TEGO 🔞❤️🌹 1---6


‘’Nilijitahidi kukata alinishika na kunisukuma kitandani niliaguka
kama mzigo ‘’
‘’hapana siwezi kufanya hivi nakuheshimu sana na ninamweshimu wazazi
wako samahani siwezi’’
‘’alinifata na kukaa juu yangu huku akiwa anavua nguo zake na
kuchukuwa mkonowangu na kuuweka kwenye ziwa lake nilimshika na
kumgeuza kitamdani,
‘’amna nakuheshimu sana siwezi fanya hivi utanisamehe sana ‘’
‘’kama hutaki jiandae kuondoka humu kwetu’’ ‘’aliogea kwa sauti ya ukali sana
‘’hapana amina isiwe sababu ya kunifanya nikafukuzwa kisa wewe ila
kama ukiamua poa tu.’’

aliniangalia kwa jicho la hasira sana aliinuka na kuondoka niliwaza
sana vitisho vyake kwakuwa alikuwa ni mototo wa mwenyenyumba ndio mana
kapata ujasiri wa kunitisha

‘’ sawa ila liwalo na liwe’’; nilijisemea a kuendelea na shughuli
zangu, siku iliofata nikiwa nafanya usafi chumbanii kwaangu mala
mlango uligongwa..

‘’ngo ngo ngo ngo….’’
‘’Nani?’’
‘’Toka nje unaitikia huku umekaa ndani toka nje’’
Ilikuwa ni sauti ya ukali ilikuwa ni sauti ya mama mwenyenyumba
niliogopa sana, nilifugua mlango na kumsikiliza
‘’Ratiba ya usafi chooni unaifahamu’’
 Nilishusha pumzi na kujibu ;’’’’Nndio naifahamu mama’’
‘’Mbona umekaa tu ndani au au upo na mwanamke’’
‘’Hapana ma….’’ ;kabla sijamaliza kuongea alinisukuma na kuingia ndani
‘’Dah mbona nanyanyasika hivi kisa nyumba ya nimepanga dah!’’
‘’Mh na wewe unakaa utafikiri unawanamke ndani bwana ningemkuta ungeondoka.’’

 nilimwangalia sana na sikupata majibu ya maswali ya vituko
ninvyoviona kwa familia hile ilindoka na nilifaya usafi na
kuenendelea na ratiba zangu
Ilikuwa majira ya saa tatu usiku nikiwa najiandaa kulala simu yangu
iliita ilikuwa ni namba ya shangazi yangu wa kijijini,

‘’Hallo… halloo.’’
‘’Ee halo shangazi mzima?’’
‘’Mi mzima hofu kwenu tu?’’ nilijibu
‘’Sisi wazima ila tunatatizo limetokea’’
‘’Tatizo gani tena sangazi? Nilishtuka sana kwa kusikia vile
‘’Ndio kunamsiba binamu yako kevi kafariki leo jioni ghafla tu’’
‘’Unnasemaa?amefariki? niliuliza kwa sauti huku machozi yakinitoka
kwenye macho yangu
‘’Ndio shangazi amefariki leo jioni’’
‘’Alikuwa anaumwa?
‘’Hapana alikuwa mzima tu imekuwa ghafla tu hali yake ilibadlika
majira ya saakumi na mbili ndo ametuacha ‘’
Nilishikwa na kigugumizi huku machozi yakibubujika maana ndie aliekuwa
mtu wangu wa karibu sana hata kipindi niponae mbali alikuwa hachooki
kuntafuta
‘’Sawa kesho nakuja shangazi ,tuliongea na kukata simu ‘’
Nililia sana usiku ule pale nilipoiona namba yake na meseji zake
kwenye simu yangu leo hiii sitaiona meseji yake ikiingia kwenye sim
yangu sitaweza kusikia utani wake na sati yake masikioni mwangu
nilijikuta nazidi kupata maumivu mara ghafla mlango ulifunguliwa……

