UNO LA MASIKINI 06 🔞

🆎©️
#Tulipoishia
Nyingine ilikuwa ni ya Mheshimiwa waziri akaifungua "Nasikia umeleta tabia za kuleta wanaume Ndani, sasa dawa yako ipo jikoni haiwezekani mimi nikupe kila kitu halafu ulete wanaume wengine ndani"

#Endelea
Kitendo cha binti kusoma ile message ile alishtuka sana akabaki anawaza, huku Tino akiwa anachambua rasta

'ni nani kampa umbea, au ni Jane au ni nani jamani' binti alianza kupata stress huku akikodolea macho sehemu moja

"njoo keti hapa mi naondoka" alisema Tino na kumtazama binti akiwa katika lindi la mawazo. 

Tino aliinuka taratibu na kumchukua binti akamuweka chini taratibu

"Acha mawazo njoo nkusuke fasta niondoke" alisema mtaalam

Ilibidi binti akaketi pale pale chini Tino akaendelea kumsuka mpaka akamaliza

"Tino hivi unanipenda kweli?" aliuliza

"daah mimi hata sielewi ila kila nikikukumbuka ninajiskia raha nahisi nina kitu ndani"

"Hahha, nashukulu kama nimekuwa furaha kwako, mimi ninaposikia ukinitekenya kwenye nywele nasikia utamu hadi natamani tena naniliu"

"Nini unatamani?" tino alimtania

"Naniiiiliiii" alisema binti na kucheka huku akiufunika mdomo wake kwa aibu. 

"haya bana, mi sisuki tena"

"Kwanini baby"

"nina njaaa" alideka jamaa

"Jamani chapati zipo kula usijali jamani"

Binti aliinuka na kuchukua chapati akaweka mezani na kumnawisha mikono Tino 

"Ule ushibe halafu please kimoko" Tina alisema na kucheka
*****
Baada ya Tino kumsuka vizuri binti aliamua kuondoka

"Jamani si uoge kwanza?"

"Oh bafuni wapi? Kwanza sina taulo" jamaa alikuwa mbishi sana katika suala zima la kuoga

"Njoo nifuate" binti alimuita na kumpeleka bafuni akamuandalia kila kitu. 

Tino alipomaliza kuoga aliaga. Ila Tina aliamua kumsindikiza hadi barabarani. 

"Baby thank you for your company Tino, please naomba usiniambie haunitaki" alisema binti huku uso kaukunja

"Sawa basi tutakuwa wote but kukuhudumia mpaka nikipata kazi ok?" alisema mtaalam

"Haina shida mimi sihitaji huduma nyingine zaidi ya kuwa mpenzi wako, nachohitaji ni mapenzi tu, ntakuheshimu sana

"Basi haina shida,"

Walipokuwa wamesimama kituo cha barabara binti aliingiza mkono kwenye maziwa yake akatoa simu ndogo, aliinunua alipoenda kwenye banda la movie kwani wanauza pia visimu vya batani

"Una namba ya NIDA kweli wewe?" binti aliuliza

"Yes ninayo"

"Parfect" Shika hii simu na hii hela halafu kasajili laini yako halafu unitafute wiki ijayo nafikiri utapata simu nzuri sa hivi hali yangu sio nzuri"

"asante sana, nitakutafuta" Tino alisema na kupokea vile vitu

Mara ilipita Gari fulani pale, wakashusha kioo

"Oya Tino mwanangu vipi huku upo na mtoto mkali nini?" alisema dereva wa gari ile huku akisimamisha gari

"Yaah, mwanangu Tony vipi kaka?" Aliuliza tino

Kumbe yule jamaa alikuwa mshikaji wake kabisa,  
"Poa ngoja niwahi naenda boko hapa mzee" aliasema yule kijana na kifanya kama anaanza kuondoa gari

"Ah man, mzee mi naenda Boko nipe lift mzee" alisema Tino 

"Pamoja wahi sasa"

"Tina, bye nitakutafuta basi" alisema mtaalam

"Pouwaaa byee" binti alisema

Gari hiyo aliyopanda Tino ilianza kutembea kwa speed sana, Tino aliketi siti ya mbele na Dereva pembeni kwenye uskani. 

Katika kupiga story Tino alisikia amekabwa koo kwa nyuma, kumbe kulikuwa na watu wawili kwenye siti za nyuma za gari ile. 

"Tony maa... An" alisema Tino baada ya kubanwa, mara wakamfunika macho na kitambaa cheusi halafu wakampiga style fulani ya kiufundi naye akakata moto. 

Gari ile haikuelekea tena Boko ilikatiza barabara ya Salasala kama vile dereva hana akili nzuri na mtaalamu Tino alipelekwa maeneo ya kifichoni sana

Baadaye mida ya saa tatu usiku Tino alishtuka akiwa amefungwa mikono na miguu akiwa kwenye kiti maalamu ambacho asingeweza kutoka mpaka afunguliwe

"Mwanangu Tony mbona unaniteka tena?" aliuliza Tino 

"Tulia, hii kazi ni ya mtu mkubwa sana mimi nimeambiwa nikulete hapa subiri hakuna mtu wa kukuumiza*

Huku Mbezi Tina alisubiri Tino amtafute sana bila kujua ametekwa na wahuni huko

"Yani mimi huyu hata simuelewi" alisema binti Mara Jane naye akaingia. 

