A TWIN SISTERS 05 MWISHO


Nilimtazama mke wangu flavian akishuka kwenye gari
aina ya nissan murano na ndani kulikuwa na mwanaume
mnene mwenye pesa zake. Nilimuona flavian jinsi
alivyopendeza sana akawa anakuja kwenye lile gari
nililokuwepo.
SONGA NAYO.
Nilipatwa na uchungu baada ya kuona mke wangu
anachukuliwa tena mbele ya mwanaume mwenzangu
nilitoka na kumfata vile vile nikiwa na bandage yangu
kichwani.
"kaka nakuomba shuka mara moja tuongee kiume"
"we mark unataka kunitibua ebu rudi kwenye gari"
alinijia flavian
"ebu niache wewe niongee na mwanaume mwenzangu"
"mwanaume mwenzako umemjulia wapi? Ebu toka hapa"
"niache nakwambia niache"
Nilimsukuma akadöndoka huku chini maana nilikuwa na
hasira nae pia kwani yeye ndio chanzo cha yale yote.
Nilifungua mlango na kumtoa yule jamaa na mtumbo
wake nikamvuta hadi nikiwa na hasira sana.
"kaka wewe ni mwanaume mwenzangu na unajua
uchungu wa mwanamke kweli unanifanyia hivi mimi na
unajua huyu ni mke wa mtu tena mke wa ndoa?"
"hapana kaka me sikujua kama ni mke wako nisamehe
sana nakuahidi nitakuachia mke wako"
Niliondoka na kupanda ndani ya gari nikawa nataka
kuondoka mara flavian akanifata na kusimamisha gari
nikafungua kioo kumruhusu aongee.
"mark kweli umenisukuma mimi na umeamua kuniharibia
sasa kwako sitarudi na kamwe usijisumbue hata kufikiria
kama una mke kama mimi pete yako hiyo hapo sikutaki
pumbafu"
"sawa mimi pumbafu kisa nimekusukuma wewe
uliyenisababishia majeraha? Sasa hata mimi nimechoka
pia na nipo tayari twende kanisani tukavunje ndoa yetu"
"sawa kesho nitakupigia twende kanisani kwaajiri ya
kuvunja hiyo ndoa"
Niliachana nae nikaenda zangu nikiwa na flaviana shem
wangu nae alichangb kwa jinsi dada yake alivyobadilika
lakini mimi nikamwambia "hata mimi sikutarajia kuwa
atabadilika lakini ndo ameshabadilika sio flavian yule
mke wangu wala yule dada yako huyu ni mwingine
kabisa ila tumuombee atabadilika lakini mimi nimechoka
na manyanyaso"
Tulifika nyumbani nikiwa nipo huru kwani moyoni
mawazo ya flavian yalinitoka kabisa hata sikumpa nafasi
tena na akili yangu iliwaza maisha kabisa.
Ilikuwa ni hatua ndefu sana kuvunja ndoa ile lakini
tulifanikiwa na mimi na flavian hatukuwa mke na mume
tena nilimpa kilicho chake na pia nikaanza mipango
yangu na mara zote nilikuwa naongea na flaviana
shemeji yangu aliyekuwa ni mwenye upendo kwangu na
tokea nilipokuwa naumwa na kamwe sikuweza
kumdharau wala kuonyesha kuna kitu kilitokea na dada
yake. Sikutaka kujua maisha flavian kwani yangenifanya
nimkumbuke na nitamani kuwa nae kitu ambacho
sikukipenda kabisa.
Niliendelea na kazi yangu ya kujichikiza nikiangalia
kama kuna uwezekano wa kupata kazi sehemu nyingine.
Ilikuwa ni ijumaa moja mtoto mmoja wa kike alikuja na
baba yake akiwa kwenye gari akaniita.
