🔐 MAUMIVU YA NDOA (36-----40) 😭😭😭😭


S2: EP 36
 
   Abdul alijikuta amelopoka na kumwambia Mkewe huku akiwa anamtazama na kumfanya Shaymaa abaki na mshangao

“Samahani sana Irina, ilikuwa ni salamu tu wala hakuna chochote kinachoendelea baina yetu”

Shaymaa aliongea na kutoa kiganja chake kwenye mkono wa Adul lakini Abdul aliendelea kuushikiria kwa nguvu na Shaymaa alimtazama jicho kali kabla ya kuuvuta mkono wake na kupiga hatua kadhaa “Naomba ukome kuwa karibu na Mume wangu” Irina aliongea na kumfanya Shaymaa asimame na kugeuka “Kumbe hata mwizi huwa ni muoga wa kuibiwa? Pole sana shost ila kuwa makini na Maganga atakuja kukuvunjia ndoa yako kuliko kuwa na hofu na Mimi”

Shaymaa aliongea na kuondoka kwa madaha huku akionekana mwenye furaha baada ya kuona Abdul na Irina walikuwa na mtafaruku baina yao.

Abdul aliwatazama kwa hasira Jack na Irina kiasi ambacho hata Jack alishindwa kumtazama Abdul na mara kadhaa alikuwa akitazama chini “Hivi nani Mume baina yenu? Siku zile uliponifanyia vulugu nyumbani kwangu ulikuwa unamtetea Mkeo au Mumeo? Ila unaonesh wewe ni Mume kwa maana hata muonekano wako siku zile ulionesha kuwa ulikuwa ni Mwanaume wa Irina”

Abdul aliongea kuwavuluga ili atazame mapokezi yao na Irina alijifanya kuchukizwa na jambo hilo huku akijifanya haelewi nini Mumewe anachoongea

“Hivi Abdul unaigiza kuchanganyikiwa ama una lengo la kunidharirisha?” Irina alimuuliza Abdul na kujifanya kachukizwa na hakutaka kusubiri majibu ya Mumewe na kumshika mkono rafiki yake na kumwambia waondoke zao
                              *****
Kauli ya Feisal ilikuwa imemchoma sana Mzee Mustapha na hakutaka kumtenga Hakeem japokuwa Mama yake alikuwa amekiri kuwa Hakeem si Mtoto wake wa kumzaa na Hakeem alimpiga Mzee Mustpaha baada ya kugundua ukweli

“Feisal wewe ni kijana Mdogo sana, fanya kazi bora utakuja kuonekana kuwa ni Mwanasheria mzuri sana. Wakati mwengine unapotaka kuonekana bora basi ni vyema ukajifunza kuchagua upande wenye haki”

Mzee Mustapha alimpiga dongo Feisal kisha alimgeukia Hakeem na kumwambia “Miaka yote umekuwa ukitambuwa kuwa Mimi ni Baba yako Mzazi naomba ibaki hivyo, Nimeshaandaa kila kitu na utaamishwa hospital ili ukatibiwe kwenye hospital maalum ambayo ni mabingwa katika swala zima la kuunganisha mifupa”

Hakeem alimshukuru sana Mzee Mustapha huku akimuita Baba “Wewe ni Baba yang utu, tafadhali naomba usiniache” Aliongea na Mzee Mustapha alimtoa hofu na kumuaga huku akimtakia siku njema na Feisal
                                ******
“Kuna Mtu amekuletea chakula” Askari alimwambia Madame na kumfanya ashangae mwenyewe “Mtu ameniletea chakula?” Aliongea huku akitabasam baada ya kusikia ameletewa chakula 

Ghafla alisimama na kubadilika sura baada ya kuona Mtu ambae amemletea chakula “Wewe Mtoto wa Shetani” Mdame aliongea kwa hasira huku akimtazama Mtu aliyekuwa amemletea chakula

Hakuwa mwengine alikuwa ni Shaymaa. Ndie aliyekuwa amekuja kumletea Chakula Mama yake wa kambo “Asia kwanini tunaitana majina machafu kiasi hicho” Shaymaa alimuita Madame kwa jina lake huku akiwa anamtazama kwa dharau kitu kilichomfanya Madame kuangua kicheko fulani cha kebehi 

“Mama yako alikufa kifo kibaya sana siku ya mwisho ya uzao wenu nyinyi Mijusi Mbwa” Madame aliongea huku akiwa ameuma meno yake na kauli hii kiasi fulani ilikuwa imemchukiza Shaymaa ila hakutaka kumuonesha Madame na badala yake alikuwa akitabasam tu ili kuficha udhaifu wake mbele ya adui wake

“Pole sana ila tambua kuwa hakuna damu ya Mtu inayoweza kumwagika pasipo malipo. Ulimuua Mama yangu, ukamuua Rayuu nab ado ukaendelea kufanya mauaji ya Liyuna na Mtoto wake. Haya yote ulifanya kwa tamaa zako za mali ambazo hautazipata hata kidogo” 
Shaymaa aliongea na Madame alishindwa kuvumilia na kujikuta akiuma meno kwa hasira na kumtimua Shaymaa na kugoma kula chakula chake “Umetumwa ili unilishe maneno nionekane kuwa niliwauwa? Nenda kamuulize vyema Baba yako ndio anajua alimuua na nini Mama yako”

Madame aliamua kumchonganisha Shaymaa na baba yake na Shaymaa alitambua hilo lakini alijikuta akijisikia vibaya sana jinsi Madame alivyokuwa anaongea bila wasiwasi “Hii kesi nitashinda ni nyepesi sana kwa upande wangu ila wewe na Baba yako ni lazima ndio mtakaonifanya niende jela” Madame aliongea na kuangua kicheko utafikiri Mtu aliyekuwa amechanganyikiwa 
                           ******

Baada ya Mzee Mustapha kuondoka. Hakeem alifuta machozi yake ya kinafki na kumshika mkono Feisal “Tafadhali naomba umsaidie Mama yangu, nitakulipa chochote endapo Mama yangu atafankiwa kushinda kesi hii” Hakeem aliongea na Feisal alimsahiisha katika hilo “Kwanini unasema nimsaidie Mama yako? Inamaana mpaka leo hautaki kuamini kuwa Mimi ni Kaka yako?”

“Samahani kwa hilo basi naomba ujitahidi kumsaidia Mama yetu ili aweze kushinda kesi hii, pia naomba usimwambie maneno machafu Mzee Mustapha mana Mimi nataka nikaanze kulipa kisasi nyumbani kwake. Maadu zetu wakuu ni Mzee Mustapha na Binti yake Shaymaa” Hakeem aliongea na katika hilo Feisal hakutaka kumuunga mkono hata kidogo

“Kwa mujibu wa Mama, Mimi na wewe Baba yetu ni mmoja hivyo maana yake Baba yetu ni Mzee Majaliwa na Shaymaa ni Dada yetu Binamu hupaswi kumchukia”

Feisal alimuelewesha Hakeem ambae alimuitikia mdomoni lakini moyoni alikuwa na kisasi na Shaymaa kwani aliona kama si yeye basi Mama yake hasingekuwa na hatia hivyo alikuwa amedhamilia kulipa kisasi juu yao
                             ******
Ilikuwa ni kazi ngumu kwa Jack kuweza kumnyamazisha Irina ambae alikuwa anaangua kilio baada ya kauli ya Abdul mbele ya Shaymaa na Abdul alionesha dhairi kuwa anajua kila kitu kuhusu yeye na Irina alikuwa anafanya siri iliyogharimu ndoa yake lakini leo katika mazingira rahisi Mumewe ameweza kugundua na kuonekana kama alikuwa na nia ya kutaka kumrejea Shaymaa kwa jinsi alivyokuwa amewaona walivyokumbatiana

“Hebu nyamaza kwanza alafu nenda nyumbani maana mimi bado nina majukumu ya kwenda kwa Hakeem pia Mama Mkwe ameniagiza niende kwenye nyumbani kwake kuna jambo nilifanye”

Jack aliongea lakin Irina aliendelea kusisitiza kumuomba msaada rafiki yake ili amsaidie katika hilo

“Ilikuaje mpaka Abdul amegundua kama Mimi na wewe zamani tulikuwa na tabia mbaya?” 

