🔐 MAUMIVU YA NDOA (31-----35) 😭😭😭😭


S2: EP 31

Maelezo ya Mustapha yalimchosha sana Madame na kujikuta akiwa hana hata jambo lolote la kuongea zaidi ya kujikuta akilia tu.

Pingu ndio lilikuwa jambo muhimu kwa wakati huo kwenda kujibu mashitaka yaliyokuwa yanawakabiri Madame na watu wake

Feisal alitoka wodini alipokuwa anafuatilia utaratibu wa operation aliyokuwa anafanyiwa Hakeem, alirudi na kushangaa baada ya kumkuta Mama yake akipigwa pingu pamoja na Watu wake ili kwenda kujibu mashitaka yanayo wakabiri

“Mbona mnamfunga pingu Mama yangu? Kuna nini kimetokea?” Feisal aliuliza na kumshangaza Mzee Mustapha baada ya kuona Feisal akimuita Madame Mama “Hapana huyu si Mama yako, kwani ulisahau kama D.N.A ilishindwa kuendana?” Mzee Mustapha alimwambia Feisal huku akiwa anamtazama

“Hapana, Feisal ni Mwanangu wa kumzaa na samahani kwa kutokwambia ukweli” Madame aliongea ukweli na kumduwaza Mzee Mustapha ambae alimtazama Mkewe na kuishia kusikitika.
                          ******
Baadaa ya kukaa chumba cha mapumziko kwa masaa kadhaa, atimae Shaymaa alipata fahamu huku pembeni yake akiwa Abdul akiwa anamtazama kwa umakini

Shaymaa alikumbuka mara ya mwisho alikuwa akiona kizunguzungu na alikumbuka kuwa alikuwa amempigia simu Feisal kwa maana ndie alikuwa ni faraja yake pindi anapokuwa na wakati mgumu, lakini siku hiyo Feisal hakuweza kupokea simu ya Shaymaa kwa sababu alikuwa ameacha simu ndani ya gari na Feisal aliporejea kwenye gari Shaymaa alikuwa tayari ameshapoteza fahamu hivyo hakuweza kuiona simu ya Feisal

“Inamaana Abdul ndie Mwanaume aliyekuja kunidaka pindi nilipokuwa nadondoka?” Shaymaa alijiuliza na Abdul hakutaka kumpa nafasi ya kutafakari zaidi na kumpa maji akimtaka anywe

“Leo itakuwa ni siku ya furaha sana kwako kwani Mtu ambae amekuwa akikusumbua wewe pamoja na Baba yako, tayari ameshaingia katika mikono ya sharia” Abdul aliongea na kumfanya Shaymaa astuke utafikiri Mtu aliyekuwa ametoka usingizini

“Vipi hali ya Baba yangu? Nini kimemkuta? Tafadhali niambie ukweli kuhusu Baba yangu” Shaymaa alikuwa akiongea kwa hofu ya hali ya juu na Abdul alimtazama na kutabasam 

“Baba yako hakuwa mgonjwa bali ilikuwa ni mbinu iliyotumika ili kuweza kumnasa mtuhumiwa ambae ni Madame na mpaka sasa tunavyoongea na wewe, tumefanikiwa kumkamata Madame akiwa ametuma Mtu ili amchome sindano ya sumu Baba yako”

Abdul alingea na Shaymaa bila hata ya kujitambua alijikuta amemkumbatia Abdul kwa nguvu na kumshukuru kwa jinsi walivyofanikiwa kumkamata Madame

Iliwachukua dakika nzma wakiwa wamekumbatiana huku Shaymaa akiwa ameshindwa kuyazuia machozi yake kwa furaha aliyokuwa nayo “Siku zote nimekuwa nikilia machozi ya udhuni lakini leo nasema asante Mungu kwani umenipa nafasi nyingine ya kunifanya nilie kwa sababu ya furaha”

Shaymaa aliongea na kujistukia baada ya kugundua kuwa alikuwa amekumbatiana na Abdul ambae alikuwa ni Mume wa Mtu
                            *****

Masaa yalikuwa yameenda huku simu ya Abdul ikiwa haipatikani jambo ambalo lilikuwa limemchukiza sana Irina.

Alikuwa ametulia huku akitazama picha ambazo alizokuwa ametumiwa na Mtu ambae hakuweza kumtambua zikimuonesha Abdul akiwa anakumbatiana na Shaymaa.

Alikumbuka jinsi ambavyo alivyoweza kwenda kule hospital lakini kwa bahati mbaya hakufankiwa kumuona Mumewe wala Shaymaa na kujikuta akizidi kuchanganyikiwa

“Inamaana sahizi watakuwa wananisaliti si ndio? Abdul kwanini unanifanyia hivi lakini? Kosa langu kubwa ni lipi ambalo nimekufanyia?”

Aliongea na kwa mara ya kwanza alijikuta akilia bila sababu ya msingi na kujaribu mara kadhaa kumpigia Mumewe lakini wapi, Abdul alikuwa hapatikani hewani 

“Nafikiri ni muda muafaka wa Mumeo kutambua ukweli kuwa wewe ni msaliti na ulibeba mimba ya Mwanaume mwengine”

Ujumbe uliingia katika simu yake na kumfanya azidi kuchanganyikiwa na kujikuta akiipiga namba iliyomtumia ujumbe lakini wapi namba ilikuwa haipatikani

“Maganga, unajisumbua bure kaa ukijua hautaweza kuaribu chochote kuhusu ndoa yangu Mimi na Mume wangu” Irina alijibu ujumbe kwa hasira baada ya kuna Mtu aliyekuwa amemtumia ujumbe anashindwa kupokea simu yake

Lakini baada ya kutafakari kidogo alianza kuhisi kuwa inawezekana Maganga siyo Mtu ambae ametuma ujumbe kwenye simu yake “Kama ni Maganga ndie aliyetuma huu ujumbe, kwanini anitumie picha za Shaymaa akiwa na Abdul na kutaka nikawafumanie?” Irina alijiuliza na kuhisi kutakuwa na Mtu mwengine nyuma ya pazia ambae alikuwa amedhamiria kuvunja ndoa yake na Mumewe kwa maslahi yake binafsi

“Inamaana Shaymaa ndie muhusika wa jambo hili? Anataka kurudi kwa Abdul? Lakini Shaymaa amejuaje kama Mimi nina mimba ya Maganga?”

