari walisaidiana kumpakiza kwenye gari nilipatiwa na dawa ya kumpa za vidonge
" Asia we panda tax tutakutana kesho sahizi muda umeenda"
" Haina shida nimeshukuru kwa msaada wako" nilitoa elfu themanini 
" Hiyo ni yamalipo yako"

Niliwasha gari na kuondoka

Sikwenda nyumbani nilitafuta jalala nilipaki gari nia yangu ilikuwa nimtelekeze pale nilishuka na kurudi mlango wa nyuma alipokaa yule kichaa

Nilifungua mlango kumbe alikuwa amepitiwa na usingizi 
" Mmh sahizi ni usiku nikimwacha hapa hakuna atakaye niona watakao mkuta asubuhi watamsaidia Mimi siwezi kuuguza mgonjwa kwanza Bora angekuwa mzima Sasa kichaa huyu si majaribu haya" niliwaza lakini pia sikutaka kumshika 
" Yani Mimi nimshike!hapana siwezi"

Niliacha

" Sasa namfanyaje huyu" nikiwa najiuliza mara kuna mtu alinimulika na tochi ilikuwa na mwanga mkali kweli kweli

" Wewe ni Nani na unafanya nini hapa?" Aliniuliza akiwa bado ananimulika
" Asee jomba Kama hujui matumizi ya tochi hebu zima" nilimwambia
 Alizima kweli kumbe alikuwa polisi niliyekuwa namfahamu
" Yani wewe ndo unanitisha nilijua mtu kumbe kijitu"
" Samahani muheshimiwa" aligwaya
" Bora umejitokeza nataka nikupe kazi"
" Kazi gani bosi"
" Nataka utafute mahali tumweke huyu mtu" nilimwonyesha kwenye gari
" Vipi kakata uzi( kafa) au?'
" Hapana kazima tu"
Sehemu zipo nyingi nitoe nikusaidie"
" We mtoe kwanza unamuuliza rickross kuhusu pesa?"
" Samahani" alisogea karibu na gari alianza kumtoa
" Bosi mbona chombo iko vizuri hii kwanini unaisusa" 
" Chombo gani we mtoe!"
" Ila muheshimiwa hujawahi kuchagua kibaya mbona huyu ni bomba hata kuliko mwamnvita, salma,debora,mwajuma,halima,Helena,agnesi,furaha,ponsiana,maimuna, Caterina,na. Wale wengine hawafikii hapa"wote aliowataja walikuwa wanawake ambao nilipita nao alafu walikuwa wazuri si mchezo Sasa kwa maneno ya yule polisi niliona Kama anazingua

" Hebu acha!" Nilimwambia

Nilisoge karibu niliwasha tochi ya simu yangu nilimmulika usoni uso ulizibwa na nywele zake

Nilizitoa nywele kwa kijiti na kuuacha uso uonekane
Alikuwa ni mzuri kweli hata kwa jinsi alivyolala umbo lake lilikuwa bomba
" Shida ni kichaa Sasa"nilijisemea

Nilimtizama kwa muda niliona sio sawa jinsi alivyo nikimuacha wahuni wanaweza kumbaka Bora hata alivyokuwa mchafu ni ngumu watu kumtamani

Nilichukua uamuzi wa kwenda nae nyumbani niliingia kwenye gari 
" Umebadili mawazo bosi?" Aliniuliza 
" Ndio nampeleka jalala lingine"
' poa niachie hata ya maji" nilichomoa elfu kumi na kumpa 

Yani kwangu watu walikuwa wakipiga kelele ya vitu vingine sio suala la pesa ukiita tu zinakuja

Nilifika nyumbani nilisimamisha gari na kwenda kufungua geti

Ile namaliza tu kufungua Peter alifika
" Harrison hii ni Mara ya tatu nakuja hapa"
" Unataka nini?"
" Kulala ndugu"
" Kalipe Kodi kalale kwako"
" Hee!"
" Ndio leo Nina mgeni"
"Kuanzia lini ukaniondoa ukipata demu Mimi si nalala chumba kingine we unapiga chumba kingine Kama kawaida"
" Nimesema sitaki!"
" Harrison mbona sikuelewi huko kwenye gari umembeba kwini?"
" Hata Kama angekuwa kijakazi wewe haikuhusu kwani lazima ulale kwangu?"

Peter alinishangaa Mana haikueahi kutokea hata Kama nikiwa na mwanamke nilimruhusu alale nami nililala na mwanamke Wangu chumba kingine

Kwajinsi nilivyokuwa najikubali na sikuwa na ukaribu na watu wasioeleweka sikutaka Peter ajue Kama nipo na kichaa kwakuhofia angenishusha thamani na kumuongelea kwa marafiki zangu wenye hadhi yangu niliona Kama ni aibu

Wakati nageuka Peter tayari Alisha ingia kwenye gari nakuwasha iliaingize gari ndani


"
  MREMBO KUTOKA JALALANI
SEHEMU YA 03
Wakati nageuka Peter tayari Alisha ingia kwenye gari iliaingize gari ndani

Endelea
" We Peter vipi"
" Naingiza gari"
" Mbona sio mwelewa jamaa yangu nimekwambia Leo kalale kwako?"
 
