UNO LA MASIKINI 08 🔞


Wiki moja baadaye Tina alikuwa katika kasino moja huko Sinza Mori, alikuwa amesimama na msichana mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Ritha huku wakipiga story

“Ritha unajua mimi nina uwezo wa kucheza video vizuri sana sema tu msanii wako huyu anaonekana hataki nicheze naye video”

“anataka sana tena jana alikuwa anasifia umbo lako na mambo yako ni hatari”

“haya bwana vipi lakini naweza nikaongea naye sasa hivi”

“ndiyo utaongea naye subiri kwanza amalize kuperform nyimbo hii ya mwisho” alisema binti

“Ok powa” Tina aliongea na kusogea pembeni kidogo akiwa ameshikilia simu akiwa anampigia simu Tino 

“baby Tino mambo”

“safi tu mambo vipi?”

“powa umenisusa hata kunitembelea hutaki kabisa, vipi?”

“hapana naogopa kuja nyumbani kwako Tina sijui ninakuogopa fulani hivi kwa sababu ya vitu fulani fulani”

“unaniona Malaya Tino ndiyo maana unasema hivo, mimi nina kipi cha kutisha?”

“Tina mimi kesho asubuhi na mapema nitakuja mpaka hapo geto kwako kuna kitu nitakuambia mpenzi”

“sawa uje, siku hizi ninaishi peke yangu rafiki yangu Jane amehama ameenda kupanga kwake mwenyewe….. halafu kuna zawadi kibao nimekununulia ziko pale nyumbani nimekuwekea dear”

“kwani wewe uko wapi?”

“niko sinza nafuatilia ile ishu yako ya kuonana na Mido Baby” alisema binti

“ok sawa mpenzi, asubuhi nitakucheki

Basi walikata simu na Tino akaenda kula kwa mama ntilie halafu baadaye akarudi na kulala ila upande wa Tina yeye alikuwa akiongea na Mido Baby ambaye alimaliza kuperform kidogo.

“inabidi Tina uchukue namba yangu na tutaongea maana hapa hatutaweza kuongea vizuri”

“sawa sawa kabisa, embu nitajie” Tina aliongea huku akiitoa simu yake mfukoni na kuandika namba ya msanii huyo ambaye Tino alitaka kuongea naye haijulikani ni kwanini

Tino yeye akiwa amelala alikuwa anakumbuka ilikuwaje hadi akataka kuwa karibu na Mido
Wakati Tino alipotekwa na kina Tony anakumbuka muheshimiwa alikuja akiwa ameshikilia bastola na alimfuata Tino na kuchuchumaa mbele yake

"Nchi yetu ni nchi ya amani sana, haya masuala ya kutekana tekana ni ya nje huko, nisamehe kwa hili" alisema muheshimiwa na kutikisa kichwa kwa kusikitika
"Mheshimiwa sikujua kama nitakuona hapa"

"Hahaa, usijali mimi ni mtu wa kawaida sana, hivi Agustino Benjamin Clement, haujui mapenzi yanauma" haijulikan jina alilijulia wap

"Najua muheshimiwa"

"sasa yule binti unahisi ni nani anamtunza halafu wewe unamtumia tu burebure bila hata mia, au ndo kipaji chako cha kuimba, umemuimbia akakolea, au ni sababu ya nywele ulizomsuka?" alisema mheshimiwa

"Wewe umejuaje haya yote baba" aliuliza mtaalam

"Samahani kidogo, mi nakufahamu sana, sasa nikuambie tu, roho inaniuma yule binti ni wa kwangu wewe achana naye labda umfuate kwa ajili ya vitu vingine sio mapenzi"

"Sawa mkuu"

"Haya, sikiliza kinachofuata mtafute Mido Baby yule binti anakufaa" alisema mzee

"Kimapenzi au kivipi mheshimiwa"

"Jiongeze wewe ni mtu mzima" mzee alisema na kuinuka akazipiga zile kamba walizomfungia mtaalamu kwa risasi, na kutoka nje

Tino naye alijitoa pale kwenye kile kiti kisha akatoka nje na kuwakuta kina Tony wamesimama kwa uoga wakijua ameuawa ndani kule. 
**

Hata hivyo asubuhi haikuwa mbali Tino alipanda gari na kuelekea Mbezi kwa ajili ya kwenda kuonana na Tina ambaye alikuwa ni mpenzi wake tayari

Hakutaka kumpa taarifa yoyote kwamba anamtembelea binti yule kwani alitaka amfanyie surprise japo aliogopa mzee Regnald akijua kwamba bado jamaa ana ukaribu naye anaweza kumfanyia kitu kibaya

“ngongongongo” aligonga mlango wa Tina kwa fujo

“nani?” aliuliza Tina akiwa anakaanga karanga

“njoo unione” alisema Tino akiwa nje, binti akaelewa kabisa kwamba ni jamaa ake.

Alitoka taratibu kwa kunyata akamrukia na Tino alimdaka wakawa wamekumbatiana
“wooooow Tinoooo” binti aliongea kwa furaha

“mambo” aliongea kwa sauti nzito sana

“safiiii, karibu ndani jamani” alisema binti na kumuachia akaingia ndani na Tino akaingia

Binti alipofika ndani alikuta karanga zinaungua “uwi Mungu wangue” alisema na kuzima jiko “Tino unaona umeniunguzia karanga zangu” alisema binti

“hahaahaha pole sana Tina” alisema mtaalam akaketi kwenye sofa na kuangalia huku na kule.