Irina aliongea na kujikuta akiwa na maswali kibao ambayo hayana majibu na ilikuwa ngumu kuweza kumbaini muhusika aliyekuwa akihusika na mambo hayo
                                 ******

Shaymaa akiwa na Abdul waliweza kutoka katika chumba maalum cha mapumziko na kwenda kumshuhudia jinsi Madame akiwa na Watu wake walivyokuwa wakipandishwa katika gari la polisi na kupelekwa kituoni, tayari kwenda kufunguliwa mashtaka

Shaymaa alikumbatiana na Baba yake huku Madame akiwa anawatazama kwa jicho la hasira kwani alina ameshindwa kumiliki mali za Mzee Mustapha kwa dakika ya mwisho kabisa

“Shaymaa nitashinda tu hii kesi na nikitoka huko ni lazima nitaanza na wewe kabla ya kumfyeka huyo mpuuzi wako” Madame aliongea mwenyewe moyoni huku akiwa anawatazama kwa jicho la hasira kabla gari ya polisi haijaondoka eneo la tukio na kuwapeleka walipokuwa wanapaswa kupelekwa.

                                *****
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu kidogo, Irina alijikuta akipitiwa na usingizi na kujikuta akistushwa na sauti ya Mtu akiwa anabisha hodi

Aliinuka huku akiwa na usingizi na kwenda kufungua mlango. Hakuwa mwengine, alikuwa ni Abdul ndie aliyekuwa anabisha hodi na alipoingia tu aliweza kusikia manukato ya Mwanamke akinukia Mumewe
“Inamaana ni kweli ulikuwa na Shaymaa” Irina alimuuliza Mumewe huku akimtazama kwa hasira “Ni kweli nilikuwa nae ila sivyo kama unavyofikiri wewe”

Abdul alingea kwa ufupi huku akiwa anaendelea kubadili nguo zake “Kosa langu nini Abdul? Hivi kweli unaweza kuniacha Mimi Mwanamke mwenye Mtoto wako tumboni na unaenda kuangaika na ma laya ambae ulishampa talaka?” 

Irina aliongea na kumchukiza Abdul ambae hakupenda kabisa jinsi Irina alivyomuita Shaymaa Malaya “Irina jifunze kuheshimu Wanawake wenzako. Mimi nilikuwa na shaymaa kutokana na kazi yangu” “Heti kazi, kazi gani mliyokuwa mkifanya kwa stayle hii” 

Irina aliongea na kumtupia picha Abdul ambae alishangaa baada ya kuona amepigwa picha akiwa na Shaymaa

Ilikuwa ngumu kuweza kumuelewa na kujikuta wakishindwa kuelewana “Hivi Irina unaonaje kama nikikupa talaka?” Abdul alingea na kumstua Irina ambae hakutegemea kusikia kile alichoongea Abdul…………

NINI KITAENDELEA? USIKOSE EPISODE YA 32

Karibu kwenye group langu bonyeza maandishi ya blue itakupeleka 

SIMULIZI TAMU NA MIKASA YA KUSISIMUA 
MAUMIVU YA NDOA 
S2: EP 32
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Ilikuwa ni kauli ambayo hakuwahi kufikiri kama siku moja Abdul anaweza kufungua kinywa chake na kumwambia kauli tata kama hiyo

Irina alikosa cha kumjibu zaidi ya kumtazama kwa hasira huku akiwa anatetemeaka midomo. “Kuoa na kuacha huo ndio utamaduni ambao umejiwekea?” Alijikuta akitulia na kumuuliza kwa sauti fulani ya uchungu na kumfanya angalau Abdul ajisikie unyonge

“Sina maana hiyo Irina lakini kama utakuwa unahisi Mimi sikutendei haki basi ni bora ukatafuta namna nyingine ya kuitafuta haki yako. Unajua nimekuoa nikiamini kuwa wewe ni Mwanamke sahihi ambae nitajjivunia baada ya kufunga ndoa na wewe na itakuwa sehemu ya furaha yangu, lakini naona imekuwa tofauti kwako kwani kila siku umekuwa Mtu wa lawama na mauogomvi yasiyo na sababu”

Abdul aliongea na kumfanya Irina aangue kilio cha unafki na kuona sasa muda wake wa kuumbuka ulikuwa umefikia “Inamaana hupo radhi Mwanao azaliwe nje ya ndoa? Asante Mimi nipo tayari kwa chochote utakacho. Najua umenitumia na umeshanichakaza, lazima unione tofauti na sidhani kama unaweza kuona thamani yangu”

Irina aliongea na kuangua kilio kilichomuumiza sana Abdul “Kiukweli una haki Mke wangu, kwa maana wewe ndie Mwanamke wa kwanza mimi kuja kunipa heshima ya kuitwa Baba, hivyo napaswa kukupa heshima yako na kutambua mapungufu yako haswa katika kipindi cha ujauzito ulicho nacho”

Huruma ilimuingia Abdul na kumuonea huruma Irina kutokana na kutamka neon la Mtoto. Kiukweli hakupenda hata kidogo kuona Mtoto wake akizaliwa nje ya ndoa. Masikini hakutambua kama ujauzito aliokuwa nao Irina haukuwa wake hivyo kumpa talaka ilikuwa sahihi kwake kwani Irina hakuwa kama vile ambavyo yeye alivyokuwa akifikiri.

Kitendo cha kumuona Abdul amejishusha kwake ndio ilikuwa furaha kwa Irina kwani alizidi kulalamika na kumlaumu Abdul huku akimwambia kuwa Abdul hakuwa na mapenzi ya dhati kwake.

Alifanikiwa kumbembeleza Mkewe na kumuomba msamaha kwa kila kitu alichokuwa anahisi atakuwa amemkosea.