Aliingiza gari kibishi alipaki na kushuka
" Harrison fungua Basi ninausingizi mwenzako"
" Oya naona hatuelewani" niliingiza mkono mfukoni na kutoa wallet nilichomoa elfu kumi na kumpa
" Chukua hiyo kalale gesti"
" Daah hata siamini kweli upo radhi unipe hela sio kulala hapa"
" We bahna shida ni kulala au kulala hapa kwangu?"
" Kulala tu"
" Haya kalale gesti"
" Poa bwana kesho"
" Poa"

Peter aliishia zake habari ilikuwa kumshusha yule kichaa
Nilifungua mlango nakumwangalia alikuwa bado kalala
" Nafanyaje sasa au nimwache alale humuhumu kwenye gari" nilikosa namna nilijikaza tu nikambeba mpaka ndani sikutaka kumweka kwenye sofa zangu nikamlaza chini Kisha nikachukua shuka chakavu na kutandika chini nikamlaza kwasababu kilikuwa na joto nikawasha feni alafu nikaa kwenye sofa 
" Nskia njaa Sana Sasa naondokaje nimwache huyu chizi akiamka kilakitu nitakuta hakifai acha tu nivumilie nitakula asubuhi"

Nikawasha ps na kuanza kucheza gemu sauti za ps zilimwamsha aliamka na kukaa Kama kawaida alinyoosha mkono akiniomba
" We chizi hebu niache mi mwenyewe naskia njaa hapa"
Hakuaacha alizidi kunyoosha 
" Huniskii" nilimfokea hapo nikawa nimemtibua alianza kulia kila nikimwbia anyamaze ndo kwanza alizidisha 
" Aisee nitakubamiza acha kelele unataka watu wajue nipo na chizi huku ndani" Kama nilimwambia azidishe marakumi alipiga kelele nilishindwa kuvumilia nilimsogelea na kumpiga kibao Cha shavu alisugua shavu lake huku akiukokota mguu wake wenye kidonda sikumjali nilisimama na kuingia chumbani kulala kwa uchovu niliokuwa nao sikuchukua mda nililala

Nikiwa usingizini nilikuwa naota Kama kuna mtu anapiga ngoma niliamka kumbe ilikuwa kweli niliskia sauti ya kitu kikipigwa nilitoka mpaka barazani nilichokikuta ni kwamba yule kichaa alikuwa akiponda TV nilikuta ipo nyang'anyang'a nilichukia mnoo 

Yani kirahisi tu apasue tv yangu sikujali ni mgonjwa Wala kichaa nilichukua mkanda wa suruali nilimchapa 
" Nakuambia utapona hicho kichaa we mwehu unajua nimenunua shingapi hii tv" niliendelea kumchapa alilia akitamka maneno

" Sitaki Robby niache Robby" ilibidi nimuache kwanza nikamsogelea nakumuuliza
" Robby Nani hapa?"
" Wewe" alijibu
" Mimi Robby?"
" Niache Robby sitaki" alirudi nyuma

Nikawaza huyu chizi atakuwa anamuogopa mtu anaeitwa Robby Basi nikawa nampima
" We tahira zoa takataka zako hapa" aliniangalia tu
" Kwanini Robby anakuambia kitu husikii?" Niakamuona haraka kajivuta mpaka kwenye Yale mabaki ya TV alianza kuyakusanya  

Nikawaza huyo Robby ni Nani Mana kichaa kumuogopa mtu mwenye akili zake ni ngumu ninavyojua Mimi watu wenye utimamu wa akili Mara nyingi huwa wanawaogopa vichaa kwa kuhofia kupigwa mawe au na kitu chochote hata kukimbizwa

Yule kichaa alikusanya mabaki yote na kuweka mwenye gauni lake na kuanza kuyachezea 
" Hivi wewe Leo tu ndo siku ya kwanza umenipasulia tv nikiendelea kukaa na wewe hapa si utanalizia kilakitu" nilimuuliza lakini Wala hakunijali aliendelea kuchezea Yale matakataka
" Oosh naweza nikapiga mpaka nikaua nikaacha kula Bata nikaishia kula maharage ya jela sijui hata nimpeleke wapi au nimwajiri Asia"

 nilipata wazo nilimtoa yule kichaa na kumpeleka stoo ambako kulikuwa na mavitu ambayo nilikuwa siyatumii Kisha nikasafisha pale barazani na kurudi chumbani kwangu haikupita muda nikaskia kelele stoo

" Jamani huyu chizi nae hataki nilale nitamtoa nje huyu ngoja nimwendee huko atanitambua" nilivuta mkanda nikidhamiria nikamchape

Nilifika stoo na kumkuta kwenye Kona kajibanza akipiga kelele ya kuomba msaada
" Robby unaniuaaa Robby niache niende" ilibidi kwanza nimwangalie kwajinsi alivyojibanza ni Kama Alikuwa na uoga Sana nilichuchumaa na kumtoa mikono aliyojizuia usoni

Uso uliloa jasho na machozi alikuwa akitetemeka mwili wote alinivuta shati na kunikumbatia akisema nimsaidie Robby anakuja 

Ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwangu sikuwa na namna nilimchukua Tena na kumpeleka barazani nikiangalia mguu wake alishajitonesha niliingia chumbani na kuchukua kitaulo kidogo nikakilowesha na kumfuta damu iliyokuwa ikitiririkia mguuni
" Robby umerudi?"
 Aliniuliza akinitazama usoni kwaupole na macho malegevu utadhani hana tatizo lolote nilijikuta navutika na macho yake nilitamani anitazame tu lakini ghafla alianza Tena kulia 
" Nyamaza basi usilie" nilimwambia nilimsogeza kifuani nikimbembeleza kwa kumsugua kichwa chake mpaka akalala kituani nilimtazama Sana usoni nilijiuliza mbona ni mzuri Sana hata kuliko wanawake wote niliopita nao Ila mawazo yangu yalisita baada ya kukumbuka kuwa ni kichaa basi kuanzia muda huo niliamua kumfanyia uungwana nilimbeba na kumpeleka chumbani kwangu nilimlaza nami nikachukua shuka nikatandika chini na kulala

Asubuhi niliamka na kwenda jikoni nilicheki mtungi ulikuwa mtupu Mana Mara ya mwisho kupika ilikuwa siku ya kuanua matanga kwenye msiba wa baba kuanzia hapo nilikuwa mtu wa kula kwenye hoteli za kifahari na kushinda klabu

Nikampigia simu Asia akaja
" Vipi Harrison usafi au"
" Hapana gesi"
" Gesi?"
" Ndio mtungi hauna gesi"
" Wewe Harrison unaumwa leo au?"
" Kwanini?"
" Nahisi Kama unamaleria "
" Mimi mzima mbona"
" Hapana hebu twende hospitali"
" Kufanya nini Sasa?"
" Kupima malaria"
" Asia Mimi ni mzima!" Nilifoka
" Umekuwaje leo hari?"
" Kwanini Asia!!!"
" Kuulizia gesi leo?"
" Aah acha Basi na wewe nipo siriazi ujue"
" Mmh haya gesi ya nini?"
" Kupika"
" Oho oho oho oho " Asia alikohoa
" Vipi umepaliwa au?"
"Wewe ndo umenipaliza Mana kupika na wewe ni paka na chui"
" Umesahau ninamgonjwa? hapa kalala akiamka hapo ataanza kunyoosha mkono Kama anaomba sadaka"
" Hapo nimekuelewa lakini nimeshangaa wewe kutaka kupika"
" Sipiki Mimi"
" Nani anapika Sasa?"
" Wewe ndomana nikakuita"
" Nilitaka kushangaa Sasa tunafanyaje?"

"Acha nipige simu niletewe mtungi wa gesi wewe toa nje mtungi"
Nilipiga simu baada ya muda honi iliskika nje Asia alitoa mtungi na kuingia na mwingine uliojaa gesi

Niliunganisha 
" Hapa una chochote Cha kupika" aliniuliza Asia
" Hamna labda ukanunue"
" Nipe hela niende" nilimpa akaenda kununua Kisha akarudi akiwa na mazagazaga yote Asia alianza kupika chai mi nikaenda chumbani kumwangalia yule Dada Kama ameamka nilichokikuta nilitamani nipige wange Mana nilimkuta yule kichaa amekatakata godoro langu kwa kunyofoa Kama panya buku anavyotoboa ardhi na kutokea sehemu nyingine 

Nilichukia nikitamani nimpige haswa Ila niliacha nikawaza hata nikimpiga atafanya tukio lingie Mana amepasua tv nikampiga Sasa godoro langu daah nilimwangalia hata hakushtuka alinochekea tu

Nikasema na ubabe wangu wote lakini nimekutana nacho sio kwa matukio haya ukicheki ndo siku ya pili ikabidi nimtoe tu pale chumbani na kumpeleka barazani Kisha nikarudi chumbani nikakaa kwenye kiti nikiwaza kweli nilimkata na panga na nimeamua kumuudumia lakini mbona imekuwa kero kila kukicha ni hasara Basi tu sikuwa na namna Ila nikasema akipona tu namtoa kwangu

Kwakuwa hela ilikuwepo nikaagiza godoro jipya lile nikalitoa nikapeleka stoo 
" Harrison" alinita Asia
" Naam"
" Vipi mbona umepoa Sana hutoki huko ndani?"
" Yani sijui Kama mpaka huyu chizi apone nitakuwa nimepoteza vitu vingapi?"
" Kwanini?"
" Njoo uone" Asia aliingia ndani na kukuta vipande vya godoro
" Kuna panya au?"
" Bora angekuwa ni panya huyu panya mtu" akaniuliza kwanini ikabidi nimpeleke stoo kuangalia hali ya godoro
" Hee mbona unashughuli"
" Ndohivyo ndomana nikasema siwezi kuishi na kichaa mkaniona ninaroho mbaya ona Sasa anachofanya usiku kavunja tv Leo godoro haya kesho ataharibu nini?"
" Mmh kweli hii shughuli lakini vumilia zikitimia siku tano ukimpeleka kutoa nyuzi tafuta mahali pa kumpeleka"
" Hata hizi siku tano naona Kama miaka mitano Ila Sasa nafanyaje"
" Pole yako vipi lakini dawa umempa?"
" Sijampa nampaje Sasa hizo dawa atakubali kunywa Sasa?""
" Hebu kalete tumpe" niliingia chumbani na kutoka na zile dawa nilizopewa na daktari Asia all chukua maji kwenye kikombe na kumpeleka alipo kaa alifungua dawa na kumwambia apanue mdomo kweli aliachama Asia akamwekea dawa mdomoni Kisha akampa maji anywe aliyapokea na kunywa kutu kazaa Kisha akajaza maji mdomoni nilishangaa maji yakinitulia usoni yani alinitemea

