MREMBO KUTOKA JALALANI 6----+10


SEHEMU YA 6

Nilitembea mwendo kidogo tu wakatokea vijana Kama watano hivi wakanizunguka niliwaangalia niliweza kuwajua nilishawahi kuwapiga Sana Tena bila kosa

" Tulikuwa tunakutafuta Sana wewe si ulikuwa ulijidai dangote una pesa Leo ziko wapi ulitupiga Kama watoto wako vile kwa jeuri ya pesa Leo tunakumaliza"

Walianza kunipiga wakinipeleka Kama mpira vile akinipiga huyu anampasia mwenzake nikapiga kelele kuomba msaada watu walifika baada ya kuona ni Mimi nao walinichangia wakisema nipigwe tu Mana niliwasumbua Sana Tena ikiwezekana niuawe kabisa 

Nilipigwa kipigo Cha mbwa mwizi huku wakinisachi a alichukua pesa na simu nguo pia walivua na kunibakishia bukta tu hata kuongea nilishindwa mpaka nikajikojolea palepale nikazimia niliamka mida ya saa nane au tisausiku naona watu walikimbia wakidhani wameniua

Nilijikokota na kuinua nikawa natembea Kama teja wa madawa ya kulevya mwenye arosto Kali

Kwakuwa ghetoni kwa Peter hapakuwa mbali na pale ikabidi niende angalau naweza pata msaada kweli nilifika na kugonga mlango Mara tatu ndipo mlango ulifunguliwa alitoka Peter alishtuka kuniona Mana hakunitambua uso wote uliumuka Kama mkate

Akaniuliza wewe Nani nikamwambia Mimi Harrison akashtuka akaingia ndani na kutoka na tochi na kunimulika usoni akasema hawezi kunipokea kwasababu ni msala nikamwambia msala wa nini akasema 
" Harrison wewe sikuhizi huna pesa na umeona huna kazi unayoijua ukaamua kuingia kwenye wizi ndomana umezibuliwa Sasa nikikukaribisha kwangu watasema nimemficha mwizi Mimi sitaki kubeba kesi yako wewe jitahidi ufike kwako"
" Peter wewe ndo wakunifanyia hivi kweli! nisaidie nilale tu"
" Hapana kwa hali uliyonayo ni kesi unanitafutia tu balaa ukinifia hapa unataka nifungwe?"
" Peter wewe ni Nani wakubashiri kifo changu kuumia ndo kufa?"
" Bwana kistaki kujua hilo ondoka hapa nisije kukuitia mwizi bure ukamaliziwa"

Peter alikuwa hatanii alinisukuma na kuingia ndani na kufunga mlango sikuwa na namna yeyote nilitoka kwa kujikongoja hivyohivyo sikufika mbali mvua ilianza kunyesha na vile sikuvaa hata shati sio baridi hiyo niliyosikia ilikuwa hatari

Nikajitahidi mpaka nikafika nyumbani nilifungua geti na kuingia ndani nilipofika mlango wa kuingia kwenye kile chumba nilichukua nalala nikavua bukta na kuingia ndani Mana ilikuwa imeloa

Sikuhangaika hata kuvaa nguo nilivuta shuka na kulala japo kwa tabu Sana Mana kila mahali palikuwa panauma nilijilaza kitandani Mana usingizi nautolea wapi

Nilikaa macho nikisikilizia mvua inavyonyesha mpaka kukata kufika mida ya saa kumi na moja ndo usingizi ulinipitia nilikuja kuamka saa saba mchana njaa inauma mwili usiseme pesa zimechukuliwa Yani tabu tupu!

Niliamka na kuchukua bukta nikavaa na singlendi nikatoka nikaenda kukaa chini ya mti uliokuwa pale ndani nikiwa pale geti liligongwa kwakuwa sikulifunga na komeo nilimwambia aingie tu 

Alikuwa ni mjumbe wa nyumba kumi alinifata nilipokaa
" Harrison"
" Naam mzee shkamoo?"
" Eeh" alishtuka hakutegemea Salam kutoka kwangu Mana ilikuwa ni ngumu Mimi kumsalimia mtu nikamwambia nimekusalimia mzee akaniambia marahaba Basi nae akaja kukaa pembeni yangu

" Harrison Nimekuja hapa kukuuliza Jambo?"
" Jambo gani?"
" Nikuhusu mwanamke mmoja mwenye matatizo ya akili"

Nilishtuka nikajua kumbe habari ya yule mwanamke kichaa kufia ndani ya nyumba yangu imejulikana nikajiandaa Sasa akili iliwaza huenda amekuja na polisi 
" Mwanamke?" Nilimuuliza nikijifanya sijui
" Ndio mwanamke aliyekuwa akiishi kwako" mmh hapo nilitulia kumbe amefahamu Sasa nimjibu nini nikiwa nawaza akasema
" Ile siku ya kuunguliwa kwa nyumba yako nilikuwa hapo kwangu nikiwa nakata matawi ya mti yaliyokuwa yamezidi huku kwako Sasa nikiwa juu ya ukuta wako nikamuona Asia akiwa anahangaika na moshi ukitokea ndani kwa inavyoonekana yule kichaa aliwasha Moto na kwa bahati mbaya alikuwa kajifungia kwa ndani alikuwa akipiga kelele tu kwahiyo Asia alipambana kufungua mlango akashindwa ndipo alitoka kuita watu wengine ili apate msaada lakini watu walikataa nikaona asije kufia ndani ndo nikaenda kuwaita watoto wangu tukaja kuvunja ukuta na chumba Cha stoo Kisha tukaingia na kumtoa" 

Ilikuwa ni habari njema kumbe hata hakufa nilifurahi mjumbe aliendelea

" Nilisita kukuambia nikikumbuka matukio yako ya kunifukuza na kunitukana Basi nilikaaa na yule mwanamke mpaka akapona majeraha na vidonda Sasa kutokana na fujo zake nikawa namfunga kamba lakini Jana nikamwacha huru akatoweka kabisa na nguo alizo vaa tulizikuta tulimtafuta hatukumuona sasa leo nikiwa nyumbani niliitwa hapo mtaa wa chini Kuna mwanamke amegongwa na gari ameumia uso wote Sasa nilitaka twende ukamuone Kama utamtambua"

Daah nilivaa suruali na t-shirt tukatoka japo nilikuwa naumwa lakini nilijikaza njia yote nilikuwa naomba asiwe yeye

Kweli tulifika eneo la tukio watu walikuwa wengi nilimsogelea yule mwanamke pale chini alikuwa hajitambui kabisa na alikuwa amevaa gauni la kupauka kiukweli sikuweza kumtambua 

Basi ikabidi wamchukue na kwenda nae hospitali mjumbe alinitaka nibaki pale mpaka hapo taratibu zote zitakapo fanyika ilikuweza kumtambua 

Nilikaa pale hospitali kwa saa nzima ndipo mjumbe alirudi akiwa na watu kadhaa walionekana kuwa familia moja
Walinifata mpaka kwenye benchi nilipokaa
" Harrison nashukuru Ila nimefanikiwa kuwapata wanafamilia wa mgonjwa wewe unaweza kwenda tu" aliniambia mjumbe

Nikasema atakuwa sio yule kichaa Mana sikuwahi kuona hata mtu akimtafuta nikasema sawa acha niende zangu 

Nikatoka pale nikatembea mpaka barabarani nikiwa Sina hili na lile Kuna gari ilipaki pembeni yangu nikaitwa "Harrison" nikageuka alikuwa ni Agnes mwanamke Wangu mwingine
" Naona umekuwa Mr.nice" alinikejeli wakigongeshana mikono na mashoga zake wakicheka aliondoa gari kwa Kasi na kufanya maji machafu yanimwagikie kweli niliamini msemo usemao pata pesa tujue tabia yako

Sikuchukia hata nikaona kama wanafanya ujinga ambao niliufanya Mimi na kubaki na majuto nikajisemea acha wafanye Ila wajue Kuna kesho ambayo watajutia hii Leo