Ni nani aliyempiga picha Abdul na kwenda kumtumia Mkewe, hilo ndio swali kubwa ambalo lilikuwa likimuumiza sana Abdul. Alishindwa kuelewa kwanini alipigwa picha na Mtu aliyekuwa amefanya jambo lile alikuwa anataka nini kwake

“Kuna mambo nikianza kuyapa nafasi yanaweza kuja kuvuluga ndoa yangu” Abdul aliongea mwenyewe na kuzichoma moto zile picha huku akiamua kuacha kila kitu kumfuatilia Mkewe na kutaka kujua kulikuwa na nini kati ya Mkewe na Maganga. Abdul alihisi kabisa akiendelea na jambo hilo itakuwa ndio nafasi ya yeye kuivunja ndoa yake kwa mikono yake yeye mwenyewe “Kuna watu wanataka kuvunja ndoa yangu kwa sababu zao wenyewe lakini katika hili nasema mwisho wao utakuwa umefika, kwani sitampa kipaumbele mbuzi yoyote ambae anataka kufanya ujinga wake mbele ya Mke wangu”

Abdul alingea mwenyewe na kurudi zake kitandani na kumkumbatia Mkewe huku akiwa anapapasa tumbo lake ambalo lilikuwa tayari limeshaanza kujitkeza
                              *****
“Ni lazima nitafute dawa sahihi ya kuweza kumdhibiti Abdul” Irina aliongea mwenyewe huku akiwa anaendesha gari kuelekea nyumbani kwa kina Jack ili kwenda kuomba msaada kwani aliona ndoa yake ilikuwa inaongezeka joto kila wakati na hakuwa na mbinu sahihi ya kuweza kuokoa ndoa yake

“Mbona ushiki simu zangu kwani tatizo nini?” Irina aliongea mwenyewe huku akiwa anaendesha gari kuelekea kwa kina Jack ili kumuelezea matatizo yake na ikiwezekana aweze kupata msaada kutoka kwa rafiki yake huyo aliyekuwa anamuamini katika mambo yake binafsi.

“Tokea Jack ameanza kujiusisha na Wanaume amekuwa akinidharau kweli sijui hata kwa nini?” Irina aliongea na kuegesha gari yake vyema baada ya kufika nyumbani kwa kina Jack

“Umefuata nini hapa?” Mama jack alimtazama Irina kwa hasira na kumuuliza

“Nina Mambo yangu Binafsi nilikuwa nataka kuongea na Jack” Irina alimjibu huku akiwa anatetemeka “Hakeem amepata hajali na Mama yake amekamatwa yupo polisi ndio Jack ameenda kumshughulikia huko” Mama Jack aliongea na kumstua Irina ambae hakutegemea kusikia taharifa hiyo na kujikuta akitaka kuondoka bila hata kuaga huku akionekana kuchanganyikiwa

Mama Jack alimshika mkono na kumvuta huku akiwa bado anamtazama kwa hasira “Nakuchukia sana Shetani mkubwa wewe, Umefurahia baada ya kusikia Hakeem amepata ajali? Unafikiri mtapata nafasi ya kuendeleza ushetani wenu?” “Hapana Mama wala sijaja kwa niaba hiyo nilikuwa nimekuja kwa Mambo ya Mume wangu tu”

Irina liongea huku akijikuta akitokwa na machozi baada ya kusikia Hakeem amepata ajali “Mnafki mkubwa wewe” Mama Jack aliongea na kumuachia na Irina hakutaka kusubiri na kuondoka haraka haraka bila hata kuaga kama kawaida yake.

Irina aliingia kwenye gari yake na kuiwasha ili ageuze na alionekana mwenye mawazo na akili yake yote ilikuwa inafikiri kuhusu Hakeem “Dada!! ……… Dada!!” Sauti ya msichana alisikika akimuita Irina 

“Samahani kwa usumbufu, nimesikia matatizo yako kuhusu Mumeo. Jina langu naitwa Chausiku, Mimi ni Mpangaji wa Mama Jack lakini naweza kukusaidia kama hautojali” Yule msichana aliongea na kumstaajabisha kidogo Irina.

“Nashukuru kukufahamu, je unaweza kunisaidia vipi?” Irina alimuuliza huku akimtazama kwa mshangao “Nina mganga wangu huyu anaitwa Babu kigozi, yani huyo kama Mwanaume anakusumbua ana uwezo wa kumtuliza na asifurukute hata kidogo, chochote usemacho wewe ni sawa”

Yule msichana aliongea bila hata kuwa na haya kiasi ambacho hata Irina hakutegemea “Hiyo nzuri sana” Irina aliongea na kujichekesha na alijifanya amefurahi lakini wapi alimchukia yule Binti kwani alimuona Kama Mtu aliyekuwa amekurupuka

“Basi wewe chukua namba yangu na muda wowote ukiitaji utanipigia” Yule Binti aliongea na kumtajia namba zake na Irina alijifanya kama anaandika kumbe wapi alikuwa hata anasubiri tu amalize kutaja kwani alichokuwa anakiandika kwenye simu yake alikuwa anakijua mwenyewe.

Baada ya kumalizana na Chausiku Irina aliwasha gari yake na kuondka huku akiwa anasonya na kuona yule Binti alikuwa amempotezea muda wake bure kwani yeye hakuwa mfuasi wa mambo hayo
                              *****

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa familia ya Mustapha baada ya kuweza kufanikiwa kumkamata Madame Mtu ambae alikuwa akiongozwa na tamaa zake mwenyewe binafsi kutaka kumiliki mali za Mumewe. 

Mzee Mustapha alimshukuru sana Othman kwa msaada wake binafsi wa kumpambania na kufanikiwa kumuokoa katika majanga ambayo hakuwahi kufikiri kama anaweza kumsaidia kwa kiasi hicho japokuwa alikuwa akimpeleleza mpaka yeye mwenyewe

 Mmoja kati ya Watu waliokuwa Watu ambao walikuwa wamealikwa katika tafrija fupi iliykuwa imeandaliwa na Mzee Mustapha alikuwa ni Feisal aliyekuwa ameonekana muda wote alikuwa na majonzi

“Samahani sana Kijana, lakini Binafsi nimetokea kukupenda sana kutokana na moyo wako wa upendo ulioonesha kwa Mama yako na ndugu yako japokuwa hawakuwahi kukutendea wema” Mzee Mustapha aliongea na kila Mmoja aliyekuwa pale hakusita kupiga makofi kumpongeza Feisal

“Asante sana, lakini nilikuwa naomba udhuru kidogo kwa sababu sidhani kama nastahili kuwa na furaha katika jambo hili hivyo naomba niwaache” Feisal aliongea huku akionekana kuwa na udhuni na kuondoka eneo lile huku Shaymaa akiwa ameshangazwa kidogo

“Feisal unataka kufanya nini? Inamaana umeudhunika kuona Mama yako amekamatwa kwenda kutumikia makosa yake?” 

Shaymaa alisimama na kumuita ndugu yake na kumuuliza “Inawezekana mdomo wako utakuwa haujui nini ambacho unakiongea ila moyo wako utakuwa unajua kila kitu nini ambacho ulijisikia pindi ulipotambua kuwa wewe pia unayo nafasi ya kuita Baba. Ndio maana ulikuwa tayari kukaa jela kwa sababu ya Babaako”

Feisal alimjibu ndugu yake huku akionekana kama Mtu aliyekuwa akitabasam lakini wapi alionekana kuudhunika sana.