Basi binti alimimina kahawa kwenye chupa na kumpatia karanga kidogo “samahani zimeungua kidogo ila zinafaa kula” alisema mtaalam

“usijali, Tina, halafu sikai” aliongea sura ikiwa imeshabadilika kidogo kwa uoga wa hali ya juu alikumbuka maneno ya Muheshimiwa

“kwanini Tino unanifanyia hivi? Unataka niteseke basi sawa bwana unaringa sana now” alisema kwa hasira huku akisusa kula

“nisamehe” alisema mtaalam

“sasa nikusamehe nini, kama wewe hunitaki basi niambie mimi nfuate mambo yangu sio kunifanyia hivyo kila siku bana aaah” aliongea kwa hasira na kujikung’uta kidogo

“Tina vipi ulipata ukaribu na Mido? Maana nina kazi muhimu ya kwenda kufanya naye?” alisema

“kazi gani ya muhimu Tino, najua unampenda yule mwanamke"

“hapana mimi ninaimbaga pia ila natafuta namna ya kutoka so lazima nitafute msanii kwanza” alisema Tino

“mmmh uimbe wewe, embu niimbie” alisema binti huku akitabasamu na kusahau maneno ya jamaa yote aliyomuambia ya kukatisha tamaa

“usijali nakuimbia ngoja nimalize kula kwanza” alisema mtaalam “na wewe ule sasa au ndo umesusa?” alisema

“jamani Tino nakula lakini please naomba usiondoke nataka tukae hapa mpaka jioni” alisema binti

“na je nikikutwa hapa?” alisema jamaa

“ukutwe na nani?” binti aliuliza

“Mheshimiwa Regnald Mwasoka” alisema maneno hayo yaliyomshtua binti kidogo ajiunguze na chai

“Tino!!!” aliita kwa mshangao na kuweka chai kwenye stuli

“nini sasa au unafikiri sijui kwamba unatoka naye?” aliuliza

“Tino jamani” binti alisema huku akilengwa na machozi “umeyajulia wapi haya yote” aliuliza

“we unafikiri kwanini sitaki kuja kwako? Ni kwamba mimi ninahofia maisha yangu, sina mtoto hata mmoja unataka nife mapema hivi?”

“Tino” binti aliita kumsogelea Tino akamlalia kwenye bega “naomba unisamehe, mimi simpendi yule mzee kweli, ila tu ni masilahi nikuambie ukweli, halafu pia Tino mimi niko tayari kuachana naye niwe na wewe” alisema binti

“Tina, tatizo sio kwamba wewe utamuacha, ila ni kwamba unaniweka kwenye hatari kubwa sana”

“kivipi?” 

“Siku ile nilipotoka hapa kwako unakumbuka ile gari iliyonipa lift?” alisema mtaalam

“ndiyo ninaikumbuka”

“waliniteka”

“nini?” aliuliza

“Waliniteka, nakumbuka kesho yake nilikudanganya kwamba nilienda kunywa pombe lakini sio kweli ni kwamba waliniteka wakanifunga kamba mpaka asubuhi ndipo muheshimiwa alikuja na kuniambia kwamba niachane na wewe la sivyo atanifanyia kitu kibaya sana”

“Tino jamani Tino jamani Tino” alisema binti kwa hasira

“lakini please usimuambie” alisema jamaaa

“sawa Tino” 

“ndiyo sasa mimi ninaondoka naenda zangu nyumbani kilichonileta kwako nishakuambia” Tino alisema na kumalizia kahawa halafu akainuka na kuanza kuondoka.

“Tino sawa unaondoka lakini ngoja nikupe zawadi yako nilikuwa nimekununulia huko Sinza, naomba uchukue maana sina pa kuzipeleka tafadhali” alisema binti na kuinuka akachukua mfuko na kumkabidhi mtaalamu

Tino alipoufungua ule mfuko kutazama ndani alikutana na Nguo kali za maana, T Shirt tatu na jeans 3 na shati moja la kisasa, halafu ndani kukiwa pia na raba moja ya maana sana

“Tina ni vya kwangu hivi?”

“ndiyo, embu jipime maana mimi siamini kama vitakutosha” alisema binti

Tino alivua shati lake na kuweka pembeni, halafu akavaa tisheti mpya moja ikamkaa “Imenitosha jamani ni nzuri sana” alisema kwa furaha
Aliivua ili ajipime ya pili lakini binti alishindwa kuvumilia baada ya kukiona kifua cha jamaa alimfuata na kuegesha mkono kifuani mwa Tino

“Tino usiondoke, nimekimiss kifua chako” alisema binti kwa hisia na kuendelea kukipapasa

Kwa kuwa Tino pia alikuwa ashaanza kupata hisia na binti basi naye alibaki akimtazama tu usoni mtoto wa kike

Taratiibu alimsogezea mdomo wakaanza kukulana mate kwa mara ya pili……..ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post