Irina alimueleza kila kitu shogaake mpaka jinsi alivyogundua kuwa Maganga aliwaona na kuamua kutembea nae ili kuficha siri yake na hapo ndipo aliposhika ujauzito wa Maganga

“Irina kiukweli Mimi sina cha kukusaidia, hata Mimi ndio ningekuwa Abdul basi nisingeweza kuvumilia Mke wangu azae na Mlinzi wangu. Kama unaweza nenda kamuombe radhi Mumeo ma wakati mwengine jifunze kutulia kwenye ndoa. Alafu Mimi sasahivi naangaika na Hakeem kwa maana hata wewe ukuwahi kuangaika na Mimi wakati nilivyotekwa na Hakeem”

Jack alingea na kumshangaza Irina ambae hakutegemea kama shogaake anaweza kumpa majibu kama hayo “Lakini si wewe ndie uliyenifundisha mchezo mbaya wa kufanaya mapenzi ya jinsia moja?” Irina aliongea kwa uchungu huku akiwa amemshikiria Jack

“Ni Mimi ndie niliekufundisha lakini Mimi siwezi kukubali Rafiki yangu aje kunivunjia ndoa yangu kizembe kama hivyo wewe pambana na hali yako. Abdul alikupa kila kitu lakini ulikuwa Mjinga wewe, Mwenzako nimejitambua sasa wala ushoga wa kipuuzi wa kudanganyana sihitaji hata kidogo. Nenda kamuombe radhi mumeo”

Jack aliongea na kuteremka kwenye gari na kumuacha Irina akiwa haamini kama angeweza kupewa majibu kama hayo
                             *****
“Nikutakie usiku mwema Mwanangu” Mzee Mustapha alimbusu Shaymaa katika paji lake la uso na kumuaga huku wote wakionekana na furaha isiyo kifani 

Baada ya kuagana na Baba yake, Shaymaa alijitupa kitandani huku akiwa mwenye furaha sana. Mawazo yake yalikuwa ni kwa Abdul na kwa jinsi alivyomuona Abdul alijua fika ndoa yake itakuwa na shaka tu

“Hebu subiri kwanza Shaymaa” Kama kawaida yake alianza kujiongeresha mwenyewe na kuonekana kushangazwa kidogo baada ya kukumbuka kauli ya Abdul aliyomwambia Irina 

 “Hili linakuuma? Unafikiri Mimi ni mpuuzi kama ufikiliavyo? Dhambi uliyotenda na Maganga nadhani haikubaliki zaidi kijamii kuliko hili uliloliona hapa”

Ilikuwa ni kauli ya Abdul aliyomwambia Irina muda mfupi baada ya Irina kumlaumu Abdul baada ya kumkuta amekumbatiana na Shaymaa

“HIvi ni Maganga gani waliyokuwa wanamaanisha? Au Maganga yule aliyekuwa Mlinzi wetu?”

Shaymaa aliongea mwenyewe na kujikuta kifuraishwa kidogo na jambo hilo “Abdul bila shaka utakuwa umepata aina ya Mwanamke uliyekuwa unamuhitaji”

Shaymaa aliongea mwenyewe akionekana kuwa na furaha kwa kile ambacho alikuwa amekishuudia baina ya Abdul na Mkewe jinsi walivyokuwa wanaumizana
                         *****
Saa saba na nusu usiku, mshale wa saa ya ukutani ulikuwa ukisoma hivyo na Abdul alikuwa bado hajarejea nyumbani. Usingizi ulikuwa haupatikani kwa Irina na alikuwa akitafakari ni vipi anaweza kuja kumjibu Mumewe

Ghafla mango ulifunguliwa na Abdul alikuwa amelewa chakali, Irina alimsogelea ili akampokee lakini alirudishwa na kibao kimoja matata kilichomfanya apepesuke na kama si kujizuia kwenye ukuta alikuwa najipigiza vibaya na tumbo lake

“Kabla sijakuuwa, naomba uniambie hilo kinda ambalo lipo tumboni kwako ni la nani?” Abdul alichomoa bastola na kumshikia Mkewe

“Nakueleza kila kitu Mume wangu” Irina aliongea haraka na kupiga magoti “Kusema ukweli Mimi Mke wako ni msaliti, hii mimba si yako ni ya Maganga nisamehe sana Mume wangu…………………”

NINI KITAENDELEA? USIKOSE EPISODE YA 37 
MAUMIVU YA NDOA 
S2: EP 37
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Irina aliendela kuongea mfululizo akimuomba msamaha Abdul, lakini ghafla alihisi kitu na kuamua kunyamaza akimtazama Abdul

“Mume wangu!! Abdul!!” Irina alijaribu kumuita Abdul kumbe wapi mwenzake muda mrefu alikuwa ameshaangusha gari.

Alishusha pumzi na kuanza kutafakari mwenyewe “Abdul leo ameamua kunitolea bastola? Inamaana ameshaujua ukweli wote?” Irina alijiuliza mwenyewe pasipo kujua nini afanye kwa wakati huo
                              ******
“Hivi wewe umechanganyikiwa? Yani kwa kipi haswa kikubwa alichokufanyia mpaka wewe unaamua kwenda kusimama kuwa Mwanasheria wake?”

Pili alichukizwa na kumsema Mumewe baada ya Feisal kumwambia ukweli kuwa ameamua kuwa Mwanasheria wa Madame ili kumsaidia kushinda kesi iliyokua inamkabiri

“Najua inaweza kuwa ngumu ka wewe kuweza kunielea. Lakini nimekaa na kujishauri mwenyewe na katika hili kwa kweli wala sihitaji ushauri”

Feisal aliendelea kushikiria msimamo wake huku akwa anaweka sawa baadhi ya nyaraka zake ambazo aliona zitakuwa Masada katika kesi aliyokuwa anaenda kuisimamia

“Hata kama Mume wangu!! Hivi Madame ana jambo gani jema kwako ambalo amewahi kukufanyia kiasi ambacho unaweza kujivunia?”

Pili alimuuliza Mumewe ambae hakuwa na hoja ya maana katika kumjibu Mkewe na kendelea kuwa na msimamo wake kuwa yeye ameona ni bora hawe upande wa Mama yake na tofauti na hapo hakuwa na majibu mengine
                            *****
Kwa kushirikiana na Oliver Irina alifanikiwa kumpandisha kitandani Mumewe ambae alikuwa hajitambui hata kidogo kutokana na pombe ambazo aliyokuwa amekunywa kwa siku hiyo.