“Hupo sahihi kwa hilo lakini tambua kuwa Mama yako hakuwa mtu Mzuri katika jamii, ameuwa Watu wasio na hatia kwa tamaa zake” “Hata wewe hupo sahihi lakini madhaifu yake hayabatirishi kuwa yeye ni Mama yangu. Nina haki ya kuumizwa na tabu yoyote ambayo anapitia”

Feisal aliongea na Mzee MMustapha alimuunga mkono katika hilo na kumwambia Shaymaa kuwa hata angekuwa yeye asingeweza kuvumilia kumuona Mama yake anaenda jela ikiwa yeye nado hajafaidi matunda yake ya kumuita Mama

Baada ya kauli ya Mzee Mustapha, Shaymaa alimsogela Feisal na kumkumbatia kwa nguvu na kumuomba radhi kwa kila kitu
                             ******
Mpango mkubwa wa Madame ulikuwa ni kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabiri. Kwa kushirikiana na Jack na baadhi ya mapolisi ambao hawakuwa waaminifu, waliweza kumkutanisha Madame na Jack na Madame aliweza kutumia nafasi hiyo kuandaa mipango yake na kumuagiza Jack nini afanye, ikiwemo kuwasiliana na Mwanasheria wake aliyekuwa anamtegemea sana.

“Mustapha, usidhani kama naweza kushindwa kesi kirahisi kiasi icho. Hata kama umefanikiwa kuujua ukweli kuwa Hakeem si Mtoto wako, lakini ni lazima utaenda kaburini na nitakuuwa kwa mikono yangu mimi Mwenyewe Mbwa wewe”

Madame aliongea mwenyewe huku akionekana akitabasam baada ya kuona kila jambo lake litaenda kama vile atakavyo kwani alijua ana Watu wengi ambao alikuwa amewashika

Ghafla alimuona Askari anakuja na kumtoa ili kwenda kuonana na Jack ili ampe taharifa ya kile kilichokuwa kimejiri huko atokako

“Vipi tena mbona unanitisha?” Madame alimuuliza Jack baada ya kumuona kama Mtu aliyekuwa amekata tamaa “Mwanasheria wako amejitoa muda mchache tu uliopita amesema hii kesi hipo nje ya uwezo wake na hawezi kujitengenezea record mbaya ya kushindwa”

Jack aliongea na Madame alipiga ngumi ukuta na kuonekana amechukizwa na taharifa hiyo “Lakini nimefika hapa nimekuta kuna Mwanasheria mwengine ambae amejitolea kuja kuisimamia kesi yako na amesema atashinda tu”

Jack aliongea na Madame aliuliza ni Mwanasheria gani huyo? Kabla Jack hajajibu chochote, Madame alipigwa na butwaa baada ya kumuona Mwanasheria aliyekuja kusimamia kesi yake si Mwengine bali ni Feisal

“Fei……s…a…l?” Madame alipatwa na kigugumizi na kuuliza “N Mimi Mama” Feisal alijibu na Madame alijikuta akibubujikwa na machozi “Wewe ni Mwanasheria?” “Ndio Mama na sipo tayari kuona Mama yangu unaenda jela wakati Mimi Mwanao nina uwezo mkubwa wa kusimami kesi yako na ukashinda vyema”

Feisal aliongea na Madame hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumkumbatia Mwanawe na kuangua kilio kama Mtoto Mdogo
NINI KITAENDELEA? KWANINI FEISAL KAAMUA KUMSAIDIA MAMA YAKE? VIPI KUHUSU IRINA NA MUMEWE?

EPISODE YA 33 INA MAJIBU NDANI YAKE

MAUMIVU YA NDOA 
S2: EP 33
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Kuna wakati unaweza usione thamani ya kuwa na Mtoto, lakini asikwambie Mtu hakuna wakati mzuri kama pale unapokuwa na matatizo alafu Watu uliokuwa nao karibu wanakukimbia na hakuna Mtu mwengine ambae hatoweza kukuacha ukilia zaidi ya Mtoto wako

Ilikuwa ngumu sana kwa Madame kuweza kunyamaza kutokana na maamuzi ambayo Feisal aliamua kuyachukua dhidi yake na hapo ndio alianza kuhisi thamani ya Mtoto wake ambae hakuweza kuitambua miaka mingi iliyopita na kuamua kumtelekeza na kufuta kila kitu juu yake akiamini Feisal alikuwa ni Mtoto aliyezaliwa ili kuaribu maisha yake

“Kwanini sijawahi kuona umuhimu wako Mwanangu” Madame alingea na kumfanya Feisal azidi kuumizwa na kauli yake. “Kila jambo lina sababu Mama wala upaswi kujilaumu” Hakupenda kumuonesha Mama yake kuwa anaumizwa sana na kumbukumbu ambazo Mama alikuwa anatamani kuzikumbuka. Aliumia sana kuona leo Mama yake anamuona muhimu wakati alimtelekeza na hata pale alipomtafuta aliendelea kumkana na kumuona si Mtoto wake

“Feisal!! Najikuta nakosa maneno dhidi yako. Leo ndio nimeamini kuwa huwezi kuitambua Dunia kama utakosa la kujifunza. Inawezekana hivi ninavyoongea na wewe muda huu basi kuna Mwanamke mwengine ambae ni mjinga kama nilivyokuwa Mimi, pengine amepata mimba katika mazingira ambayo hakuyatarajia au ana Mtoto na anatamani kumtelekeza kutokana na changamoto ambazo anakumbana nazo. Najaribu tu kufikiri ni jambo gani napaswa kumwambia ili asifanye icho anachotaka kukifanya kwa maana ipo siku anaweza kutamani kulia machozi ya damu ili tu kujaribu kufuta maumivu yatakayokuwa moyoni mwake”

Waliongea vitu vingi na Feisal alimtoa hofu Mama yake na kumwambia yupo kwa ajili yake wala hapaswi kukata tamaa kwani pengine Mungu alipanga hiwe hivyo ili watengane na Mtoto aje kumsaidia Mama baadae. Ndio maana wahenga walinena alipangalo Mungu hakuna wa kulitenganisha.

