IN'BOBO 11 lovestory

Ilipoishia.

"nimesema achana nae mbona unakuwa hunielewi??"niling'aka.kibaya sasa simu ilikuwa jirani na pili,kwa hiyo alichofanya pili alimua kuichukua na kuipokea yeye,aisee kilikuwa nikitendo cha ghafla ambacho sikukitegemea.

"Hellow"pili aliongea baada ya kupokea simu.

ENJOY.

"Hellow.....hellow.....helloooo"pili aliongea mfululizo,nadhani hakuwa akipata ushirikiano kutoka kwa aliyekuwa akizungumza nae na ndio maana neno 'hellow' alilitaja mara kadhaa.muda huo mi roho ilikuwa inanipwita balaa,manake nilijua lazima pili angezungumza na mariana tu kivyovyote vile,lakini ninachoshukuru hakukuwa na maelewano ya kimawasiliano hivyo kufanya mazungumzo yasieleweke.

"Tunda una bahati nakwambia......yani huyu kikaragosi angeongea mbona angenitambua"pili aliongea baada ya kuiweka simu yangu chini.

"Ushaanza wivu wako wa kijinga,unajua mi sipendi onhoo..."

"heeee nisikuonee wivu kisa nini ilihali we ni bwana'angu,yani angeongea aone ninavyo mporomoshea mijitusi ya haja,mpaka angekoma kupiga simu...nakwambia"pili aliendelea kunipiga mkwara.

"Huo upuuzi sasa,ipo siku utakuja kutukana na ma bosi wangu mwehu wewe...."

****

siku na miezi zikazidi kusonga mbele,maisha yakiwa yanasonga vyema pasipo shida.mungu aliendelea kunijalia ridhiki iliyokuwa ikinifanya niendelee kuwa na afya iliyo thabiti pamoja na uwezo wa kutatua vijitatizo vyangu vya hapa na pale.ndani ya muda kadhaa mungu alikuwa amenijalia kupata vijifaida na kunipelekea kununua kajiwanja ambacho niliona kwamba siku za usoni naweza kujenga kijinyumba changu hapo,na kuendelea na maisha yangu ya siku zote.faida niliyokuwa nikiipata katika biashara yangu,niliweza kuigawa gawa katika sehemu mbalimbali ambazo niliona zinafaa.kwani ipo faida ambayo niliiingiza kunako pango la chumba nilichokuwa naishi,nyingine nikaweka bajeti ya msosi,nguo na mambo mengine madogo madogo.maisha kiujumla yaliniendea vizuri japo sio sana.

usiku wa siku fulani mishale ya saa nne nne hivi,nilipigiwa simu na namba ambayo kwa namna nilivyoiona haikuwa ya kawaida,kwani vile ilivyokuwa imeandikwa aisee ilinitia mashaka sana kuipokea.

"Hii namba itakuwa ya majini sio bure,maana haya manamba namba namna yalivyoandikwa mmmnhh!!sijawahi onaga namba kama hii kabla..."niliwaza hivyo huku nikiichunguza ile namba kama ni ya majini kweli sambamba na nilivyokuwa nikifikiri au la(lakini zilikuwa ni fikra zangu tu zisizo na ukweli,sidhani kama majini nao huwaga wanatumiaga simu kama za wanadamu,bhasi tu ulikuwa ni ule uvivu wa kufikiri,ndio maana kwa haraka haraka nikajua kuwa hiyo namba ilikuwa ni ya majini)

"Lakini isijekuwa ni namba ya mtandao........,sasa ni limtandao gani lenye linamba la ajabu kiasi hiki....."bado niliendelea kuwaza,muda mwingine nikifikiri kitu kisha kujikosoa mwenyewe kana kwamba fikra zangu hazikuwa na ukweli.mwishoe niliikata ile simu ambayo namba yake niliiona kwamba haikuwa katika mfumo wa namba niliokuwa nimeuzoea kuuona.nakumbuka kuna siku niliwahi kusikia kuwa eti kulikuwako na namba ya ajabu ambayo ilikuwa ikitumiwa na mtu asiyejulikana ni nani.endapo namba hiyo ingetumika kukupigia,bhasi mpokeaji hufariki ghafla,mara tu apokeapo simu kutoka kwenye hiyo namba.kiukweli hicho ndicho kilinitia wasiwasi zaidi.cha ajabu baada ya kuikata simu kwa Mara ya kwanza,muda kidogo ikaanza kuita tena.namba ile ile ilirudia kunipigia tena.nikaona hapa sasa naelekea kukumbwa na balaa,nilichofanya nikaikata kisha simu nikaizima kabisa.sikutaka tena upumbavu wa kupigiwa na ile namba isiyoeleweka.usiku huu sikutaka kufungua simu hadi kulipokucha asubuhi ndipo nilipoifungua.