“Wewe kuna jambo nataka nikuulizie” Irina alimuita Oliver huku akiwa anamtazama kwa dharau

Oliver alisimama na kugeuka huku akionesha dhairi na jinsi ambavyo Irina alivyomuita “Kwanini unanitazama hivyo? Mimi na wewe tunachangia Mume au Mimi ni Boss wako?” “Heshima umfuata yule mwenye kujiheshimu kwanza, huwezi kuniita wewe utafikiri Mimi Mbwa wako” Oliver alimjibu pasipo kumuogopa

“Unaweza kuniambia Abdul alifuata nini mule chumbani kwako?” Irina alimuuliza na Oliver aliamua kutumia fursa hiyo ili kumuumiza moyo “Alisema kuna barua ambayo Maganga alimuandikia kuhusu mahusiano yenu wewe na Maganga. Hivyo alienda kuitafuta na alipoipata aliamua kuondoka”

Oliver aliongea na safari hii Irina alishindwa kuwa kiburi mbele ya Oliver na bila kutarajia alijikuta akikosa hata nguvu ya kumfanya asimame na kuonesha dhiaka mbele ya mwenzake

Taratibu Irina alijikokota mpaka kwenye kitanda na kujikuta akimtazama Mumewe na kujikuta akijilaumu mwenyewe. 
                          *****
Shaymaa akiwa mwenye furaha, ghafla alisikia mlango wake ukigongwa na Mtu akiwa anabisha hodi. Aliinuka na kwenda kufungua mlango 

“Baba alikuwa anaomba kukuona” Alikuwa ni kijakazi ndie aliyekujakumgongea na kumpa taharifa hiyo
Hakuweza kupinga hilo, alijiandaa na kwenda kuonana na Baba yake ambae siku hiyo alionekana kuwa tulivu tofauti na siku zote.

“Baba hupo sawa lakini?” Shaymaa alimuuliza Baba yake baada ya kumuona yupo tofauti na jinsi alivyokuwa amemzoea

“Sipo sawa ila ni wewe ndie utakae weza kunifanya niwe sawa Binti yangu” Mzee Mustapha aliongea na kutulia kidogo akimtazama Binti yake huku Shaymaa akiwa makini kumsikiliza

“Hupo tayari kunikata kiu yangu Mwanangu?” Mzee Mustapha aliongea na kumstua Shaymaa na kumfanya amuulize ni kiu gani iliyokuwa inamsumbua 

“Kuna mambo mawili ningependa nikuombe na kama utanikubalia basi nitakupa zawadi kubwa mno” 

Mzee Mustapha aliongea na safari hii walau kidogo aliweza kuonesha tabasama “Sikuwahi kutamani kupata mjukuukutoka kwa Hakeem, na inawezekana moyo wangu ulikuwa mgumu kufungua ili labda tu kwakuwa Hakeem hakuwa damu yangu. Lakini kwako nimejikuta nikitamani kupata mjukuu Mwanangu na kama hutojali ningependa kukuona ukiolewa”

Mzee Mustapha aliongea na kumfanya Shaymaa afurahi kuona Baba yake anatamani kumuona akiolewa na kupata Mtoto “Mimi pia natamani Baba hivyo wala usijali kwani karibuni Mimi na Mume wangu tutarejeana tena”

Shaymaa aliongea na kumstua Mzee Mustapha baada ya kusikia Shaymaa anataka kurejeana na Abdul 

“Mwanaume aliyekutesa kiasi ambacho ulitaka kujiuwa unawezaje kukubali kurudi katika himaya yake upya?”
“Ilikuwa zamani Baba na inawezekana Malaika alisimamia ili walau nipata kukujua Baba yangu ila kwasasa Abdul amebadilika na kuwa kijana mpya kabisa”

Shaymaa aliongea na Baba yake na kummwagia sifa Abdul na hakuona shida kumulekeza Baba yake Abdul, ambae alikuwa ni Mwanaume wake na Mzee Mustapha baada ya kugundua kuwa Abdul mwenyewe ndie yule kijana mpelelezi aliyefanikisha kukamatwa kwa Madame akishirikiana na kina Othman. Mzee Mustapha alifurahi na kumtakia kila la kheri Mwanae.

Jambo la pili ambalo Mzee Mustapha alimuomba Binti yake ilikuwa ni kumtaka akubali ombi lake la kuwa Mmoja kati ya wakurugenzi wanaosimama kampuni yake na Shaymaa alitafakari kidogo kabla ya kukubali ombi la Baba yake na kumfanya Mzee Mustapha afurahi na kumuahidi mwanae kuwa kesho atamtambulisha binti yake kwenye kampuni na kumfanya ashike majukumu yake haraka hiwezekanavyo.
                                *****
usingizi ulikuwa haupatikani kwa Irina na muda wote alikuwa akitafakari ni vipi anaweza kuuficha ukweli ambao ulikuwa unakaribia kuivunja ndoa yake.

“Mimi ni Mwanamke mpumbavu sana” Hiyo ndio kauli ambayo aliweza kuitoa katika kinywa chake na kumfanya ajikute akiangua kilio

Kitendo cha kushika mimba ya Maganga kilikuwa kinamuumiza sana, lakini si kuzaa na Maganga tu bali kitu kibaya zaidi ni kuzaa na Mwanaume mwengine wakati akiwa katika ndoa yake

“Nitaweza kuja kumwambia Mtoto wangu kuwa Mimi ni Mama bora kwake wakati najua fika dhambi ya usaliti itakuwa inautafuna moyo wangu?” 

Yupo wapi Mtu aliyesema fikiri kabla ya kutenda? Hivi alitufundisha tufikiri kabla ya kutenda au tufikiri kabla ya kufikiri kutenda? 

Irina alijikuta akijuta kwa yote aliyokuwa ameyafanya, alitamani siku zirudi nyuma ili aweze kurekebisha baadhi ya mambo lakini wapi, alikuwa ameshachelewa kufanya hivyo kwani wakati huu alikuwa anaitaji muujiza zaidi kuweza kuinusuru ndoa yake
                            ******
Baada ya kutafakari sana Irina aliona ana kila sababu ya kuweza kuinusuru ndoa yake kabla haijaingia mchanga zaidi

Alidamka asubuhi na mapema huku akiwa anatafakari ni kitu gani anaweza kufanya ili kuinusuru ndoa yake

“Samahani kwa usumbufu, nimesikia matatizo yako kuhusu Mumeo. Jina langu naitwa Chausiku, Mimi ni Mpangaji wa Mama Jack lakini naweza kukusaidia kama hautojali”

Alikumbuka kauli ya Chausiku Mdada aliyekutana nae nyumbani kwa kina Jack ambae alionesha dhairi alitaka kumsaidia baada ya kugundua kuwa anamatatizo katika ndoa yake 

“Nina mganga wangu huyu anaitwa Babu kigozi, yani huyo kama Mwanaume anakusumbua ana uwezo wa kumtuliza na asifurukute hata kidogo, chochote usemacho wewe ni sawa”
Aliendelea kukumbuka kauli za Chausiku na hapo aliona alikuwa ni mjinga kupoteza kwa makusudi namba zake

“Samahani sana Abdul, lazima nikuloge ili nimalize hili tatizo kwa sababu siwezi kukubali kuachika na fedhea ya namna hii”

Irina aliongea na kumtazama Abdul aliyekuwa bado anachapa usingizi.

Njia nyepesi ya kumpata Chausiku ilikuwa ni kwenda kwa kina Jack, japokuwa alikuwa amegombana na Jack, lakini hakutaka kujali sana kuhusu hilo na aliamua kuingia kwenye gari na kuelekea nyumbani kwa kina Jack
                              *****

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa Shaymaa kuweza kukubaliwa na Baba yake ili aolewe na Adul.

Alichukua simu yake na kumpigia Abdul ili amuombe kama anaweza kumsindikiza kwenye hafla yake ya kutambulishwa kwenye kampuni lakini kwa bahati mbaya Abdul hakuweza kupokea simu ya Shaymaa.

“Mpuuzi sana wewe Mwanaume yani ukiwa na huyu Mwanamke wako ni ngumukupokea simu yangu eeeh?” Shaymaa aliongea mwenyewe na kukata simu kabla ya kuwasha gari yake na kuelekea ofisini kwa Baba yake
                           ******
Abdul hakuwa amelewa kama ambavyo Mkewe alivyokuwa amefikiria bali alichokuwa amekifanya ni kumuigizia Mkewe ili aweze kuuupata ukweli juu ya mimba ya Irina

Ilimuuma sana baada ya kugundua Mke wake ni kweli ana Mimba ya Mwananume mwengine.