Niliendelea na mwendo nilikuwa nimechoka Mana hata naili ya daladala sikuwa nayo nilitafuta kivuli nikakaa zangu tumbo lilianza kupiga kelele minyoo walikuwa wakishindania mabaki ya chakula Cha Jana yake usiku

Unajua tena Kama huna hela na njaa nayo inazidi spidi ya 5G nikaegemea mti nikafumba macho sura ya yule mwanamke kichaa ilinijia akiwa na tabasamu Pana usoni nikafumbua macho

Nilichokiona nikajua bado nimefumba macho nikafikicha macho yangu Tena na kuangalia vizuri daah alikuwa ni yule kichaa aisee alikuwa amechafuka na tope alivaa kigauni tu kifupi sijui alikitoa wapi mkononi alikuwa amebeba mfuko ulionekana ndani kunavitu aliweka

Sikujali na uchafu wake nilimkumbatia palepale watu waliopita walinicheka Kuna aliyesema
" Kweli ukiwa na pesa alafu zikakukimbia unakuwa chizi ona amekutana na kichaa mwenzie" aliwambia wenzake Basi wakacheka Sana Wala sikujali maneno yao

Nilimkalisha chini kando yangu
" Ulienda wapi sasa jamani" nilimuuliza
" Robby" alijibu
" Ulienda kwa Robby?"
" Alitikisa kichwa kukubali"
" Umemuona?"
" Ameenda na sabrah"
" Sabrah?"
" Ndio na hataki nilale kwake hataki tule ananipiga Sana hataki tucheze"

Aliongea alichoona ni sawa kwake kwajinsi tulivyokuwa tukiongea utadhani naongea na timamu mwenzangu na kwa harakaharaka unaweza kusema ma chizi wawili wanaongea
" Basi twenzetu kwetu Kama hataki ulale kwake sawaee?"
" Nitamkuta Robby?"
" Eeh yupo nitamwambia mcheze wote sawa?"

Alikubali tukasimama ili tuondoke lakini nikaona Bora atupe ule mfuko lakini aligoma katakata nikasema isiwe kesi asije akachukia na kuondoka zake

Tuliondoka Yani kila nilipopita watu waliambizana eti muone kafulia hana hela ya kununua wanawake ameamua amdanganye kichaa akamtumie mimi sikuwasemesha lolote tulienda mpaka nyumbani nilifungua geti tukaingia nikafunga zangu geti

Nilimbembekeza atue mzigo wake nikimuahidi nitamleta Robby akakubali kwa namna alivyokuwa isingewezekana aingie ndani nilijikaza nikaenda nae bombani 

Bomba lilikuwa karibu na nyumba kubwa nikaona niingie nae kule ndani nilitafuta mpira na kuuchomeka bombani Kisha nikauvuta mpaka ndani 

Kwakuwa tulikuwa wawili tu nikaamua tu nimuogeshe nilitafuta sabuni ya unga nikapata nikamvua nguo zake na kuanza kumuogesha kwa jinsi alivyokuwa na umbo zuri sura pia daah ilikuwa ni ngumu kwa mwanaume rijali kuvumilia

Nilimsugua miguu Mana alikuwa akitembea peku na kichwani pia kulikuwa Kama alitwishwa chungu Cha masinzi Mana kilikuwa kichafu balaa ukicheki alikuwa na nywele ndefu hatari nilimaliza zoezi la kumuogesha japo kwa kukaza roho nikatoka na kwenda nje kuangalia Kama kutakuwa na mtu sikuona

Nikarudi na kumchukua tukaingia kwenye chumba nilichokuwa nalala( kibanda Cha mlinzi) nikatafuta pensi yangu ambayo nilikuwa siivai baada ya kukonda kutokana na hali ya maisha yangu

Nikamvalisha pensi na t-shirt langu alipendeza Sana nilikagua kucha zake zilikuwa ndefu kwakuwa sikuwa na hata wembe nilimkata kwa meno

Baada ya kumvalisha tulitoka na kwenda kukaa chini ya mti nikamuona yule kichaa akinyanyuka na kwenda kuchukua mfuko wake

Alirudi na kukaa karibu yangu alifungua mfuko wake na kutoa kitu kimoja kimoja alitoa Rasta ambazo zilikuwa zimeshatumia alitoa matakataka kibao Mwishowe alitoa mkate na kunipatia

MREMBO KUTOKA JALALANI

SEHEMU YA 7
Alirudi na kukaa karibu yangu alifungua mfuko wake na kutoa kitu kimoja kimoja alitoa Rasta ambazo zilikuwa zimeshatumika alitoa matakataka kibao mwishowe alitoa mkate na kunipatia

ENDELEA
Kusema ule ukweli njaa ilinibana sikuweza kukataa niliuchukua mkate nakuukatatnt katikati nikachukua nusu na yeye nikampa nusu tulikula

Tulikunywa maji matumbo yalijaa Sasa shida ni huyu mwenzangu alitaka tucheze michezo ambayo alitaka yeye Mara alileta matope nilipokataa kucheza alinipaka usoni Kuna muda nilijipumzisha lakini alinimwagia maji aliyokuwa ameyafumbata mdomoni Yani basi tu ilikuwa kero wakati mwingine nilipo kataa kucheza nae alinuna na kucheza pekeyake

Ugumu nilikuwa napata kwenye kulala yeye alilala kitandani Mimi nililala chini lakini ikitokea nikaamka usiku nakuta amelala kihasarahasara tu yani kwajinsi alivyokuwa Kama ingekuwa kipindi ambacho niliweka mbele wanawake na starehe basi nisingeweza kujizuia 

Kuna wakati akili ilinijia nimwingilie tu Mana lakini nikasema hapana sio sawa hata Kama ni kichaa lakini ni mtu kama Mimi basi nikavunga tu kigumu

Kingine ambacho kilinipa ugumu ni pale anapoingia mwezini ilibidi nichane shati langu na kumstiri nikawa namchunga asiende mahali asije watu wengine wakamuona kwenye hali yake Mana hata akili ya kujitunza hakuwa nayo kwa Wakati ule

Nilishazoea vituko na vitimbi vyake Kuna muda nilitoka nae nakutembea mtaani watu walinishangaa Sana 

Japo maisha yangu yalikuwa magumu Sana ilifikia hautua ya kulala njaa bila kupata chochote lakini nilijifariji kwakuwa nipo na mtu japo hakuwa na utimamu kama Mimi Ila michezo yake ilinifanya nisahau shida

Kuna wakati nilicheza nae kwenye maji tope ilimradi tu nimfurahishe nami niondoe mawazo 

Siku moja nilikosa kabisa chakula lakini sikujitazama Mimi nilimtazama yule kichaa lakini hata hakujali alijichezea zake tu asijue yanayoendelea duniani

Usiku tulilala kama kawaida Sasa tukiwa tumelala Asia alikuja na kugonga mlango nilitoka na kumkuta amesimama pembeni ya mlango 
 "Harrison vipi?"
" Poa kuna usalama kweli mbona usiku Sana?"
" Usalama upo Ila sio usiku Sana itakuwa umewahi tu kulala Mana sahizi saa nne mi ndo natoka zangu kazini"
" Kumbe!"
" Ndio"
" Vipi mmekula nini usiku huu"
" Kiukweli Asia leo sikuwa na kitu kabisa"
" Nimekuja na chakula kutoka kazini Kama vipi tule wote"
" Poa " Basi nilimkaribisha ndani

Aliweka chakula ili tule nikaona nimwamshe na mwenzangu tule lakini Asia alinizuia akiniambia nimwache kwanza sisi tule ndipo nimwamshe akihofia fujo