TEGO

Epsod 2
Mara ghafla mlango ulifunguliwa…….endelea nayo…
…..nilipotazama alikuwa ni amina
 ‘’hivi hikichumba unafungua kama chumbani kwako ustaarabu gani
huu’’;Niliongea huku nikitetemeka kwa hasira
‘’Samahani sanji kama nimekukwaza ila haya yote sababu nakupenda’’
;aliongea huu akiwa amenikazia macho san
‘’Nikwambie mara ngapi labda ili unielewe sikutaki amina sihitaj mtu
kwenyemaisha yangu nakuchukia ‘’; yaikuwa ni maneno makali sana
yaliomfanya amina aanze kumwaga machozi,
‘’Hata kma unanichuki sitoacha kukusumbua ‘’
‘’Poa tu toka nje’’, nilijibu kwa hasila mno
‘’Sitoki kama nimeingia kwa ridhaa yangu nitatoka kwa ridhaa yangu’’
‘’Toka nje nitakupiga toka’’ ; yalikuwa ni majibizano yalionifanya
nipande hasira na kumsogelea na kumpiga kibao’
‘’Paaaaa’’ ; alinsukuma na kuondoka nje

‘’Hii nyumba mi nahama wamezidi kuninyanyasa’’Niliongea na kwenda
kupumzika ili kesho niende kijijini asubuhi kulipokucha nilijiandaa
na kuelekea kijijini nilifika na kupokelewa nilikuta watu wengi sana
wamejaa nilipokelewa na kufaanya shughuli ya mazishi tulipomaliza
siku iliofuta tulikaa kikao cha familia alisamaa baba mkubwa ili
kuongoza kikao’’
‘’Jamani nashukuru tumemaliza mazishi ya mpendwa wetu ila ninajambo
nataka niwaeleze, hiki kifo sio cha kawaida ni cha kutatanisha sana
hivyo nashauli tumuite mtaalam aje atuagalizie familia yetu,
Lile swala lilizua mjadala mzito sana maana tulikuwa ni watu wa imani
tofauti tofauti muafaka ulifika kuwa aletwe mchungaji ili aombee Siku
ilipofika aliletwa mchungaji na tulifanyiwa maombi.
Tulikaa kama siku 4 hivi huku tukisubilia harobaini siku ya nne
tulivyoamka asubuhi tulipatwa na msiba wa mdogo wangu maana sisi
tulizaliwa sita kaka angu na wadogozangu wanne yaani mimi ni mtoto wa
pili familia yetu ,msiba ule ulituchanganya sote maana ni kama wa
binamu yangu ni ghafla tu tulipomaliza mazishi tulimwiita mganga ili
atungalizie familia yetu,

‘’Dah! hii familia mpo kwenye wakaati mgumu sana’’
‘’Kwanini mganga’’; aliuliza shangazi
‘’Familia yenu ipo katikati ya tego kubwa sana na hilo tego
limetokana na kevi’’
‘’Kevi?’’ ; wote tulistaajabu kwa kusikia vile,
‘’Ndio kevi alifanya ualifu wa kuiba mfugo kwa mama mmoja nje ya
hiki kijiji, ila siwezi mtaja’’
‘’Tutajie mganga twende tukaombe radhi,’’ tuliongea huku tukiwa na uoga sana,
‘’Siwezi waambia na hata kama mkaenda kuomba radhi hamtweza maana huyo
mama ameshapoteza maisha ila bado linazunguka katika familia yenu
njia ya kuokoka dawa ya kupona ipo’’
‘’Kama ipo tusaidie mganga ,’’aliongea shangazi huku akiwa na uoga sana
‘’Sawa kama mpo tayali inahitajika vijana watatu’’
‘’Tupo mkuu,’’; tuliitikia vijana wote tuliopo katika kikao
‘’Kama mpo itahitajika mtoke hapa muende mlima sinjo uliopo
mashariki mwa hapa juu yamlima huo kuna pago mtachukua hi dawa
mtamwaga mlangoni alafu mtaingia mkishaingia inahitajika mkachukuwe
mgomba mlete hapa leo juma tatu kabla juma tatu ijayo inahtajika
muwe mmeshawasili ‘’
Sawa tuliitika na kuchaguliwa watu watatu nikiwemo na mimi siku
iliofuata tulichukuwa kila mtu na baiskeli zetu huku tukiwa tumebeba
begi la chakula safari ilianza…..

TEGO

Epsod 3

Endeleaa nayo…..

