UNO LA MASIKINI 2 🔞

#Tulipoishia
Alijikuta amemuwazia mtu ambaye ndiyo mara ya kwanza kumuona yaani mpaka akaaishia usingizini akiwaza imekuwaje kijana yule akamsaidia....

#Endelea sasa
Asubuhi na mapema Tina aliamka huku akiwa ameimiss Instagram yake, alitakiwa pia aende maeneo ya Makumbusho kuna video alikuwa akacheze huko yeye na msanii Harmonize

Ilibidi afanye kujiandaa haraka haraka yeye pamoja na Rafiki yake Jane wakachukua bajaj na kuelekea maeneo ya Makumbusho, walifika moja kwa moja hadi katika ofisi kuu za Tigo kwa ajili ya kurenew line ya Tina iliyopotea jana kwenye simu

"Naomba namba ya NIDA tafadhali" alisema mhudumu

"19960218312540000322" Tina aliitaja na yule muhudumu alimsaidia kufanya process za kurudisha laini ile

"Njoo weka kidole cha pili hapa"

Tina alisogea taratibu na kufanya kama alivyoagizwa

Baada ya kumaliza kila kitu yule kijana alianza kumchokoza

"Christina"

"Abee"

"Na mimi nichukue hii namba nini?" aliuliza kijana yule baada ya kumuona binti anavyong'aa

"Haina shida" alijibu binti

"Poa basi nitakucheki"

Binti na rafiki yake waliondoka moja kwa moja na kuchukua tena Bajaj hadi maeneo ya Kariakoo ili kuweza kununua simu mpya na kali

"Sijui tutawahi kurudi"

"Kwanini tusiwahi? ni chapu tu bana" Jane alisema

Walienda hadi Kariakoo na kuvuta simu nzuri ya laki nne halafu Tina akatia laini yake na kuunga bando ili kui-update

"Samahani Tina hatutafanya video leo tutafanya kesho" alituma sms Jose wa Mipango ambaye ni Rafiki wa karibu sana wa Harmonize

"Jamaaniii hawafanyi ile video leo" alisema Tina 

"Whaaat" Jane aliuliza

"SMS hii hapa" alisema Tina huku akimuonyeshea ujumbe Jane

Basi ilibidi waondoke na kurudi mitaa ya kwao huko Kimara lakini wakiwa njiani Tina alianza mbwembwe

"Jane, twende zetu kule kwa wavuvi tukasafishe macho"

"Mmmh shoga angu, kule tena umepapendea nini?" aliuliza

"We twende tu nataka nikamshukuru yule kijana aliyenisaidia jana"

"Makubwa shoga angu, wewe ni wa kummiss kijana yule mchafu?"

"Wewe twende bana au wewe tangulia nyumbani ukapike mi nakuja" alisema Tina

"Aya mi naenda nyumbani bwana nimechoka zangu"

"Powa basi"

Baadaye kidogo kila mtu alifuata mambo yake, Jane nyumbani na Tina Baharini kuwaona wavuvi

Leo Tina alipofika mule alimkuta yule kijana akiwa amejiinamia analia sana, leo alikuwa amevalia pensi ya rangi ya Maziwa, na fulana nyeusi

"wewe kaka mambo" binti aliongea kwa mshtuko baada ya kumuona mtaalam akilia

"Safi da.. Da kwema" alisema huku akijifuta uso na kufuta machozi ili binti asishtuke

"Kwema, mbona unalia" alisema

"Hapana silii dada angu"

"Haulii vipi wakati unaonekana macho mekundu na sauti ni ya huzuni hiyo, niambie ukweli kaka"

"Daaah dada yangu ni wiki sasa ninahudhuria hapa sipati kazi, nina njaa sana sijala tangu jana asubuhi najihisi kufa eti" kijana yule alisema

"Oooh jamani, pole sasa usilie, twende hivi" alisema binti na kumshika mkono akaanza kumvuta, jamaa lililegea kwa njaa

"Kwanza unaitwa nani kaka?" binti aliuliza

"Naitwa Tino" alisema "Kwa kirefu Agustino" alimaliza

"Ahaaaa mimi mwenyewe naitwa Tina, haha kwa kirefu Christina" alisema na kutabasamu huku akimuangalia yule kijana ambaye naye alitoa tabasamu kwa mbali sana "Kwa hiyo Tino na Tina" binti alisema

"haya sawa, sasa unanipeleka wapi?" mtaalam aliuliza

"Ukale"

"No hizi hoteli ni za ghali sana dada angu"

"usijali mimi ndiyo nalipia"

Basi walienda hadi hotelini wakala wote, binti akalipa hela za kutosha, halafu akamchukua Tino wakatoka hadi nje ya hoteli