Feisal aliomba faragha na Mama yake ili apate kumuuliza maswali muhimu ambayo aliona yanaweza kufaa katika kumnasua kwenye mashtaka yaliyokuwa yanamkabiri
                             ******
Kuna nyakati bora mara nyingi Mtu upitia ama kuna Watu wema Mtu anaweza kubahatika kukutana nao pasipo yeye kutambua hilo. Ndio maaana Watu usema Mtu hawezi kutambua kitu kizuri mpaka pale atakapokuwa amekipoteza. 

Alishindwa kujielewa ila dhairi Abdul alijikuta tu binafsi akijutia kumpteza Shaymaa katika mazingira ambayo hata yeye mwenyewe alishindwa kuyatambua. Changamoto kubwa iliyokuwa inamkabiri ni vipi anaweza kumrejesha Shaymaa katika himaya yake wakati alishamwambia kuwa yeye ni Mchumba watu na anataka kuolewa. Alijikuta anachukia kuona Shaymaa anaolewa na Mwanaume mwengine wakati ni yeye mwenyewe ndie aliyekuwa akimwambia kuwa yeye ni Mwanamke bora hivyo anapaswa kutafuta Mwanaume bora tofauti nay eye. Lakini leo anajikuta akimuona Shaymaa ni Mwanamke bora ambae anastahili kuwa katika himya yake, tena mbaya zaidi alikuwa akimuona anazidi kuwa mrembo 

“Kama Uliandikiwa kuwa na Shaymaa basi kaa ukijua kuwa hipo siku utakuja kuwa nae tena katika maisha yako, kama si kuishi nae tena kama Mkeo basi utakuja kupata Mtoto ambae atafanania kila kitu na Shaymaa hivyo upaswi kujikatia tamaa. Unapaswa kuamini kuwa inawezekana” Amina alimwambia Abdul ambae walitoka wote kuelekea ufukweni walipokuwa wameenda kupunga upepo baada ya kazi nzito waliyokuwa wameifanya kwa muda mrefu na kufanikiwa kumtia kwenye mikono ya Sheria Madame na Watu wake aliokuwa anashirikiana nao

“Amina nafikiri wewe unanijua zaidi, hebu niambie ilikuaje mpaka nikajikuta nafunga pingu za maisha na Irina? Hivi ilikuwa ni akili yangu ama kuna kilevi nilikuwa natumia? Inamaana nilishindwa kabisa kutambua kuwa Shaymaa ni Mwanamke bora kuliko Irina aliyekuwa ananizuzua huko nje?” Abdu alimuuliza Amina huku akiwa anamtazama na kumfanya Amina atabasam kidogo na kutafakari

Lilikuwa ni swali zito kwa Amina kuweza kumjibu Abdul ambae alikuwa ni Boss wake lakini alikuwa ni Mtu wake wa karibu sana

“Siku zote ni rahisi kuvuna chochote kile unachokipanda kwenye mapenzi, Shaymaa alikuwa ni Mwanamke bora sana kwako lakini hakuwahi kupata hata robo ya thamani ambayo alistahili kupewa kutoka kwako. Ulikuwa unampenda sana Shaymaa lakini ulikuwa hujaweza kujitambua kama unampenda ila nadhani kwa sasa utakuwa umeshatambua kwanini utakuwa ulimuacha Shaymaa na kumuoa Irina”

Amina aliongea na kiasi fulani alimuweka njia panda Abdul ambae alijikuta mwenye maswali zaidi baadala ya kupata jibu la swali lake “Bado sijakuelewa Amina” Abdul alimuuliza na Amina alimuelezea kuwa Mungu umuondoa Mtu mwema kwako kama endapo atahisi kuwa wewe siyo Mtu sahihi na ufanya hivi makusudi hili upate angalau muda wa kujifunza kutoka na mapungufu yako”

Abdul alitabasam baada ya kusikia maelezo ya Amina na hapo aliweza kumuelewa Amina kuwa Mungu alimtaka amuoe Irina ili apate nafasi ya kujifunza kwa yale aliyokuwa anafanyiwa na Shaymaa alafu akawa anachukulia kawaida ili siku nyingine aweze kuthamini upendo wa Mtu ambae atajitoa kufanya kila kitu kwa ajili yake. Mtu huyo upaswa kulipwa upendo wa dhati na si vinginevyo

“Mke wako alitumiwa picha ambazo hupo na Shaymaa Pale hospital, Vipi aliweza kukuonesha?” Amina alimuuliza Abdul na kumfanya Abdul astuke na kumuuliza alijuaje kama Mkewe alitumiwa picha zake

“Najua kila kitu Abdul mana picha hizo nilizituma Mimi kwa Irina na Mimi ndie Mtu nilie tuma Mtu akupige picha, hata zile jumbe za simu unazotumiwagwa huwa ni Mimi ndie ninae tuma kwakoo na kwa Mkeo” Amina aliongea na Abdul alistuka zaidi na kushindwa kumuelewa Amina

“Kwanini umekuwa ukifanya yote hayo?” Abdul alimuuliza Amina huku akionekana kuchukizwa kidogo “Nitaomba unisamehe sana kwa hili mana nimekukosea sana Boss, ila kiukweli nilikuwa nimejipa kazi binafsi ya kuakikisha namtoa yule kinyago nyumbani kwako”

Amina aliongea na ilikuwa ngumu kidogo kwa Abdul kuweza kumuelewa na kujikuta akifokewa kwa maamuzi mabovu ambayo aliyoamua kuyachukia bila hata kumshirikisha

“Mambo ya ndoa ya ngu wewe yanakuhusu nini? Kwanini unaigombanishe na Mke wangu? Hivi unajua jumbe zako zimetuletea taharuki kwa kiasi gani? Unafikiri Irina akisikia kama ni wewe ndio unacheza michezo hii atajisikiaje?’ 