Nikasema hata Kama ni kichaa hawezi kunifanyia Mimi Kama chizi mwenzake nilimsogelea nimnase hata Kofi Asia anilizuia
" Niache Asia nimpige hawezi nitemea mimate yake huyu"
" Hari elewa huyu Hana utimamu wa akili tofauti na wewe mwenzio hapo alipo anaona kilakitu sawa hajui jema Wala baya huyu"
" Hapana acha nimzabe aniogope"
" Siwezi kuruhusu wewe uliamua kumsaidia wee msaidie Mana ulijua kuwa ni kichaa sasa kwanini umpige"
" Asia atanizoea huyu"
" Msamehe tu bahna " nilitulia na kukaa mezani hata yeye muda huo alikuwa ametulia 

Asia alitenga chai na tambi Sasa ile kuona chai alichukua na kuigugumia nikashangaa katupa kikombe chini na kuanza kulia alikuwa ameungua na chai
" Nawe huoni chai ya Moto hii Yani akili imefyatuka hata macho yamefyatuka inamaana hujaona mvuke ukipanda" nilimfokea Sana hata Asia alisikitika

" Harrison ukiendelea hivi sitakuwa nakuja kukusaidia ujue kuwa Basi na roho ya utu"
" Kwani Mimi ninaroho ya mnyama?"
" We hujioni unakuwa Kama gaidi fulani akati wewe ni kijana Safi tu yani kwajinsi muonekano wako upo ni vigumu mtu kujua tabia yako unaonekana uko smart kumbe ni mtu mmoja mbaya Sana hujali mtu"
" Mtu gani huyu chizi?"
" Chizi sawa lakini ni binadamu Kama wewe"
" Bwana usiniimbe Mimi Basikunyweni nyinyi Basi mi sinywi"
" Acha bahna we usitupeleke sisi"

Niliwaacha na kutoka nje ile nafika tu getini nilikutana na Peter nikajua hapa kumekucha alafu ubaya ni kwamba Peter sio msiri hata kidogo inamaana angemuona tu lazima angeenda kutangaza Peter alinisalimia
" Vipi Harrison?"
" Poa niambie!"
" Shwari mbona hivyo unaenda wapi?"
" Naenda zangu mtaani"
" Bila gari?"
" Nataka nifanye mazoezi ya kutembea"
"Twende basi Mana leo nipo free nikasema nije tushinde hapa kwako tule ngoma"

Kwakuwa sikutaka aingie ndani nikamwambia anisubiri nichukue gari basi nilichukua gari tukaondoka zetu kwenda misele kwanza nilikuwa nimemisi madem zangu nikampigia simu Catherine
" Bebi Mambo?"
" Poa mzima wewe"
" Mi mzima ukowapi naona umenipigia asubuhi asubuhi"
" Nipo hapa lete raha bar"
" Kwahiyo?"
" Njoo chap nimeshachukua chumba"
" Sawa bebi nakuja hapo sasahivi"

Nikaagiza k.vant kubwa pale na nyama tukaanza kula taratibu na jamaa yangu Peter ndani yanusu saa Catherine alifika akiwa ametinga short pensi na kibrauzi alikuwa amedamshi mbaya nikajisemea cathe ndo atanituliza hasira zangu 

Nikmjaribisha nae akanywa kidogo nikamwambia twenzetu chumbani tukaingia Sasa nikawa nimemkumbatia Mara simu ikaita alikuwa ni Asia
Nikaipuuza iliita mpaka ikakata nikawa naendelea tu kucheza na Catherine Mara simu ikaita Tena kwa hasira nikaamua kupoke
" We vipi asee mbona msumbufu"
" Acha ujinga njoo chap Mana Mimi yamenishinda huku"

 
MREMBO KUTOKA JALALANI 

SEHEMU YA 4
Nikawa naendelea tu kucheza na Catherine mara simu ikaita Tena kwa hasira nikaamua kupoke
" We vipi mbona msumbufu?"
" Acha ujinga njoo chap Mana Mimi yamenishinda huku"

SONGA NAYO
"Bwana mi siji pambana nae si ulikuwa unamtetea"
" We Hari Mimi naondoka utajua wewe utakachokikuta huku"
" Achana na Mimi bwana" nilikata simu

Catherine akaniuliza ni Nani huyo nikamwambia ni mlinzi akashangaa akasema kuanzia lini ukawa na mlinzi nikamwambia nimemwajiri kwa Leo tu Mana kuna mbwa anasumbua akasema poa Sasa Kwanini umemwambia anasumbua nikasema aah achana nae hana lolote basi Catherine akaridhika tukaendelea na yetu tukakaa huko mpaka saa mbili usiku 
" Cathe Mimi acha niende nyumbani"
"Sawa twende"
" Namaanisha Mimi sio wewe"
" Si tunaenda wote"
" Hapana Leo naenda mwenyewe"
" Jamani Hari acha utani Basi utaniachaje hapa usiku huu" 
" We si unaenda kwako"
" Mi siendi nataka niende na wewe kwako"
" Ila kuna wageni kule"
"Tangu nikijue sijawahi kukuona ukimkaribisha mtu kwako zaidi ya yule Asia mfanya usafi haya hao wageni wamefika kutoka wapi na ninavyojua hata ndugu huna au Kuna mwanamke mwingine huko kwako?"