"mwalimu mark nakuomba mara moja samahani" aliniita
yule mzee
"bila samahani mzee shikamoo"
"marakhaba pole na kazi lakini nikuja hapa kwa lengo
moja, binti yangu amekuwa akipenda kusoma hapa na
sasa anaingia kidato cha nne nakuomba sana umsaidie
kwenye masomo ya biashara maana ameniambia
unafundisha vizuri sana mimi nipo tayari kukulipa kwa
kiasi unachotaka"
Nilijisikia vizuri kupata ile nafasi hata hivyo sikujua
niseme nini maana kwangu ilikuwa ni bahati iliyoje.
Nilikubaliana bei na yule mzee niwe namfundisha
mwanae kila jioni na kesho yake ndo ilikuwa nianze
kazi.
***
Siku ya tatu toka nianze Kazi ya kumfundisha jesca yule
mzee alikuja na kuanza kuniuliza baadhi ya mambo
baada ya kuzoeleka na kuwa moja kati ya wanafamilia.
"mwalimu hivi unafundisha shule gani?"
"dah mzee mimi sijasomea ualimu kabisa ila nimesomea
accountancy/akaunti"
"eh bwana mbona unafundisha kama mwalimu kabisa
sasa mbna ufanyi kazi ya professional yako/kazi ya
taaluma?"
"shida tu mzee ndio maana unaniona hivi"
"mimi nitakusaidia ebu kesho niletee vyeti vyako"
Nilitoka pale nikiwa mwenye furaha sana na nilijua fika
wakati wa mungu kunibariki umefika baada ya mimi
kupitia wakati mgumu baada ya kufukuzwa kazi.
Nilifika nyumbani na kuanza kazi ya kutafuta vyeti
vyangu mahali nilipoviweka nilifanya kazi hiyo kwa saa
nzima nikakumbuka vyeti vyangu na vyeti vya flavian
vilikuwa pamoja palepale nikampigia simu flaviana.
"hallo shem naomba unisaidie kuangalia vyeti vyangu
kwenye vitu vya flavian"
"mmh sijui kama vyeti vyake ameviweka humu ndani
ngoja nikutafutie shem wangu"
Niliketi pale nikingoja ripoti kutoka kwa flaviana,
ulikuwa usiku wa saa nne simu yake ikaingia na
kunifanya nipagawe na taarifa nitakazopewa nikapokea
simu.
"uwiiii! Nimeshoka kweli wangu, yani hvyo vyeti
nimekuja kuvipata chumbani kwa mamdogo"
"nashukuru sana kwa kuvipata flaviana maisha yangu
yatabadilika muda si mrefu ooh asante mungu"
kesho yake palipokucha nilioga vizuri nikaweka kila kitu
sawa nikaingia kazini na kuanza kufanya kazi yangu ya
kufundisha watoto.
Ile jioni nilimkabidhi yule mzee vyeti vyangu palepale
akampigia simu sijui meneja gani wa bank na kumueleza
kuwa kijana mwenyewe anazo quality zote za kuajiri
hata akiwa na haja na interview nikawa nashangilia
moyoni na kumrudishia mungu sifa na utukufu maana
hakuna sehemu ningeweza kupata kazi kirahisi namna ile
tena kumbe kazi yenyewe na mhasibu mkuu msaidizi
kwenye bank stanbic bank ilikuwa ni kitu ambacho
sikukifikiria katika maisha yangu tena jiji la arusha
sehemu ambayo niliiota kuwa siku moja nikaweke
makazi yangu.
***
*upande wa flavian*
Maskini mimi flavian maisha yangu yalianza kuwa
magumu bada ya kumdanganya derick kuwa sijaolewa
na Leo amegundua ukweli achana na hilo nimemvumilia
mengi sana kwani ana wanawake wengi sana huko nje na
wengne nimewahi kumfuma nao lakini sina ubavu wa
kumuasha kwani itakuwa fedheha kwangu kwani mark
nimeachana nae na huyu tena nitaonekana mimi ndo nina
matatizo. Ila kuna siku uvumilivu ulinishinda ni baada ya
kumkuta ametembea na msichana wa kazi ilikuwa ni
kitendo cha aibu kumwambia ukweli ikawa tatizo
alinipiga na kunichania nguo nilizovaa.
