A TWIN SISTERS 03


"carl jua wewe ndo umenileta kwenye ulimwengu wa
mapenzi lakini tazama una mwanamke mwingine na sijui
kabla ya huyo ulikuwa nao wengne wangapi?"
"sio hivyo sophy huyu nimekutana nae baada ya
kupotezana lakini usijari nakuja hapo nje unikumbushe
yale mambo ya kipindi kilee" nililia sana baada ya
kumaliza kusoma.
SONGA MBELE..
Nilitafakari mambo mengi na kukuta mazingira
yaliyomkuta sophy yanaweza kunipata na mimi pia, carl
ni mwanaume wangu wa kwanza na pia nimetokea
kumpenda kuliko kitu ingine na yeye pia alionyesha
kunijari sana kumbe ananing'ong'a laiti ningetambua
mapema ningeachana nae ona sasa amerudia na sophy na
huko kazini kwake sijuí anao wengne wangapi ila sophy
ni mwanamke mwenzangu nitamuita na kumwambia
ukweli najua atanielewa ila kwa carl ni lazima
nimuonyeshe msimamo wangu. Ebu ngoja nikapate
uhakika.
Nilinyanyuka nikawa kama naenda toilet huku nafanya
uchunguzi wa kugundua ni wapi walipo nipate ushahidi.
Mpaka naingia chooni sikuweza kumuona mtu nikawa
nimesimama karibu na mlango wa sophy nikawa
namsikia carl akimshukuru sophy kwa penzi motomoto
alilompa na kumuahidi ni lazima afunge nae ndoa yani
ahadi zote alizokuwa ananiambia mimi ndo zile zile
alizokuwa anampa sophy nilirejea chumbani kwangu
nikazima taa na kujifunika na blanketi.
Nilimuona carl anakuja huku ananyata nilimtazama tu ile
anataka kulala nikawasha taa, akaumbuka alikuwa na
boxer tu mwanaume mzima hata aya hana, akaanza
kujibaraguza.
"eeh mpenzi upo nilienda chooni mara moja hapo vipi
lakini?"
"poa tu, ebu angalia simu yako naona inaita sijui"
Nilimtazama alivyokuwa anatafuta maelezo ya kunipa
baada ya kugundua ile simu aliificha ndani ya mto then
anakuja kuiona nampa mimi mkononi, ataniambia lipi
nimuelewe ngoja nimsikie atajiteteaje maana kichwani
kwangu tayari nilishapata jibu la kumpa.
"mpenzi wangu naomba nisamehe huyu msichana
ananitaka kwa nguvu tokea tupo shule lakini nakuomba
unisamehe kwa yote"
"haya ebu tumuite huyo sophy atamwambie ukweli juu
ya hilo"
"haina aja ya kumuita mpenzi wangu tuyamalize sisi
wawili"
"haya sawa hamna tabu"
Nilimwambia lakini moyoni mwangu ajui ninachofikiria
akaanza kunishika shika nikatoa mkono wake huko na
kumwambia "kwani wewe haujalizika bado au niache na
mimi nilale basi" nilitalala zangu mpaka ilipotimu saa
moja asubuhi nikaenda kumuita sophy kipindi hicho carl
alikuwa bado amelala. Baada ya sophy kuingia ndani
nilimuamsha carl alipomuona sophy hakuamini macho
yake akawa anatetemeka mwanaume mzima hata
kuongea alishindwa aibu ilimjaa sijawai kuona.
"haya sophy karibu shoga yangu wala usiogope
nakuomba uongee ukweli wako wote usifiche neno hata
moja"
"kiukweli carl nimemjua tukiwa chuo na yeye ndo
alikuwa mwanaume wa kwanza katika maisha yangu
ilifikia kipindi alinipa ujauzito na hii yote kutokana na
kuniforce tufanye ngono wakati nilikuwa kwenye tarehe
mbaya baada ya kunipa ujauzito akawa ananikwepa sasa
nikimpigia simu hapokei au anazima tokea hapo
nikaashana nae mpaka leo hii namuona kwako"
"carl mimi na wewe tumekutana wapi? Si tumekutana
casino tena wanapojiuza wanawake, uliambiaje kipindi
tunakutana? Sasa ngoja nikwambie kitu umenisaidia
mengi sana ila mimi sipendi kunyanyaswa hata kidogo
nadhani unaweza kwenda ebu amka hapo kitandani
uende kwako na kama mimba nitarea mwenyewe hata
sihitaji msahada wako tena"
"flavian unanifukuza kweli?"