Basi tulikula baadae nae nikamwamsha akala nikawa napiga stori na Asia yeye akiwa anacheza na mashuka Asia alitazama saa yake ilikuwa ni saa Saba
"Hari unajitahidi Sana yani angekuwa ni mwanaume mwingine asingeweza kufanya haya yote"
" Nikweli Asia japo ni changamoto Sana kwangu"
" Hongera kwa kweli unathibitisha kwa jinsi gani umebadilika"
" Mtu hujifunza kupitia changamoto Mimi nimejifunza mengi kwa kipindi ambacho maisha yangu yameyumba nimejifunza kuishi na kuheshimu mtu kwa kutokujali hali yake na kitu ambacho sikujifunza kabla nilijiona naweza mudu kila kitu kumbe si kweli nimeamua niishi tu na huyu angalau hata nilipe kwa Yale niliyoyatenda kwa watu binafsi naami yote yaliyotokea kwangu yanasababu ona zaidi yako hakuna aliye upande wangu ni huyu ndiye ananifariji"

" Anakufariji inamaana una...una..?" Alibabaika nilielewa anamaanisha nini alitaka kuuliza kitu
" Sio hivyo Asia naishi nae kawaida na hakuna chochote "
" Sawa nimeelewa"
" Asia muda umeenda sana vipi nikusindikize?"
" Hapana Kuna rafiki yangu nilimpa ufunguo Sasa ameniambia amepata dharura Sasa siwezi kwenda kulala nyumbani"
" Kwahiyo?"
" Kama hutojali naomba nilale tu hapa"
 " Hamna shida lala nae hapo kitandani Mimi nalala hapa chini"
"Atalala sahizi kweli"
" Ngoja nimbembeleze"

Niliinuka na kukaa kitandani nilimvutia yule kichaa karibu yangu na kumlaza mabajani kwangu nikimbembeleza kwa kuchezea nywele zake hatimaye alilala nikashuka zangu chini
" Harrison kweli u namuwezea ningekuwa peke yangu ningekesha mbona"
" Nishazoea hanipi tabu Sana poa bahna usiku mwema"
" Nawe pia"

Nilivuta shuka na kujifunika haikupita muda nililala nilikuja kushtuka baada ya kuhisi mkono wa mtu ukipita kutoka mgongoni mpaka kifuani niliamka kumbe alikuwa Asia 

" Asia unafanya nini?"
" Nisamehe tu jamani Harrison nimeshindwa kuvumilia mwenzio nakupenda"
" Hee wewe Asia hebu niache Sina hisia na wewe tafadhali nakuomba niache nakuheshimu Kama dada tu"
" Yani kweli hari Mimi najua kwa Sasa huna mwanamke nifanye Mimi kuwa wako jamani"
" Hapana Asia hebu acha basi" nilimtoa mkono kifuani kwangu

" Harrison nimekuwa nawewe kipindi chote kweli umeshindwa kunifikiria unajua ni jinsi gani nilivyokuwa naumia unapokuja na wanawake zako?"
" Asia maisha yanabadilika Harrison huyu sio yule"
" Hapana nakijua wewe ukipata pesa utakuwa tofauti nipo tayari kuvumilia hata ikitokea unamwnamke mwingine"
" Asia nielewe basi kwasasa sifikirii masuala ya mahusiano nawaza nipambane na maisha yangu tu nijue nawezaje kuishi"
" Najua hilo basi nisaidie kwa leo"
" Hapana" Asia alikomaa alianza kunipapasa ukicheki nilikuwa na wakati mgumu nilivumilia nilishindwa
" Basi Leo tu sitaki unisumbue"

Asia alikubali lakini zile hisia nilizokuwa nazo kwa Wakati ambao Asia alinichombeza zilipotea nilipokumbuka tu yule kichaa yumo ndani nilisita
" Vipi Hari" aliniuliza Asia baada ya kuniona sionyeshi ushirikiano
" Asia sio sawa"
" Kwanini?"
" Huoni tupo wangapi humu ndani?"
" Kwahiyo unataka kuniambia unamuogopa huyo kichaa?"
" Sio Kama namuogopa Ila sio haki kabisa"
" Jamani Hari bahna acha utani kuanzia lini ukamjali mtu hivyo akati ulikuwa unafanya yako hata marafiki zako wakiwepo?"
" Asia hapo unaongelea nyakati huu ni wakati mwingine kabisa"
" Kwahiyo nilale zangu"
" We Rudi kitandani ulale"
" Yani hata siamini"
" Itabidi uamini tu Asia"
" Mh sawa" aliitikia

Nilivuta shuka nikijua ameridhia niligeukia upande wa mlangoni na kulala kabla usingizi haujanipitia Asia aliingia ndani ya shuka ile nageuka alipanda juu yangu Tena alikuwa mtupu
" Asia .. Asia.." nilimsukuma huko
" Yani Harrison unamthamini huyu chizi kuliko Mimi?"
" Asia unakosea sana sio wewe uliyenifundisha kuishi na watu sawa? nilipotaka nimwache hospitali ulisemaje nimsaidie Sasa Kama nimeamua kumsaidia iweje nisiheshimu utu wake?"

" Hata Kama hari kwahiyo unataka kuniambia huyu atakutimizia haja zako?"
" Kama nitamuhitaji" nilimjibu
" Unakosea sana hari utajutia kwa hiki"
" Kwa kipi Asia unahisi nimefanya kosa kwa kukataa unachokitaka?"
" Nikosa kubwa sana haiwezekani nakuambia nakupenda wewe unanichukulia poa tu alafu mademu zako uliokuwa unawasaidia leo hawaonekani kwahiyo msaada wangu huuoni ama?"

" Ukisema hivyo unakosea Mana nakumbuka mlinambia Kama namsaidia mtu nimsaidie bila kutaa mrejesho kwake Sasa iweje wewe unanisaidia lakini unahitaji mrejesho kutoka kwangu Mana Kama ulinisaidia kipindi kile nilikuwa nakulipa pesa zako Tena nyingi kuliko kazi yako Sasa Kama msaada wako ulikuwa unahitaji malipo utanisamehe nikipata pesa nitakupa kadri ya ulivyonisaidia"
" Eti utanilipa unadhani unaweza kupata pesa uliyoichezea kwa kazi gani?"
" Asia toka nje!"
" Sitoki" nilisimama na kumbeba nilikusanya na nguo pamoja na vyombo vyake nikamtoa nje ya geti na kufunga

Nilirudi ndani nikiwaza haya majaribu yataisha lini ukweli ni kwamba hata Mimi nimwanadamu Tena mwanaume rijali kabisa daa ulikuwa ni mtihani kwelikweli

Akili ikanituma bila kutafuta kazi hapa naweza nikaingia kwenye Mambo sio kabisa mtu ataona Sina kitu atataka anitumie anavyotaka Mana hawatasema lengo wataanza na misaada midogomidogo mwishowe nao watahitaji msaada kutoka kwangu.usiku ulipita niliamka nilikuta taayari mwenzangu ameshaamka
" Robby" aliniita
" Unasemaje?"
Alinyoosha mkono nikajua njaa itakuwa inamuua nilisimama na kumshika mkono tukaenda kunaa uso kisha tukatoka

Niliwaza niende kwa rafiki yangu mmoja ambae alikuwa na gereji yake Mana kabla wazazi hawajafa nilikuwa nimejifunza masuala ya gereji hivyo nikawaza nikamuombe angalau nifanye kazi pale kwa muda

Nilifika na mtu wangu nimemshikilia mkono Mana akiona watu alitaka kuwakimbiza au kuwalenga mawe
" Harrison "alikuwa rafiki yangu kefa
" kefa" tulikumbatiana
" Za siku nyingi asee"
" Safi tu"
" Unajua niliwaza nije kwako" aliniambia
" Kwangu?"
" Ndio ujue sikuwepo kabisa tangu Mara ya mwisho tulipokutana pale bilcanas nilipata Safari nikaenda Mombasa Yani hapa Sina hata wiki"
" Kumbe?"
" Ndio, Ila nimeskia kilichokukuta jamaa yangu aisee pole Sana?"
" Nimeshapoa Yani"
" Kwahiyo unaishije hapa mjini"
"Niponipo tu Sina mishe"
" Kwani haswa kilitokea nini( akivuta kiti na kunipa nikae)