Abdul aliongea kwa hasira akimfokea Amina ambae alikuwa tuli akimsikiliza “Boss samahani sana lakini nikwambie tu huna sababu ya kujivunia Mwanamke kama Irina tena ni bora umuache kabla haujapata fedhea zaidi”

“Fedhea? Nipate fedhea kivipi?” Abdul aliuliza huku akiwa makini kumsikiliza Amina “Irina alikuwa ni msaliti kwako tena alifanya upuuzi huo kwa kutembea na Maganga katika chumba chako pindi ambapo wewe unakuwa haupo” “Whaat? Maganga alikuwa akitembea na Irina?” Abdul alistuka na kumuuliza Amina kwa Mshangao wa hali ya juu huku akiwa na shauku ya kutaka kujua zaidi
                              *****
Katika chumba maalum cha mahojiano Feisal akiwa na Mama yake walikuwa wanatazamana kwa sekunde kadhaa kabla ya Feisal kuvunja ukimya na kumuongelesha Mama yake 

“Madame Asia, ningependa tuzungumze kama Mtu na Mteja wake na si kama Mtu na Mama yake, tafadhali ningependa ibaki kuwa wewe siyo Mama yangu Mzazi katika wakati huu mgumu ulio nao. Naomba unitambue kutokana na kazi yangu iliynileta hapa”

Feisal aliongea na kumfanya Madame ashushe pumzi na kutafakari kidogo kabla ya kuzungumza “Unafikiri itakuwa rahisi kwangu?’ “Ni lazima hiwe rahisi kwako kwa sababu bila kufanya hivyo unaweza kupoteza haki zako za msingi”

Madame alitafakari kidogo na kuunga mkono hoja ya kijana wake na sasa alikubali kumtambua kama Mwanasheria Feisal ambae yupo hapo ili kumuhudumia

“Madame Asia, ni rahisi sana kupangua mashtaka yote yanayokukabiri, endapo tu utanipa ushirikiano. Kama hautojali ningependa uniambie ukweli wote pasipo kunificha jambo lolote kuhusu kile anachoshitakiwa na Mimi ndio nijue ni vipi naweza kupindisha sheria ili kuukwepa ukweli“

Abdul alimuuliza Madeame swali ambalo lilikuwa gumu kidogo kwa upande wake kuweza kulijibu na kuonekana akitafakari kwa dakika kadhaa huku uso wake ukiwa ummebadilika kidogo

“Hauna njia nyingine ya kuweza kunisaidia Mr Feisal?” Madame aliuliza kwa sauti tofauti ambayo hata Feisal alishangaa kidogo kwani ilikuwa ni sauti fulani ya msisitizo iliyokuwa inamaanisha kitu fulani kutoka moyoni mwake

“Napaswa kutambua ukweli ili ninapoenda kusimama mahakamani kukutetea nijue ni vipi naweza kukutetea Madame na si kwa maana mbaya kama wewe unavyoweza kufikiri”

Kauli ya Feisal iliweza kumtoa chozi Mama yake na kujikuta akimshika mkono wake na kumbusu “Feisal Mwanangu, nakwambia siri hii kwakuwa wewe ni Mtoto wangu wa kukuzaa na najua hupo hapa kwa niaba ya kunisaidia tu na si vinginevyo tafadhali namba isiwe tofauti na fikra zangu. Lakini pia naomba umtunze sana ndugu yako endapo Mimi nitakosa dhamana” 

Madame alingea huku Feisal akiwa makini kusikiliza na kumtoa hofu akimuahidi kuwa hawezi kumtelekeza Hakeem 

“Ni kweli Mimi nilimuua Mama yake Shaymaa, Rayuu. Liyuna na Mke wa kwanza wa Mzee Mustapha na hapa nilikuwa nipo mbioni kumuuwa Mzee Mustapha ili kumiliki kila kitu ambacho alikuwa anamiliki. Wewe na Mdogo wako Hakeem Mama yenu Mzazi ni Mimi na Baba yenu Mzazi ni Marehemu Mzee Majaliwa Mjomba wake na Shaymaa”

Madame alingea kwa ufupi na kumfanya Feisal astuke na kumtolea macho Mama yake na kujikuta akiutoa mkono wake taratibu kwenye kiganja cha Madame na kumstua Madame aliyekuwa amemshika Feisal katika wakati wote aliokuwa anakiri maovu yake

“Kwanini ulifanya mauaji yote hayo?” Feisal alimuuliza tena Madame na kumfanya Madame hawe na mashaka kidogo juu ya swali la Mwanawe “Feisal una fanya yote haya kwa moyo wako au kuna Mtu Mwengine yupo nyuma ya pazia amekutuma? Mbona maswali yako kama yanaonesha kuwa unataka kunitia hatiani?” Madame aliongea huku akiwa amemkazia macho Feisal
                                ******

Abdul alimtolea macho Amina akitaka kupata uthibitisho kama kweli Maganga alikuwa akitembea na Mkewe na ilikuaje mpaka Amina alikuwa akiyatambua yote hayo

“Si kutembea nae tu yani hata mimba ya Irina si yako bali ni ya Maganga na ndio maana alikutungia uwongo ili umtimue Maganga ili usije kugundua ukweli kwani Maganga alikuwa yupo tayari kutubu dhambi zake kwako” Amina aliongea na kumfanya Abdul apigwe na butwaaa na asijue nini cha kufanya juu ya kile alichokuwa amekisikia kutoka kwa msaidizi wake…………………

NINI KITAENDELEA? ABDUL ATAFANYA MAAMUZI GANI? VIPI KUHUSU FEISAL NA MAMA YAKE? USIKOSE EPISODE YA 34 sorry sehemu ya 34 haijapatikana ko tuendelee na ya 35
MAUMIVU YA NDOA 
S2: EP 35
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Katika maisha unaweza kukosea jambo lolote na unaweza kujipa muda katika kurekebisha kosa lako. Lakini hakuna kosa kubwa kama Mtu kukosea kuchagua mwenzi wa kufunga nae ndoa, kwani hata kama utahitaji kurekebisha hilo unaweza kufanikiwa lakini itakuwa ni ngumu kufuta doa ambalo utakuwa umeliingia.

Ilikuwa ni siku ngumu kwa Abdul kuweza kuvumilia maelezo aliyokuwa anapewa na Amina kwani hata yeye alianza kuhisi kuna ukweli katika yale ambayo alikuwa ameambiwa na Amina

“Lakini uliwezaje kumuamini Maganga?’ Abdul alimuuliza Amina na kumfanya afikirie kidogo kabla ya kumjibu “Baada ya kupata maelezo ya Maganga nilianza kufanya uchunguzi binafsi pasipo kukujuza wewe ndipo Oliver aliponipa taharifa ya kuokota barua iliyokuwa imeandikwa na Maganga akiwa amekuomba radhi”

Amina aliongea na kuzidi kumchanganya Abdul aliyekuwa muda wote anafuta jasho lingi lililokuwa linatoka kwenye mwili wake utafikiri alikuwa amemwagiwa maji.