"derick kweli unathubutu kunipiga kwa kosa ulilofanya
wewe me naondoka derick naondoka"
"we mpumbuv ondoka tu hapa penyewe unazibia nafasi
malaya tu wewe na ndio maana mwanaume wako
amekushindwa nitakuweza mimi tena nilishndwa
nitakufukuza kwa kosa gani kwani mke wangu na watoto
wanatoka durban wanakuja wiki ijayo bora uondoke na
unirudishie gari langu mchenzi hauna adabu unanijia juu
mimi"
"nipo chini ya miguu yako derick nisamehe nitachekwa
mwenzio sina msahada mwengne derick na hata hvyo
sikujua kuwa umeoa kama ningejua nisingekubali"
"ndo umejua ondoka me nilikuwa nakupima kama
unamsimamo nimegundua hata nikiwa na wwe siku
nikishoka utanikimbia nakuomba toka"
"derick nakuchukia wewe mwanaume kwani
umenìharibia maisha me naondoka ila mungu atanilipia"
"hahaha fungu la kukosa wa kupenda vya dezo, alafu
nakusihi nenda kapime afya na ufate ushauri wa daktari
kama mimi mwenzio natumia vidonge vya arv sina
wasiwasi"
"haina aja ya kushuku mara zote tumekuwa tukifanya
mapenzi bila kinga nahisi inaweza kuwa tatizo hapo
baadae"
"toka huko mwanaume we mnafki yani nakuchukia kama
shetani kweli umeniambukiza ukimwi"
Niliondoka pale nikiwa nimechanganyikiwa nilifika
balabalani hata nikakuta watu wakisubiri kuvuka mimi
nilitamani kuwa nikajikuta navuka ghafla bajaj
ikanigonga mgongoni palepale nikapoteza fahamu
sikujua kilichotokea baada ya hapo.
Nilikuja kujikuta nipo hospitali ya moe nikawa nataka
kunyanyuka nikashindwa mbele yangu alikuwa mama
nikamuomba anisaidie kunikarisha nae akafanya hivyo
nikaketi lakini nilikuwa sijielewi kuanzia mgongoni
hapa mpaka chini. Mara akaingia daktari.
"mama nadhani kama nilivyokwambia wewe nenda
kakamilishe malipo na mtoto wako kisha uchukue
wilchair/kiti cha walemavu"
"sawa dokta nimekuelewa"
"mama ina maana nimekuwa mlemavu?"
"hapana mwanangu umepalalaizi ila nitaongea na baba
yako utaenda kutibiwa india usijari"
"hapana mama msipoteze hela kwa ajiri yangu mimi wa
kufa tu hapa nilipöina ukimwi na tena mlemavu sistahili
kuishi mama nimemkosea sana mungu sistahili kuishi
laiti ningejua ningetulia na mume wangu mark
nimeamini majuto ni mjukuu naombeni mtafuteni mark
nimuombe msamaha kabla sijafa"
"we flavian usiseme hvyo ebu"
"mama ni lazima nisime ninapaswa nitubu ili nikifa
mungu anipokee"
***
*Upande wa mark*
Maisha yalikuwa mazuri nilikuwa mhasibu kwenye bank
ya NBC nilipewa nyumba na gari la kutembelea na
niliishi njiro mji wa arusha.
Flaviana alikuwa mtu wa karibu kwangu na taratibu
tulijikuta tukiwa wapenzi na mara zote tulikuwa
tunaongea mara kwa mara akiniuliza umekula, umeamka,
umetoka kazini, unafanya nini now? Haya yalikuwa
maswali yake kila siku ila leo nilishangaa toka
aliponisalimia asubuh akuweza kunijulia hali tena mpaka
nilipompigia.
"hello honey leo mbona kimya sana unaumwa au?"
"hapana! matatizo mpenzi sema siwezi kukwambia
ulisema uhitaji kujua"
"hapana mpenzi niambie"
"dada flavian ameashana na yule mwanaume na
amemuambukiza ukimwi na hakapata ajali iliyopelekea
kupalalaizi hapa alipo anataka uje akuombe msamaha"
"dah masikini mimi nilijua hayo yatampata ndo wanaume
wa mjini lakini mungu atasaidia nitakuja wikiendi hii na
kama nitakuvisha pete ya uchumba kabisa"
"mpenzi mama ataki unioe"
"amesema kwanini ataki nikuoe?"