" Hapana dear ni wewe tu jamani ndo mwanamke Wangu Sina mwingine"
" Sasa Kama hakuna Leo nataka twende wote huko nikawasalimie wageni na uwaambie Mimi ndo mkewako"
" Ohoo ujue nini ni viongozi wa dini"
" Kuanzia lini ukawa na ukaribu na viongozi wa dini si unawatimuaga kwako wewe?! Hata Kama hao ndo wazuri Mana hata ndo tutafungishwa hukohuko"

Catherine hakutaka kuelewa kabisa
niliona Kama ananchanganyia habari ukicheki sikumuweka moyoni Wala nini wanawake wote niliwachukulia Kama starehe tu nikaamua Bora nimwage tu Mambo ya kuleteana habari za ndoa mi sinaga
" Oya naona hatuelewani kuanzia leo kilamtu afanye yake tusitafutane"
" Jamani Harrison tunaachanaje hivi kwasababu nimesema habari za ndoa?"
" Tunaachana Kama ifuatavyo Mimi naondoka ukitaka utaondoka na wewe Kama hutaki lala hapa bili ikiongezeka utalipia"
" We usinitanie Yani unitumie uniache"
" Nimekutumia tumetumiana okay nimekupunguza wapi?"
" Hujanipunguza"
"Nimekuweka alama?"
" Hapana"
" Umeumia?"
" Hapana "
". Naona uko sawa Kama ulivyokuja Cha kukusaidia chukua kaki( elfutano) hii itakusaidia nauli ya kurudi kwako"
" Jamani Harrison kwa kukupenda kote unaniacha?"
" Umenipenda au umependa pochi yangu alafu nyie mademu mkiona mtu ananoti ndo mnagaaanda Kama ruba"
" Unamaana gani kusema mademu inamaana unao wengi"
" Si nilikwambia ukopeke yako Yani nikitoka hapa ndo nitampata mwingine"
" Jamanii"
" Jamaika watalam wa kufuga Rasta ukitaka nenda"

Nilitoka na kumpitia Peter wakati huo alikuwa amelewa hajitambui tukaingia kwenye gari na kusepa ilibidi niingie gharama Tena badala ya kwenda kwangu tukaenda kwa Peter huko nako nikakutana na mizinguo mwenye nyumba alitia kufuli mlangoni akidai Kodi 

Nikamshusha Peter na kumlaza pembeni ya chumba chake nikaamua niende tu nyumbani ile kufika nyumbani nakutana na watu wa kutosha
" Kuna nini hapa" niliwauliza
" Unauliza nini inamaana huoni au? " Nilijibiwa na jirani mmoja 
" Hilo sio jibu niambie kunanini" 

Akaniambia nisiulize maswali mengi niingie ndani niliingia getini daah yalikuwa ni machafuko nyumba yote iliteketea kwa Moto nguvu ziliniisha kwajinsi nilivyokuwa naipenda nyumba yangu ndo hiyo pekee niliyoachiwa urithi alafu imeungua akili nikakumbuka jinsi Asia alivyonipigia simu akinitaka nije haraka kumbe ilikuwa ni kwaajili hii nikageuka na kuwaendea wale watu
Nakuwauliza Kama wamewaona wadada wawili Asia na yule kichaa kilamtu akasema hajawaona ni mmoja tu ndo akaniambia alimuona mdada mmoja tu jirani ambae ni Asia. 

Nilishtuka Sana nikasema Kama Asia hajapata madhara Basi yule kichaa atakuwa kaungua sikuwaza Tena kuhusu nyumba akili ilihamia kwa yule kichaa nikasema kifo chake Mimi ndo sababu laiti nisingempuuza Asia ningeweza kuokoa maisha yake niliumia mno lakini hakuna aliyenijali kutokana na Mambo niliyokuwa nikiwafanyia kuwapiga kunyang'anya wanawake za watu kuchukua vitu kibabe hivyo yani kwao ilikuwa Kama furaha 

Kuna waliosema afadhali kinyumba chake kimeungua tuone atatamba na nini labda hicho kigari wengine wakisema Bora hata nayeye angekuwa yumo ndani afe kabisa mbwa huyu alijifanya mungu mtu Sana huyu nakutuona wengine sio watu apambane Sasa 

Maneno yao niliyasikia lakini sikuwa na nguvu hata ya kuwajibu Mana waliongea ukweli kabisa nilikuwa mtu wa dharau Sana na kuwaona wengine sio daah niliinama chini nikiangalia moto ambao ukimalizikia kwenye maua niliishiwa pozi

Lakini nikajifariji pesa ipo nitafanya marekebisho ya nyumba lakini je huyo kichaa wa watu nitaongea nini siku ya hukumu Mana sikumchukulia Kama mtu wa kawaida nilimuona Kama ni msumbufu kwenye maisha yangu 

Nilikaa pale kilamtu aliondoka eneo lile nikabaki peke yangu nikiwaza nikahisi namuona yule kichaa ananililia na kuniomba msaada nilinyanyuka na kwenda kumshika kumbe ilikuwa hewa tu nikajua kumbe roho yake inanidai

Nilirudi kukaa kwenye gari machozi yalinitoka nikijilaumu Bora hata ningekuja mapema ningeweza kumnusuru Imani yangu ilinituma hivyo Mana kwajinsi mguu wake ulivyokuwa ni ngumu yeye kukimbia 

