UNO LA MASIKINI 3. 🔞

Kisa chenye ukweli ndani yake

🆎©️
Mida ya asubuhi Tino aliwahi kuamka, akachukua simu ya mwenzake na kutoa lock maana yeye hakuwa na Simu

Kama utani aliandika namba ya Tina ambayo alikuwa ameikariri alipotajiwa na Tina ilikuwa 0654433281

"Mambo" aliitumia sms namba ile wakati huo Tina alikuwa akivaa nguo kwa ajili ya kwenda kwenye video shooting huko Makumbusho.

Binti aliisoma sms na kujibu "Poa nani?" alijibu kwa mbwembwe

"Tino" 

Kwanza cha kwanza binti alipoisoma ile message aliushika moyo wake kwa sababu uligonga kwa kasi ya ajabu. Hakuamini kama kijana angeshika namba yake kiurahisi wakati alimtajia mara moja tu namba

"Haupo serious Tino" alimtext huku akiketi vizuri

"Kwanini?" Tino aliuliza

"Kwa sababu haiwezekani wewe uishike namba yangu kirahisi rahisi vile"

"hahaa mbona kawaida na wee" alisema Mtaalam

"Hahaa Genius" binti aliandika kwa furaha

"Whose number is this?" aliuliza kwamba namba anayotumia tino ni ya nani maana alimwambia kwamba hana simu

"Unasemaje mbona sijaelewa kiingereza" Tino alisema

"Daaah, Samahani sikujua jamani nimekuuliza hii namba unayotumia ya nani?" alisema binti halafu akamgeukia Jane "Hahaa Shoga angu nachati na Tino hajui kiingereza hata kidogo" binti alisema kwa dharau kidogo

"Tino ndo yupi?" aliuliza Jane

"Yule kijana mvuvi na we" binti alisema

"Hahahaaa"alicheka tena

Mara tino alijibu message "sawa, simu ni ya mshikaji wangu aitwaye Dickson"

"Powa, nitakucheki mida naenda kishuti video ya Harmonize"

"Harmonize???" mshkaji alishtuka sana

"Ndiyo mbona kama umeshtuka"

"Msanii mkubwa sana huyo mbona" alisema mtaalam

"Kawaida" alijibu binti "Byee mwaya baadaye nitakutafuta"

Ilibidi Tino amrudishie simu Dickson, bila hata kufuta namba ya Tina. 

Dickson akaweka simu mfukoni na kuelekea zake kwenye Jobu lakini Tino akaketi zake chini huku akitafakari namna ya kupata kazi

Hata hivyo Tina na Jane wakiwa kwenye bajaj walikuwa wakipiga story za kudanga

"ina maana jana Mheshimiwa alionyesha shoo au ndo hamna uno kabisa" Jane aliuliza

"Kimoja tu chali nikasepa mimi"

"Bila hela?" Jane alipenda hela sana

"Weee alinipa hela yangu, ila Unajua Tino ni mstaarabu sana?" Binti alisema alijikuta akimchanganya Tino kwenye story zisizomuhusu

"Toba, Tino katoka wapi tena huku? We Tina nimeshtuka ushampenda yule kijana mchafu bila kujua" Jane aliongea

"Hapana siwezi nikampenda yule, mimi sipendagi mwanaume wewe"

"Haya tutaona" Jane alisema

Safari yao ilishia katika maeneo ya Derm Plaza, hapo ndipo walitakiwa washuti kideo cha wimbo mpya wa Harmonize ambao pia jina halikujulikana kwa watu wengi maana ulikuwa haujatoka.