"eti nitaitia familia yetu mikosi kwanza eti wewe maskini
una nyuma wala mbele pili wewe ndo umepelekea hata
flavian amepelalaizi yani anakuchukia sana lakini mimi
nimemwambia ukweli kuwa sitakuacha kamwe"
"sasa huo mtihani sema nitakuwa wikiendi hii nijue
mbivu na mbichi"
"hapo itakuwa vyema baby i should wait for you/
nitakusubiri wewe"
"okey baby usiku mwema"
***
***
Sikuamini kama itafikia siku nitakuwa mzigo kwa familia
kama nilivyo leo hata sioni raha ya kuishi maisha
yamebadilika na kunifanya nikumbuke enzi zile ambazo
nilikuwa na msimamo haswa mwanaume akuweza
kunichezea kama alivyoniraghai lile janaume na
kunisababishia matatizo makubwa namna hii nalia na
moyo wangu.
Mama alinibadilikia hakuwa yule tena alikuwa mbogo
kwangu kuna wakati alinipa kazi ngumu za kumfulia,
kupika na kuosha vyombo wakati anajua nina matatizo
ya kupalalaizi kwanzia huku chini, namshukuru pacha
wangu flaviana ndo Amekuwa msahada mkubwa
mkubwa kwangu hasa ninaposhndwa unilisha na
kunipeleka chooni na kuniogosha mara zote nilipohtaji
msahada kutoka kwake. Sikuwa flavian wa kugombaniwa
na wanaume tena ule urembo wote ulipotea nilikuwa
kama kituko hata muda mwingne mama kama ana wageni
wake ataki mimi nitoke pale sittingroom/sebureni anahisi
nitamchafulia mambo yake sijui?
"flavian mdogo wangu nasikia umepata mchumba
anataka kukuvalisha pete"
"aah ahapana dada bado bado ila ikiwa tayari atakuja tu"
"mbona kigugumizi flaviana au upendi dada yako nijue
mambo yako ya ndani sana?"
"hapana dada we ni dada yangu unapaswa sana dada ila
wakati ukiwadia nitakwambia usijari"
"sawa mdogo wangu ila jitahidi utulie usije kufanya
kama mimi nilivyomtendea mark wa watu matokeo yake
napatwa na matatizo haya nakuomba mdogo wangu"
"saaawa daada nimekuelewa"
Nilishndwa kuelewa ni kwanini flaviana alikuwa
anapatwa na kigugumizi lakini nikayaasha yale nikawa
namtazama tu akicheza game kwenye laptop aliyotoka
nayo shule kenya.
"hvi sista flavi bado unampenda mark?"
"khee wee flaviana umefikiria nini mpaka unaniuliza
swali kama hilo?"
"nataka kujua dada"
"ndio nampenda xana sema sina nafas tena ndani ya
moyo wake hasa kwa yale niliyomfanyia isitoshe hata
akitaka turudiane haitawezekana leo mimi mremavu na
tena nina ukimwi siwezi kuwa flavian yule tena labda
mungu aniumbe tena"
"dada jamani unanitia huruma jamani mpaka natamani
kulia hata sielewi nifanyaje"
"flaviana flaviana flaviana nini tena"
Flaviana aliongea yale maneno huku anatokwa na
machozi akatoka na kukimbilia nje. Nilipoona ile hali na
mimi nikaendesha kigari changu kuelekea alipo lakini
wakati natoka nilisahau kama pale sebureni nilikatazwa
nisikanyage mimi nikaenda nilipoinua macho nilimuona
mark akiwa na rafiki zake nilishtuka sana nikaburuza kiti
kwa mbele kumbe pale kuna ngazi nikajisahau na
kuanguka vibaya nikaangukia mikono na kichwa.