Safari ilianza tulitoka alfajiri sana tulitembea sana sikuile hadi
usiku huku tukiwa tunaulizia huo mlima sijo tulitembea sana hadi
ilipofika jioni tulilala kwenye kichaka kimoja hivi hadi hasubuh,
illipofika tuliamka na kuendelea na safari siku iliofuata tulindelea
na safari hadi usiku kwa bahati mbaya giza lilitukutia tukiwa kwenye
pori kubwa mmno ilibidi tusogee hadi tutakapokuta makazi ya watu
tulitembea sana baada ya muda tuiona kwa mbali kunataa inawakaa libidi
tufuate kule taa inakowaka zilikuwa ni nyumba kama tatu hivi zikiwa
zimekaribiana,

‘’Ngo..ngo..ngo..ngo;’’ tuligonga mlango, baada ya muda mlango
ulifunguliwa alitoka binti mmoj mrembo sana

‘’Samahani dada mzee tumemkuta?’’ Tuliuliza
‘’Yupo ila kwa muda huu kalala.’’alijibu huku akituangalia kwa makini sana
‘’ sawa ila samahani dada tulikuwa tunaomba hifadhi ya kujistiri
hapa kwa siku hii ya leo tafadhari’’ ;niliongea ili tuweze pata
msaada

‘’Mh! kwani nyie mnatokea wapi?’’ ;aliuliza huku akionyeha mshangao
‘’Tumetoke mbali kidogo na hapa ila kunasehemu tunaenda kwahiyo
tunaomba hifadhi’’

‘’Sawa ngoja niongee na baba.’’ ;aliingia baada ya muda alitoka nje
‘’Amekubari mnifuate ‘’;tulimfuata hadi ndani ilikuwa ni nyumba yenye
ua tuliingia hadi ua
‘’Mtalala kenye chumba kile sawa’’
‘’Sawa’’ ; alitukabidh chumba kimoja killichopo nyuma ya nyumba ile,
tulikubali na kuingia ndani ili tujipumzishe asubuhi kulipokucha
ilikuwa ni siku ya halhamisi toka tuanze safari tuliamka ila
chakushangaza mwenzetua likuwa ameshikwa na homa kali sana ilibidi
tumuite baba mwenyenyumba ,

‘’Vipi tena mbona mwenzenu yupo hivyo kunani?’’ ; Aliuliza baba mwenyenyumba
‘’Anaumwa inabidi tumpeleke hospitali ‘’
‘’Hahahaahah hospitali?’’ ; Alionyesha kushangaaaa ssana neon hospitali
‘’Ndio hospitali,’’
‘’Huku hamna hospitali ni miti shamba tu ,’’
‘’Ha! Kwahiyo huku hakuna huuduma za jamii?’’
‘’Hatuzijui hizo sisi tunatibiwa na huduma za miti shamba tu,’’
;Tulishtuka sanaa kusikia hivyo tulihisi tumefika kijijini sana,
‘’Aha sawa kwahiyo matibabu yake tutayapateje ?’’ iliuliza kwaa udadisi zaidi
‘’Msiwe na shaka ngojeeni kidogo’’; aliingia ndani kenye nyumba
kubwa kisha akarudi akiwa ameshika kitu mkononi alipofika pale
alichukua kile kitu akakiweka mdomoni kisha akawa anampulizaa Yule
usoni Yule mwenzetu ambae alikuwa anaitwa jamari alimpuliza huku
akimzunguka baada ya muda akaaacha

‘’Huyu mwenzenu atapona, ila itahitajika akae hapaa ndani ya wiki
mbili vinginevyo jumapili hafiki anafariki ‘’

‘’Mh! Hadi jumapili wakati inatakiwa turudi jumatatu na kile
tulichoagizwa.’’; Tuliongea kwa sauti za chini tukijadiliana mimi na
mwenangu anaeitwa suma ,
‘’Hapana mzee tunaomba utupe dawa tumtibu huku tunaendelea na safari
,’’ ; aliongeaa hivyo suma tena akiweka msisitizo zaidi,,
‘’Hapana hamuwezi mtibu huyu inahitajika awe hapa ndani ya hizo siku’’
‘’Ila si kunasehemu tunahitaji tufike panaitwa mlima sinjo sijui
unapafahamu’’; ilibidi tumuulize ili tupate msaada wa kufika huko,

‘’Ahaaaa napafahamu kumbe ndio mnakoelekea.’’ alijibu kwa shahuku
kubwa tuliona nuru ya kufika inakaribia ilibidi tukubari alivyokuwa
akihitaji ila tulikubaliana tutakaa ndani ya siku moja pale
Usiku ulipofika majira kama ya saaa moja hiivi ghafla hali ilibadilika ………….TEGO