Nilimkalisha mtu wangu Mimi nikakaa chini
" Vipi Harrison huyu chizi vipi uko nae au?" Aliuliza baada ya kumuona Mambo aliyokuwa anafanya Mara achukue makopo
" Niko nae"

Nilianza kumuhadithia kilakitu mpaka kuhusu yule kichaa na mpaka ishu ya benki
" Duuh nikuambie kitu Hari?
" Niambie"
" Hapa mjini Kuna watu wengi Sana lakini hebu fikiria huyu hakwenda kwa watu wengine alikuja kwako huwezi jua mungu amekuletea huyu mtu kwa sababu gani"
" Ndo hivyo kefa nimechukua juku la kukaa nae"
" Mmh inakuwaje Sasa hapa"
" Kuhusu nini?"
" Naona chombo imetulia hapo ni kichaa unamzingatia vipi angekuwa anajisimamia mwenyewe si tungeuana hapa mtaani lakini hujapita kweli?"
" Hapana bahna kefa hayo mi nishaachaga"
" Hahaha nakuaminia nikajua umeshakichafua hapo?"
" Hakuna kawaida tu mbona nimetulia"

" Poa bwana ila nilichotaka kuja kwako nina shida aisee"
" shidaa?, jamaa unazingua Sasa shida gani naweza nikakutatulia?"
" Unaweza Kama utataka"

MREMBO KUTOKA JALALANI

NA ADELINA ADOLAT
SEHEMU YA 8
"Poa bwana ila nilichotaka kuja kwako nina shida aisee"
"Shidaa?,jamaa unazingua sasa shida gani naweza nikakutatulia"
"Unaweza ukitaka"

SONGA NAYO
"Sawa niambie labda naweza nikakutatulia"
"Acha nikuambie Mimi shida yangu ni gari yako"
" Gari yangu?"
"Ndio naomba uniuzie gari yako"

Nikawazaa nikajisemea hata Kama nisipoiuza inafaida gani siweki mafuta ipo tu Kama pambo na ukiangalia pesa sina nikaona acha niiuze hata Kama sina uzoefu wa biashara naweza nikatatulia baadhi ya Mambo yangu huenda nikapata akili ya kufanya Jambo kubwa Mana nilipiga hesabu gari bado mpya Yani tangu ninunue sikulitumia hata miezi sita na nilinunua milioni thelathini nikasema hata nikimuuzia milioni ishirini kwa bei ya hasara si mbaya Mana kwa hapa nilipo Sina hata pakushika

Sawa kefa nimekubali nilimwambia akasema hapo sawa Basi nikamwambia gari yangu tangu ninunue sikuitumia hata Miezi sita na nikamtajia pesa niliyonunulia akasema atanipa milioni nane kwa msaada

" Kefa jamaa yangu kweli gari jipya hivyo mbona unataka kuniumiza"

" Sio Kama nakuumiza kwanza gari yenyewe imekaa muda bila kutumika unafikiri bado itakuwa ni nzima Mana hapo Kuna vitu nitabafilisha na kutengeneza"

" Gari bado mpya Sana ile jamani au kwa vile unajua Sina kitu ndugu yangu ndo uniue hivyo?"

" Sikuui we ni jamaa yangu hiyo gari ikiendelea kukaa tu ndo itakufa kabisa utakosa mtu wa kumuuzia Bora uokoe hilo mapema"

" Kefa mbona unaongea Kama vile unanivunja moyo unamaanisha kwa muda wote huo nitakuwa sijapata pa kushika kweli?"

" Hari kwa nijuavyo Mimi mtu akipoteza pesa kuzipata Tena ni ngumu we jamaa umepoteza pesa nyingi Sana kwahiyo hapo ulipo unamatumaini ya kuzipata Tena? Unachekesha kweli Nani aliekuambia ukitumia pesa hovyo zitarudi hilo sahau wewe chukua hiyo milioni nane kafanye Mambo mengine ujitafutie maisha kama ukiweza kutunza pesa"

" Kwahiyo kefa unataka kutumia hali yangu kwa kuninyonya hivyo ndugu yangu maisha hayataki hivyo ukumbuke nilikuwa na pesa Kama wewe sawa Mimi nimezichezea mwenyewe lakini sio kila mtu anapoteza pesa kwa kuzichezea tu Kuna vitu vingi vinaweza kukufanya ukaanguka kefa usitumie udhaifu wangu kwakuwa umeona Sina kitu ?"

" Kwahiyo unazitaka hizo pesa au unataka kubaki na gari yako Kama pambo Mimi Kama nakusaidia tu Sina shida na gari used ( iliyotumika) Kama yako ninauwezo wa kununua mpya tu"

Nikasema hata Kama ni msaada sio huu ni unyonyaji kwa jinsi gari yangu ilivyokuwa mpya hata haikuchubuka mahali Mana nilikuwa nikiitunza Kama nini eti milioni nane kweli lakini sikuwa na namna Mana hata hiyo milioni nane sikuwa nayo hata ningekanyaga nyanya za watu sikuwa hata na Cha kulipa

" Sawa bwana nimekubali" 
Nilimwambia lakini moyoni sikuwa nimeridhia kabisa 
" Sasa fanya hivi wewe tangulia Mimi nakuja na fundi wangu tuje tuiangalie kwanza alafu tufanye makabidhiano ya pesa"
" Sawa acha nikuache utanikuta"
" Poa"

Niliinuka ili nimchukue mtu wangu( yule kichaa) Mana alikuwa akichezea chezea matope alipokuwa amekaa nilisogea karibu yake sikuamini nilichokiona nilimkuta ameshika kijiti akiwa anaandika andika lakini nilipoyaangalia maandashi yalielekeweka na kusomeka yalikuwa ni majina yalisomeka hivi juu aliandika"Babo"
Upande wa chini mkono wa kulia aliandika" sabrah" na mkono wa kushoto aliandika"Robby" ni majina matatu Tena aliyaandika akiwa ametengenenza kitu Kama duara hivi

Nikajiuliza kumbe huyu alikuwa na akili timamu Sasa nini kilimkuta mpaka akawa hivi nikamuuliza
" Robby ni Nani?"akanijibu ni shetani
"Na sabrah?" Akasema ni ibilisi
" Na Babo" akanijibu mnyonge

Nikashangaa Sana kwa jinsi alivyo nijibu nikahisi huenda akili zake zimerudi nikamuinua 
" Wewe ndo Babo?" Nilimuuliza badala yake alinicheka na kunipaka matope aliyokuwa nayo mikononi baadae akaanza kulia
" Basi basi usilie twende zetu nyumbani sawa" nilimbembeleza akanyamaza tukaenda mpaka nyumbani tuliingia ndani

Akilini niliyakumbuka Yale majina ambayo aliyaandika yule Dada 
Lazima kutakuwa na kitu hapa haya majina matatu Yana maana kwa huyu kichaa au Babo ndo jina lake huyu nilijisemea mwenyewe tu Mara niliskia honi ya gari nje ya geti nikaenda kufungua alikuwa ni kefa nilifungua geti wakaingia 

Basi nikawapeleka kuliona gari walikagua gari ilikuwa Safi haikuwa na tatizo lolote baada ya hapo kefa akanipa pesa zangu namimi nikahakikisha zilikuwa zimetimia nikampa ufunguo wakaondoka zao

Pesa nilipata nikasema Sasa hapa Cha kwanza ni kununua chakula hayo mengine ni ya kesho sasa nikaweka pesa ndani Kisha nikachukua elfu hamsini nikahakikisha mlango nimefungua tukaondoka kwenda dukani nikafanya mahitaji yote muhimu nikanunua najiko pamoja na mkaa tukarudi 
Kitu Cha kwanza ilikuwa ni kupika nikawasha jiko la mkaa nikaanza kuchambua dagaa 

Muda huo ilishafika saa kumi na mbili jioni Basi nilipomaliza kuchambua dagaa Moto nao ulikuwa umeshakolea nikapika dagaa nikaweka pembeni nikaanza kupika ugali pale nilipoivisha nikapeleka ndani ili tule nikachota maji nikamnawisha mwenzangu tule 