"mama mama mama mama dada flavian ameanguka"
"mpumbav huyu nilimkataza hakutaka kusikia yeye
anajijua ana matatizo lakini bado anatusumbua yani
sijui nimtupie nani huu mzigo"
Roho iliniuma sana japokuwa flavian niliashana nae
lakini yale maneno ya mama yake yaliumiza sana.
Tulienda kumnyanyua na kichwani alikuwa anavuja
damu na muda ule alikuwa uncouscious/ametoza fahamu.
Kufika hospitali walimpeleka chumba maalumu cha
wagonjwa mahututi maana hata pumzi ilianza kuisha,
muda wote flaviana analia sana maana flavian ni pacha
wake kabisa na kama ujuavyo mapacha wanauguaga
sana mateso ya mmojawapo ndo alivyokuwa flaviana
nilikuwa nambembeleza atulie mara zote lakini yeye
anajua dada yake amekufa.
Kama kunakipindi flaviana nilimshuhudia akilia ni leo na
muda wote nilikuwa nikimnyamazisha ananyamaza
lakini akikumbuka tu anaendelea kulia nilipata shida
sana nilipumzika aliposinzia kwenye mapaja yangu.
Mama alikwenda pembeni na kumpigia mume wake
aliyepo nairobi akamwambia kila kitu na kumjaza
maneno ya uongo kuwa mimi ndie chanzo na nimekuja
kuivuruga familia yao. Mzee aliongea maneno makali
juu yangu na la mwisho nilisikia akisema "mwambie
asiniletee upumbav nitamtwaga risasi" niliyasikia
maneno yote japokuwa nilijifanya kama sijui kitu
kumbe masikio yangu yanasikia mbali sana. Mama
alipomaliza alikuja pale akiwa anatabasamu lakini
nilishajua ni la kinafki.
"khee huyo amelia wee mpaka kapitiwa na usingzi"
"yeah unajua tena hana uchungu na dada yake"
"yani hapa nimechoka kweli nasubiri taarifa za dokta
niende nikalale zangu maana"
"ni kweli"
Nilijikuta namuitikia ili mradi tu lakini moyoni mwangu
nilishamjua vizuri yule mama ni mtu wa aina gani.
***
Flavian alipata nafuu akiwa na bandage kichwani alitoka
hospital nikampakia kwenye gari kumrudisha nyumbani
muda wote huo flavian alikuwa anaongea mwenyewe
nikajua tayari atakuwa kachanganyikiwa maana
alianguka vibaya na isitoshe alikuwa ameshapalalaizi na
yale mawazo ya kuashwa na mwanaume na mimi kuwa na
mdogo wake yalimchanganya sana kweli mapenzi
yanaua na yanauisha.
Tulimlaza kwenye sofa akawa amepumzika na sisi
tukawa tunaongea mawili matatu mara mlango
ukafunguliwa nikaona miwani ya macho khee mara mwili
wote alikuwa ni baba mkwe aliyekuwa na nyuso ya
hasira na jazba kama mbogo aliyejeruhiwa, nilitamani
kukimbia lakini nisiwe.
"nilikuwa hospital kumbe tumepishana nyie mmeshafika
nyumbani"
"ndio dokta alimruhusu" alijibu mama mkwe
"khee kabla sijasahau, hivi wewe kijana unaitafutia nini
familia yangu? Sasa leo utanijua mimi ni mtu wa aina
gani"
Mzee alitoa bastora na kunielekezea mimi wakati huo
nilikuwa nimekaa kiti kimoja na flaviana mkojo ulianza
kunitelemka kwa kasi ya ajabu.
Nilitetemeka na mkojo ukaanza kunitoka sikuamini
kama mzee anaweza kuniönyeshea silaha ya moto na kwa
pale nilivyokuwa sikuweza hata kujitingisha hata kidole.
"dady please don't commit adultery he is innocent men/
baba tafadhari usiue huyo hana hatia"
"wewe flavian unanijua vizuri huwa sipendi kuingiliwa
kwenye mambo yangu sasa wewe sogea nitakuamishia
wewe ili balaa pumbav"
"lakini baba subiri nikwambie ilivyokuwa itakuwa mama
ajakwambia, mimi ndio nimekosea baba na mungu
ameamua kunipa pigo hili unaloliona mimi sikuzaliwa na
tabia hizi kweli nimeamini ule usemi asiyefunzwa na
mamae ufuzwa na ulimwengu baba ulimwengu
umenifunza kamwe sitakuja kusahau mpaka naingia
kaburini"
"flavian ebu nieleze nini kilitokea?"