“Samahani sana Shaymaa” Abdul aliongea mwenyewe baada ya kuona alikuwa amemkosea Shaymaa

Katika hilo wala hakuitaji ushauri wa Mtu. Alichukua tape recorder yake ambayo aliitegesha ili kunasa maongezi ya Mkewe na kuirejea kila wakati ili asikilize yale maneno aliyokuwa anaongea Mke wake kipindi kile alichokuwa amemuigizia kuwa amelewa

Alichukua peni na karatasi na kumuandikia Irina Talaka tatu bila kusita na kujutia maamuzi yake ya hapo hawali ya kumuacha Mke wake “Nilikosea sana kukuoa wewe Shetani……………

NINI KITAENDELEA? ABDUL AMESHATOA TALAKA KWA AJIILI YA IRINA NA WAKATI HUO IRINA ANAENDA KWA CHAUSIKU KWENDA KUMLOGA ABDUL

VIPI KUHUSU MADAME NA WATU WAKE? USIKOSE EPISODE IJAYO 
MAUMIVU YA NDOA 
S2: EP 38
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Yalikuwa ni maamuzi magumu ambayo Abdul aliamua kuyachukua lakini hakuwa na jinsi, aliona hiyo ndio zawadi pekee ambayo Irina alikuwa anastahili kupewa, baada ya kumbebea mimba ya Mwanaume mwengine tena akifanya uchafu huo katika kitanda chake

“Wapi nitaficha sura yangu?” Abdul aliongea mwenyewe huku akionekana kuchanganyikiwa zaidi “Shaymaa najua nimekupoteza kwa upuuzi wangu. Shaymaa mpende sana Mwanaume ambae umeamua kumkabidhi moyo wako mana Mimi ni Mwanaume mjinga sana” Abdul aliongea mwenyewe huku akiwa anakunywa pombe mfululizo
                            ******
“Nakuchukia sana wewe motto uliye kwenye tumbo langu” Irina aliongea mwenyewe huku akiwa anaendesha gari kuelekea nyumbani kwa kina Jack ambapo alikuwa amepanga kwenda kuonana na Chausiku ili ampeleke kwa Mganga wa kienyeji kwenda kumloga Abdul ili amfanye hawe zuzu mbele yake na hasiwaze chochote kuhusu mimba iliyokuwa tumboni mwake.

Aliffanikiwa kufika nyumbani kwa kina Jack na kuegesha gari yake vyema na kama bahati ilikuwa upande wake kwani Chausiku pia alikuwa nje anachezea simu yake ya mkononi

Chausiku alimpokea vyema Irina kwa tabasam la hali ya juu na kumkumbatia utafikiri walikuwa wanajuana zaidi “Shogaangu nataka unipeleke kule…………” Irina aliongea na Chausiku alimkatisha kwa ishara akimaanisha anyamaze na kumuoneshea ishara Mwanaume aliyekuwa pembeni anafua

“Mume wangu huyo, si unamuona? Huyo hapindui kitu mbele yangu anafanya nitakalo Mimi na zamani alikuwa na mdomo kweli” 

Chausiku aliongea na kumuonesha kwa vitendo Irina kuwa anachokiongea ni kutu cha kweli kwanii hata yeye amefanikiwa katika hilo.

Kiasi fulani Irina alihisi kupata faraja katika moyo wake kwani aliona kama amepata mkombozi wa matatizo yake

“Chausiku, nikifanikiwa jambo langu nitakupa zawadi kubwa mno, tafadhali naomba msaada wako nifanikiwe katika hili” Irina aliongea na Chausiku alitabasam na kumtoa hofu kuwa hasijali kwenye hilo

“Lakini mbona haujanipigia simu kabla?” Chausiku alimuuliza Irina ambae alikosa majibu ya kumjibu lakini alijitahidi na kumdanganya kuwa namba alisave vibaya kwenye simu hivyo ilipotea
                          *******
Baada ya jarada la kesi la Madame kuweza kukamlika, Madame alipelekwa mahakamani kwenda kusomewa kesi iliyokuwa inamkabiri yeye na Viajana wake.

Alisomewa Mashitaka yake na Madame alikata rufaha juu ya kesi yake na kutaka ipelekwe kwenye mahakama kubwa zaidi ambayo aliona ndio ilikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi yake.

Rufaa yao ilisikilizwa na kesi ilisogezwa mbele ili kusikilizwa kwenye mahakama ambayo ilikuwa na uwezo zaidi
                            ******
Abdul aliwaza sana na kuwazua juu ya kile kilichokuwa kimemkuta. Aliona aibu kwa maamuzi aliyofanya ya kumuoa Irina na alijiona ni Binaadam asiye na faida katika ulimwengu huu.

Kitu pekee ambacho aliona anapaswa ni kujiuwa ili kukwepa aibu ambayo ilikuwa inamkabiri “Amina anajua kama Mke wangu katiwa mimba na Maganga, lakini hata Oliver Mlinzi wangu wa hapa nyumbani nae anajua kila kitu kuhusu Mimi” Abdul alizidi kujiuliza maswali na kuona dhairi kuwa jambo lake litaenea taratibu na mwishowe itakuwa fedhea kwake.

Alitazama tala aliyokuwa amemuandikia Irina na kujipongeza kwa kile alichokuwa amekiamua “Nimefanya maamuzi sahihi sana, Kabla sijafa Irina anapaswa kupata talaka. Siwezi kufa alafu niendelee kumuacha Irina hawe Mwanamke wangu”

Abdul aliongea huku akiwa anaitazama ile talaka aliyokuwa ameandika kwa ajili ya Irina kisha akachukua karatasi nyingine na kuanza kuandika barua kwa niaba ya kumuomba msamaha Shaymaa kwa kile alichokuwa amemfanyia katika kipindi chote ambacho alikuwa anemuoa na kumfanyia maovu.

“Shaymaa wewe ni Mwanamke mwema ambae ulilipwa uovu kwa upendo wako wa dhati dhidi yangu. Nakumbuka jinsi ulivyokuwa umejitoa kwa ajili yangu alafu heti mpuuzi mmoja kama Mimi nikawa nauchoma moyo wako. Ujinga wangu umenifanya nitambue thamani yako baada ya kuachana na wewe wakati nilipaswa nitambue hilo na nikulipe mapenzi ya dhati”

Abdul aliandika barua huku machozi yakiwa yanatiririka katika paji lake la uso utafikiri hakuwa Mtoto wa kiume.

Kuna wakati mapenzi yanaweza kukupa furaha na kuna wakati unaweza kuumia kwa sababu ya mapenzi. Leo hii Abdul alionja radha ya kumuumiza Mtu kwenye mapenzi na kupima yale ambayo aliyokuwa anamtendea Shaymaa na kugundua kuwa alikuwa anamkosea sana Mtoto wa watu.
                             ******
Halikuwa jambo dogo kama ambavyo Shaymaa alivyokuwa anafikiria kuhusu kutambulishwa katika kampuni na kupewa majukumu yake kama Mkurugenzi mpaya wa kampuni ya Baba yake.

Mzee Mustapha alikuwa ameandaa tafrija fupi iliyokuwa imewakutanisha wafanya kazi wa kampuni na baadhi ya watu mashughuli katika Nchii hii ili kumkaribisha Mtoto pekee wa Mzee Mustapha katika majukumu mapya.

Mzee Mustapha aliitazama saa yake ya mkononi na kuona Shaymaa ameshindwa kabisa na wakati kama ambavyo yeye kama Baba yake alikuwa amempangia “Naomba tumuongeze nusu saa itakuwa amepata dharula siyo kawaida yake” 

Mzee Mustapha alimwambia Mshereheshaji na bila kusita alifuata agizo la mzee na kuomba radhi wageni waalikwa.

