UNO LA MASIKINI 4. 🔞

🆎©️
#TULIPOISHIA
"nikuambie sentensi ya mwisho ili nilale maana nimechoka sana Tino"

"Niambie basi"

"Nakupenda then Gooodnight" Tina alisema na kukata simu.

#ENDELEA
Maneno haya yalimshangaza sana Dickson ambaye mda wote alikuwa akisikiliza maongezi ya Tino na Tina kwenye simu

"Huyu demu sijui yukoje, yaani ananitongoza man" alisema Tino na kumpa Dick simu yake

"We ni fala, mkubalie huyo ukamchape mtoto ana kipururu" Dick alisema 

Tino hakujibu chochote alilala zake na Dick akawa anachati kwenye simu mpaka mida ya saa tisa usiku naye akajilaza

Ilipofika asubuhi saa moja kamili Dick aliamka na wenge la usingizi akachukua mswaki na kutoka nje ya chumba akapiga lakini simu aliiacha ndani

Haikukawia kuingia sms kutoka kwa Tina

"Dickson naomba umpe Baby Tino simu niongee naye" 

Tino aliifungua simu na kuangalia sms akakuta ni ya Tina, akatabasam kidogo
"Kananipenda aisee" alisema mtaalam kwa sauti ndogo

"Tina, Mimi Tino Nipigie tafadhali"

"Wooooow, nakupigia my lovee subiri nimtoroke shoga angu maana mbea huyo mh" alituma binti

Tina hakupenda Jane aelewe kwamba anampenda mtaalam hivyo aliamua kutoka nje kimya kimya na kwenda kukaa sehemu tulivu halafu akapiga simu

"Hallow" Tino alisema baada ya kupokea simu

"Hallo Tino, mbona hivyo unaongea kwa uchovu unajua sauti yako inanipa tabu moyoni Tino lakini!!" binti alisema sasa kumbe Jane naye alikuwa akimfuatilia taratibu kwa nyuma na kusikuliza bila Tina kumuona

"Sauti yangu mbona ya kawaida Tina"

"Ya kawaida vipi jamani, ingekuwa ya kawaida nisingekusifia ila tu acha nikuambie ukweli unanifanya usiku usingizi hauji hata kidogo"

"Kwanini unanipenda" 

"Sijui ni hisia tyu Tino mimi huwa napendwa na watu wenye pesa na wakubwa na maarufu sana lakini na mi siwapendagi nashangaa wewe umenitawala kama Mjerumani kwenye moyo wangu yaani I love you sana wala sitaki unijibu mi naamini na wewe unanipenda sana tyu"

"Mmmh haya basi nimekuelewa lakini naomba kitu kimoja"

"Kitu gani usikute ni kunikatalia ombi langu"

"Mimi nakuomba tu ujaribu kunisahau kwa sababu mimi sio type yako"

"Tino usinifanyie hivyo, jamani hadi nimekuambia mwenyewe jamani au ndo ushaniona malaya sasa"

"Hapana wewe ni binti mrembo sana tena kifaa, hata rafiki yangu anakusifia sana ila mimi nashindwa kwa sababu kwanza sijui kupenda"

"Sawa Tino asante kwa kuumiza moyo wangu, ila naomba tuonane kwa mara ya mwisho leo, halafu sitakusumbua tena"

"Ok tuonane wapi?" alisema

"Njoo mpaka Mbezi shule" alijibu binti

"Ok poa nitakuja saa nne"

"Sawa Tino, halafu hela ya Nauli Unayo?"

"Ndiyo ninayo" alijibu mtaalam

"Ok mi saa nne ntakaa pale barabarani nakusubiri wewe"

"haina noma"

Binti alikata simu na kuiweka kifuani halafu akavuta pumzi na kugeuka nyuma kidogo, ile amegeuza shingo si akamkuta Jane anacheka, alishtuka

"Vipi J"

"Hahahaa si nilikuambia ushampenda?" alisema na kucheka tena hadi akachuchumaa

"Mmmh hamna namzuga tu jamani"

"Hakuna kuzuga hapo, umemfia shoga angu" alisema Jane

"Bhana na wewe kumbe wapenda kufatilia fatilia mambo ya watu bhana aah" alisema

"Haya mwaya sawa, ila muheshimiwa akijua mbona itakuwa pambe" 

"Ajue, kwani yeye ni nani?" alisema binti na kuinuka akaenda ndani kwa hasira. Hata masuala ya kwenda kwenye video shooting hakutaka tena