“Inamaana na Oliver anafahamu kila kitu kuhusu hili?” Abdul aliuliza na Amina alimjibu kuwa anafahamu na hapo alimfungua Abdul ambae alikumbuka mara ya mwisho alipoenda nyumbani kwenda kufanya uchunguzi binafsi alimuona Oliver ni kama Mwanamke aliyekuwa na hofu dhidi yake

“Kwanini umefanya yote haya?” Hilo ndio swali la karibu ambalo Abdul aliweza kumuuliza Amina

“Katika maisha yangu uliwahi kunishirikisha dhambi ambayo mpaka leo nimejikuta naijutia kwa kuitenda bila lidhaa yangu” Amina aliongea na kumfanya Abdul kuwa na shauku ya kutaka kujua ni dhambi gani ambayo alimfanya Amina aitende bila kulidhia “Wewe ulinituma nimdanganye Shaymaa ili akubali umpe talaka. Bila ya kauli yangu pengine usingemuacha Shaymaa. Hivyo baada ya kusikia upuuzi wa Irina nikaamua binafsi kujipa kazi ya Kumrejesha Shaymaa kwako” 

Amina aliongea na kumfuraisha Abdul ambae alimkumbatia kwa nguvu kabla ya kumtazama usoni huku akiwa amemshika kwenye mabega yake “Samahani sana Amina, akika nilikuwa mpuuzi katika hili” Abdul aliongea na kumfanya Amina atabasam

“Lakini wala usiangaike na Shaymaa kumtaka arejee kwangu, Mimi nilikuwa mpuuzi hivyo niache nile matunda yangu. Shaymaa ni Mke wa Mtu mtarajiwa lakini pia kama utakuwa radhi ningependa nikuomba uachane na ndoa yangu. Nafikiri bado nina nafasi ya kushughulika na mambo yangu binafsi kwani kwa kuingilia ndoa yangu utakuwa umefanya makosa mno”

Abdul aliongea na kutaka kujua kama kweli Amina atakuwa tayari kukubali kuachana na mambo ya nda yake huku akimtaka jambo hilo liwe ni siri baina yake yao na hasijue Mtu mwengine

“Nilikuwa naomba unikutanishe na Maganga haraka hiwezekanavyo”

Abdul aliongea na kuagana na Amina akionekana mwenye furaha pasipo kuoneshwa kuumizwa na chochote kile ambacho kilikuwa kimetokea pale
                            ******
Irina alifanikiwa kufika kituo cha polisi na kujaribu kuangaza kama anaweza kumuona Jack na kweli alifanikiwa kumuona akiwa nje ya kituo akiwa anasubiri katika eneo ambalo wageni walikuwa wanasubiri kuweza kuhudumiwa.

Jack nae alimuona Irina akiwa katika Maegesho ya magari na kila mmoja alimkimbilia mwenzake kwa hisia na kukumbatiana utafikiri walikuwa wamepotezana 

“Irina kwanini Mimi sina bahati? Irina Hakeem wangu anaumwa mimi!!” Jack aliongea huku akiwa amekumbatiana na Irina huku akiwa analia na wakati huo Irina nae alishindwa kujizuia kwani sasa ndio aliweza kuamini kuwa Hakeem amepata ajali.

Wakiwa wamekumbatina hivyo huku kila mmoja akijaribu kuonesha hisia zake kwa mwenzake. Wakati huo Abdul alikuwa amekuja hapo kituoni kufuatilia mambo yake binafsi. Abdul alistuka baada ya kumuona Mkewe amekumbatiana na Jack tena wakiwa wamefanya hivyo kwa dakika nyingi kidogo

“Anawezaje kufanya hivi mbele ya halaiki ya Watu? Inamaana wanataka kila Mtu ajue kama wao ni Mke na Mume?” 

Abdul alijiuliza mwenyewe huku akiwa ameshangaa kuwatazama. Alijikuta akichukizwa na kitendo kile na kutaka kupiga hatua ili kwenda kuwanasua na kuwezekana kuwafanyia vulugu. Unajua siku zote Abdul alikuwa ni Mtu ambae alikuwa hawezi kuimiri hasira zake.

“Wivu ni sehemu ya upendo kwa yule Mtu umpendae, lakini wivu huo huo ukizidi unaweza kuwa chanzo za kuuvuluga upendo wenu” Ilikuwa ni sauti adhimu ya Mwanamke iliyemfanya asite kupiga hatua zaidi

Ghafla sura yake ilitawaliwa na tabasam na kujikuta akibadilika na kugeuka taratibu “Shaymaa” Aliongea mwenyewe Moyoni wala hakupata shida kuweza kuitambua sauti ya Mwanamke huyo.

“Kwanini umesema hivyo Shaymaa?” Abdul aligeuka na kumuuliza Shaymaa ambae hakuacha kutabasam kama ilivyo kawaida yake na wakati huu Abdul alijikuta akimkodolea zaidi Shaymaa “Nimesimama hapa muda kidogo na nimegundua hasira yako baada ya kumuona Mkeo akiwa amekumbatiana na yule msichana. Sasa yule ni Mwanamke mwenzake je ingekuaje kama ungekuta amekumbatiwa na Mwanaume Mwenzio? Ama kweli unampenda sana Irina, Mimi sijawahi kupata hata robo ya upendo ambao unampatia Irina leo hii”

Shaymaa aliongea na Abdul alitabasam na kugeuka kumtazama Mkewe kama alikuwa anawatazama lakini kwa bahati Irina na Jack walikuwa wameshaondoka eneo hilo. Lakini moyoni mwake alitamani hata kumueleza ukweli Shaymaa kuhusu usaliti wa Irina kwa kutembea na Mlinzi wake, lakini pia alikuwa akishiriki mapenzi ya jinsia moja na huyo aliyekuwa amekumbatiana nae

“Shaymaa, Irina hakuwahi kupata upendo ambao niliwahi kukupa wewe hata kidogo” Abdul aliongea na kumfanya Shaymaa afurahi kidogo

“Hapana bwana Abdul, Mimi nafikiri Irina unampenda kuliko ulivyonipenda Mimi, lakini hakuna shida Mpenzi wangu wa sasa ananipa kila kitu ambacho nilikuwa nakikosa kwako. Nafikiri ulikuwa sahihi kuniacha na kunaimbia nitapata Mtu muhimu kuliko wewe, na kweli Mchumbaangu ni Mwanaume bora anaejua sana kujali na kuheshimu upendo wangu kwake. Nitampenda daima na wewe usikubali kupoteza chaguo lako”