"carl usifukuzwe wewe umekuwa nani. Mama yangu au?
Ebu toka bwana utaenda kuoga huko kwako" nilitoa
viatu vyake na kumtupia nje huku natoa shuka ili atoke
zake mimi siwezi kubembeleza mwanaume hata kama
nilimpenda sana.
"flavian unanifukuza kweli"
"iiiih carl usifukuzwe umekuwa nani! Mama yangu au?
Ebu toka nenda kwako bwana utaoga huko huko kwako"
Nilitoa viatu vyake na kuvitupa kwa nje nikarudi ndani
na kulitoa shuka ili aamke.
TIRIRIKA SASA.
"flavian haufanyi sawa wangu sio njia nzuri bwana hiyo"
"toka bwana wee na wewe si malaya tu utaniambia nini"
"baba nakuomba amka uwahi kwako hapa sikutaki"
Nilikuwa na hasira hatari na mimi katika maisha yangu
sipendi kunyanyasika so sioni shida kumtimua mtu
anayenifanyia ujinga. Carl aliamka akavaa suruali yake
na kutoka nje kuchukua viatu vyake akavaa na kurudi
tena ndani muda huo mimi nilikuwa nimesimama huku
sophy akiwa amekaa kitandani, carl alinitazama na
kuniambia.
"flavi kosa moja haliashi mke nakutakia maisha mema
kama ukipata shida usisahau kunipigia simu hela hiyo
hapo ya matumizi"
Niliendelea kumtazama ile hela akaiweka kitandani na
kuondoka zake mimi nilianza kujifikiria kwa kile
nilichokifanya kama ni sahihi au laa. Nilimuona sophy
kama anataka kuniambia kitu lakini anasita
nikamwambia "unasemaje sophy"
"nimetokea kukupenda sana flavian yani nimewahi kuwa
na marafiki ila sijawahi kuona mwenye msimamo kama
wewe naomba tuwe marafiki maana umenifundisha kitu
kikubwa sana katika maisha yangu"
"usijari sophy nitakupenda kama ndugu yangu kwani
hapa unaponiona sina ndugu zaidi ya pacha mwenzangu
nae kama amenisusa wala haji hata kuniona nakuwa
mpweke muda wote"
"usijari wangu mimi nakupenda sana naomba usijisikie
upweke"
Alinikumbatia na huku kichwani nikiwa namfikiria
flaviana mdogo wangu aliyenisusa hata akutaka kuniona
kabisa, nilimtazama sophy nikawa namchukulia kama
flaviana tu kwani yeye alikuwa mdogo kwangu au
inawezekana tukalingana.
***
Mimi na sophy tulikuwa marafiki wakubwa sana kiasi
kwamba akanitafutia kazi pale hotelini kwao traveta
hotel iliyopo mpakani mwa tz na kenya na ilikuwa ni
hotel kubwa ya kitalii. Niliweza kuweka pesa zangu
kwenye account ili nije kuanzisha biashara yangu.
Siku ya wikiendi mimi na sophy tuliamua kwenda kwa
yule mama ambaye alikuwa anatutunza mimi na flaviana,
tulikuwa tunatembea mitaa hiyo ya njiro kwa miguu
huku tunapiga stori zetu mara gari kubwa aina ya nissan
terrano likaja kupiga breki mbele yetu na kioo
kikafunguliwa kutazama alikuwa ni bamdogo peter
aliyeenda ulaya kusoma toka nikiwa na miaka 10 leo
nakuja kumuona akiwa na miaka 22 ni zaidi ya miaka
kumi na mbili imepita.
"eeh flavian upo wewe?"
"nipo shikamoo"
"heee yani nimewaulizia sana kwa shangazi zako kila
mtu anaonyesha hana muda na nyie ebu pandeni kwenye
gari twende sehemu tukaongee"
"haa bamdogo tumekuja kumuangalia flaviana hapa
maana sijaönana nae muda mrefu"
"wewe kwani wewe unakaa wapi hapa nyumbani vipi
umeondoka?"