Sikuwa na msaada wowote nilitoka pale na kwenda kwa Asia nilifika na kumkuta akijipaka asali kwenye vidonda alivyo ungua aliponiona alilia Sana na kunilaumu
" Harrison wewe ni mnyama hufai ni Bora ungezaliwa punda ubebeshwe mizigo kuliko kuwa binadamu usiye na faida kwenye jamii umekuwa ukiishi Kama chui kwa watu ona leo umefanya tukose msaada kwa watu nimeungua Mimi nashukuru nipo hai yule Dada wa watu amefia kule ndani  
Kwa Sababu yako wewe katili "

Kiukweli roho iliuma mnoo nilitami hata yule kichaa angekuwa mzima Basi nimtendee japo wema mmoja tu nisamehe dhambi zangu lakini haikuwa hivyo nilimkumbatia Asia nilimuomba anisamehe Sana hakunijibu zaidi ya kulia
 
Baada ya muda aliacha akiniambia Harrison Mimi nitakusamehe vipi kuhusu roho iliyotoka kwa maumivu makali nikamwambia hilo limeshatokea Sinabudi kukabiliana nalo Kama dhambi nimeshaibeba akasema sawa yeye Hana pesa za kujitibia inabidi nimsaidie nikamwambia usijali 

Basi nikaelekea duka la dawa nikanunua dawa ya Moto na ya maumivu nikampa Asia nikapanga asubuhi niende benki nikatoe pesa

Asubuhi ilifika uzuri kadi ya benki nilikuwa natembeaga nayo Kama nguo zangu nilichukua gari nikaenda benki nilimpatia kadi na kutaja kiasi Cha pesa ninayotaka kutoa
" Kaka samahani huwezi kupata pesa unazotaka"
" Kwanini yani benki mmekosa milioni ishirini ya kunipatia Sasa mnafanya nini hapa si Bora mfunge tu"
" Hapana sio kwamba hakuna pesa"
" Ila?"
" Kwanye akaunti yako Ina milioni tatu tu"
 "Milioni Tatu unakichaa nini we manamke Yani akaunti yangu isiwe na pesa acha utani wewe" 
" Kaka akaunti yako Haina pesa hiyo!! "
" Alinitupia kadi" nikaona hanijui nilizunguka na kumvamia 

Nikampiga makofi akapiga kelele baada ya kukolea kipigo walinzi walifika chapu kwanza hawakuuliza tatizo walinipiga mpaka nikawa sioni mbele mpaka meneja alipotoka ndo ikawa pona yangu kwakuwa tulifahamiana Sana alikuwa Kama rafiki yangu

Aliwatuliza watu na kunichukua tukaingia ofisini kwake uso wote uliloa damu nguo zangu zilichanwa

" Imekuwaje Harrison unaleta vurugu hapa nisinge toka si wangekuua?"
" Muhudumu anazingua mkuu"
" Nini tatizo?"
" Nimekuja kutoa pesa eti ananiambia Sina pesa akati najua akaunti yangu inapesa za kutosha"
" Sikiliza Harrison mashine hazidanganyi"
" Hapana labda zimeharibika angalieni vizuri"
" Okay twende tukaangalie kwa Mara nyingine"

Basi tulitoka na meneja na kwenda kuangalia Tena jibu lilikuwa lilelile kulikuwa na milioni tatu pekee
Tukarudi ofisini kwa meneja
" Harrison ujue kwa kumbukumbu zangu nakumbuka tangu ukabidhiwe mirathi yako na kilakitu hukuwahi kuja kuweka pesa zaidi ya kutoa tu nilikuwa nakushauri Sana Mali bila daftari huisha bila habari unapoambiwa daftari sio daftari Kama unavyojua daftari ni mipango na hesabu ya pesa ipo kwenye kuendeleza kile ulichonacho sio kutumia pasipo kuingiza chochote ona Sasa hapo ulipo hakuna ulichofanya chochote Kati ya Yale niliyo kushauri au naongopa?"

" Hapana"
" Ulishajiwekeza kwenye kitu chochote?"
" Hapana"
" Hilo ndo tatizo kwani hizo pesa ulitaka kufanyia nini?"

Nilimweleza yaliyonikuta 
" Duuh pole Sana matatizo hayana hodi na ndio maana tunaambiwa akiba ni muhimu laiti ungejiwekea akiba leo ingekusaidia ningekushauri uchukue mkopo lakini hujakidhi vigezo Mana hujawahi kuweka pesa zaidi ya kutoa benki haiwezi kukuamini na mteja wa namna hii"

Kweli kauli yake ilininy'ong'onyesha Sana nikasema okay Bora nichukue tu hichokiasi Cha pesa kilichobaki kinisaidie hata kumtibia Asia na kujikimu

Nilitoa pesa zote na kuacha akaunti yangu nyeupe pee nikarudi zangu kwa Asia nikampeleka hospitali alipewa matibabu nikaambiwa kila baada ya siku mbili niwe nampleka kusafishwa 

Basi nilifanya hivyo mpaka pale alipopona na kuendelea na shughuli zake nilibakiwa Kama na milioni mbili na laki tano tu mfukoni ikabidi ninunue bati za bei rahisi na mambao ya kuezekea nyumba yangu Mana iliungua bati zote na mbao pamoja na vitu vya ndani

Pesa kidogo iliyobaki nikanunua nguo Mana sikuwa na nguo Sasa mbao na bati nilipata Ila pesa ya kumlipa fundi na kurekebisha kule ndani ikawa mlasa

Nikawaza nimtafute Peter jamaa yangu Mana tangu nipate ajali ya Moto hatukuwahi kuonana nikasema atakuwa hajui kilichonikuta na ndio maana hajaja hata kunijulia hali

Nikampigia simu iliita na kupokelewa
" Haloo"
" Eeh Peter jamaa yangu vipi?"
" Poa kwani wewe Nani?"