Shaymaa aliongea makusudi kumchoma Abdul na kweli sura ya Abdul lionesha dhairi kuumizwa na kauli za Shaymaa kwani hakupenda kusikia hata kidogo habari za Shaymaa kuwa na Mwanaume mwengine

“Sawa nikutakie kila la kheri na asante kwa muda wako Mchache uliopoteza kwa ajili yangu” Shaymaa aliongea na kutaka kumpita lakini Abdul alimshika mkono na kumrejesha na kumtazama ipasavyo machoni kiasi ambacho hata Shaymaa alijisikia aibu kumtazama Abdul

“Una nini wewe mbona unanitazama hivyo? Tafadhali usifanye hivyo, Mchumbaangu akiniona anaweza kuhisi vibaya ujue” Shaymaa aliongea na kuzidi kumchoma Abdul

“Inamaana ni kweli unataka kufunga ndoa na Mwanaume mwengine?” Abdul alimuuliza na Shaymaa aliendelea kumdanganya kwa kumwabia ni kweli wala hamdanganyi.

Abdul hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuendelea kumshikiria Shaymaa huku jicho likiwa limemtoka
                           ******
Mzee Mustapha hakuwa Mtu wa visasi kama ambavyo Madame alivyokuwa, japokuwa alijua kila kitu kuhusu Hakeem siyo Mtoto wake wa kumzaa lakini aliamua kumuhudumia kama Mtoto wake wa kumzaa.

Hakeem akiwa ameshafanyiwa operation ya mguu alishangaa baada ya kumuona Baba yake anaingia kuja kumtazama, alistuka na kujikuta akiogopa kwani alikuwa hana taharifa kama Mzee Mustapha alikuwa ni Mzima wa afya.

“Wala huna sababu ya kuniogpa Mwanangu, Baba yako ni mzima wa afya” Mzee Mustapha aliongea na kumfanya Hakeem ashindwe kuamini kwa kile ambacho Mzee Mustapha alichokuwa anakizungumza

“Lakini kuna taharifa mbaya juu ya Mama yako kwani mpaka sasa tunapozungumza Mimi na wewe Mama yako yupo katika mikono ya sheria ili kujibu mashitaka yanayomkabiri”

Mzee Mustapha aliongea na kauli hii ilikuwa ni ngumu kwa Hakeem kuweza kuivumilia na kujikuta ikimfanya atiririkwe na machozi baada ya kusikia Mama yake yupo katika mikono ya sheria 

“Tafadhali Mzee, najua Mimi na Mama yangu tumekukosea sana lakini naomba msamaha kwa niaba ya Mama yangu na ikiwezekana ningeeomba ujaribu kufanya huruma dhidi yake na umpe talaka ili akaendelee na maisha mengine lakini siyo kwenda jela” Hakeem alilia na kumuomba radhi Mzee Mustapha tena hakutaka kumuita Baba baada ya kujua ukweli kuwa hakuwa na sababu ya kuendelea kumuita Baba Mzee wa watu kwani Mama yake alikuwa amefanya uhuni kwa kumbambikia Mtoto Mzee Mustapha.

“Mama yako bado haijathibitishwa kuwa ana hatia lakini ni Mtuhumiwa, hivyo kama itathibitika kuwa na hatia basi sheria itachukua mkondo wake na Mimi sitakuwa na ubavu wa kupinga hilo. Kitu kikubwa ninachokuomba ni wewe kutovaa viatu vya Mama yako kwani mwisho wa uovu ni hukumu. Jela imejengwa kwa ajili ya Watu waovu hivyo ni haki yako kuchagua ni upande gani utapenda kuishi, huwe Mwema ama huwe Muovu”

Mzee Mustapha aliongea na kukatishwa na kauli ya Feisal aliyekuja kumtazama ndugu yake “Mama atarejea tu uraiani, wala upaswi kulia kwani nikiwa kama Mwanasheria wake naamini Mama yetu si Mtu mwenye hatia”

Feisal aliongea na kuwashangaza wote waliokuwa pale “Feisal” Mzee Mustapha alimuita kwa mshangao wa hali ya juu “Kwanini umeamua kumtetea Mama yako wakati unajua fika kuwa Mama yako ni muovu” Mzee alimuuliza na Feisal alimtazama kwa kutabasam 

“Hakuna mwenye uthibitisho huo” “lakini Mama yako alikutelekeza?” Mzee alipigilia msumari na kauli hii ilimkwaza kidogo Feisal lakini alimeza mate na kumjibu bila wasiwasi “Hayo ni mambo ya Dunia tu ambayo yanaweza kumkuta Mtu yoyote, kwani wewe una tofauti gani na Mama yangu? Mbona na wewe unapambana kila njia kumkana Mtoto wako wa kumzaa huyu? Hivi unajua Hakeem amepata ajali baada ya kuathiriwa kisaikoloji baada ya kusikia kuwa umemkana siyo Mtoto wako wa kumzaa”

Feisal aliongea maneno ya kutunga ili tu kumvuluga Mzee Mustapha ili kumtoa katika reli katika kesi dhidi ya Mkewe
                            ******
Abduli alishindwa kuvumilia na kujikuta akimvuta Shaymaa na kumkumbatia kwa nguvu na ilikuwa ni raha isiyo kifani kwa Shaymaa kumuona Abdul nae akiteseka kwa ajili yake

Wakiwa wanaendelea kukumbatiana walisikia wanapigiwa makofi na haraka Shaymaa alijinasua katika mwili wa Abdul na kutazama. 

Alikuwa ni Irina akiwa na Rafiki yake Jack wakiwa wamewakuta Shaymaa akiwa amekumbatiana na Abdul.

“Hivi huwa huna haya ya kukukumbatiana na Wanaume za watu? Hivi haya mnayofanya mnadhani yanakubalika kijamii?” Irina aliongea na Abdul alimshika mkono Shaymaa na kumtazama Irina na kuongea kwa hasira “Hili linakuuma? Unafikiri Mimi ni mpuuzi kama ufikiliavyo? Dhambi uliyotenda na Maganga nadhani haikubaliki zaidi kijamii kuliko hili uliloliona hapa”

Abdul aliongea na kumfanya Irina astuke na kupigwa na butwaa akiwa haamini kile alichokisikia kutoka kwa Mumewe

WEWE UNAFIKIRI NINI KINAENDA KUTOKEA? USIKOSE EPISODE YA 36


 

Post a Comment

Previous Post Next Post