Epsod 4
Ghafla hali ilibadilika ……endeelea nayo
Mvua ilianza kunyesha kubwa saana na radi zikiwa zinapiga sana
tulilala hadi asubuhi aubuhi kulipokucha niliamka nilienda kwenye
begi langu na kuanglia baadhi ya vitu nilishtuka baada ya kutoina
ile dawa ya Yule mganga ,

‘’Oya hivi ile dawa kunamtu kaichukuwa ile dawa ya tulio pata kwa
mganga ?’’ niliuliza ili nipate uhakika
‘’Hapana icheki vizuri kenye begi toka ulivyokabidhiwa wewe hakunamtu
alieichukua’’
Nilichnganyikiwa sana nilivyoisikia hivyo nilitafuta ile dawa kila
kona sikuiona niliishiwa nguvu baada ya kutoiona ile dawa niliamini
uwenda tuliiangusha niliamua kutoka nje labda naweza iona
ikufanikisha kuiona nilizidi kuchoka ikabidi nimueleze mwenyenyumba,
‘’Samahani mzee sisi kunaadawa tulipewa na mtu tuipeleke huko mlimani
ila cha kushangaza imepotea katikamazingira ya kutatanisha sana’’

‘’Hivi we kijana nani unadhani atakuwa kakuibia hiyo dawa yako au
unaniivunjia heshima ‘’; aliongea huku akiwa kakasirika sana
 ‘’Hapana mzee nilikuwa nakueleza kama unaweza tusaidia tusaidie maana
tumebakiza siku chache tu ya kukaa’’ niliongea kwa upole sana baada ya
kuona kama nimemkwaza Yule mzee

Hebu funga mdomo yaani kuwapa hifadhi, leo hii mnataka kuniammbia mimi
mwizi eti au ndio’’’’ tenda wema nendazako usingoje shukurani ?’’
aiongea kwa ukali sana hadi ilinifanya niogope niliondoka na kuelekea
nje kwa wenzangu

‘’Vipi mbona mnyonge hivyo?’’ aliniuliza suma
‘’Amna yaani nilichokipata huko ni bora nisingeenda’’
‘’Kwanini?’’ Niliwasimulia yote yaliotokea huko
‘’Ila yupo sahihi maana katupa hifadi, alafu leo hii tunampa kesi ya uwizi’’
‘’Ila sio kesi tulienda kuuliza kuuiza sio ujinga suma’’ ;
nillijibu kwa hali ya kutoridhishwwa na kilichonikuta kule,

‘’Dah! tuachane nayo hayo kwahiyo tunafanyaje
‘’Ila mi nahisi kitu Yule mze mwanga yanii anaimani za
kishirikina,’’; aliongea hivyo jamari huku kiwa na uoga sana
‘’We acha zako hizo yani nakutibu lafu unasema mshirikina we acha
kulaani’’ alliongea suma kwa kucheka sana,
‘’Haapana silaani unajua sikuile kipindi ananipa tiba alikuwa kwa
chini alikuwa ananisukumm na kidole cha mguu’’

‘’Sasa ndio dawa ilikua inaingia vizuri, hahahaha yani na wewe acha
kumzingizia mbaba wa watu mabaya’’ ;kipindi tunaongea ghafla alikuja
Yule binti chumbani kwetu alifungua bila kupiga hodi,

‘’Vipi dada kunatatizo mbona hivyo ‘’ tuliuliza ,;Alituangalia kwa
jicho kali sana na kusema
  ‘’Nahitaji kitu kwenu’’
‘’Kitu gani ?’’ niliuliza kw mshangao
‘’Naitaji penzi kutoka kwenu wote watatu,’’ ; tulichek sana tulimuona
chizi kabisa
‘’We unatutakaje sisi watatu kwa mpigo acha zako tunakuheshimu sana ‘’
‘’Hamniamini au?’’aliuliza huku akianza kutuonyesha maungo y mwili wake,
‘’Sio hatukuamini hatutaki yani we nendaa zako jiheimu bwana,’’:
nilijibu huku tukicheka alituangalia na kuondoka kwa hasira sana
‘’Mademu wengine bwana we sisi watatu tunakuwaje na yeye mjinga kweli
huyu’’ ;tulijiongelesha huku tukia tunafurahi sana
Usiku ulipoingia tulilala ili kuisubiia siku ya jumapili kipindi nipo
 usingizini nilihisi baridi kali sana mithili ya barafu yaani kali
mnoo ghafla nilihisi kushikwa na mtu……