Tukaanza kula mwenzangu kwenye kula hakuwa msumbufu Mana nilikuwa nikimwelekeza jinsi ya kula Kuna muda alijitemea chakula nikawa namsafisha kula tulimaliza nikasema nimuogeshe yeye nami nioge ili tulale wakati nataka niende bombani nikaskia ngo ngo ngo getini 

Ikabidi nirudi getini ile kufika tu yani nilipigwa na kitu kichwani mpaka nikawa naona nyotanyota zikielea elea Kama zinataka kudondoka lakini hazidondoki nikiwa kwenye hali ya mawenge niliwaona watu wakiingia mmoja akabaki pale niliposiamama Yani Kama akili ilihama sikuwa naelewa chochote kwa takribani dakika kadhaa hivi ndo kidogo akili ikawa inarudirudi nikaanza kusikia kelele za Yule Dada kichaa akiwa analia tena ziliskika kwa nje ya geti nikataka nifate lakini niliongezewa kipigo kingine ambacho kilinifanya nianguke Kama mzigo

Nilipata fahamu nikiwa eneo lingine hata sikupafahamu nilikuwa kwenye jengo flani hivi Kama vile ilikuwa sehemu ya kuhifadhia chuma chakavu kilicho nishangaza hapakuwa na mtu hata kulisikika sauti za popo tu wakirukaruka niliinuka kutoka nilipokuwa nimelala 

Niko wapi hapa na niwakinanani walionivamia na wanataka nini kwangu wakati najiuliza nikakumbuka jinsi yule kichaa please pale alivyokuwa akipiga kelele nilikurupuka nikaanza kuita bila majibu yoyote

Nikatoka hadi nje ya lile jengo nikimtafuta nilizunguka Sana kwenye lile jengo lakini sikuona mtu yeyote kwa mbali niliona jengo lingine nilitembea kulifata lile jengo

Nilifikia lile jengo lilikuwa ndo linajengwa nikaona dirisha nikapanda nakuingia sikuita Tena nikawa tu natembea kwa kunyata ili kujihami Mana kwa usiku ule ni ngumu kujua kama Kuna mtu au hakuna 

Nilitokezea koridoni kordo ilikuwa ndefu niliweza kuona mwanzo mwisho lakini hakukuwa na ishara ya kuonyesha Kama kunauwezekano wa kuwa na mtu yeyote kwa ukimya ulivyotawala nilianza kuhisi uoga 

Kwakuwa ilikuwa ni usiku hata sikujua ni saa ngapi nikasema acha nijikalie tu mule kwenye jengo ili kukikucha niweze kujua nipo wapi na nijue namtafutaje yule kichaa

Basi nikanyata hadi kwenye chumba kimoja nikitaka kuingia Cha kushangaa niliskia sauti za kunong'ona
" Mimi nilisema mumzimishe tu Mana huyu ni kichaa nyie mmemuua Mimi sikutaka mumuue lengo langu ilikuwa pesa tu zirudi Sasa nyinyi mmeua"

Sikuweza kuitambua sauti Ila kwa maongezi Yale nilijua Basi yule kichaa atakuwa ameshauawa lakini nikajiuliza kutokana na yule aliyesema shida yake ilikuwa ni pesa tu inamaana alitaka zile pesa na alijuaje ninapesa basi Kama ni pesa si wangechukua tu kwanini wamuue mtu ambae hata hajui nini kinaendelea huku duniani kwani aliwakosea nini nililia kimoyomoyo niliogopa kutoa hata sauti Mara nikaskia mwingine akijibu

" Ni bahati mbaya bosi baada ya kumpiga yule jamaa kichwani na kuzimia nikaingia kuchukua zile pesa wakati natoka huyu chizi akawa ananizuia nakuanza kupiga kelele ndo nikaamua nimchukue na kuondoka nao wote Sasa akawa ananivamia ndipo nikampiga na hiki kigongo Cha kichwa na kuanguka"

" Ni ujinga huo si ungembeba umtupie hata huko njiani Sasa ulikujanae huku wanini?"
" Acha tu nikuambie ukweli Mimi nilimtamani kwa jinsi alivyo nikawaza atanifaa usiku waleo"

"Mwehu kweli wewe unajidai wewe ndo mwanaume peke yako si ndio unajua ni jinsi gani nilivyompania huyu mwanamke?"
" Samahani"

" Samahani kitu gani wewe huyu demu Mimi nilimpangia tangu alipokuja gereji na Hari"

Hapo ndo niligundua kumbe haya yote msimamizi ni kefa amakweli dunia hadaa walimwengu shujaa yani gari achukue kwa bei ya hasara alafu tena na pesa kachukua isitoshe alimmezea mate yule kichaa

Tamaa zimesababisha mpaka wakamuua Dada wa watu moyoni niliumia vibaya mno nikasema ndo imetokea hivyo sasa nitashtaki wapi vituo karibu vyote vya polisi nilishaharibu Nani atakaekubali kusimamia kesi yangu Manahakuna Hata polisi aliyekuwa ananitakia kheri wengi walitamani hata nife kwa matukio niliyowafanyia

nikapata akili acha nijitokeze na huyu kefa atanitambua Kama liwalo na liwe hawezi nifanyia unyama Kama huu achanirudie unyama Mana nimaemua kuwa mpole wanataka wanishike mpaka mkia

Yani nirijirusha ndani sikujali Kuna mawe Wala vijimawe wote walishtuka na kuniangalia 
" Nyie wote tokeni namtaka kefa tu" niliwaambia

ukitaka kulipia nijulishe inbox au WhatsApp namba hii pia ni ya malipo voda ni 0754201697 jina adelina ndimbo 

Jamani hapa niweke sawa Mana kunawatu wanahitaji simulizi ambazo sihusiki nazo
Hizi ndo simulizi zangu
1 MREMBO KUTOKA JALALANI
2 BABA SITOKUSAMEHE WEWE NA MKEO
3 MCHORAJI YASMIN 
AMBAZO NIMEZIWASILISHA KWENU

👇👇👇👇👇👇👇 namba ya WhatsApp
Mnaotuma pesa kutoka mtandao tofauti na voda na tigo chagueni mitandao Kama ni tigo au voda 
Usikose SEHEMU YA 9 

MREMBO KUTOKA JALALANI

SEHEMU YA 9

Yani nilijirusha ndani sikujali Kuna mawe Wala vijimawe wote walishtuka na kuniangalia
" Nyie wote tokeni namtaka kefa tu" niliwaambia

ENDELEA NAYO
Hakuna aliyepinga Mana waliujua Moto wangu wote walikimbia kefa nae alitaka kukimbia nikamkamata nikavuta shati lake likachanika nikalifanya kamba nikamfunga mikono na miguu akawa analia akiniambia nisamehe Hari jamaa yangu ilikuwa ni tamaa tu usinifanye kitu kibaya, nikamwambia we tulia nikamwacha nikamwendea yule kichaa akiwa amelala chali akiwa ametulia tuli

Niliinama nikamwinua na kumuegemeza kifuani kwangu nilishindwa kuvumilia nililia Kama mtoto 

Nilikuzoea Sana nilikupenda kuliko chochote japo haukuwa timamu lakini nilikuridhia kwanini umeniacha peke yangu? Japo kwenye magumu uwepo wako ulinifariji Sasa nabakije mwenyewe Nani atakuwa karibu yangu ni wewe tu ndo ulikuwa upande wangu marafiki zangu wote wamenikimbia ukabaki wewe tulicheza pamoja kwenye tope ilimradi tu nikufurahishe lakini mbona umenitenga

Nimaneno ambayo niliongea nikiwa nalia Sana nilimlaza Tena nikainuka nikasema huyu kichaa ndiye aliyenibadilisha maisha yangu japo amefanya nikose kilakitu lakini naamini Kuna sababu Sasa kwanini umuue Kama ulitaka pesa ungechukua tu na sio kumdhuru mtu asiye jua chochote 

Nilimwambia kefa moyoni nilidhamiria Kama kilakitu nimepoteza aliyekuwa upande wangu Tena nimempoteza nikasema Bora niende jela kuliko kumwacha kefa aishi nilimsogelea na kumwinua kwa kumkamata shingoni kisawasawa
 
" Kefa yaliponikuta Mimi hakuna aliyenisogelea najua urafiki wetu upo kwasababu ya kitu sawa niliridhia yote mliponitenga chaguo langu lilikuwa ni huyu kichaa ambae watu waliniona Mimi nimechanganyikiwa huyu ndiye aliyenifundisha Mimi kuishi na watu wa aina yoyote bila kujali hali yao watu walinicheka Mimi lakini sikuchukia kwasababu Mimi ndiyo chanzo nilichezea Mali zangu mwenyewe lakini sikutaka niwe mzigo kwenu ndomana nikachagua maisha yangu mwenyewe Sasa nimeona hasara yake kukaa kwangu kimya na kukosa kilakitu ndo mnataka mniendeshe mnavyotaka?"