Mzee Mustapha alichukua simu yake ya mkononi na kujaribu kumpigia Shaymaa lakini simu ya Shaymaa haikupokelewa na kuzidi kumtia hofu na mashaka Mzee Mustapha
                        ***** 
Ghafla tu Shaymaa alikosa nguvu ya kuendesha gari na kujikuta akiegesha gari yake pembeni huku akionekana kuwaza sana kiasi ambacho moyo wake ulikuwa ukienda mbio mno

Simu yake iliita na aliichukua na kuitazama, aliona ni Baba yake ndie aliyekuwa akimpigia simu “Kwanini moyo wangu unasita kwenda huko?” Shaymaa aliongea mwenyewe kabla ya kutupa simu kwenye siti ya na kuendelea kutazama Baba yake akiwa anapiga simu

“Samahai Baba” Shyamaa aliongea baada ya kukata shauri na kugeuza gari na kuelekea sehemu ambayo aliona kwake ni sahihi kwa wakati huo
                           *******
Irina na Chausiku waliongozana mpaka kwa Mganga wa kienyeji ili kwenda kumloga Abdul ili atulie na kuikubali mimba ya Irina bila kasumba yoyote.

“Jambo dogo sana hilo” Mganga wa kienyeji aliongea na kuangua kicheko ambacho kilimstua na kumuogopesha Irina
“Nitafanya kila kitu na Mwanaume wako atakuwa mpole na kukusikiliza kwa kila kile utakachotaka wewe, cha msingi unapaswa kumuwekea dawa kwenye chakula utakachokuwa unamuandalia kwa muda wa siku saba” Mganga aliongea na Irina alikuwa makini kusikiliza huku Chausiku akiwa anachombeza na kumuuliza baadhi ya maswali Mganga akitaka kujua Rafiki yake anawezaje kumaliza jambo hilo

“Fanya kila nilitakachokueleza na baada ya siku saba utakuwa umepata mafanikio yako”

Mganga aliongea na kutaka malipo ya milioni moja kwa ajili ya kazi ambayo ameifanya na Irina hakutaka kusita kwani alichokuwa anafikiria kwenye akili yake ni Abdul wake tu na swala la pesa halikuwa tatizo kwa upande wake.

Baada ya kumpatia pesa Mganga wa kienyeji, Mganga aliendelea kutoa dawa nyingine ambazo Irina alipaswa kuzifanya “Unapaswa kwenda kuvunja nazi katikati ya Mji ili kumaliza midomo ya Watu wote”

Mganga aliongea na hilo lilikuwa ni jambo gumu kwa Irina kuweza kulifanya na aliambiwa alipie laki mbili ili Mtu afanye kwa niaba yake. Irina hakuwa na ubishi katika hlo, alitoa pesa kumkabidhi Mganga kwani alichokuwa anakitaka ni Mume wake kuwa mpole katika mimba aliyokuwa ameibeba na kumfanya hawe mpole mbele yake
                          ******
Ilikuwa ngumu kuweza kujielewa kwanini aliamua kufanya maamuzi hayo, lakini kwa mara ya kwanza Shaymaa alijikuta anakanyaga mafuta kuelekea nyumbani kwa Abdul ili angalau apate kumuona na ikiwezekana amsindikize kuelekea kwenye tafrija aliyokuwa ameandaliwa na Baba yake

Ilimchukue dakika kadhaa mpaka kufika nyumbani kwa Abdul na kuegesha gari yake nje na kuonekana akitafakari mwenyewe.

“Nitamdanganya kuwa Baba amenituma nije kumuomba nimsindikize” Shaymaa aliongea mwenyewe na kutabasam kabla ya kushuka kwenye gari yake na kubisha hodi

Oliver alifungua geti na kuonana na Shaymaa ambaye alijitambulisha jina lake na kumuuliza kama amemkuta Abdul.

Jina la Shaymaa halikuwa geni masikioni mwa Oliver, hivyo alipomuona alijikuta akifurahi na kumpokea kwa heshima zote

“Kaka Abdul yupo ndani wala hajatoka leo” Oliver alijibu na Shaymaa alitaka kujua kama Irina yupo lakini Oliver alimjibu kuwa ametoka mapema sana na hakuaga ni wapi alipokuwa anaenda

Shaymaa alishukuru na kufurahi baada ya kusikia Irina hayupo. Aliingia ndani kwa Abdul huku akiwa na kumbukumbu ya mara ya mwisho alipoondoka katika nyumba hiyo.

“Abduuuuuuuuuuuuuuul” Shaymaa alipiga yowe baada ya kumkuta Abdul akiwa chini huku akiwa anatokwa na povu. Alimkimbilia na kumjaribu kumuamsha lakini wapi, hali ya Abdul ilikuwa mbaya sana

Oliver aliweza kusikia kelele ya Shaymaa na kukimbilia ndani na yeye kupatwa na mstuko baada ya kumkuta Boss wake akiwa katika hali mbaya “Amekunywa sumu” Shaymaa aliongea baada ya kuona chupa ya sumu iliyokuwa pembeni ambayo Abdul alikuwa ameifakamia……………

NINI KITAENDELEA? USIKOSE EPIOSODE IJAYO

MAUMIVU YA NDOA 
S2: EP 39
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Kuna msemo wa kiingereza unaosema “Love is like the wind, you can’t see it but you can feel it.” ”Yani Upendo ni kama upepo hauwezi kuuona lakini unaweza kuusikia”

Mara nyingi huwa inakuwa hivyo, unaweza kujizuia usifanye ngono lakini ni ngumu kujizuia usipende endapo moyo utakuwa umetekwa na bahari ya upendo na kumpata yule ambae moyo unaweza kumpenda kwa dhati

Moyo una nguvu kubwa sana katika mwili wa Binaadamu, kuna wakati moyo unaweza kuizidi hata akili yako endapo tu moyo utakuwa umependa kwa dhati. Unapaswa kutumia akili zaidi kuushawishi moyo kubadili maamuzi la sivyo akili yako inaweza ikawa inaendeshwa zaidi na moyo wako, na utakapofika hatua hiyo inakuwa ni ngumu kwa wewe kushaurika.

Akili ya Shaymaa ilikuwa inamtuma kwenda katika hafla maalum iliyokuwa imeandaliwa na Baba yake na kukabidhiwa majukumu mapya kama Mkurugenzi wa kampuni. Lakini Moyo wake ulikuwa na msimamo mwengine tofauti na akili yake ilivyokuwa inataka.

Ilimchukua dakika kadhaa kutafakari aamue nini kwa wakati huo kabla ya kufikia maamuzi ya kwenda nyumbani kwa Abdul pasipo kujali nini kinaweza kutokea baina yake yeye na Irina, baada ya kumuona Shaymaa amekuja kumtembelea Mwanaume ambaye sasa ni Mumewe yeye. 

Unapompeda Mtu kwa dhati basi ni rahaisi kuweza kushiriki baadhi ya matukio yake ambayo yanakuwa yanamtokea. Watu wa zamani walikuwa wanajua hili, na ilikuwa ni rahisi kuweza kutambua nini kimemkuta Mkewe/Mumewe hata kama yupo mbali nae kutokana na utambuzi sahihi wa moyo wake. Kwani kwao ilikuwa ni rahisi sana kutambua hilo kutokana na kufutailia zaidi mapigo ya mapigo yao ya moyo yatakavyokuwa yanadunda kulingana na baadhi ya matukio yatakayokuwa yanatokea

Shaymaa alifika mpaka nyumbani kwa Abdul na kujikuta akitabasam baada ya kuiona tena nyumba ambayo alikuwa akiishi na Mwanaume aliyekuwa amempenda kwa dhati. 