"ni stori ndefu bamdogo nitahadithia ngoja nimuangalie
flaviana"
Nilipiga hodi akafungua mlinzi aliyekuwa ananikumbuka
nikamuuliza "vipi mama yupo?" akasema "ndio yupo"
nikamuuliza tena "flaviana nimemkuta" hapo nilikuwa
kama nimemkumbusha kitu.
"sesesese! Dada yani ukimuona uwezi kuamini sio
flaviana unayemjua wewe"
"kwanini jamani mbona unanitisha"
"sasa hivi anajiuza hapa nina kama mwezi sijamuona"
"yani dada ukimuona sasa hivi uwezi amini amebadilika
sana"
"mbona unanitisha amekuwaje?"
"sasa hivi anajiuza uwezi kuamini kama ni flaviana yule"
TIRIRIKA NAYO.
"bamdogo peter umesikia hayo?"
"eeh jamani imekuaje amefikia kote huko?"
"nitakwambia uncle"
"haya pandeni kwenye gari twendeni kwangu
tukapafahamu"
Tulifika mpaka kwenye nyumba yake aliyoinunua
ilikuwa ni nyumba kubwa sana na yenye uzio mkubwa
mno humo ndani kulikuwa na bembea za watoto,
swimming pool, garden house iliyozungukwa na maua
mazuri ya rangi mbali mbali. Kwa pale bamdogo alikuwa
peke yake na wafanyakazi mke wake yeye yupo dar,
yeye baba anafanya kazi shirika la ndege la kenya
"kenya airway" kwahiyo kipindi cha likizo ukitumia kuja
kuspend na wanafamilia Tanzania. Tulikaribishwa
kwenye garden nzuri penye upepo mwanana na
maongezi yakaanzia pale.
"kwanza pole kwa kufiwa na wazazi, ila napenda kujua
ilikuaje baada ya matatizo yale kuisha?"
"bamdogo ni story ndefu lakini kipindi msiba
ulipokwisha tulikabidhiwa kwa bamkubwa ambaye
familia ilimteua kama msimamizi mkuu wa mirathi lakini
cha ajabu akutusomesha na kibaya zaidi akauza ile
nyumba tuliyokuwa tunaishi tukaamia mtaani na kulala
kwenye vibaraza vya watu tukikoswa koswa kubakwa
nilijitahidi kutafuta kazi ya kufanza ila kazi zilikuwa
ngumu kupatikana hata zikipatikana mpaka utoe rushwa
ya ngono tumepata shida nakumbuka katika
zungukazunguka zetu ndo tulipita hapa kama bahati yule
mama aliyenunua hapa aliamua kutuchukua ndo mpaka
leo yupo na flaviana mimi nilikataa kujiuza ndo
nikaamua kuondoka ila ndugu hata mmoja akuwai
kutujari kwa lolote matokeo yake flavi ameamua
kujiuza"
Uncle aliumia sana akaanza kutoa machozi, nilimuonea
hadi huruma tukanuia kumtafuta flaviana kwa udi na
uvumba.
Ilikuwa ni ijumaa usiku tulimkuta club de casino
akinywa mvinyo huku amevaa nguo fupi hamna mfano
na mkononi alishka sigara nilimsogelea na kumvuta
mkono mpaka nje alipokuwepo bamdogo peter nae
aweze kujionea kwa mara ya kwanza "flaviana
umepungukiwa na lipi mpaka upo huku?"
"maisha tu bamdogo usijari yote haya yatakwisha
nikipata maisha safi hapa natafuta sembe"
***
Flaviana alipelekwa shule kenya akaanza sekondari mimi
nikaenda kusoma mambo ya biashara chuo cha CBE hapo
dsm tena mji wenye mrundikano wa watu na kila aina ya
starehe. Sikutaka kuweka utani kwenye masomo kabisa
kwani ndo kila kitu kwangu, nilimaliza certifate
nikaunganisha na diploma nakumbuka matokeo yangu ya
mwisho yalikuwa mazuri niliweza kucompite/
kushindana
na wavulana na kuwashinda hapo ndo nilianza
kujulikana na chuo na wakufunzi pia.