"dady wakati fulani mark alifungwa kutoka na wizi
uliotokea kwenye kitengo chao na mimi nilijaribu kila
njia kumtoa ikashindikana nikaenda kumueleza mama
nae akaniambia mimi ni mtoto wa kike inabidh nijue
kutafuta pesa kwa namna yeyote ile kwani yeye ataweza
kunilisha mimi na mume wangu mark kama vile yeye
ametulazimisha tuoane, nilishanganyikiwa nikaondoka
wakati nipo chuo bwana mmoja alinifata na kuja
kunishawishi atimae akanibaka na huyo ndo chanzo cha
haya yote kwani nilivunja ndoa na mark kumbe na yeye
alikuwa ameoa tayari akaja akanisaliti ndo
niliposhanganyikiwa na kupata ulemavu huu yani najuta
kwanini nilikuwa na tamaa namna hile"
"mama flavi unaona haya hivi flavian angekuwa mwanao
wa kumzaa ungemfanyia ulivyofanya au kwasababu ni
watoto wa kaka yangu wewe hawakuhusu, ni mara ngapi
nimetuma hela kwaajiri ya flavian na mwenzie? Me
nakuomba ondoka niachie familia yangu"
"hapana dady mama asiondoke huyu ndo mlezi wetu
kama angekuwa mtu mbaya usingetukuta tulivyo sasa,
me ninachoomba tujadili ndoa ya flaviana na mark
itakavyokuwa haya yameshaisha sasa majuto ni mjukuu
hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho mama na baba"
***
Nilifurahi sana kukubaliwa kumuoa flaviana na hiyo yote
ni kwa juhudi za flavian mzee alishakataa katakata kuwa
haiwezekani mwanaume mmoja amuoe mtu na dada yake
lakini mwisho alikubali na harakati za ndoa zikaanza na
ndoa ilipaswa kufungwa nairobi kenya anapoishi mzee
kikazi na hata mimi nilipata michango karibu mil11.4
niliyoipata kutoka kwa marafiki zangu kule kazini na
hata mabosi na wafanyakazi wenzangu ni kumbukumbu
nzuri sana katika maisha.
***
Siku ya ndoa iliwadia na ukumbi wa kanisa ulifurika
watu mpaka nje wapo rafiki wa mzee na marafiki zangu
kutoka arusha nilifurahi sana ila wakati tunafunga ndoa
kumbe huku nyuma flavian alitoka nje kama anaenda
chooni akatafuta sehemu tulivu akajifungia na kutoa
sumu ya panya kwenye pochi yake akanywa na kupoteza
maisha. Huku ukumbini sherehe ilipamba moto
tulikunywa tukala sasa wakati uliposonga tukapata
taarifa kuna mwili umekutwa chooni watu wote walitoa
kilio hasa baada ya kumtambua alikuwa ni flavian.
Miezi mingi ilikatika baada ya ule msiba na mke wangu
alikuwa amekaribia kujifungua lakini aligundulika ana
kifafa cha uzazi, nilikuwa kama chizi kichwa kinauma
kwani niliogopa kumpoteza mke wangu.
Ilikuwa jumapili jioni mei 23siku ambayo sitakuja
kuisahau mke wangu aliyopoteza maisha na kuniashia
katoto ka kike ambaye amenipa shda katika malezi yake
ila kila ninapømuona huwa namkumbuka mama yake
kwasasa yupo standard four lakini mungu amesema
tushukuru kwa kila jambo. AMEN!!!
*KILA JAMBO NA WAKATI WAKE KUNA WAKATI
WA KUZALIWA NA WAKATI WA KUFA JIANNDAE
NA NYAKATI ZOTE*
**MWISHO** 

Post a Comment

Previous Post Next Post