TEGO

Epsod 5
Ghafla nilihisi kushikwa na mtu……edelea nayo

Huku nikisukumwa ila kwa mbali nilisikia sauti ikiniitiita sanji
sanji sajii amka uone
Nilifumbua macho kwa uchovu sana maana nilihisi uchovu uliopitiliza
nilipofumbua macho na kutazama sikuamini niichokiona tulikuwa tumeloa
matopemwilizima na tukiwa tumelala uwani huku pembeni yaakiwa
mjembe matatatu yakiwa yanamatope mengi mno

‘’ Ha vipi tena mbona hivi?’’ Niiliuliza
‘’Yani hata siwenyewe hatujui tumeamka tukiwa hapa sanji inamaanisha
sisi huwa tunalimishwa sanji ‘’aliongea kwa uchuku sana jamari,Kipindi
tupo kwenye mshangao alitokea Yule baba
 ‘’Hivi nyie vijana yani mpo humu ndani kwangu bila kufanya kazi nyie
akina nani hasa lazima mnifanyie kazi zangu hebu tokeni hapa’’
;Tulitoka mbio na kwenda ndani
‘’mi si niiiwaambia huyu mzee si mnona vimenza kututoke puani,’’
:tulichoka sana tena sana hasa kwa kupotelea na dawa ambayo ni muhimu
sana katika afari yetu hatukuweza kupata nguvu ya kuoga wakati ule
maana tuliaanza kuon mwisho wa safari yetu umeishia pale
Kipindi tunajiuliza nini tufanye tulisikia kishindo cha ajabu nje
tulifungua mlango na kuangalia nje tulimuona yule baba kachukuwa kinu
kaweka katikati ya uwanja ambapo ni katika nafasi iliozungukwa na
mabanda(uwani) pia tulimuona Yule binti akija na vitu kwenye ungo
Walichukua chungu kilichokua na kibuyu ndani yake kikiwa pamoja na
kitu kama mkia wa g’ombe hivi wote walikuwa wamevaa nguo nyeusi Yule
baba alichukua ule mkia wan g”ombe na kuanza kuulusha lusha huku ule
ungo wenye kibuyu kikubwa akiwa ameushika mkono wa kushoto huku mkia
akiuzungusha pande zote zote za kile kinu alizunguka kama mara tatu
hivi alisimama na kuchukua kile chungu na kumkabidhi Yule dada,

‘’Dah tumeisha sanji kwa hiki kinachotokea ni kifo yani’’, aliongea
kwa uwoga sana suma,;
‘’Tungalie mwisho wake nini “ nilijibu huku nikiwa natetemeka sana,;

 alichukuwa ule mkia na kuingiza kunako chungu kisha alikuwa anafany
kama anapuliza hivi alipuliza mala tatu ghafla tuliona moto wa ajabu
ulitoke na ilisikika sauti kama ya radi hivi angani yani alikuwa
anawanga asubuhi kweupeee
Bada ya hapo alichukua kile kinu alikigeuza na kule kwenye mdomo
alikugeuza upande ambao kipo chumba chetu alifanya tena vile vile yani
radii ya ajabu ilitokea ilitufanya tufunguemlango na kuanza kukimbia
ovyo tulikimbia ovyo hadi nilipofanikisha kutoka nje nilisimama kando
na ile nyumba huku nikiwa nawaza hali ya wenzangu niliowaacha ndani
mara nilimuon suma akitoka mbio mule ndani na kuja upande niiopo mimi
aliangua mbele yangu kama mzigo
‘’Puuu’’ ilitamani kucheka ila nilishindwa
‘’Sasa vipi hali ya jamari sasa;’’ tuulibaki tukiulizana bila kupata
jibu huku tukiwa tumebakiza siku moja mbele yani karibia siku ya
kupeleka mgomba kijijini kwetu
 huzuni ilinitanda baada ya kuto muona jamri akitoka nje ten
nilihofia sana kutokana na afya yake kutokuwa vizuri kipindi tuo
kwenye kiulizo mara akapita mama mmoja hivi mbae hatukufaham wapi
alikotokea