Mark ni kijana aliye mwaka wa pili diploma nilimfahamu
kupitia rafiki yangu scolastica wakati tunarejea hostel
ndo tulianza kupiga stori mbili tatu akanipa namba yake
ya whatsap akawa ananitumia picha, videos na music
audios kiukweli he is charming/ni mchangamfu, nilianza
kuchat nae kwa kutumia simu na ilikuwa ikifika saa nne
usiku ni lazima tuongee. Hapohapo akaingizia mambo
yake kama ujuavyo wanaume sio wavumilivu katika
maswala haya, nilikuwa nawachukia wanaume na kwa
wakati huo sikuhitaji mwanaume nilihitaji kufanya
malengo yangu kama nikiwa nae basi ni rafiki.
"flavian me najua ni kiasi gani upendi wanaume lakini
jua kama ilivyokuwa uwepo wa wabaya duniani basi hata
wazuri wapo believe on me aliyekukosea ni mmoja
usichukie dunia nzima"
"it can't be true kwani wewe umetoka sayari nyingine,
nyie wanaume mnakuaga na maneno matamu kama
utamu wa big g lakini ule utamu ukiisha unaona big g
haifai tena, uwezi kunishawishi nikakubali maana nyie
wanaume suruali mvaayo wote ni moja na fundi wenu ni
mmoja"
Nilimpa maneno mark mpaka hakuwa hana pa kujitetea
akabaki kijetetea kwa yaleyale lakini hakuwa na jipya
nilimwambia nataka kulala nikamuaga na kukata simu.
Mark akuchoka aliendelea kunisumbua mara aniletée
zawadi lakini wapi sikutaka kuzipokea zawadi zake
nakumbuka hapo mwanzo alikuwa ni rafiki yangu
mkubwa lakini nilianza kumchukia tokea aliponiambia
upuuzi wake. Infront of majority nilimuumbua, ilikuwa
hivi.
"flavian nimeandaa lunch kwa ajiri yako please naomba
tuelekee basi"
"hivi mark unataka nini zaidi kwangu mbona
nimeshakwambia tokea mwanzo kuwa sihitaji chochote
kutoka kwako mbona unakuwa mgumu kuelewa lakini?
Wewe ni msomi wa namna gani sio muelewa?
"naomba nisamehe sana flavi nafanya yote haya because
of love please naomba nielewe tafadhari mimi sioni aibu
kutetea penzi langu"
"bwana eeh kwani mwanamke ni mimi peke yangu khaa
sitaki bwana"
Niliondoka zangu nikamuasha pale kasimama yupo na
rafiki zangu sijui walikuwa wanamshauri nini mimi
nilienda mpaka nyuma ya chuo nikaketi nikaweka
earphone zangu nikawa nasikiliza music.
Kwa kipindi kile nilitokea kuwachukia wanaume tokea
nilipoashana na carl nikatoa na mimba yake iliyokuwa na
mwezi mmoja. Nakumbuka ilikuwa jumamosi jasmine
aliniambia twende coco beach tukapunge upepo
nilimkubalia tukajipanga hao mpaka coco sasa
nilimshangaa mwenzangu yupo besy sana anachat
nikitaka kuangalia anakwepesha simu nikasema ngoja
nimuashe.
Tuliagiza chakula na vinywaji tukawa tunakula huku
tukitazama meli na watu wanaogelea mara ghafla mark
alikuja pale nikajua ule ulikuwa ni mpango wao na
jasmine na alipokaa tu jasmine alinyanyuka.
"jamani mimi ngoja ninyoshe nyoshe miguu nakuja
muda si mrefu"
Niliitikia japo kwa shingo upande huku nikitamani
nimfate, mark alianza kuangea maneno yake hata tention
yangu haikuwa kumsikiliza maana ndo maneno yao ya
siku zote, lakini kadili alivyokuwa anaongea nilianza
kumuelewa kama kuna kitu cha maana anataka kusema
akameza funda la mate na kusimama mbele yangu
akanichum kwa nguvu bila ya mimi kutaka then akatoa
pete ya uchumba na kunivalisha.