" Hapana Hari nipo chini ya miguu yako nisamehe Kama pesa na gari yako nakurudishia?"

" Hivyo vyote najihesabia nilishapoteza Ila Cha thamani kuliko vyote ni huyu mwanamke mliyesababisha mauti yake unadhani ninachakukusamehe hapa?" Nilimuuliza kwa jazba kwanza nikamtupa chini Kama mzigo
" Aahh?" Aligugumia

 n
Nikamkamata Tena nikamfungua kamba miguuni na mikononi nikasema nataka nikupige Kama mtu sitaki nikupige Kama mzoga kwa kukufunga nakupiga ukiwa unajitetea hata nikifungwa najua ulinitoa jasho 

Nilirusha ngumi ikampata ya mdomo mpaka akatema meno kadhaa na damu zikiwa zinamwagika na kuangukia juu ya yule mwanamke kichaa

Nikamwambia aliyekuruhusu umguse ninani Yani kama nilichanganyikiwa nilimchukua na kumgongeza ukutani
" Utaniua Harrison!"
" Hata hivyo nataka ufe Kama huyu mwanamke hapa chini" nilimwongezea kipigo mpaka akawa anatambaa akaniambia Harrison naomba nisamehe sikujua huyu chizi wa thamani kwako nikamwambia Tena usithubutu kusema ujinga huo 

Nilimsukuma na kuchukua jabali kubwa ilinimpige nalo la kichwa kabla sijashusha mkono nikaskia mtu kapiga chafya niligeuka sikuamini alikuwa yule kichaa kumbe alipoteza tu fahamu nilitupa jiwe na kumkimbilia
" Umeamka!" Nilimkumbatia aisee
" Harrison" kwa Mara ya kwanza aliita jina langu nikahisi labda sijaskia vizuri nikamuuliza umesema
" Harrison!" Aliita tena niliona Kama moyo unataka ukimbie mahali pake kwa furaha nilimbeba sikutaka aongee kingine kuita jina langu ilitosha Sana kwangu

Nilimgeukia kefa ambae alikuwa akihemea juu juu nikamfata nikamwambia unabahati Sana kwakuwa nimzima Sasa nipe funguo ya gari langu kaniambia nichukue kwenye mfuko wa suruali yake Mana kwanilivyomponda hata kuingiza mkono mfukoni ilikuwa kazi akaniambia gari yangu ipo mbele ya lile jengo 

Nilitoa funguo nikambeba na mwenzangu mpaka mahali ambapo gari ilikuweko nikaminya rimoti gari ikajibu nikafungua mlango na kumuweka yule mwanamke nikataka niwashe gari niondoke lakini nikaona acha tu nimchukue na kefa Kama adabu ameipata nilirudi na kumchukua nikamweka kwenye buti Mana alichakaa damu mwili wote

Nikawasha gari nikampeleka mpaka hospitali kila nesi aliyemtazama alitaka kibali kutoka polisi
" Hivi nyie mnataka awafie hapa mpate kesi nimemuokota huko alivamiwa Sasa kwahali aliyonayo Bora polisi au matibabu?"
"Sisi tutakuwa na uhakika gani Kama amevamiwa ndomana tunataka kibali kutoka polisi!"
" Kwahiyo Mimi haniamini sio kwahiyo ningemwacha pale pale afe! Muulizeni yeye nimemuokota wapi" nesi alimsogelea kefa na kumuuliza kwasababu kefa alinielewa shoo yangu akasema nimemuokota mtaroni na waliomvamia hawajui nesi akasema basi sawa walimpokea nikamwambia Mimi naondoka wanasema naondokaje namimi ndo nimemleta mgonjwa

" Naenda kuwaita ndugu zake watakuja" 
" Sawa" tukaondoka zetu kwasababu nilikuwa najua vijana ambao wenye uwezo wa kufanya tukio Kama lile la kunivamia nikaamua niende mpaka magethoni 
Kwao nikawakuta Kama walivyo baada ya kuniona tu kila mtu alitafuta pakupitia wengine waliruka dirishani mmoja nikamdaka

" Sijaja hapa kufanya shoo yoyote Nimekuja kuwaambia mgonjwa wenu yupo hospitali"
" Broo ujue mi nakuogopa isijekuwa ni mtego" nikamwambia acha utoto Mimi siwezi kuhangaika na nyinyi njiwa wadogo mnaotegemea kulishwa nikamuacha nikaondoka na yule dada tukarudi nyumbani

Kitu Cha kwanza baada ya kufika nyumbani tukiwa hata hatujashuka kwenye gari nikamuuliza
" Unaitwa nani?"
" Naitwa Babo"
" Babo?"
" Ndio yani Babra Ila watu walizoea kuniita babo" aliongea vizuri tu yani akili zake zilirudi kuwa kawaida tu akaniuliza
" Kwani hapa ni wapi"
"Unamaanisha mtaa au?"
" Hapana namaanisha wilaya"
" Hapa ni kinondoni" akashtuka
" Inamaana nipo dar?"
" Ndio kwani kwenu wapi?"
" Kwetu ni mbeya chunya"
" Ooh ulifikaje huku na nini kilikukuta" aliinamisha kichwa chini machozi yalianza kumtoka
" Unaonekana Kuna kitu kilikuumiza Sana usijali ukiwa sawa utaniambia" 

Basi tukashuka bale tukaingia kwenye chumba chetu akawa anashangaa mazingira ya chumba 
" Kwahiyo unaishi hapa?"
" Ndio na tumeishi wote hapa kwa miezi Saba Sasa"
" Hee kivipi?"

Nilianza kumpa stori tangu Mara ya kwanza kukutana nae akiwa kichaa mpaka tukio la kuunguliwa na nyumba mpaka pale tilipofikia
" Harrison tumeishi kwa kipindi chote hapa kwenye chumba kimoja Nani aliyekuwa akiniogesha na kunivalisha nguo na vipi nilipoingia mwezini Nani alichukulia uangalifu juu yangu?"
" Ni Mimi"
" Inawezekana je mwanaume kufanya haya yote?"
" Nilifanya kwasababu wewe ndiye uliyebakia upande wangu marafiki zangu wote walinitenga"

Alihisi aibu Sana akaniambia bafu liko wapi nikamuonyesha bafu tulilokuwa tunalitumia alikimbilia bafuni alikaa muda mrefu mpaka nikashikwa na wasiwasi ikabidi nimfate nilifika mlangoni nakumuita
" Babo!" Kimya kilitawala ikabidi niingie nikamkuta amechuchumaa analia

Nikamnyanyua nakutokanae hadi chini ya mti ambapo tulizoea kukaa
" Babo mbona unalia?" Nilimuuliza

" Yani sijawahi kuona mwanaume kama wewe Harrison Yani kwa miezi yote tumeishi Tena ukinifanyia kilakitu na nipo sawa"
" Upo sawa kivipi?" Sikumwelewa anamaanisha nini
" Nipo sawa Hari nashukuru Sana pengine isingekuwa wewe ningeharibiwa usichana wangu"

