SIMULIZI:MAPENZI YA KWELI HAYAFI*TRUE LOVE❤ NEVER DIE* 2



Tulipoishia wiki iliyo pita.

Tuliishia pale Juma baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kuweza kumfanyia kitu kibaya rafiki yake huyo ambaye aligeuka kuwa adui yake tena mkubwa sana kisa Mapenzi.
  Endelea nayo ndugu msomaji mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha.

  Juma baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji alimlipa pesa ili mganga kufanya kazi yake ya kumuondoa kijana kutokana na jinsi Juma alivyotaka,ilikuwa siku ya Ijumaa kuamukia jumamosi Hamis aliweza kusikia kitu kikimkaba kwenye koo akiwa amelala kumbe aliyekuwa akimkaba kijana huyo alikuwa ni mganga wa kienyeji ambaye alipewa pesa ili amuondoe Duniani Hamis kisa wivu ya mapenzi aliyokuwa nayo Juma juu ya Zuhura.

      Asubuhi ya Jumamosi jua lilipo chomoza tu Juma aliamkia kwa mganga huyo ili kujua kilicho tokea kwa upande wa adui yake Hamis mganga alimwambia kuwa kazi alisha imaliza toka usiku wa ijumaa,Juma alifurahi sana baada ya kusikia hivyo ,aliamini adui yake aliye mnyanganya mrembo zuhura hayupo tena hivyo aliamini kuwa Mrembo Zuhura atakuwa wake kwanzia siku hiyo.

   ""Nyumbani kwa Kina Hamis walishangaa sana kutomuona Hamis akiamka kwakuwa haikuwa kawaida yake kulala hadi saa nne,haikuwa kawaida kwao kwan ilikuwa kawaida ya Hamis kuamka mapema ya saa kumi na mbili asubuhi kwa ajiri ya kupiga mazoezi na kukimbia kwenda milimani ili kujijenga kiafya zaidi,baada ya kuona Hamis haamkii waliamua kwenda kumngongea mlango, ila yote waliyo yafanya Hamis hakufungua mlango .

    """Ikabidii wavunje mlango na waingie ndani baada tu yakuingia ndani walitahamaki sana baada ya kuuona mwili Wa Hamis ukiwa chini duuh!! Mama Hamis alimkimbilia mwanae pale chini akajaribu kumwita na baada ya kuona kimya alimgeuza ili kumfungua macho na kumungalia vizuri mtoto wake ambaye kwa mda huo alikuwa amekwisha kukauka kumbe usiku wa siku hiyo mganga alimuua kijana huyo.
 Endelea nayo ndugu msomaji

    ""Majirani baada ya kupats taarifa hizo walijikusanya kwa kumdariji Mama Hamis huyo ambaye alikuwa na mtoto mmoja tu,Mazishi ya lifanyika,mda huo Mpenzi wake Hamis hakuwa na taarifa yoyote kuhusu Hamis,Rafiki yake aliyeitwa Furaha alimpekekea taarifa hizo akawa amemwambia kuwa Hamis amepoteza maisha hata kabla hsjamaliza kumuuelezea Zuhura alidondoka chini na kupoteza fahamu.

   ""Furaha aliita watu ili wamkimbize hospitalini ili kuokoa maisha yake,Mrembo huyo asingeweza kuishi bila Hamis kwakuwa alimpenda sana na hakuna mtu ambaye angeweza kuwatenganisha wapendanao hao,walipo fika hospitalini ya hapo kijijini Gombanila,Dokta alijaribu kunusulu maisha ya Zuhura ila alikuwa amesha chelewa Dokta huyo aliwaletea taarifa kuwa Zuhura amesha poteza maisha alisema kuwa Zuhura alipata mshituko wa moyo"Heart attack" ambao ulipelekea kifo chake.

  Wazazi wa Zuhura walipo pata taarifa hizo waliumia sana na familia yote ya wakina Zuhura waliamua kufunga safari ili kuja kijijini Gombanila ambacho kilikuwa kikipatikana mkoa wa Tabora.

  Juma baada kupata taarifa hizo kuwa Zuhura ameweza kufariki kisa Hamis na yeye pia alichanganyikiwa alijilaumu sana kwa maamuzi aliyo yafanya dhidi ya Rafiki yake ambaye walikuwa wakipendana sana.

  ""Familia ya Zuhura walifika kijijini hapo na cha kwanza walitaka kujua chanzo cha kifo cha mtoto wao,Baba Zuhura ambaye aliitwa Ommary Iddy alikuwa ni mwanasheria mkubwa sana jijini Dar es salaam,hivyo baada ya kufika hapo kijijini aliiomba serikali ya kijiji iweze kufanya uchunguzi wa kina juu ya kifo cha watu wawili hao ambapo mwanasheria huyo alitambua kuwa kifo cha Hamis ndicho kilikuwa chanzo cha kifo cha mtoto wake Zuhura.
  
  Ndugu msomaji unadhani baada ya upelelezi kukamilika na ikajulikana kuwa Juma ndio chanzo cha vifo vyote vya watu ambao ilikuwa ni Hamis na Zuhura unafikiri Juma atachukuliwa hatua gani na mwanasheria huyo?

  Usikose sehemu ya Tatu ndugu msomaji hadithi ya kusisimua na kuelimisha. 

Post a Comment

Previous Post Next Post