MREMBO KUTOKA JALALANI

SEHEMU YA 5
Nikampigia simu iliita na kupokelewa
"Haloo"
"Eeh Peter jamaa yangu vipi?"
"Poa kwani wewe Nani"
********************

Ilikuwa ni ngumu kuamini Kama Peter angeweza kuniuliza Mimi ni Nani  
Nilikata simu na kuangalia vizuri namba labda nimekosea niliicheki Mara mbilimbili Kama ni yenyewe ilikuwa ni yenyewe nikapiga Tena nijitambulishe Mana huenda mtu alibadili simu au la namba zikapotea
Simu ilipokelewa
" Eeh" aliitika
" Ase Peter Mimi ni Harrison"
" Harrison vipi?"
" Sio poa jamaa yangu nimepata matatizo ndugu yangu"
" Kwahiyo unataka nini" 

Nilishangaa Peter hakuniuliza matatizo yangu alihitaji kujua nataka nini khaa sikuamini kabisa eti haikuwa kawaida kabisa ninapo mwambia ninajambo lazima aulize Jambo gani swali lake lilinifanya nijiulize au atakuwa anajua nini Sasa kwanini akae kimya sikuridhika Wala nikamwambia shida yangu
" Oya Peter ee mwenzio nimeunguliwa na nyumba yangu Sasa nimeenda kutoa pesa nikaambiwa Sina pesa kwenye akaunti yangu nilikuwa naomba..."

Kabla sijamaliza alinikatiasha
" Oya Niko kazini nitakutafuta baadae" nikamwambia poa sikumuuliza kuhusu kazi Mana kwa kipindi ambacho tuliachana Mara ya mwisho alikuwa Hana kazi ndio maana alishindwa hata kulipa Kodi

Ikabidi nisubiri mpaka pale atakapo nipigia nikakumbuka rafiki yangu mwingine anaitwa abdala nikampigia simu ili nimwambie kilichonikuta nilimwambia matokeo yake akaniambia Bora hata limekutokea wewe Mana ingekua ni mimi mbona ningetaabika we mwenzangu unajiweza tengeneza nyumba mambo yaendelee

Daah hata shida yangu sikumweleza aisee nikamtafuta demu wangu mwamnvita Mana kidogo alikuwa na uwezo
" Haloo bebi"
" Nani bebi wako nyumba imeungua ndo unataka kunililia shida samahani mimi na wewe mkataba umeisha isije nikaanza kulea mtumzima bure"

Baada ya maneno hayo alikata simu yake nikavuta pumzi nikaweka simu pembeni na kuanza kufanya usafi wa nyumba nzima Mana nilikuwa nalala tu kwenye chumba Cha nje ambacho baba alijenga kwa ajili ya mlinzi .Asia nae alipata kazi sehemu nyingine Mana sikuwa na uwezo wa kumlipa tena 

Siku zote nilizo kaa tangu nyumba iungue sikuwahi kuzunguka hata nyuma ya nyumba yangu siku hiyo kwenye kufanya usafi ndipo nikaona ukuta wa nyumba kutokea chumba Cha stoo umebomolewa na ukuta wa fensi pia

Nikasema ninikilivunja nyumba au wezi lakini mbona hapakuibiwa nilikumbuka Mara ya mwisho nilipo mpeleka yule kichaa stoo ilikuwa nzima kabisa hata siku ya pili kulikuwa Safi Sasa lini kulivunjwa hilo ndo swali nilijiuliza
Ila nikasema ndo imetokea haina jinsi mzigo ukawa umeongezeka Mana tofali nazo zilitakiwa ili kuziba kuta zote mbili

Nikamaliza kufanya usafi muda wa saa moja jioni nikaoga nikawa nimekaa tu mule ndani ya chumba Cha mlinzi nikiwaza maisha mazuri ambayo nilikuwa nikiishi marafiki kila Kona wanawake ndo usiseme lakini leo hata marafiki ambao nilikuwa nakula na kunywa nao siwaoni

Nikapata jibu kuwa marafiki wa kweli ni wale unaowapata kwenye shida na matatizo sio wale ambao utakuwa nao kwenye kipindi Cha raha hata wanawake wote niliokuwa nao niliamini walinipendea pesa

Nilijuta Sana kutumia pesa vibaya ona Sasa nataabika niliokula na kunywa nao hata mmoja hakuna anayenipa sapoti Mana wengine walikuwa ni majirani tu lakini hawakukanyaga hata mmoja

Nikabadili mwelekeo nikawa na shinda ndani tu kuogopa aibu Mana hata jeuri ya kwenda sijui baa club disko sikuwa nayo kwa Wakati ule

Maisha yangu yaliyumba mnoo nilitami hata kuiba Mana kuna muda nililala njaa kwa kukosa pesa hata mafuta mazuri ya kujipaka nilishindwa kununua pesa napata wapi sasa

