RISASI YA KICHWA SEHEMU YA MWISHO (14)

 Jeshi la mtu moja agent Neema alizidi kutafuta kwenye lile poli sehemu ilipo tokea risasi.......


Genero Tonga alikuwa wa kwanza kuwaona wakina Abdi wakitaka kuaza kupambana ila alisimama na kutaka kuangalia uwezo wa Abdi ukoje......


 Abdi alimsogelea sneapear na kuaza kumpekea ngumi za uso... Mpaka sneaper alidondoka chini... Maana zilikuwa ngumi za chereani zilimpega fasta fasta..... Abdi alinyanyuka kwa kujinua kwa kujifuta kwa juu na kukunja ngumi na kuaza mapigano na Abdi....

Abdi alishambuliwa kwa mateke ya haraka haraka aliyofanya ayumbe na kurudi nyuma kwanza huku akiwahi kuyaondoa yale mateke kwa mikono yake miwili na kisha kukaaa sawa na kumuwahi kwa haraka kwa kumpiga sneaper teke la mzunguko lilomfanya sneaper hawaone kizungu Zungu kwa kupigwa teke zito mpaka chini........


Baada ya kupigwa lile teke na Abdi.... Sneaper alishindwa kunyanyuka Bali alibaki kuogelea maumivu huku damu zikimtoka tumboni..... Abdi alimtazama vizur kwa kumuangalia kipi sababu zinazo mfanya atokwe na damu kwenye tumbo.....


Genero Tonga alikuwa tu anangalia ule mchenzo unavokuwa mpaka Sneaper ameaza kutokwa na damu tumboni.....



Wakati mambo yote yanatokea pale agent neema naye alikuwa kashafika katika lilo eneo na kuaza kuwanyatia kwa taratibu taratibu wakina abdi walikuwa na kuwona mchenzo mzima wa mapigano..... Hivyo aliwahi haraka haraka kabla ya abdi hajamshika sneaper pale chini maana alijua tu Abdi anataka kumalizia mwezake kumbe sivyo.....


Abdi alimsogelea kwa ukalibu pale alipodondoka chini na kuaza kumkagua ni sehemu ipi alipo umia .... Alistuka kwa kuona kisu chake mwenyewe sneaper kimezama katika mgongo wake mwenyewe.......

Na ndipo alikumbuka. Alivompiga teke la mzunguko kwa sneaper na jinsi lilovoweza kumgaulausha mpaka chini alikuwa ameweka kisu kwenye kiuno chake na ndicho kilicho muwa sneaper........

Abdi na Frida wakiwa wameshikana wakimshangaa sneaper anavo kata roho...... Mala....


"Nyie nyote wekeni mikono juu haraka mikono juuu weka mikono juuu" yalikuwa maneno ya agent neema huku akiwaoneshea bunduki wakina Abdi na mwezie Frida.....

Frida alikuwa na hofu sana walivo oneshewa pistor na askari 

Abdi nae alistuka akawa hana chakufanya ....

Na ndipo agent aliaza kuongea huku akiwa anangalia mwili wa sneaper kama ni mzima au laa akiwa anashamgaaa tu sneaper .... Abdi alinyanyuka haraka na kumuwahi agent Neema na kumpokonya pistor yake na kumuweka telo agent neema....


"Haya tulia kama ulivo".... Aliongea Abdi huku akimtishia pistor.... Agent...

Agent alitiiii na kuwa mpole kama maji mtungini...

Sasa akiwa anamuweka telo Agent Neema mala anasikia anaitwa abdi na sauti ya kiume nyuma yake.....

Na ndipo aligeuka haraka kwa tahadhali na kumuona Frida akiwa tayali akaekewa Bisu katika shingo yake........


Na ndipo Abdi alirudisha kumbu kumbu baada ya kumuona generO Tonga..... Na kukumbuka ile siku ya mwisho walikuwa wamekwenda kufanya uvamizi katika meli ya watu wa misri ambao ulikuwa na mzigo wa muheshimiwa rais.........


"Abdi....... Umebadirika kabisa umekuwa tofauti na zamani.. Umeuwa ndugu zako kwa kisa huyu mwanamke.... Si ndio.... Kumbuka nimekuokota wapi wewe ulikuwa chokolaaa kabisa usikuwa na wazazi... Na ulikuwa unakuka vyakula vichafu ma dampo ..... Nimekuchukua na kukufundisha kila kitu na leo umewauwa.... Ndugu zako...wote... Sasa huyu malaya na muondosha duniani....." Alizungumza genero Tonga... Huku akiwa amemuwekea bisu la shingo frida....


Abdi alibaki ameduwa tu kwa maneno anayo ambiwa na genero Tongaa aliishia na nguvu gafla tu........ Lakini agent neema aliliona lile na kumuona genero Tonga anarudisha mkono wake nyuma na kuweka sawa kwa ajili ya kutaka kumchinja... Frida...


Agent aliwahi kwa haraka na kupokonya pistor yake Abdi... Na kushooot kwa haraka pale alipo simama genero Tonga.... Frida alistuka na kufumba macho kwa kujua ndo mwisho wake ndo umeshawadia tayali..... Lakini anakuja kushangaa mtu alie mkaba anadondoka chini kama zigo vile la mchele....


Anamtizama vizuri genero Tonga amepigwa risasi ya kichwa Tena kwenye paji la uso........


Abdi alibaki kuchoka tu na ndipo alipodondoka chini kwa kuthilai.....


Agent Neema aliwaita jeshi la polisi na kuchukua maiti za watu wale walio uwawa katika kambi ya genero...

Serikali ilipata vitu vingi katika kambi ya genero hususa mabomu ya mbali na silaha kubwa kubwa za ushambulizi.... Na hivyo waliweza kuona nyaraka mbali mbali zikiandikwa jina la wazir wa mambo ya ndani aliyekufa..... Hivyo walibaini kuwa wazir nae alikuwa msaliti wa nchi yake......


Abdi aliguuza kidonda chake na kuaza maisha mapema na mahusiano na doctor Fridaa........




  MWISHO 
BY DKINGA2015

Post a Comment

Previous Post Next Post