RISASI YA KICHWA 03




 Genero Tonga na vijana wake walikuwa wameshavamia bandari na kuanza kuchinja walinzi moja moja. Na ndipo genero alimuaru sneaper atafute Sit zuri ambayo ataweza kuwalinda kama kutakuwa na jeshi lolote litakalo kuja kuwavamia. Waliyona meli ya ki misri ikiwa imetia nanga bandarini na ndani yake kulikuwa na walinzi walio toka misri.

"Abdi mimi nawew na majeshi machache tutaingia ndani ya meli . na rose na jeshi lako mtakaaa nje kudumisha ulinzi.

Walingia ndani ya maji na kuingia katika meli ya ki misri na kuanza kuchinja walinzi walikuwa kilinda ile mali. Na ndipo alimbakisha mlinzi wa kimisiri na kuanza kumuaji huku wakiwa wamemnyooshea pistor . 

Genero alimuliza kwa kiarabu yule misri kuwa mali zimewekwa sehemu gani? Lakini yule mlinzi alinyamaza kimya kwa ujeuri tu. Na ndipo genero alimuona uyu mlinzi hawezi kumjibu chochote alikoki pistor yake ndogo na kumshoot risasi ya mguuuu yule askari.


Askari wa kimisri alipiga kelele kwa maumivu aliopata kwa kupigwa risasi ya mguu.

" nakuliza tena kwa mara mwisho mali zimewekwa sehemu gani". Aliuliza genero kwa jazba kali huku akiwa akimkodolea macho.

Yule askari alisema Mali zilipo fichwa zipo katika store ya meli ambayo ilikuwa chini kidogo ya meli.  

Na ndipo genero alimpiga risasi ya kichwa yule askari wa ki misri. Na kuelekea zilipo kuwa Mali .

Abdi aliziona masanduku takribani matano na ndani yake kulikuwa na vipande vya dhahabu za kila aina.


"Chukuweni dhahabu zote na Tiaeni katika mabegi yenu" alizungumza genero na kuwalakisha vijana wake.

Sneaper alipokuwa nje kule kwa ajili ya kudumisha ulinzi aliaza kuona kuna viboti vidogo vidogo na kulikuwa na jeshi la majini tena walikuwa wengi mno mpaka sneaper akaaza kupatwa na hofu sasa maana majeshi ya majini walikuwa wengi mno. Na ndipo alipo amua kuwasiliana na genero Tonga na kumwambia kuna majeshi ya kiserikali wameshazunguka iyo meli. 

Genero alivo sikia hivyo alikazanisha vijana wake wachukuwe Mali haraka haraka. Lakini kabla hawajamaliza kuchukua Mali waliaza kusikia Tangazo nje ya meli walikuwa wakiiiba.


"Naomba mujisarimishe nyie wote kabla hatujaamua kuwashambulia nyie nyote mulikuwa katika meli hiyo." Alizungumza meja wa jeshi la majini kwa kutoa tahadhari.

Lakini genero Tonga aliamuru vijana wake wajiandae na mashambaulizi hawezi kamwe wakamwate na jeshi la kiserikali.

Na ndipo genero alitoka nje kwanza peke yake huku akiwa ameshikilia pistor ndogo mkononi kwake. Meja alivo muona nae akamuru vijana wake wamuweke target genero Tonga.

Genero aliposimama alikuwa anangaliana uso kwa uso na jeshi la kiserikali na ndipo alipo amuru vijana wake wajitokeze washambulie vile viboti vya kijeshi. 

Basi waliaza kushambuliana ana kwa ana kwa kutumia bunduki zao . mashamulizi yalikuwq makali Sana watu wa vijana genero Tonga walishambuliwa sana na jeshi la majini.

Sasa genero Tonga akawa anajiuliza kwanini snepear ashambulii wale wanajeshi . na kila akijaribu kuwasiliana na snepear na simu yake apokei simu. Na ndipo akaingiwa na Imani ya kuwa kule alipokuwa sneaper tayali atakuwa ameshakufa . na ndipo Abdi alipo mwambia genero wake waondoke maana kama mali washazipata .

Lakini sneaper pale alipokuwa hakutaka kuwashambulia jeshi la serikali bali alikula kiapo lazima amuendoshe Abdi duniani. Hivyo alikuwa macho yake yote yalikuwa yana muangalia Abdi sehemu alipo. Na ndipo alimuona Abdi alipokuwa akiendelea kushambuliana na madui zake na abdi alikuwa anawadungua vizuri tu maadui zake.

Sneaper alimuweka target ya kichwa vizuri Tu na kumlenga risasi ya kichwa Abdi. Genero alishangaa na kumuona Abdi akidondoka katika maji tena akiwa huku amebeba lile begi la vipande vya dhahabu .

Genero alishangaa kumuona Abdi kijana wake wa nguvu akiwa amepigwa risasi . Tena risasi yenywe ni ya kichwa . aliacha kushambuliana na jeshi la majini na kuangalia kwa umakini kule risasi ilipotoka na kule risasi ilipotoka na ndipo alipo muweka kule kijana wake sneaper.

Akiwa anazidi kushangaa genero anajikuta anawekwa chini ya ulinzi na jeshi la majini.

Na hatimae genero alingia mikononi mwa serikali .

Vyombo vya habari vilitangaza juu ya kukamatwa muarifu mkubwa aliekuwa anasumbua serikali kwa mda mrefu.

Muheshimiwa rais alistushwa sana kusikia meli iliokuja kutoka misir imevamiwa na magaidi lakin kwa Bahati ya mzuri wameweza kushambuliana nao mpaka wameweza kurudisha baadhi ya Mali zilizo taka kuibiwa. Hivyo mahakama ikatoa hukumu ya genero kwenda gerezani kwa kesi ya uwalifu na uwizi.


Katika fukwe moja ilio kuwa kalibu na bahari kulikuwa na mzee moja ufukweni akiwa anakarabati mtumbwi wake anaoutumia Mara nyingi sana kwenda kuvulia samaki. Lakini katika fukwe anauwona mwili wa binadamu ukiwa upo kalibu na fukwe na ndipo yule mzee akaenda kuutizama ule mwili na kuwangalia yule mtu mzima au.........



ITANDELEA........ 

Post a Comment

Previous Post Next Post