Asubuhi hii,sikuwa na ratiba ya kwenda job kwangu kwa sababu mzigo sikuwa nao,hivyo nilikuwa nipo hapa nyumbani nimetulia tu,nikivuta muda niende kuzunguka zunguka mtaani,siunajua mara nyingi huwaga nipogo kazini,so hata nafasi ya kutembea huwa siipati,lakini leo niliona ndio siku yangu ya kuzurula mpaka bhasi.kama saa mbili,nilitoka kwenda gengeni kununua mkate kwa ajili ya kunywea chai,siwajua kwamba lazima tumbo lipate chochote kitu nyakati za asubuhi,bhasi iko hivyo.pale gengeni kwa bahati mbaya bhana nikakutana na sophie(nadhani unamkumbuka),bhasi nae alikuwa hapa gengeni sikujua alikuwa akinunua nini,ila katika wateja waliokuwa wakingoja huduma bhasi nae alikuwa miongoni mwao.aliponiona alinitolea tabasamu ambalo kwangu halikuwa na faida yeyote,zaidi niliendelea na mambo yangu tu pale dukani.Nikanunua mahitaji yangu kikaanza kutoka....

"Wee tunda ndo kujishaua au.....mbona unanipita kama hujaniona vile"Sophie aliongea kipindi nataka kuondoka.niligeuka kisha nikatikisa kichwa ishara ya kuipuuza kauli aliyoiongea muda punde.

"ndo nini hivyo" Sophie aliongeza swali.

"kwani we unataka nini Sophie mbona kama unanichokoza chokoza ilimladi niongee,shida nini?"nami nilihoji.

"Sio shida nini,salamu nayo imekuwa dili jamani"

"Ni dili ndiyo,kama isingekuwa dili nawe ungenisalimia kabla ya kungoja kusalimiwa"

"Mmmnh!!sijawahi ona mwanaume mwenye maringo kama wewe......haya baba jiendee zako mwaya,mbona salamu sio lazima"

Baada ya Sophie kuongea vile sikutaka kupoteza muda nikachapa zangu kuelekea maskani kwangu.huko nikaandaa chai nikainywa,baada ya hapo nikaingia kwa bafu nikafanya usafi wa mwili then nikarudi room kujikomelea viwalo,nilipotinga vyema nikatoka kuelekea misele(kuzuga zuga mtaani),mida hiyo ilikuwa kama saa tano hivi na ushee kuelekea saa sita.kwa mwendo wa aste aste nilikuwa taraatiiibu nikitembea kukata mitaa jirani na nilipokuwa naishi,sikuwa katika mwendo mkali sana,nilikuwa katika miondoko ya kawaida tu,siunajua sikuwa na pa kuelekea zaidi nilikuwa nauza nyago kitaa.huwezi amini,mwendo wangu wa taratibu ulinifikisha mbali sana pasipo uchovu wowote.ata daladala sikutaka kutumia,ilikuwa ni kiguu na njia tu.

Airport,ndiko nilikokuwa nimefika,ni umbali mrefu kiasi,kutoka nilikokuwa naishi hadi hapa uwanja wa ndege.nikiwa nafuata barabara ya mataa,sikuwa na haraka nilitembea kwa umakini mkubwa kukwepa boda boda na baadhi ya watu niliokuwa nakutana nao maeneo haya.bhasi bhana nikavuka mataa,ambako kwa nyuma yake kulikuwa na pub Fulani hivi ambayo kwa hapa mjini ilikuwa na sifa sana kutokana na kwamba maeneo hayo,yaani karibu na kwenye hiyo pub,mida ya usiku kulipatikanika wasichana wanaojiuza.kwa mbele kidogo,kulikuwa na barabara ambayo iliekea mashariki,yenyewe iliitwa jamhuri road,nikaishika hiyo na kuanza kutembea kuelekea mashariki,yani ilikuwa ni kiguu na njia tu,kwa sababu leo niliamua kutembea haswaa.Kwa mwendo wa dakika kadhaa nilikuwa nikitembea kulifuata barabara hilo la jamhuri ambako nilikata kulia,mara baada ya kufika katika kanisa la wasabato ambalo lilipakana na kituo cha redio cha tbc taifa,kanda ya kati.nikazidi kuchapulisha miguu kusonga mbele,mpaka nikajikuta ndani ya soko la sabasaba.

nikiwa nakata vichololo mule ndani ya soko,simu yangu ikaita,mpigaji ni mariana,nikapokea huku nikiendelea kupiga hatua za maana kusonga mbele.