Nilibaki kushangaa inakuaje kwa mtu niliyemdharau
akanivalisha pete ya uchumba ambayo hata carl akuwahi
kufikiria kunifanyia hivyo zaidi aliishia kunitumia
akanitia mimba na kuniasha nililia sana na kumkumbatia
mark kwa machozi mengi yaliyoambatana na makamasi
mepesi nisiamini kinachotokea.
Tulianza kupitia kwenye courtship/uchumba huku
nikiendelea kumchunguza mark tabia zake lakini huyu
mkaka alikuwa ni mwenye heshima, mpole, anajari
wengne na pale chuo alipewa tuzo ya mwanafunzi bora
mwenye nidhamu na ushirikiano mzuri na jamii
iliyomzunguka, nilienjoy sana sana kuwa nae.
Nakumbuka kuna siku mimi na rafiki zangu pamoja na
wanafunzi wengine tulipita kwenye notesbody kuangalia
japo matangazo na matokeo ya mtihani wa semister ile
ya kwanza. Wote tulistaajabu tulipoona mark ameongoza
kwenye kozi yake na kumpita mbali sana anayemfatia.
Kuna mdada alianza kuongea.
"unajua hapo mwanzo huyu mkaka nilijua
wanampendelea ila baada ya kumuona niliamini kuwa
kuna watu wamepewa mafunzo na wazazi wao sio bure"
"we acha ukimuona mkaka mwenyewe mpole ana muda
na mtu huyu ndo anafaa kuwa rais wa wanafunzi sio yule
mwakatobe"
Niliwaangalia wale wadada wakimsifia mark huku
wanaondoka zao na kutuasha sisi tukiwashangaa, mara
wakaja wavulana wengne inaonekana anasoma anasoma
nao.
"ebwanaa kwa mara nyingine tena huyu jamaa
anatukimbiza check point alizokuasha john?"
"hapa kuna upendeleo haiwezekani huyu jamaa anipite
namna hii"
"bwana john wee kubali umeshindwa we point zote hizo
bado unasema umeonewa"
Tuliondoka na kuwaasha wanabisha pale, na yule
wanamuita john ndo alikuwa wa pili sasa amepitwa
points nyingi lakini ataki kukubali kuwa amepitwa
anaona kama kuna upendeleo.
****
Niliweza kufunga ndoa na Mark tena kanisani
tukihudhuriwa na na watu wengi mno na bamdogo
aliweza kughalamia kila kitu pale, na uzuri pia mark
alipata kazi NMB tawi la mbagala zakhem kama wakala,
nilifurahi sana kuolewa maana ndo lilikuwa hitaji kubwa
la moyo wangu.
Nilianza maisha mapya ya ndoa nikiwa naenda shule na
kurudi nyumbani kwangu kumuandalia mark mume
wangu chakula na maji ya kuoga pindi arejeapo kutoka
kazini. Hayo ndo yalikuwa majukumu yangu kama mama
mwenye familia kilikosekana pale ni mtoto nae tulipanga
baada ya mwaka tuzae.
Kila mtu alituonea gere baada ya kuona maisha yetu
kawa watoto vile, ile asubuhi ilikuwa ni lazima tuoge
pamoja ananipa dozi moja me naenda shule yeye
anaenda kazini. Ni lazima anibebe mpaka nje na wakati
wa kwenda kulala pia alinizoesha hivyo. Na kuna kipindi
tukiwa tunaangalia tv pamoja najifanya nimelala ili
nibebwe yani nilikuwa malkia kwenye dunia yangu.
Maisha yalisonga nilikuja nikapata ujauzito ila baada ya
miezi miwili ile mimb ilitoka ikawa kila nikipata mimba
inatoka mpaka mimba ya pili tena jumla mimba tatu na
ile aliyonipa carl niliumia sana ila mpenzi wangu
alinivumilia na kunifuta machozi kila niliapo alikuwa ni
zaidi ya mume kwangu kuna muda nilimuita dadie maana
kazi anayoifanya kama dadie at the sametime ni mume.
Mke wa bamdogo alikuwa anakuja sana pale nyumbani
na kunishauri na alikuwa ni mama mzuri kwangu ila
wakati tunaongea mara aliingia mume wangu mark akiwa
kama ameshanganyikiwa akamsalimia mama juu juu
akapitiliza chumbani niliamua kumfata ndani.
