UNO LA MASIKINI 07 🔞

🆎©️
#Ilipoishia
"paah,........paaaaaah.... ... Paaah....... Paaaah" Sauti za bastola zilisikika mara nne ndani alipokuwa Mheshimiwa na Tino

"Mungu wangu" Tony alisema kwa mshtuko. 

Halafu muheshimiwa alitoka ndani na kupanda gari yake akasepa.

#Endeleaaaa
Kina Tony walipagawa hawakuamini kilichotokea, kila mmoja aliogopa kwenda ndani kushuhudia kile kilichokuwa kimetokea

Ghafla waliona Tino ametoka kule ndani akiwa mzima wa afya kabisa na wala hakujali.

"Tino mwanangu" Tony alisema "Hajakushuti?"

"Hahaaaha hamna kapiga zile risasi ili kukata kamba mlizonifunga nazo"

"Ok daaah niliogopa sana"

"Haina noma, nipeleke geto mwanangu" Tino alimuomba Tony 

Uso wa Tino ulionekana usiokuwa na wasiwasi hata kidogo, kukutana na muheshimiwa wala yeye hakujali,

Tony alimpeleka hadi nyumbani "Samahani mwanangu kwa kukuteka ni suala la mkwanja tu shika hii" alimpooza na elfu hamsini Tino akashukuru na kuzama ndani

Muda huo huo Tina alikuwa akimsumbukia Tino, hakujua ameishia wapi

"Jane naomba unisaidie kumpigia Dickson halafu umzuge kama yupo karibu na Tino" aliomba binti Tina 

"Haaaaah, leta namba yake"

Tina alimtajia Jane namba ya Dickson ili aweze kumsaidia kupiga simu ajue kama Tino yupo

"Dickson, mambooo" alisalimia Jane

"Safi niajeee" Dick alifurahi kuisikia sauti ya kike

"Pouwa jomoni mbona kimya sanaaa" Alimzuga ili apate gia ya kumuingia aseme ukweli kama yupo na Tino 

"Aaah mbona nipo jamani, vipi pande gani?" Alisema 

"Niko Basihaya jamani, hata rafiki yako Tino simuoni sijui yuko wapi, mpo naye hapo au leo upo peke yako Dickiiii" aliongea kimahaba sana mpaka Dickson akasahau kumuuliza jina

"Aaah, Tino bwana tangu jana asubuhi hayupo na sijui yuko wapi simu pia hana ningempigia" alisema Dickson

"Haya bwanaa natamani nikuoneee" Jane aliongeza mbwembwe ili Dick asishtuke 

"Aaaah utaniona tu aamhhhhh samahani lakini. Unajua mpaka mda huu bado sijakupata lakini" alisema Dick

"Utanijua tu, subiri nitakucheki" Alisema Jane na kukata simu wote wakacheka kwa nguvu

"Anasemaje?" aliuliza Tina

"Tino eti hajamuona Tangu jana asubuhi"

"mmmmmh Jane, kweli kasema hivyo?" aliuliza

"Ndiyo wallahi vile"

"Sasa atakuwa ameenda wapi jamani huyu mwanaume?"

"Mh halafu vipi jana ulimpa?" Jane aliuliza

"Mmmh ninaachaje kwa mfano, niliona anazubaa zubaa nikaingiza mwenyewe...... Tamu hiyo" alisema binti

"hahahahaaaaaa huuuuuu" walicheka na kugonga kwa nguvu

"Ana mauno mwanaume yule ni kimoja tu lakini weeeeeee..... Haki siwezi kumnyima haki yake yaani mh"

"ni wa Tangaa nini" aliuliza Jane

"Haswaaaa, wa kule kule"

"Lazima awe mtamu wee"
Simu ya jane iliita na aliyekuwa akipiga ni muheshimiwa

"Christina Daudi Mwaipopo" aliita mheshimiwa majina yote matatu ya binti yule

"Yes Baby" Binti aliitikia style ya kumchanganya mheshimiwa

"Jana ukaona haina haja ya kujibu sms yangu mimi"

"Samahani mpenzi niliogopa sana balafu baadaye nikaishiwa na kifurushi ndiyo maana sikujibu"

"Sawa, lakini, naomba leo tuwe wote chumva 061 JingoMoja"

"Sawa mpenzi" aliongea binti na mheshimiwa alikata simu

Haikuisha dakika nyingi SMS ikaingia kwamba ameungwa na kufurushi cha mwezi ni kubonga, kuchat na kuperuzi tu

Dakika tano baadaye simu iliita tena na sasa ilikuwa ni namba mpya

"Hallow" Alianza Tina

"Hallo mambo vipi Tina"

"Jamaaani sauti nimeshaijua hiyo mpenzi jaman jaman jaman jamani, ulipotelea wapi kwanzaa" aliongea binti kwa uchangamfu baada ya kusikia sauti ya Tino

"Hahaha, Jana wale washkaji wakanipeleka bar, nilikunywa mpaka nikasizi" alisema Tino kwa kudanganya kwani hakutaka binti ajue kwamba alitekwa

"Jamani babe T, usinywe pombe sana" 

"Usijali, sinywagi mara kwa mara mpenzi

"Sawa mpenzi namba yako hii?".

"Ndiyo honey asante kwa kunirudisha hewani" alisema Tino

"Sawa baby upo wapi maana mi naenda zangu Kijitonyama kutembea ntarudi baadaye" alisema

"Niko home tu leo, nataka nifuatilie ishu ya kusajili laini ili nipate hata kazi na mi"

"Sawa baby lakini kazi kama hiyo mh, ila sawa......"

"Ok baby sikiliza, hivi unamfahamu mdada mmoja anaitwa Mido Baby?" Tino aliuliza

"si ndo msanii aliyeimba nyimbo ya Utandu Uzandu?"

"Yaaaap ndiyo"

"Kwani kafanyaje sasa"

"Aaaah samahani naomba unisaidie, nipate ukaribu naye" alisema

"Ukaribu gani, na wewe umeshaanza sitaki" alisema binti kwa wivu

"Sio wa kimapenzi nataka tu hata kwenye kushuti video na mimi niwepo napenda sana nyimbo zake" alisema

"Haya bana basi nitakuambia nikionana naye maana, mi sinaga mazoea naye"

"Sawa dear sitakusaliti nakuahidi" alisema

"Poa mpenzi baadaye nitakucheki" alisema 

Baada ya kukata simu Tino alikuwa amejilaza anatafakari.

"Mido Baby, Mido Baby.." alimtafakari huyo msanii wa kike haijulikani ni kwanini..... TUTAFAHAMU UKWELI KWENYE SEHEMU INAYOFATA

OFA INAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post