"Huo uchocholo uliopitia umeuona?.....rudi nao huku ulikotokea mi nipo flemu ya tatu imeandikwa 'babyanka fashion',njoo umenipita hapa...nilikuona sema nilikuwa kama nakufananisha vile ndo nikaamua kukupigia."Mariana aliongea akinipa maelekezo namna ya kufika pale alipo,lakini hapo ilikuwa ni baada ya salamu za hapa na pale.ni kama alivyosema,yeye aliniona ila mimi sikuwa nimemuona,hivyo alinipigia kuhakikisha kama ni mimi.sikubisha kwa sababu nilikuwa katika matembezi ya kawaida niliamua kurudi nyuma kufuata maelekezo ya Mariana.na kweli aisee kwa kufuatisha maelekezo yake nilifika hadi pale alipokuwako mwanadada Mariana.

"Mambo zenu.......mko pouwa?"niliwasalimia wote niliowakuta mle ndani ya ile flemu,ni kama ilikuwa saloon ya kike lakini pia humo humo walikuwa wakiuza na nguo za kike pamoja na viatu.hata waliokuwemo ndani walikuwa ni wasichana kama watano hivi akiwemo na Mariana mwenyewe.

"tuko pouwa,mzima wewe?"mmoja kati ya wale mabinti niliowakuta mule kwenye flemu aliitikia kwa niaba ya wenzie.

"Mi mzima kabisa......,enhee Mariana ulinionea wapi manake kwa wingi wa watu humu sokoni sio rahisi kumtambua mtu kwa uharaka."niliitikia salamu kisha nikahamishia mazungumzo kwa Mariana.

"Mmnh!!lucky yani kwa nilivyokuzoea wewe,ata kama ukiwa kizani tu mi nakutambua,sembuse mchana kweupe hivi jamani,eti nisikutambue sini maajabu haya"

"Siwezi jua inaweza ikawa mchana na usinitambue pia"

"No haiji kutokea nisikutambue ata mara moja........,heeey girlz ngoja niwatambulishe.....huyu anaitwa goodlucky au ukipenda waeza muita lucky ama tunda,ni mtu wangu wa karibu sana tangu nimeingia mkoani hapa......"mariana alitoa utambulisho wa ghafla ambao sikuutarajia.

"Oky,ndio yule uliyetuambiaga enhee"mwanadada mmoja aliuliza,ni kama kuna stori yangu fulani ilifahamika kwa hawa madada.swali hili lilidhihirisha hilo.

"Wee nawe chaumbea hunaga kaba lione vile ng'ong'o ng'ong'o za nini mjinga mkubwa we"bhasi wale mabinti wakaangua vicheko kwa kauli ya Mariana.

"eeee.......mtajichekeshaje muda wote huo......ninyamazieni huko"Mariana aliwanyamazisha wenzie baada ya kuona kicheko kimezidi,kisha akaendelea....

"lucky....(aliniita then akaendelea)....,hawa unaowaona ni mabest zangu,yule pale anaitwa munah,yule mwingine maya,huyu hapa ni rusi,na huyu anaitwa grolia."mariana alimaliza kwa kuwataja marafiki zake hao huku akiwasonta kwa vidole.

"Nashukuru kuwajua."

"Oky,aaanmmh....lucky twende nikupeleke ulikokuwa ukienda bhasi au......"

"Sikuwa na sehemu maalumu ya kwenda,nilikuwa nanyoosha miguu tu siunaelewa kukaa nyumbani peke'angu sio poa....nikaona sio mbaya nikaja maeneo haya nizuge kidogo"

"Hahahaa,sawa.nifuate bhasi kuna mahala nataka unipeleke"

"Hamna shida twen'zetu"Bhasi bhana Mimi na Mariana tukaongozana kuelekea huko alikosema mariana nimpeleke.matokeo yake tukaingia kwenye daladala,safari ikaanza.yani mi ata sikujua ni wapi tunaenda zaidi niliendelea kusubiri hadi mariana atakaponiambia tushuke ndipo ningefanya hivyo.