"mume wangu nini tatizo?"
"kazini kumetokea wizi mkubwa kwahiyo
nimesimamishwa kazi"
Mke wa bamdogo alikuwa ananitembelea mara kwa mara
pale nyumbani na alikuwa ananishauri kwa mambo
mengi kusema ukweli alikuwa ni mama bora kwangu.
Wakati tunaendelea na maongezi aliingia mume wangu
mark akiwa kama amevurugwa alitusalimia juu juu
akapitiliza chumbani kiukweli nilishtuka ikabidi nimfate
nijue kilichomsibu.
"vipi mume wangu nini tatizo mbona hivyo?"
"mke wangu kuna wizi umetokea kazini nami
nimehusishwa ndo nimesimamishwa kazi"
TIRIRIKA NAYO.
"jamani mume wangu upaswi kuwa hivyo matatizo
kaumbiwa binadamu usiofu mume wangu haya yote
yatakwisha"
"jamani mke wangu tutaishije hapa mjini huu ndio
mwanzo wa kuumbuka na kwenda kuomba misaada kwa
watu, na nina wasiwasi kesi isije kwenda mahakamani
maana wizi umetokea kwenye kitengo ninachofanyia
kazi mimi, masikini mimi nilianza kukubalika pale ofisini
ndo haya yanatokea?"
"usijali mume wangu mungu atakusaidia utapata kazi
sehemu nyingine"
Nilimfariji mume wangu aliyekuwa amechanganyikiwa
kabisa lakini baada ya kumpa kumpa kumbatio langu
alitulia kama ndege kwenye kiota, tena nikamuandalia
chakula akala na maji ya kuoga palepale alipata usingizi
akalala.
Nilimweleza mamdogo yaliyomkuta mark alitamani hata
kulia akatoa laki na nusu akanipa za matumizi kwani
mara zote amekuwa akitumia pesa na bamdogo kupitia
bank ya bacleys kwani yeye anafanya kazi kenya airport
na huko ndo mdogo wangu/pacha mwenzangu flaviana.
Ile pesa tuliitumia kwa matumizi ya pale nyumbani na
nauli yangu ya kwenda chuo na kibaya zaidi nilitakiwa
kwenda field arusha pesa nayo haikuwepo nilikuwa
kwenye wakati mgumu sana. Nakumbuka ilikuwa
jumamosi asubuhi alikuja mtu na kugonga mlango
nikafungua akanipatia bahasha na kuondoka hata
akuingia ndani nikampelekea mume wangu ambaye
alikuwa amepanga kutoka.
Ile barua ilikuwa inamtaarifu kuwa anahitajika
mahakamani jumatatu saa4 asubuhi kichwa kilianza
kumuuma ghafla akapoteza fahamu nilipata kibarua
kumpepea mpaka alipozinduka nikaanza kumbembeleza
hadi alipotulia. Yani mark hakuwa kwenda polisi hata
mara moja hali hiyo ilimsumbua sana.
***.
Nilibaki kulia tu na kitanda nilikiona kikubwa mark
akuwepo nami alikuwa mahabusu juu ya kesi, nilikuwa
kwenye hali ya upweke sana hata mambo yangu
hayakwenda vizuri.
Nilikuwa nawaöa rafiki zangu wakitoka na mabwana
wenye hela zao na nilipata ushawishi mkubwa kutoka
kwao lakini nilimuheshimu sana mume wangu na nafsi
yangu iliona kama vile yupo karibu nami hivyo
nilishindwa kufanya lolote baya juu yake.
Nilienda kwa mamdogo kumuomba pesa kidogo kwa
ajiri ya matumizi lakini sikutegemea kauli aliyoniambia.
"mama kila siku utaomba hela mpaka lini najua mume
wako hayupo lakini changamka mtoto wa kike wewe
alaa"
"sasa mama unataka mimi nifanyaje?"
"jitume mwanangu kwani unataka kusema wanaume
huko barabarani na chuoni kwenu hawakufatifati?
"
"wananifata mama lakini namuheshimu mume wangu"
"khaaa utakufa na njaa shoga me mwenyewe nitachoka
mwenzangu kukuhudumia jitu zima na minanilii yako"
ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post