Japokuwa alitabasam mdomoni lakini moyo wake bado ulikuwa na hofu kubwa juu ya Abdul na alishindwa kabisa kutambua kipi kimetokea katika moyo wake kwani ilikuwa tofauti na jinsi anavyojitambua.

Alishuka katika gari yake na kusalimiana na Oliver kisha akajitambulisha na Oliver aliweza kumtambua haraka kwani jina lake halikuwa geni masikioni mwake, kwani alishawahi kuongea na Amina kuhusu Shaymaa Mwanamke aliyekuwa Mke wa zamani wa Abdul, na Amina aliwahi kumwagia sifa Shaymaa kwa upendo wake kwa Abdul na ukarim wake tofauti na Irina

Shaymaa alimuulizia Oliver kuhusu Abdul na Irina lakini alijibiwa kuwa Irina hayupo na Abdul alikuwa bado amelala. Kauli hiyo ilimpa hauweni kiasi na kuhisi moyo wake walau umepunguza kupatwa mshituko baada ya kusikia Abdul yupo ndani na mbaya wake alikuwa ametoka

Baada ya kusalimiana na Oliver, Shaymaa aliingia ndani na kustushwa na kile alichokuwa amekikuta ndani kwa Abdul

“Abduuuuuuuuuuuuuuul” Shaymaa alipiga yowe baada ya kumkuta Abdul akiwa chini huku akiwa anatokwa na povu. Alimkimbilia na kumjaribu kumuamsha lakini wapi, hali ya Abdul ilikuwa mbaya sana

Oliver aliweza kusikia kelele ya Shaymaa na kukimbilia ndani na yeye kupatwa na mstuko baada ya kumkuta Boss wake akiwa katika hali mbaya “Anaonekana atakuwa amekunywa sumu” Shaymaa aliongea baada ya kuona chupa ya sumu iliyokuwa pembeni ambayo Abdul alikuwa ameifakamia kabla ya Shaymaa kuingia humo
                              ******
Tofauti ya Irina na Shaymaa kwa Abdul ilikuwa ni kubwa mno. Wakati yote yakiwa yanaendelea mpaka Abdul anaamua kuandika talaka na kunywa sumu ili kukwepa aibu ya kubambikiwa mimba na Mkewe kiasi ambacho Shaymaa alipata ishara maalumu kupitia moyo wake na kuamua kwenda kwa Abdul.

Irina hakupata hisia yoyote na alichokuwa anasubiri yeye ni kupata tiba maalum ya kumfanya Abdul hawe zuzu mbele yake na hasiulize chochote kuhusu mimba yake na ikiwezekana ampelekeshe vile atakavyo “Ama kweli kosea njia usikosee kuowa au kuolewa”

Baada ya kukabidhi pesa, Irina alitakiwa kufanyiwa dawa maalum ambayo ingeweza kumfanya Abdul amsikilize kila kitu Mkewe pasipo kupinga chochote “Unapaswa kuvua nguo zote na utavaa hilo shuka” Mganga aliongea na kumtupia shuka jeupe Irina ambae alibaki ameduwaa na kumtazama Chausiku

“Unapaswa kufanya hivyo shogaangu, naamini ukitoka hapa wewe mwenyewe utafurahi” Chausiku alichombeza na Irina aliinuka na kuelekea kwenye chumba maalum ambacho alielekezwa kinafaa kubadilishia nguo huku akionekana mwenye wasiwasi

Alivua nguo zote zilizokuwa katika mwili wake mpaka ile nguo ya mwisho kabisa na kubaki kama alivyozaliwa na kabla hajavaa lile shuka ambalo aliambiwa anapaswa kulivaa alisikia mlango unafunguliwa na Mganga aliingia huku na yeye akiwa amevua nguo na kuwa kama alivyozaliwa.

Irina alistuka na kuokota shuka haraka na kuuziba mwili wake na kupiga kelele za kuogopa “Umefuata nini huku?” Irina alihamaki na kumbatiza Mganga huku akiwa anamtazama

“Ni lazima uingiliwe na kiti wetu. Mwanaume analogwa kwa kupitia Mwanaume mwenzie. Lazima Kiti ale chakula cha Mumeo na baada ya hapo Mumeo anapaswa kula chakula chake bila wewe kuoga au kujimwagia maji tofauti na dawa hii ambayo utaogeshwa hapa”

Mganga aliongea huku sauti yake ikiwa tofauti na ile aliyokuwa anongea hapo kabla.

“Hapana siwezi kufanya hivyo naomba utoke kabla sijapiga kelele zaidi na kujaza watu hapa” Irina aliongea kwa sauti na Mganga alizidi kumsisitiza ni lazima amkaribishe kula chakula cha Mumewe la sivyo hatoweza kumtuliza Mumewe kama anavyotaka

Baada ya mabishano ya dakika kadhaa Chausiku alisikia na kuingia kule kwenye chumba maalum ambacho Irina alikuwa ameambiwa akabadili nguo na Mganga aliingia ili kutaka kumuingilia

“Chausiku! Tiba gani hii ambayo Mganga wako anataka kunifanyia?” Irina aliongea lakini alishangazwa baada ya kuona Chausiku kupnekana kutoshtushwa na jambo hilo, lakini pia hata Mganga wala hakutaka kuuficha Mmea uliokuwa umeota shambani kwake baada ya kuingia Chausiku na ilionesha dhairi kuwa ilikuwa ni kawaida yake na Chausiku anajua hilo

“Dada wala hupaswi kupiga kelele, huyu wala hafanyi yeye ila hiyo ni moja ya tiba zake, akishamaliza kukiingilia ndio tiba yenyewe” Chausiku aliongea huku akimtazama Irina aliyekuwa ameuma meno yake kwa hasira akiwatazama kwa zamu Mganga na Chausiku

“Inamaana hana tiba nyingine zaidi ya kuniingilia kimwili?” Irina aliuliza na Chausiku alimjibu kuwa ni lazima amuingilie kwani hata yeye aliingiliwa ndio akafanikiwa kile alichokuwa amekitaka.

Chozi la uchungu lilitiririka kutoka katika mboni ya Irina na swali kubwa ambalo lilikuwa katika kichwa chake ni nini afanye kwa wakati huo? Agome na kuondoka zake au akubali kuingiliwa na Mganga ili amzibiti Abdul wake ambae alina dhairi anaenda kumpoteza

Kuna mambo ukiyaruhusu katika maisha yako basi unaweza kufanyiwa udhalilishaji wa ajabu sana ambao unaweza usione madhara yake lakini wengi wao ujutia baada ya kukubali kufanya upuuzi kama huu ambao alikuwa anataka kufanyiwa Irina.

“Tafadhali naomba usinifanyie hivyo, matatizo yangu yasiwe fursa ya wewe kunidhalilisha ki jinsia” Irina alimuomba Mganga na kumfanya Mganga achukizwe kwa kitendo icho na kumtaka Irina avae nguo zake na kuondoka zake kisha Mganga alitoka nje na kumuacha Irina akiwa na Chausiku wakitazamana huku Irina akiwa analia kilio cha kwikwi

Chausiku alitumia kipawa alicho nacho kumshawishi Irina ili akubali huku akimuakikishia kuwa kama atafanikiwa kuingiliwa na Mganga basi kila kitu chake kitakuwa kimeenda poa na hatojuta kufanya hivyo kwani hata yeye aliogopa hivyo hivyo ila baada ya kutembea na Mganga alipata mabadiliko na hajawahi kusumbuliwa na Mume wake tena.
                               ******
Katika vitu ambavyo hakupenda kuona inatokea ni kumuona Abdul anakufa katika mikono yake “Abdul inamaana moyo wangu ulinisukuma nije kwako ili nikuone jinsi unavyaga Dunia?” Shaymaa aliongea huku akiwa analia na wakijitahidi kumpa maziwa

Baada ya kufanikiwa kumpa huduma ya kwanza Abdul, Shaymaa na Oliver walimpakia Abdul katika gari ya Shaymaa ili kumkimbiza hospital

Wakati gari ya Shaymaa inatoka kwa kasi, Irina nae alikuwa ndio anafika nyumbani. Alishangazwa kumuona Oliver anamalizia kufunga geti na kukimbilia gari ya Shaymaa na wanatoka kwa kasi utafikiri kuna tukio la ujambazi limefanyika

“Kitu gani wameiba hawa wapuuzi?” Alijiuliza mwenyewe na kutopata jibu. Hakuitaji kupata muda zaidi ili kuweza kutafakari hilo alikanyaga mafuta na kuanza kulifukuzia gari la Shaymaa ili awazuie na kukagua ajue ni kitu gani walikuwa wameiba nyumbani kwake.