Ilipofika mida ya saa nne Tina alivaa kipensi cha kubana, cheusi halafu juu akavalia blauzi fulani ndefu mpaka ikafunika kile kipensi maana ilifika hadi magotini

Alitokea hasa halafu akafunga vifungo vichache na kuvaa kiatu kizuri akaenda mpaka barabarani akaketi kwenye viti vya barabarani akimsubiri Tino. Mkononi alishikilia Mo Passion kubwa na muhindi wa kuchoma

Tina alikaa akitafakari sana, kama Tino akija ataenda naye wapi

"Au nimpeleke tu geto" alisema binti kwa sauti ndogo mara akapita muuza Rasta 

"Sister Rasta rasta rasta" alisema yule machinga

"Samahani wauzaje" aliuliza

"Buku tatu aina yoyote"

"Nipatie yeboyebo tatu na mimi nikapendeze"

"Asante dada yangu" alisema yule jamaa na kumtolea

Sasa wakati wanazidi kupeana hela mara gari kutoka Mabwe Pande nayo ilifika kumbe ndiyo aliyopanda Tino na alishuka kwenye gari

Binti alilipa haraka haraka na kumchangamkia Tino 

"Samahani kaka, wewe ndo Tino?" Tina alimtania

"Hapana naitwa Aqbist Fabley Dox Dox" alisema mtaalam

"Hahahahaaaaaaa muone vile" binti alisema na kumfinya kwenye shavu bila kumuumiza halafu akamkumbatia kidogo huku akinyanyua mguu mmoja juu na kumbusu shingoni saa ngapi Tino asione aibu 

"umenunua rasta" alisema ili kumpotezea

"Ndiyo nataka nikasuke na mimi nipendeze" alisema binti

"Nikakusuke?" Tino alisema na kuzishika zile rasta

"Hahaa ndiyo kanisuke" binti alimtania maana alijua jamaa hawezi kumsuka

"Haya poa"Alisema Tino binti alimuangalia mtaalam usoni akacheka

"Nisubiri hapa" alisema binti na kuondoka akikimbia akaingia katika frame moja ya kubani movies ndani ya dakika tatu akatoka na kumfuata tino "Twende kwangu" alisema

Tino hakuwa mbishi walianza kutembea ikabidi Tina amuandikie sms Jane ili aondoke awaache yeye na Tino.

Baada ya dakika chache walifika ndani Tino alishangaa sana maana ni geto nzuri yenye kila kitu

"Karibu" alisema binti na kumuangalia usoni Tino.

Tino aliketi kwenye sofa na nguo zake chafu halafu binti akaenda nje kuleta chapati na kurudi ndani 

Alimkuta Tino akizichambua zile rasta
"Tino mbona umefungua rasta zangu" binti aliuliza kwa mshangao

"Si ulisema nije nikusuke?" Alisema Tino

"Ah mh wewe kwani unajua kusuka" aliuliza binti

"Ndiyo sasa kwanini nkudanganye we keti hapa chini mimi sili mpaka nikusuke"

"Tinooo!" binti aliita kimahaba

"Ndiyo mimi si ukae hapa na wewe au hutaki kupendeza"

Ilibidi binti aketi chini na kukaa katikati ya miguu ya Tino ili asukwe
"Chana iko wapi" aliuliza Tino 

"Mmmmh hii hapa" alisema binti na kumpa

Jamaa alianza kumfinya finya mtoto wa kike kichwani binti alikuwa akitabasamu tu akijua masihara,

"Hivi we kabila gani una vituko hivi?" Aliuliza

"Msambaa" 

"Mh.... haya" alisema binti

Dakika tano, kumi, ishirini, zikapita

"Embu jiangalie kwenye kioo" alisema mtaalamu na kuinuka akachukua kibunda cha rasta kingine

Binti naye aliinuka akachukua kioo akajitazama

"Tino!!!!!" binti aliita kwa mshtuko akamgeukia Tino maana hakuamini kwa alichoona kichwani mwake hakuamini Tino anajua kusuka kiasi hicho. 

Aliweka kioo mezani na kumkumbatia kwa nguvu halafu akamdosha kitandani, rasta alizoshika Tino zikaanguka kule

Binti alimbusu mtaalam kinywani kwa nguvu hadi ndimi zikakutana, wote walisikia raha, huku binti akimfunika Tino usoni kwa rasta zake chache alizokuwa amesukwa

"Tino mi nina hisia na wewe" Binti alisema na kumpa denda.... JE NINI KITAFUATA 

Post a Comment

Previous Post Next Post