SIMULIZI:MAPENZI YA KWELI HAYAFI*TRUE LOVE❤ NEVER DIE* 3 FINAL



Tulipoishia wiki iliyo pita.

  Wiki iliyopita tuliishia mda ule ambapo Mzee Omary Iddy alipo iomba serikali ya kijiji Cha Gombanila kufanya upelelezi wa kina ili kumtambua Muuaji wa vifo vyote viwili.

 Endelea nayo ndugu msomaji
     ""Baada ya Serikali ya kijiji ya kufanya upelelezi wa kina chini ya usimamizi wa Mwanasheria Mzee Omary Iddy,katika kijiji cha Gombanila raia wote walikuwa na hofu sanaa juu ya Juma ambaye mda wote huo alishikiliwa vilivyo na serikali kama mshitakiwa mkuu, huku upelelezi wa kina ukizidi kuendelea dhidi ya kesi hiyo ya vifo vya watu wawili kwa mkupuo.

  """Mda huo upelelezi uliendelea kufanyika baada ya kupita wiki moja Shahidi wa tukio hilo alipatikana ,shahidi huyo alikuwa ni binti aliyetambulika kwa jina la "Neema", Neema alikuwa ni jilani yake na Juma hivyo katika kutoa ushahidi wake alisema kuwa siku moja kabla ya siku ya tukio alimshuhudia Juma akiamka asubuhi na Mapema,Juma alikuwa mkononi amebeba vyungu viwili na Jogoo mkubwa mweupe,mda huo Juma alikuwa akiangaza na kupepesa macho yake katika kila kona ili kujua kama kuna mtu alikuwa akimuona kwakuwa ilikiwa asubuhi mapema sana aliamini majilani zake wote walikuwa bado wamelala mda huo ilikuwa saa Kumi na mbili asubuhi .

Endelea nayo ndugu msomaji
     Baada ya Neema kumuona Juma katika hali hilo alihisi kuna jambo lilikuwa likiendelea kwa kuwa Juma alionekana mtu mwenye mashaka na wasiwasi,Neema aliamua kumfuatilia Juma ili kujua anaenda wapi baada ya kumfuatilia aliona Juma akitokomea msituni,Neema hakukataa tamaa aliendelea kumfuatilia,mda wote huo Juma alikuwa ni mtu mwenye wasiwasi ambapo kila mda alikuwa akigeuka nyuma huku akipepesa macho yake ili kuona kama kuna alikuwa akimuona katika wakati huo.

  """Neema aliendelea kumfuatilia kimya kimya bila Juma kujua kama kuna mtu alikuwa anamfuatilia, Neema mwisho alimuona Juma akiingia kwenye kinyumba cha Mganga wa kienyeji,hakika Neema alishituka sana akijiuliza mwenyewe Duuh!! ''Jaman juma atakuwa amekuja kwa Mganga wa kienyeji asubuhi hii kutafuta nini na kufanya nini''????,yalikuwa ni maswali aliyo kuwa akijiuliza Neema akilini mwake.

     ""Neema aliona asogee karibu ili kumsikiliza Juma na kujua zaidi kitu kilichokuwa kikiendelea kati ya Juma na Mganga huyo alipofuatilia vizuri alisikia Juma akimuomba Mganga ili aweze kumuua na kumumaliza kabisa Hamis,akimuahidi kumpa pesa,Mganga alikubali akisema hiyo ni kazi ndogo kwake,baada ya makubaliano hayo kati ya Mganga na Juma kupita ,Juma akatoa kiasi cha shilingi 40,000/ na kumkabidhi Mganga huyo akimuahidi kuwa endapo kazi yake itamalizika vizuri bila shida yoyote kutokea angemuongezea kiasi kingine.

    """Baada ya Neema kusikia mazungumuzo yote yaliyoendelea kati ya Mganga na Juma alirudi nyumbani kwao huku akijiuliza maswali mengi kichwani mwake"kwa nini Juma anataka kumuua Rafiki yake kipenzi Hamis" alijiuliza sana kuhusu Juma ila alishindwa kupata jibu,Neema aliamua kuachana na mambo hayo kwa kuwa aliona akiendelea kuyafuatilia yangeweza kumchanganya bure kwasababu 'hakujua yameanzia wapi ' na pia hakujua kilichokuwa kikiendelea kati ya Juma na Hamis juu ya Ugomvi wao wa kimapenzi waliokuwa nao.

    """Neema aliitwa Mahakamani ili kutoa ushahidi wake juu ya chanzo cha kifo dhidi ya Hamis na marehemu Zuhura ,vifo vya wapendanao hao katika kijiji hicho cha Gombanila ilikuwa tishio sana hapo kijijini,baada ya ushahidi kutolewa na ikaonekana mshitakiwa Juma hana mshahidi yeyote wa kumtetea Hakimu na Mwanasheria alipitisha "hukumu" juu yake kutokana na kesi yake ya mauaji aliyo yafanya ya kumuua rafiki yake kipenzi kwa njia ya kishirikina ambapo kifo cha Hamis kilipelekea kifo cha Zuhura.

      Hakimu alipitisha ""hukumu ya Kifungo cha Maisha kwa Juma" kutokana na mauaji aliyo yafanya ya kumuua Hamis ikifuatiwa na kifo cha Zuhura ambapo Zuhura aliamua kujiua kutokana na Kifo cha Mpenzi wake Hamis ambaye alikuwa akimpenda sana, Zuhura""aliamini bila Hamis asingeweza kuishi bila yeye kwakuwa alimpenda sana alikuwa radhi kufa pamoja na yeye.

Endelea nayo ndugu msomaji
  """ Juma alifungwa kifungo cha Maisha gerezani na kwakuwa Juma mwenyewe alikili kwa makosa aliyoyafanya alikubali kutumikia kifungo katika maisha yake ya kunyea debe ndani ya Jera,Juma alijutia sana Maamuzi yake aliyo yafanya kwa kumuua rafiki yake kipenzi kisa wivu ya Mapenzi akiamini kuwa '"baada ya kumuua Hamis angeweza kulipokonya Penzi la Mrembo Zuhura" ila ilikuwa tofauti kwake kwakuwa hakujua kama wapenzi wapendanao kwa dhati kamwe hawawezi kutenganishwa kwa kuwa mioyo yao inakuwa imeungana.

  Katika Kijiji cha Gombanila kwa kilicho tokea ilikuwa fundisho na ilibaki ni historia kwa Marafiki hao wawili ambao ni Juma na Hamis ambao walipendana sana, ila wakawa maadui wakubwa sana na wakatenganishwa kisa Mapenzi ambapo Juma alitaka Kulazimisha Mapenzi kwa Zuhura kitu ambacho kilishindikana.

      ""Mwisho Juma alifungwa kifungo cha Maisha na akazeekea jera na mwisho wa siku alifia jera kwa kosa alilolifanya la Mauaji ya Hamis na Zuhura ,wapenzi ambao walipendana sana na ambao """walikuwa wamekwisha wekeani ahadi ya kutotenganishwa na binadamu bali watengenishwe na kifo tu" na ndivyo ilivyo kuja kutokea.

"""". Ndugu msomaj huu ndio mwisho wa hadithi yetu ya ""Mapenzi ya dhati hayafi'" *True Love Never Die*.

Usisite kukomenti na kulike,
Ndugu msomaji endelea kufuatilia hadithi na simulizi kemu kemu zijazo,Yajayo yanafurahisha.

Asanteni kwa ushirikiano wenu. 

Post a Comment

Previous Post Next Post