Oliver ndie aliyekuwa anaendesha gari ya Shaymaa huku Shyamaa akiwa amemkumbatia Abdul huku akiwa analia kama Mtoto mdogo na alikuwa akimuomba Abdul hasife kwani kuna jambo alikuwa anataka kumwambia

“Abdul tafadhali, kwanini umefanya hivi? Abdul fumbua macho yako nikwambia kitu tafadhali naomba uumbue macho yako” Masikini Shaymaa sasa aliweza kuonesha dhairi kuwa na upendo wa dhati na Abdul kwani ilikuwa ni ngumu kumuona Mwanaume anaempenda anakufa katika mikono yake
                            *****
Kitendo cha Shaymaa kutokufika katika hafla fupi iliyokuwa imeandaliwa na Baba yake, kulimfanya Mzee Mustapha achukizwe sana na hilo

Kilikuwa ni kitendo cha fedhea dhidi yake kwani alionesha dhairi hana nidhamu mbele ya Wanahisa wengine waliokuwa wameudhulia hafla hiyo.

“Nafikiri kutakuwa na jambo baya ambalo Binti yangu litakuwa limempata kwa maana hii sio tabia yake kabisa” Mzee Mustapha alizungumza na kuzima kipaza sauti kabla ya kumgeukia mshereheshaji kughailisha kila kitu na kuwataka wajumbe watapewa utaratibu mpya

Baada ya hafla hiyo kuaghairishwa, Mzee Mustapha alisimama na kuelekea ofisini kwake huku akiwa amechukizwa sana na kitendo ambacho alikuwa amekifanya Binti yake.

“Umenitia haibu kubwa mno” Mzee Mustapha aliongea huku akiwa anazunguka kwenye kiti cha ofisini kwake”

Kwenye maisha tunapaswa kujifunza kutopenda kukimbilia kutoa hukumu kabla pale hatujapata uthibitisho kwa kile ambacho tunakitolea hukumu.

Mzee Mustapha aliishi kwa kudhani kuwa Shaymaa alifanya kiburu kutofika kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili yake. Lakini pia Shaymaa alikuwa amefanya makosa makubwa sana kwa kutomshirikisha Baba yake kwa maamuzi yake ya kupitia kwa Abdul lakini pia angemjuza hata kwa kile ambacho alikuwa amekutana nacho nyumbani kwa mpenzi wake
                          ******
Irina alikuwa ni dereva mzuri sana mwenye uwezo wa kuendesha gari utafikiri hakuwa mwanamke. 
Alifanikiwa kukanyga mafuta na kuikaribia gari ya Shaymaa na alikuwa anamuwashia taa Oliver akimtaka asimame “Irina anatutaka tusimame”

Oliver alimjuza Shaymaa ambae alimsihii hasijaribu kupoteza muda na ajitahidi kuongeza kasi ili wamkimbize Abdul hospital.

Baada ya kuona Oliver ameshindwa kufanya kile alichokuwa anakitaka, Irina alizidi kuwa na shaka na kina Oliver na alihisi watakuwa wameiba nyumbani kwake hivyo alijitahidi kutafuta upenyo na kujifanya kama anataka kuwapita na ghafla akaenda kuwazinga kwa mbele.

Oliver alipatwa na mstuko na kujitahidi kukanyaga break ili kuzuia kile ambacho kilikuwa kianenda kutokea, lakini kwakuwa gari ilikuwa kasi sana ilijikuta ikiseleleka mpaka kwenye gari ya irina ……………………

“Mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!” Kelele ilisikika na haikujulikana ni nani aliyekuwa anapiga kelele

NINI KITAENDELEA? NINI KIMETOKEA? VIPI KUHUSU ABDUL? TUKUTANE KESHO INSHAALLAH. 
MAUMIVU YA NDOA 
S2: EP 40
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Ujasiri ulimshinda Irina na kujikuta akipiga kelele mwenyewe baada ya kuona gari ya Shaymaa inakuja kugonga gari yake.

Oliver aliweza kujitahidi kuyumbisha gari na aliweza kumkwepa kidogo Irina lakini aliweza kumpunyua na kuvunja side mirror.

Shaymaa alijipiga kiasi katika gari baada ya gari kuyumba lakini hakuweza kuhisi maumivu na badala yake aliendelea kumng’ang’ania Abdul ili hasipate madhara zaidi.

“Hivi wewe una akili timamu kweli? Oliver alimfokea Irina baada ya kusimamisha gari

Irina hakutaka kumjibu kitu na badala yake alisogea mpaka kwenye gari ya Shaymaa na kufungua mlango akitaka kujua ni nini walichoiba nyumbani kwake.

Alistuka na kuduwaa baada ya kumuona Abdul akiwa amekumbatiwa na Shaymaa huku akiwa hajitambui ”Wewe umemfanya nini Mume wangu?” Irina alimuuliza Shaymaa huku akiwa amemkazia macho

“Dada tafadhali naomba endesha gari tumuwaishe Mgonjwa hospital” Shaymaa aliongea akimtazama Oliver bila kuali uwepo wa Irina na hakutaka kumjibu chochote.

“Hivi wewe una akili kweli? Yani nimekufuma ukiwa na Mume wangu katika mazingira ambayo siyaelewi alafu unaleta dharau?” Irina aliongea na safari hii akiwa ameonesha dhairi kuchukizwa na kitendo cha Shaymaa kutomjibu na kutaka kuondoka
“Shetani mkubwa wewe, Heti unajiita Mke wa Mtu? Hivi huyu ndie Abdul niliyekuwa nimekuachia kweli? Sasa nikwambie tu Mwenye nyumba karudi mpangaji tafuta kwa kupanga mana ndicho ulichokizoea”

Shaymaa aliongea kwa hasira pasipo hata kuwa na chembe ya uoga kiasi ambacho hata Irina alishangaa baada ya kumuona Shaymaa mwengine tofauti na yule aliyekuwa amemzoea.

Oliver alikanyaga mafuta na kuondoka sehemu hiyo ambayo watu walishaanza kujaa wakiwa wanashangaa tukio ambalo lilikuwa limetokea muda mchache uliokuwa umepita
                            ******
“Asante sana mwanangu” Madame alimwambia Feisal baada ya kumtembelea mahabusu, lakini Feisal alichukia na kumnyamazisha 

“Madame kwanini unataka nirudie kauli moja kila siku? Mimi sipendi niwe Mtoto wako, naomba tuwe kama ilivyokuwa hapo hawali kwani nilishakwambia kuwa kwenye sheria kuna neon la kilatini linalosema “Nemo judex in causa sua, ikimaanisha kuwa hakuna Mtu anayehukumu kwa sababu yake mwenyewe”

Feisal alimwambia Mama yake huku akiwa makini hasisike na Mtu kama yeye ni Mtoto wa Madame kwani alina kama ataonekana Mteja wake ni Mama yake mzazi basi inaweza kuwa ni moja ya kitu ambcho kitamfanya ashindwe kusimamia ipasavyo kesi inayomkabili Mama yake

Waliongea machache na Feisal akihitaji vidokezo muhimu ili ajipange kwa kesi ambayo ilikuwa inaenda kusikilizwa kwenye mahakama ya juu zaidi baada ya kukata rufaa katika mahakama ile ya hawali.