Kulikuwa na shamra shamra Hanscana huyu hapa, Jose wa Mipango, Konde Boy huyo hapo, Ibraa Tz n.k

"Mtotooo" Hanscana alianza mbwembwe

"Hahahaha, wewee Hanscana ushaanza" binti alisema 

"Nikumbatie basi jamaniiiiii" Hanscana alimtania

"Sitakiiiiii" Alisema binti

"sawa, na ntamwambia kaka Kondeboy asikulipe shauri yako" 

"Hahaha bwana, embu kwanza nitumieni wimbo huo niusikilize kidogo"

"Weee ukausambaze wakati hautoki siku za karibuni, utasikilizia hapa na kuuacha hapa hapa" Alisema Konde

"Haya bwana"
"Tushuti vipande vya kwanza sasa, wee nendeni mkabadilishe mavazi" Hanscana alisema

Basi ilikuwa ni shamra shamra za kuchukua video tu mpaka usiku ndiyo waliweza kurudi nyumbani

"Mambo" Tina alituma sms kwenye namba ya Dickson ajue kama ataweza kuchat na Tino

"Safi, samahani Sipo home nikifika nitampa Tino achat na wewe" alisema Dickson mara Binti akampiga

"Hallooo mambo kakaa angu, usisahau please and please unisaidie niongee naye" alisema binti

"Usijali maa" mtaalam alijibu

"pouwaaaah" Alisema Tina na kukata simu

"Daaaaah kudadadeki huyu demu gani ana sauti kama hii, halafu ndo anamsumbua Tino kudadadeki" Alisema Dick kwa mshangao

Ilibidi aingie whatsapp aangalie DP ya huyo binti ili ajue ana kasoro gani hadi amtafute Tino 

Alipofungua DP ni chombo ya maana, akachanganyikiwa, hakutaka jamaa afaidi kabisa alitamani yeye ndo awe na kile chombo

Mida ya saa sita usiku ndipo Dick alirudi nyumbani akiwa haamini kile kinachoendelea

Alimkuta Tino ameketi akila maandazi ya Bakhresa

"Tino" aliita jamaa huku akitoa simu mfukoni na kuingia whatsapp akaikuza dp ya yule binti 

"Unamfahamu huyu demu?" aliuliza mtaalamu Tino akaitazama picha na kujibu

"Ndiyo, si ndo nilikuwa nachat naye asubuhi kwa simu yako"

Mara sms ikaingia kutoka kwa Tina, "Jamani hujamuona tyuuu?" aliandika binti. Tino alipoisoma akatabasamu kidogo

"Nipigie" alimtumia sms, na sekunde kumi nyingi simu ikaita

"Haloo" Tino alisema

"Halo, nimeshajua ni wewe nimesikia bezi hilo mkaka" Alisema binti akitabasamu

"Hahahaa, una mbwembwe, vipi Harmonize hayupo hapo niongee naye" aliuliza Tino

"Jomonii, ashaenda kwakee, mi niko na shoga angu nimekumisss" alisema binti

"Tina, usinimiss bhana sina hadhi ya kumissiwa na wewe"

"Unayo tena sana tena kesho nataka tuonaneee" alisema binti kwa hisia

"Wapi?" 

"Popote tyu nataka nikupe zawadiii" alisema kwa kubana pua binti

"Zawadi gani sasa Tina"

"hata busu si zawadi" alisema binti huku akicheka Cheka kama vile hataki, Tino huko alipo tayari alishadindisha mdaa, hakuamini

"Busu utathubutu?, nikikutwa na mtu wako" alisema Jamaa

"Sina jamaa wa kukutishia yeyote nataka uwe wewe wa kuwatishia wengine"

"Tina usiseme hivyo, mimi na umasikini wangu sitaweza kukupa furaha kabisa hata kukutunza siwezi, tazama kazi sina"

"Uishie hapo hapo, mimi nina nguvu ya kujitunza mwenyewe"

"Tina"

"Tino" waliitana "Huoni hata majina yetu yanaendana"

"Daaah Tina sawa majina tunaendana lakini hadhi tofauti"

"nikuambie sentensi ya mwisho ili nilale maana nimechoka sana Tino"

"Niambie basi"

"Nakupenda..... then Gooodnight" Tina alisema na kukata simu.....ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post