"Wewe umeshiba sasa Tino?" binti aliuliza huku akimkagua mtaalam kwa macho legevu yaliyoonesha kumjali sana mshikaji

"ndiyo nimeshiba sana dada yangu asante" alisema jamaa na kuinama kidogo kwa nidhamu ya hali ya juu

"Haya basi powa, unakaa wapi?" aliuliza binti huku akiwa anafungua pochi yake na kutoa noti moja ya 5000

"Boko" alijibu Tino

"Haya hii itatosha nauli na kula Maana nahisi hauna mke wewe" binti aliongea akiwa anatabasamu huku akimkabidhi ile noti

"Asante jamani, mimi sina mke pia"

"Haya, samahani unaweza chukua namba yangu halafu ukaniandikia message hata na simu ya rafiki yako maana kesho kutwa nataka nije nikusalimie nione unapoishi wewe" alisema binti kisha akachukua kitambaa na kujifuta kidogo usoni

"nitajie tafadhali"

"Una pakuandika?" aliulizia

"wewe taja tu"

"Hee unaweza kushika kichwani kweli?" binti aliuliza

"We taja usiwaze" Tino alisema akiwa anatabasamu

"Haya, 0654433281" alitaja binti haraka haraka

"Poa" Tino aliongea binti akashtuka

"Tino, haupo serious kama hutaki namba yangu wewe sema wala sikulazimishi ah" binti alisema kwa hasira huku akiifunga pochi yake na kuondoka kwa hasira

"Vipi kwani Tina?" Jamaa aliita kwa mshangao

Tina alipoondoka alikuwa akifoka sana kwa hasira
"Mwanaume mwenyewe huna chochote halafu unaringa, unahisi mimi nakutaka au, yani mshenzi kweli mfyuuuu" aliondoka binti kwa hasira na kupanda bajaji huyo akasepa zake nyumbani. 

"Ehee niambie shogaangu" alisema Jane baada ya kumuona mwenzake "Haiwezekani Tina haiwezekani, yaani wewe umempenda masikini kama yule"

"nani kakuambia nimempenda na we mi silipendi lipumbavu lile, mwanaume gani hana hata nguo za kung'aa naweza kupiga naye hata picha kweli?" binti alisema huku akiwa anavua hereni zake akiwa bado ana hasira na Tino alivyomtambia kuandika namba yake

"umemuona lakini?" Jane aliuliza

"Usinitajie yule mpumbavu bwana taja watu wenye hela zao" Binti alisema kwa hasira

"Oooh ningesahau shoga, Mheshimiwa kanipigia anadai hupatikani eti kwenye voda" alisema Jane

"Aaaah Voda si imepotelea kwenye simu jamaani, ile mi nilisajili kwa kitambulisho cha mtu ndo maana nashindwa kurenew" alisema binti

"ahaa, nilimueleza kwamba umepoteza simu sasa kasema eti mkutane JingoMoja Hotel usiku wa leo" alisema Jane

"mmmmmh nitampiga kizinga atakoma" alisema Tina

"sasa unafikiri hatotaka mfanye"

"Hata akitaka ni kimoja tu si najua lizee lile haliwezi kunichosha mimi bado mbichi, embu hujapika shoga?" Tina aliuliza

"Nimepika mwaya check kwenye Hotpot, kitu kitamu we"

"Hahahaaaaa, nakukubal Baby Jane huuuu kelele ya kwanza kwa Shoga ake" waliongea maneno mengi huku wakiwa wananyoosha vidole vitatu juu si unajua waswahili tena

"wee" Jane alijibu wote wakacheka

**
Usiku saa nne kamili Tina alipanda gari na kwenda mpaka, JingoMoja Hoteli ikiwa ni bonge la hoteli mjini hapo. 

Binti alikuwa amependeza balaa, na leo alitakiwa kwenda kuonana na lizee liheshimiwa ambapo katika serikali hii alikwa ni Waziri wa sanaa na michezo, Mh Regnald Mwasoka Kalumbile

"Hey, 072" binti alikutana na wapambe wa muheshimiwa wakamuelekeza chumba cha kwenda kumkuta mheshimiwa kwa signal. 

Binti alienda moja kwa moja akaingia chumbani huko alikuwa ameandaliwa vizuri na alikuwa anahitajika amburudishe muheshimiwa kwa siku hiyo usiku kucha kwa bei ghali. 

Hizi ndo zilikuwa kazi za mabinti hawa wawili na ndizo ziliwaweka mjini, walifanya pia kazi ya kucheza video za mastaa mbali mbali hata kwenye wimbo wa Darassa uitwao Muziki walionekana.....ITAENDELEA

JE ITAKUWAJE UPANDE WA TINO? 

Post a Comment

Previous Post Next Post