Baada ya kupata alichokuwa amekifuata, Feisal alimuaga Madame kama Mteja wake na hakutaka kujifanya kama Mtoto wake hili kulinda haki yake ya msingi ya kumsimamia Mama yake apate kushinda kesi

Dakika chache baada ya Feisal kutoka kumuona, ghafla Madame aliitwa tena na kuambiwa kuwa kulikuwa na Mgeni wake ambae alikuwa amekuja kumtembelea

“Mgeni?” Madame alijiuliza mwenyewe huku akionekana kushangazwa kidogo baada ya kusikia taharifa hiyo.

Aliinuka na kwenda kumtazama Mgeni aliyekuja kuonana nae pasipo yeye kutambua ni mgeni gani aliyekuja kumuona.

Alikuwa ni msichana mrembo aliyekuwa amevaa na kupendeza ipasavyo. Madame alimsalimia huku akiwa ameonesha tabasamu utafikiri alikuwa mwema kiasi hicho. 

“Naitwa Pili ni Mke halali wa Mwanaume aliyethubutu kusimamia kesi yako” Pili aliongea na Madame alifurahi zaidi “ooh kumbe wewe ni Mkwe wangu? Kumbe Mwanangu Feisal amebahatika kupata Mke mrembo kama wewe? Nashukuru kukufahamu kwakweli na endapo nikifanikiwa kushinda kesi hii, wewe na na Mwanangu nitawapa zawadi nono’ Madame aliongea na Pili alitabasamu kabla ya kuangua kicheko fulani cha kebehi

Pili alichea huku akimuoneshea kidole utafikiri alikuwa anamcheka Mtu aliyekuwa ametokwa na haja katika umati wa Watu “Umetuwa? Wewe ni nani?” Madame alimuuliza na Pili ambae alikuwa amekatisha kicheko na kumtazama Madame kwa jicho kali utafikiri alikuwa anataka kumvamia

“Shetani Mkubwa wewe, hivi leo ndio unaona thamani ya Feisal? Hivi hna haibu? Mwanao yupi unae muongelea hapa? Au Mwanao yule uliyemtelekeza kwa miaka kadhaa iliyopita akiishi kwa tabu na mateso huku wewe ukiponda raha?” 

Pili aliongea na Madame aliuma meno kwa hasira huku akiwa anamtazama kwa kumtamani angalau amkunje

“Sidhani kama utakuwa ulimzaa Feisal wangu, kwanini ulimpotezea haki yake ya msingi kwa kumuacha alelewe na familia yake? Kwanini ulimuiba Feisal hospital na kujifanya Mtoto wako?” 

“Wewe ujui lolote kuhusu Mtoto wangu” Madame alishindwa kuvumilia na alijikuta akiongea huku akiwa anatokawa na machozi baada ya kuumizwa na maneno ya Pili

Pili alifurahi baada ya kauli ya Madame na kuzidi kuvuta utambi ili kumuumiza zaidi Madame “hivi huna haya kuendelea kumuita Feisal Mtoto wako? Wewe ni Mama wa aina gani ambae unamtelekeza Mtoto kisha unamkana na baadae unategemea msaada kutoka kwake? Huu ndio wakati sahihi wa wewe kubeba dhambi zako kwa yale yote uliyokuwa umeyatenda”

Pili aliongea na kuondoka na kumuacha Madame akitiririkwa na machozi. Ulikuwa ni ukweli mtupu ambao Pili alikuja kumwambia lakini kwanini amekuja kumwambia katika wakati aliokuwa nao?

“Laiti kama nitafanikiwa kutoka hapa, hesabu kuwa utakuwa wa kwanza kulamba mchanga”

Madame aliongea huku akiwa amekunja ngumi akimtazama Pili akiwa anatoka eneo lile ambalo walikuwa wakizungumza
                            ****** 
Abdul aliweza kuingizwa katika wodi maalum ili kupatiwa matibabu ya dhalura kutokana na hali yake ilivyokuwa.

Irina aliweza kutambua kila kitu kuhusu Mumewe kunywa sumu. Aliumia sana na alijua kila kitu itakuwa Abdul ameamua kunywa sumu kwa sababu yake.
“Lakini jana wakati namuomba msamaha si alikuwa amelala?” Irina alijiuliza mwenyewe huku akiwa anatembea tembea pale hospital.

“Unapaswa kufanya sherehe baada ya hili wala upaswi kuudhunika kinafki namna hiyo” Shaymaa alimwambia Irina ambae aligeuka ghafla kumtazama baada ya kusikia sauti ya Shaymaa

“Unaongea nini wewe? Yani umempa sumu Mume wangu alafu unatarajia nitakuacha?” Irina alijibu na Shaymaa alimchapa kibao cha haja ili kumuweka katika ufahamu.

“Umetudhalilisha sana wanawake wenzako, yani wewe wa kutembea na Maganga?” Shaymaa aliongea na Irina alichukia na kuinuka kwa hasira akitaka kumpiga Shaymaa

Lakini ghafla kabla hajafanya hivyo alistuka kuona amedakwa mkono, aligeuka na kutazama ni nani aliyekuwa amemdaka?

Alikuwa ni Mwanamke mrembo aliyekuwa amevaa na kupendeza lakini urembo wake ulikuwa tofauti na muonekano wake kwani alikuwa na nguvu utafikiri Mwanaume aliyekuwa anafanya mazoezi

“Amina na wewe hupo nyuma ya hili?” Irina alimuuliza baada ya kumuona Amina ndie aliyekuwa amemdaka mkono baada ya kumuona akitaka kumchapa kibao Shaymaa

“Unafikiri naweza kuwa upande wako? Yani ubebe mimba nje ya ndoa alafu umpakazie Boss wangu na mimi nakutazama? Wewe huna adhi ya kuwa na Abdul, na hawezi kufa kwa ajili yako katu”

Amina aliongea na Irina alistuka baada ya kusikia hata Amina alikuwa anajua siri yake.

Ilikuwa ngumu kabaki hapo kwani siri yake ilikuwa imeshavuja na hakupenda kuona hilo linatokea.

Irina aliondoka kwa hasira pasipo hata kuongea chochote na kuondoka utafikiri alikuwa amechelewa ndege.

Aliingia katika gari yake na kuelekea nyumbani kwake huku njiani akiwa na mawazo kibao.

Alifika nyumbani kwake na kuingia ndani na kweli alikuta mazingira yakiwa yamevulugika na kuonesha dhairi Abdul alikuwa amekunywa sumu.

Wakati anaangaza mazingira ya ndani ndipo alipokumbana na bahasha iliyokuwa imeandikwa juu talaka si Mke wangu.

Irina alistuka na kuifungua ile bahasha huku akiwa anatetemeka mikono utafikiri mzee wa miaka 200

Aliifungua taratibu huku chozi likiwa linatiririka na kutoamini kile alichokuwa anakiona.

Baada ya kuifungua na kuisoma ile talaka, Irina aliishiwa nguvu na kujkuta akijibwaga chini

“Abdul umeniacha kwa talaka tatu?” Irina alistuka na kujiuliza mwenyewe huku akiwa haamini kama kweli inaweza kutokea kwake…………….

USIKOSE EPISDE YA 41 

Post a Comment

Previous Post Next Post