‘’Vipi nyie vijana mbona mnalia mnaogopa nini sasa wakati ni chaguo
lenu’’; aliongea Yule mam huku akisogea karibu yetu
‘’Chaguo letu?’’ Tuliuliza kwa mshangao
‘’Ndio chaguo lenu la kuhitaji kufa’’
Apana mama sisi… kabla sjamalizia kuongeyule mama alivua nguo yake
aliyoivaa kwa juu alipovua alikuwa amevaa kkaniki nyeusi ni mtu wa
aievaa mairizi shingoni kwenye mkono na zingine zikiwa zimeshonwa
kwenye nguo ‘,Tulishituka na kutaka kukimbia
‘’Msikimbie mi nahitaji kuwasaidia’’
Alitooa kioo kimoja na kukionyesha kule kwenye nyumba…..


TEGO

Epsod ya 6

alichukua kioo kimoja na kuonyesha kule kenyenyumba …….
Alichukua kitu chenye muonekanooo kama pembe ndogo la mnyama
alinyoosha kule kenye ile nyumba .alituangalia na kutuambia
‘’kaeni nyuma yangu’’ kule Yule menzenu wanataka kumfunga kwenye kinu
na ile dawa ipo pale kwenye kile chungu kahiyo kunakazi nzito sana ya
kumwokoa mwenzenu
 Alichukua cheni yake moja yenye irizi na kunivisha mimi na nyingine
livisha pale kwenye kioo alianza kuongea maneno ya ajabu mala radi
ilipiga na kupig pale tulipo kuwa sisi yaani tulisukumwa na ule
mshindo wa radi ila mimi pamoja na mwenzangu hatukuweza mwachia
tulimshikilia kwa nguvu sana tuliinuka na kusimama tena upya

‘’Wewe usiekuwa na irizi nenda pae kwenye ule mti wa kisamvu kasimame
chini yake’’;sumaa alikimbia na kukaa chini ya ule mti mimi nilishika
nguo ya Yule mama ili nnisiiweza kaanae mbali
Wewe kijana nenda kwenye ule mlango mlioingilia siku ya kwanza
ukapite pale maana hapa bila hivyo kuondoka itakuwaa ngumu nilikimbia
hadi kwenye ule mlango nilipotaka kupita tu nilihisi mtu kanisukuma
nilianguka chini kama mzigo

Nilisimama na kuvua ile irizi na kuitanguliza mbele nilijikutsa
nafanya mambo ambayo sikuwahi yafanya nliiweza ingia hadi ndani ile
natokea uwani niliogopa baada ya kuona radi kali zikipiga zikielekea
pale aliposimama Yule mzee, nilipoangalia vzuri nilimuona yule mama
katikati yao akiwa anapambana na ile familia niijitosa na kwenda pale
kwenye kinu, yani akili sijui nilizipata wapi yaani niliamini ile
cheni ya irizi sana nilipofika palenilitaka kushia kile kinu
niisukumwa na yule dada
Niliinuka na kumuangalia nilimfuata kwa kasi sana na kumkumbatia
kipindi nimemubatia nilihisi maumivu makali sana mgongoni mwangu
yaani siku iyo niliingia kwenye vita ya wachawi nilimkumbatia ka
nguvu sana nilichukua ule cheni ya irizi na kumvisha yule dada
taratibu Yule dada alilegea na kuanguka chini nilimburuza hadi pale
kwenye kile kinu niligeuza na kuchuku kile kinu huku nikikionyesha
kichani mwa Yule dada nilimvua taratibu ile cheni huku nikielekeza
kwenye kile kinu
Nilifanikisha kuweka ile cheni kunako kile kinu na kumuona jamari kiwa
ndani yake alionekaana ni mdogo sana niimshika na kumvuta nje
nilifanikisha kumvuta yani radi ziliendelea kupiga huku kule wakiwa
bado wanapambana nilimchukua jamari nilichukua Yule binti na kutoka
na nje ile tumetoka nilichkua baiskel zetu na kutoka nje ile natoka
nje tu radi ili ilitoka ndani na kupiga katika ule mti wa kisamvu na
kukauka palepale ghafla kule ndani ukimya ulitawala huku ule ukufu
ulianza kunanibana sana baada ya muda uliacha kubana na kutulia
niliona kama paka hivi akifika mbio huku tulipokuwa tumesimama…… 

Post a Comment

Previous Post Next Post