Hapo nikajua kumbe bado alikuwa mwanamwali nikasema okay Bora hata nilizuia tamaa zangu Mana ningemuharibia usichana wake bure

Akaniuliza Kama nilishaona au kusikia tangazo lolote Kama taarifa ya yeye kutafutwa nikasema sijawahi au pengine kwasababu sikuwa na fatilia taarifa za habari akasema anataka ajue kwanza Kama alitafutwa au la nikamwambia poa tutaenda kwa mzee fulani hivi anapenda Sana kufatilia taarifa za habari huenda Kama matangazo yalirushwa basi tutajua huko

Basi usiku ule akenda kuoga Mimi nikabaki nje hata alipoingia kuvaa nilikaaa nje Mana kipindi ambacho akili zake hazikuwa sawa nilikuwa nikimfanyia Mimi nikaonabsi sawa Kama akili zake zimerudi niwe namwangalia hata hivyo ingekuwa ni rahisi kuingiwa na tamaa tofauti na vile nilikuwa nikimchukulia Kama alivyo

Usiku tulilala vilevile mzungu wa nne mpaka asubuhi nikaamka na kutoka nje na yeye akaja akanawa namimi nikanawa uso akaniambia Harrison inabidi tufanye usafi nyumba nzima hata Kama haina paa kwavile chini pako vizuri tu nikamwambia poa

Tukaanza kufanya usafi mpaka saambili nyumba iko Safi kabisa Mimi nikawasha jiko na kupika chai yeye akawa anaosha vyombo na kufua kwasababu kilakitu nilinunua vyombo kidogo,mchele unga dagaa na mazagazaga baadhi nikapika wali mkavu tukanywa na chai

Babo akaniambia Harrison Basi twende kwa huyo mzee nikamwambia twenzetu basi tuakenda Hadi kwa mzee dunia alikuwa akiitwa hivyo kwasababu hakuna taarifa ambayo ilimpita alikuwa akifahamu vitu vingi Sana 

Tukaenda hadi kwa yule mzee tukamkuta anatengeneza redio yake
" Shkamoo mzee" nilimsalimia
" Marahaba kijana sikuhizi sisikii habari zako mbaya nasikia tu umekuwa kichaa mwenye akili zake"
" Kwanini mzee"
" Nimeambiwa baada ya kupoteza kilakitu ukaamua uchukue chizi ukaenae na wewe umekuwa Kama yeye vile"
" Hapana mzee" nikamwelezea pale akaelewa

" Kumbe ni wewe binti?" Akaniuliza Babo
" Ndio Babu ni Mimi"
" Pole Sana na mshukuru sana Harrison kwaninavyojua hapa mtaani usingeachwa Salama"
" Nikweli Babu namshukurusana"

" Naona mmeamua mnitembelee" aliniuliza
" Ndio babu tunashida"
" Shida gani"
" Najua wewe unafatiliaga Sana taarifa za habari tumekuja kuuliza Kama umeona taarifa yoyote kuhusu kutafutwa kwa huyu Dada"

" Nikweli nafatilia Sana taarifa za habari kila chaneli na kila stasheni redio sijawahi kusikia Ila kwenye tv naonaga tu picha za watu wengine wakitafutwa Ila huyu binti sijaona hata picha tu ya pua yake ikitangazwa"

MREMBO KUTOKA JALALANI

Sehemu ya 10
Nikweli nafatilia Sana taarifa za habari kila chaneli na kila stasheni redio sijawahi kusikia Ila kwenye tv naonaga tu picha za watu wengine wakitafutwa Ila huyu binti sijaona hata picha tu ya pua yake ikitangazwa"

Endelea
Baada ya mzee dunia kutupa maelezo hayo Babra alianza kulia
" Binti unalia nini?" Aliuliza mzee dunia
" Nasikitika Sana wazazi wangu kutonitafuta wameonyesha ni jinsi gani hawanipendi na hawatamani kuniona kabisa"
" Kwani uligombananao?"
" Nistori ndefu babu acha tuondoke" Babo aliniitaka tuondoke Basi nikamuaga mzee dunia tukarudi zetu nyumbani

Nilimwacha alie mapaka achoke ili hasira zake ziishe kweli alilia mapaka akanymaza mwenyewe ndipo nikamuuliza
" Nini kilikupata?"
" Harrison achatu kila mtu anatamani na kuona fahari pale anapoona wazazi wanamsapoti na kumsikiliza Ila ni ajabu pale mzazi anapomtenga mtoto mmoja na kumpenda mwingine eti kwasababu zizizoepukika Kama vile ugonjwa au hali fulani"
" Sijakuelewa babra"
" Ni hivi Mimi nina dada yangu anaitwa sabrah kwenye familia tupo watoto wawili tu baba na mama waoni wafanyakazi binafsi na wenye hadhi ya juu kiuchumi" alisita kidogo

" Endelea Babo"
" Kipindi namaliza kidato Cha nne nilipata ufaulu wa division4 ya 28 kwangu sikupenda Sana Ila sikupenda Ila nilijua kwanini nimefeli kwasababu Kuna wakati nilipatwa na ugonjwa fulani wa kukakamaa Sasa utakuta miezi hata sita siendi chule nilikuwa naenda kipindi cha mitihani. Tu nikasema acha niwaambie wazazi baada ya kuwaambia hakuna aliyefurahi Wala kuchukia waliona ni kawaida tu yani walikuwa Kama wameskia habari za mtu tofauti na Mimi mi nikaona poa kwasababu ni wazazi pengine walitamani nipate division one huenda ingekuwa ni furaha kwao nikawaomba nirudie shule Mana ile hali ya kukakamaa uliisha kabisa wakasema watanipeleka siku zilipita ikafika wakati wa kwenda shule nilipowagusia habari za shule wakaniambia hawezi kutupa pesa zao kwa kunisomesha Bora wanipe kreti za bia niwe bar maid iliniuma sana wakati Mimi wakinikatalia kwenda shule dada yangu ambae ni sabrah akaomba pesa za kwenda kutalii huko Tanga amboni kwenye mapango yeye hakuulizwa alipatiwa Kiasi alichotaka nikachukulia poa kwasababu ni hasira za wazazi"

" Enhee ikawaje?"
" Basi nikawa nipo tu nyumbani nikisaidiana na mdada wa kazi baada ya muda wakamwachisha yule Dada kazi ili Mimi nichukue nafasi yake kwakuwa sikuwa na namna nilifanya Kama wao walivyo taka wakati huo dada yeye alikuwa ni mhasibu ikatokea siku moja kulikuwa na tafrija baba na mama walikutana na wafanyabiashara wenzao namimi nikajiandaa vizuri nikapendeza ikafika wakati wa kila mfanyabiashara akawa anatambulisha familia yake baba alipotakiwa kutambulisha familia yake ilikuwa hivi..........................