"Shogaa mambo" alisema Jane, Tina akamwangalia vibaya maana anajua kabisa yeye ndo kamuambia muheshimiwa kwamba yupo na Tino "Mbona wanaiangalia vibaya hivyo?" aliuliza Jane

"Hivi Jane kwanini una roho mbaya kiasi hicho" alisema kwa hasira Jane akashtuka huku akivua hereni 

"Nimefanya nini tena Tina?"

"Kilichokutuma ukamwambie Mheshimiwa kwamba mimi niko na mwanaume nini?" aliuliza tena

"Nini? Mi nimuambie muheshimiwa kweli Tina?" alikana

"Kumbe nani? sasa ni nani mwingine anayejua kwamba mimi nilikuwa na Tino kama sio wewe tu"

"Jamani Tina, mimi kweli sijamuambia"

"Ni wewe mwanaharamu, halafu unakaa kwangu huna hata shukrani" aliongea kwa hasira

"Kama ndo hayo tu shoga mimi nitahama kwako hamna shida" aliongea kwa kiburi 

"Mfyuuuuu" alisema binti

Simu ya Tina iliita na alikuwa anapiga Dickson

"Hallo" aliongea binti

"Hallo Mambo Tina" aliongea Dick

"Safi tu jamani za uzima"

" Uzima uko poa vipi Tina upo na Tino hapo?" alisema mtaalamu

"Hapana Tino niliagana naye muda sana kwanza nilijua yeye ndo anapiga"

"Hapana sijamuona bado"

"Mmmh atakuwa wapi jamani?" aliuliza

"Achana naye bwana, ni mtu mzima yule. Vipi hivi wewe mtoto unakaa wapi maana naona unang'aaaaa hatari" alianza kumsifia

"Nakaa Mbezi Kimara"

"Ok, kesho nitakuwa huko vipi tutaweza kuonana tuongee?" alisema mtaalam

"Hapana, kwani wewe unataka tuongee nini?"

"Aaah unajua Tina mtoto mzuri kama wewe unapaswa kukaa sehemu fulani hivi Amazing ule bata unavyopendeza nilitaka tule bata wawili kesho jamani"

"Duuuuh, dickson, ntakupa namba ya Rafiki yangu labda, lakini mimi hapana kwa kweli mi niko na rafiki yako siwezi kula bata na wewe" alisema.

"Jamani Tina, taratibu usiwe na papara unajua wewe ni msichana mrembo unapaswa uishi maisha mazuri, vipi utakubali nikununulie kagari kadogo kakutembelea"

"Mfyuuuuuuu" binti alikata simu kwa hasira "Hauna jipya"

Dickson akapiga tena lakini binti akakata

"Jane jamani si upike eti, nina njaa halafu kichwa kinauma sana eti" aliongea vizuri na shoga ake halafu akafunua kitambaa kwenye nywele

"umeenda kusukia wapi shoga mbona umependeza sana leo"

"Hahaha, hapa hapa ndani kwetu" binti aliongea kwa furaha na kuchukua mafuta anapaka upande wa mbele wa nywele ili rasta zisiume

"Nani kaja kukusuka jamani wewe si ulikuwa na Tino huku leo?" aliuliza binti

"Ndiye kanisuka" aliongea huku akitabasamu

"Muongo"

"Kweli bibie, yaani Tino anasuka vizuri sana Jane"

"Jomooonii, yule kaka kumbe ana uwezo hivi?" alisema Jane

"Yaaani" alisema binti Tina "Lakini sijui yuko wapi, naona kama vile mapichapicha rafiki yake ananitaka, sijui ndo ananipima kama mimi malaya"

"Hahahahaa, ngoja mi nipike jamani" alisema binti Jane na kuinuka

×*********×

Asubuhi saa mbili kamili katika lile eneo ambalo Tino alikuwa amehifadhiwa, alikuwa na njaa sana.

Kwa nje ya jengo lile ilipaki bonge ya gari Mara akashuka Muheshimiwa, kumbe ndiyo aliamuru mtaalam atekwe kwa sababu anakula chombo yake

Wale vijana waliomteka walimsujudia, akapita na kuingia ndani

"Naombeni wote mtoke nje nibaki mimi na kijana huyu tu" Alisema mheshimiwa na kuchomoa bastola yake iliyokuwa kwenye kiuno halafu akaikoki krrraaa! 

"Sawa mkuu" walisema kina Tony na kutoka nje. 

Walipofika nje mzee alibaki ndani akiongea na Tino

"daaaah asije akamuua mshikaji" alisema Tony maana japo alimteka Tino ni rafiki yake sema tu mkwanja ndiyo tatizo la usaliti. 

Ndani Tino na Mheshimiwa Regnald Mwasoka walizidi kuongea mambo ambayo hayakusikika nje na wala haikujulikana wanaongea mambo gani

"paah,........paaaaaah.... ... Paaah....... Paaaah" Sauti za bastola zilisikika mara nne ndani alipokuwa Mheshimiwa na Tino

"Mungu wangu" Tony alisema kwa mshtuko. 

Halafu muheshimiwa alitoka ndani na kupanda gari yake akasepa....... JE NINI KITAFUATA

TINO KAFA? NA JE TINA AKISIKIA TINO KAFA ITAKUWAJE? 

Post a Comment

Previous Post Next Post