Kuna wakati nilimpigia Asia aniletee hata chakula alichopika alinipa wakati mwingine alikataa akisema hawezi kunisaidia angali bado Nina nguvu nikaona ni sawa tu Mana Kama maisha niliyachezea mwenyewe na yeye ni mwanamke asingeweza kupambania maisha yake anipambanie na Mimi kula Wala sikuchukia hata

Siku moja nilitoka nyumbani nikawa nazuga tu mtaani muda uende nikalale zangu ulikuwa ni usiku wa saa mbili nikapitapita mtaani watu walininyooshea vidole na kuongea walivyo weza

Nikaingia mtaa mmoja hivi njaa ilikuwa imenikamata si kitoto hadi nikawa nasikia kichefuchefu nikachuchumaa ili nitapike nikaskia mtu akinigombeza
" We Kaka katapikie kule jalalani sio hapa njiani unataka tukanyage matapishi yako" niligeuka ili nimuombe samahani kwanza nikifurahi pili sikuamini kilichofata

" Helena!" Nilimwita alikuwa ni mwanamke Wangu pia alikuwa akinipenda sana
" Harrison?"
" Ni Mimi mzima wewe"
" Mi mzima hapa umefata nini?"
" Napita tu"
" Ohoo sawa mbona kwa miguu vipi?"
" Nafanya zoezi tu"
" Usiku huu?"
" Ndio kwani wewe ndo unakaa hapa"
" Ndio nakaa humu ndani ya fensi"
" Nimefurahi Sana kuonana na wewe"
" Mmh"
 " Aliguna"
" Vipi mbona umeguna hujafurahi kukutana na Mimi?"
" Nimefurahi Sana kuonana na wewe pia ningependa ukaribie ndani"

Nilifurahi moyoni sikubisha Wala nini nilimfuata na kuingia nae ndani
" Naona upo na mgeni?" Jamaa mmoja alimuuliza Helena
" Ndio alikuwa anapita huko nje nikaona nimkaribishe
" Kumbe karibu aisee"
" Asante nilishukuru na kukaa kwenye kiti Cha pembeni yake"
" Helena Nani huyu?" Aliuliza
" Huyu ni.ni.. alikuwaga jirani yetu tu"
" Kumbe?"
" Ndio nimemuita kunamzigo nataka nimpatie anipitishie pale kwa Anita"
" Sawa"

Nilikaa kusubiri nikishangaa mazingira ya pale ndani ulikuwa mjengo wa maana wenye kilakitu Cha kuvutia nikasema Helena atakuwa anafanya kazi za ndani pale

Baada ya muda Helena alitoka akiwa na mfuko mdogo 
" Acha basi nimtoe nje" alimwambia jamaa
" Sawa Helena"

Tulitoka nikiongozana na Helena moyoni nilijua Helena ameniita kwasababu ya mapenzi yake kwangu
" Harrison" aliniita baada ya kutoka nje kabisa
" Leo nimeamua nikurudishie vitu vyako"
" Vitu??"
" Ndio" alitoa cheni na Pete ambayo nilimpaga aliponiambia ananipenda Sana na nilikuwa nikimpelekesha Sana kwenye mapenzi hata naweza kuwa na mwanamke pembeni yake na asiseme kitu na endapo atasema nilimpa kipondo Basi akaniambia Mimi naondoka na Pete na cheni hii itakuwa Kama ishara ya upendo wangu kwako na Kama nitaacha kukupenda basi nitakurudishia vitu vyako

Sikutaka kuamini kuwa ameacha kunipenda Tena
" Harrison nilikuvumilia kwa mengi mazuri na mabaya yako nilikupenda kuliko nilivyojipenda mwenyewe Sasa nimekaa na vitu vyako nimeona najidanganya upendo wangu kwako I lishaisha na nimekukaribisha ndani uone si kila nilichokipoteza kwako kitapotea milele nimepata mtu wa kutuliza maumivu na kuziba vidonda ulivyovisababisha wewe hapa ni kwangu na mume wangu kipenzi sijuti kukufahamu nashukuru nimejifunza mengi na kupitia wewe nikaukataza moyo kupenda pasipopendeka moyo ukaniitika na mwishowe nilipendwa na hapa ndipo ninapo pashika chukua vitu vyako sepaa!"

Alinitupia asee ikabidi niokote na kuondoka hata kichefuchefu kiliniisha nikizitazama ile cheni na Pete nakumbuka nilinunua jumla laki tatu na nusu 

Sikupoteza muda nilienda kwa sonara nikampatia vile vitu akapima akaniambia atanipa laki moja kwakuwa sikuwa na pesa nikakubali tu nikachukua pesa na kuondoka kuelekea kwa mama ntilie nikanunua ugali dagaa nikala nikashiba 

Angalau nilipata nguvu hata minyoo waliokuwa wakigombana tumboni walitulia nikatoka pale nikawa narudi nyumbani kichwani nilishazipigia zile pesa hesabu ya kununua vyakula niweke ndani

Nilitembea mwendo kidogo tu wakatokea vijana Kama watano hivi wakanizunguka niliwaangalia niliweza kuwajua nilishawahi kuwapiga Sana Tena bila kosa

Tukutane SEHEMU YA 6
 

Post a Comment

Previous Post Next Post