Kwa majina naitwa Eric mwaipopo nina mkewangu huyu anaitwa Matilda na nina mtoto mmoja kwa jina la sabrah hebu popote alipo asogee mbele sabrah alitoka mbele na kupunga mkono Kisha akapigiwa makofi nikasema labda amenisahau nikataka niende na Mimi mama akaniita akasema nisiende nisije nikaanguka mbele za watu ikawa aibu kwa akili yangu nilijua mama yupo sahihi kipande fulani lakini baba angenitambulisha tu hata bila kutoka angalau angesema nimepata dharura eti kabisa mtoto mmoja moyoni nikasema sio sawa hata kidogo mbona Kuna walemavu lakini wazazi wao hawawafichi iweje Mimi sikuwa na lakufanya nilitulia tu nilifuta machozi kimyakimya nikiamini huenda ugonjwa wangu ni waajabu 

Babo akaendelea akasema baada ya baba kumtambulisha sabrah pekee alijiskia vibaya Sana nakujiona asiye na haki akawaza kweli tatizo ni.kupata ufaulu huo au Kuna Sababu nyingine bado alikaa kimya hakuongea chochote

Babo akaniambia
" Harrison sikutegemea kabisa ule wakati alitakiwa muhudumu agawe vinywaji baba na mama walinichagua mimi Kama muhudumu kweli niligawa nikamaliza na baada ya shughuli kwisha tulirudi nyumbani wao wakiwa kwenye gari yao Mimi nikapanda daladala mpaka nyumbani siku ikabidi niwaulize nini sababu ya kumtambulisha sabrah pekee wakaniambia Nani anataka aibu eti kabisa wanitambulishe mbele za watu ghafla nikianza kukakamaa si nitawaaibisha alafu wakiuliza Nina Elimu gani ningesemaje Mana kidato Cha nne nilipata four nikawaambia kwani Mimi niliomba huo ugonjwa au nimefeli kwa makusudi basi wakaniambia ndo hivyo hawataki maswali na nitabaki hivyo hatakama nikiulizwa niseme hivyo maisha yakawa yanaendelea sabrah na wazazi wetu wakawa pamoja Sana hata kuwasogelea Kama ikitokea mgeni kaja ni marufuku kukaa nao meza moja 

Sabrah akaanza kusambaza habari mtaani kuwa Mimi ninakifafa nilichukia Sana nikamfata nakumuuliza akanijibu alivyotaka kwakuwa nilikuwa na hasira nikampiga Kofi akaenda kusema kwa baba na mama Basi nilipatiwa adhabu ya kushinda njaa siku mbili 

Siku moja nikiwa zangu mtaani nikakutana na Kaka mmoja sikufahamu kabla akawa amenichangamkia tu akajitambulisha jina lake namimi nikamtajia la kwangu basi siku zikaawa zinaenda nikienda sokoni nakutana nae tunapiga stori za hapa na pale basi anaondoka namimi naondoka zangu Sasa yule Kaka akaniambia ananipenda Sana sikumkubalia moja kwa moja ilatu nikawa Nampa ahadi 

Siku moja akaja karibu na kwetu nikamuona nikiwa juu ghorofan ikabidi nimfate nikamuuliza umefata nini akaniambia amefata jibu langu nikamwambia basi poa nimekubali lakini usiwe unakuja hapa nyumbani akasema sawa basi mahusiano yetu yakaanza hivyo kisiisiri nashukuru hakutaka chochote yoka kwangu tulipendana Sana siku hiyo wakati sabrah mama na baba wakiwa kazini yule Kaka alikuja Tena akaniambia Babra nataka twende ukamuone mama angu basi tukaondoka mpaka kwao kumbe walikuwa ni matajiri wakubwa hata sikujua mamayake alinipokea vizuri tu mtindo ukawa ndo huo nikawa natoroka naenda kwao kumsalimia mama ake Kisha narudi kabla ya wao kurudi kutoka kazini

Mama ake akasema kwavile Mimi sio mwanafunzi inabidi wakatoe taarifa nyumbani sio tabia nzuri kwenda kwake pasipo wazazi kufahamu namimi nikaona sawa Bora watoe taarifa hata nikiolewa niwaondolee mzigo kwao Mana nimekuwa Kama mzigo"

Siku ilifika kunamtu akaja kutoa taarifa nyumbani wazazi wakakubali wanasema wanataka kumuona huyo muoaji basi yule Kaka akaja akiwa amependeza Sana baada ya salamu akajitambulisha na kumtaja mama ake baba na mama walishtuka Sana wakamwambia aje siku nyingine

Baada ya kuondoka yule Kaka waliniita wakaniambia siwezi kuolewa na yule Kaka Sabrah ndiye anafaa kuwa na mwanaume kama yule kwakuwa wote wasomi na familia ya kitajiri Mimi nitawatia aibu nikienda kukakamaa kwa watu moyo wangu ulihuzunika sana basi hata yule Kaka aliporudi Mara ya pili aliambiwa kuwa mimi ninakifafa na kifafa kinarithi Sasa Kama wapo tayari kujaza kifafa kwao wanichukue yule Kaka akasita akasema yeye hataki kifafa kwao na Kama ni huyo sabrah yupo tayari kumuoa basi wazazi walipitisha hilo bila kujali maumivu yangu lakini nikasema Kama Alikuwa ananipenda kweli angenikubali na hali yangu nikaju hakuwa na upendo wa kweli Basi nikawa naugulia moyoni siku zilienda hatimaye ndoa ikapita"

Babra alimaliza hadithi yake nikamuuliza huyo kijana ndo Robby akasema ndio nikasema basi mapenzi ndivyo yanavyokuwa Ila usivunjike moyo nikamuuliza sababu ya yeye kuchanganyikiwa ni nini mpaka akaja dar akaniambia baada ya sabrah na Robby kuoana akatokea mchumba mwingine mzanzibari wazazi wakasema hawataki muislamu kwao nikabaki hivyo ikatokea Tena akaja mtu wa mwanza nilikikutananae nikienda kuomba kazi ya kufanya usafi ofisini kwake kwasababu pale nyumbani walisha mtafuta Dada wa kazi wakasema nianze kujitegemea kwa kilakitu basi yule Kaka wa mwanza nilimkubalia baada ya kumpeleka nyumbani wakakubali 

Siku hiyo alikuja na wazazi wake nyumbani kwetu Sasa wakamuuliza anafanya kazi gani akasema anamiliki migodi ya madini baada ya mazungumzo yule Kaka na wazazi wake wakatajiwa Mahali zilikuwa ni nyingi tu lakini akasema haina shida watalipa na hiyo siku dada na mumewe walikuja kututembelea na Wakati wanaondoka wale wageni yule Kaka akasahau saa moja nzuri Sana alikuwa ameivua muda flani nakuweka mezani nilivyo watoa nje yule Kaka akaniambia nimesahau saa nikamwambia acha nikakuchukulie nikarudi ndani nikamkuta dada ameshika ile saa nikamwambia anipe nimpeleke akasema kwani lazima umpelekee saa imetengenezwa kwa madini tupu hii alafu urudishe acha upuuzi nikamwambia sitaki kuiba Cha mtu kwasababu chake kitakuwa changu na changu kitakuwa chake mama akasema Nani kasema nitaolewa na huyo Kaka wewe Kama hujui wewe unamkosi na ndio maana hatutaki uolewe Mana utatutia hasara Sana kwanza nilikuzaa wakati wa njaa Kama nini na siku uliyozaliwa tu nyumba yetu ilikumbwa na kimbunga kwahiyo unataka huko kwa watu ukalete maafa alafu tuje kulipa sisi? Nikaanza kulia baba akasema Tena wewe kuzaliwa kwako kwetu mkosi na ndio maana hata vidole viwili vya miguu huna! Wakati tunabishana pale ndani Mara yule Kaka akaja kunifata

Sabrah ndiye akawa wakwanza kumdaka akamuuliza umefata saa akasema ndio Sabrah akasema mwenzio Babrah alitaka kuificha ndo baba na mama wakawa wanamgombeza nilishangaa Sana hata walipoulizwa baba na mama pamoja na Robby wote wakisema kweli nikitaka kuificha saa nilijitetea Sana lakini haikusaidia yule Kaka alikataa kunioa Tena akisema hawezi kumuoa mwizi Mana kazi nilizotakiwa kwenda kuzisimamia Kama mke zilikuwa nizaidi ya saa hivyo hawezi oa mwizi waliondoka zao

Nikabaki nalia Sana wakaniambia labda kutoa mkosi nije kuoga maji ya bahari niliamini huenda kweli ninamkosi kwa maneno yao nikatafuta pesa na kuamua kuja huku dar nilipofika ubungo kichwa kilianza kuniuma nikashuka kwenye gari baada ya kufika chini sikujua kilichoendelea na hapo ndo akili yangu ilichanganyikiwa

Babra alinisimulia mkasa uliompata mpaka nikalia nikamwambia 
" Babra wewe si mkosi hata kidogo kwangu wewe ni dhahabu tena ya viwango vya juu"

Tukutane sehemu ya 11


Post a Comment

Previous Post Next Post