Daladala ilitembea kwa karibu dakika ishirini na kitu.ndipo tukafika katika kituo ambacho mariana alihitaji kushukia,wote mimi na yeye tukashuka.kisha akakodi bajaji nyingine,kidume nikasema heee,kazi ipo.manake tulivyoshuka nikajua tumefika kumbe tena safari ilikuwa bado..duuu.nayo bajaji ikakamata barabara kuelekea kusini mwendo wa dakika saba,ikakata kona kwenye moja ya daraja kisha kwa mbele kidogo ikaingia kwenye nyumba Fulani ya hadhi ya kati,ikasimama hapo.Mariana akaniomba kushuka.katika nyumba hii kwa pembeni kidogo walijenga vyumba vya kupangisha hivyo baada ya kushuka tukaelekea kule ambako kulionekana vyumba vya kupangisha.Mariana akafungua moja ya chumba tukaingia humo.

"Lucky karibu.......jisikie uko kwako"nilisikia Mariana akinambia hivyo mara tulipoingia ndani ya chumba alichokifungua.nikawaza 'hee nijisikie kama niko nyumbani tena.....mbona hii kaliii!!", ila kwa sauti nikasema.......

"asante"

"hapa ni kwangu,ambako naishi.....hiyo nyumba kubwa ndiyo nyumba ya shangazi ninayeishi nae........"

"sawa.mbona hukuniambia kama tunakuja kwako,ilihali ulinambia kuna sehemu ulihitaji nikupeleke.......kwa hiyo sehemu yenyewe ndo hapa?"

"ndiyo lucky ni hapa,kama ningekwambia tunakuja kwangu,usingekubali"

"Kwa hiyo mjanja wewe si ndio?"

"Mnhhh.....mnhhh,siwezi jua"

"Duu sawa, kwa hiyo tunatoka wote au unaniacha niende mwenyewe we unabaki"

"tunatoka tena?........tusitoke bhana tutatoka baadae"

"Ok,kama we unabakia sawa,ila kwa Mimi lazima nitoke"

"Usinifanyie hivyo lucky jamani,unajua umekuwa kama mgeni wangu,so huwezi kutoka hadi nikuivishie chakula ule then mambo mengine yatajulikana."

"Lakini hatukupanga,Mariana.unanikosea unajua"

"nisamehe bure kama nimekukosea,lakini siwezi kukuruhusu uondoke kabla sijakupikia ule"

Ndo hivo bhana Mariana aliendelea kushikiria msimamo wake wa kutotaka niondoke eti mpaka aniandalie chakula,sikuwa na namna tena nililazimika kufuata anachokitaka Mariana.

*****

Mida ya saa kumi hivi tulikuwa mezani tukila msosi ambao Mariana aliuandaa,tulipomaliza tukashushia na soda za baridi kabisa kuusindikiza mlo wetu huo ambao tayari matumbo yalikuwa yameshauhifadhi.baada ya kupata vinywaji,Mariana alinitaka radhi kidogo kwa kuniambia kuwa anatoka then angerejea baada ya muda.bhasi Mariana akatoka na kuniacha mwenyewe chumbani.karibu nusu saa zima alikuwa hajarejea bado,mpaka dakika arobaini na kitu ndipo niliona mlango ukisukumwa na Mariana kuingia ndani,lakini akiwa katika muonekano mwingine tofauti na ule aliotoka nao,manake kwa sasa alikuja na min-sketi Fulani hivi ya blue,ambayo kwa chinu ilikuwa na malinda ya kutosha kuifanya ijichanue endapo Mariana angejizungusha,ufupi wa sketi hiyo aliyokuwa ameivaa Mariana,ulifanya nusu ya mapaja yake yabakie nje kiasi ambacho baada ya Mimi kuyaona tayari mambo yalikuwa si mambo ndani ya suruali yangu,ila tu nikajifanya kukausha.

"Lucky apo vipi nimependeza eeh?"Mariana aliniambia hivyo huku akijizungusha na kufanya taiti yake ionekane vyema kutokana na kuchanua kwa sketi yake ile baada ya kujizungusha kwake.maskini roho yangu ilianza kunipwita kwa kasi kama saa mbovu,tayari tamaa ya kumla maria iliniingia.manake ni kama alikuwa akinitega,nami kiasi Fulani kuanza kukubali kuingia kwenye mtego wake.

"Luuuckkyy,mbona hunijibu eti,nimependeza au nikazivue hizi nguo......."Mariana aliniuliza kwa mara nyingine tena baada ya mimi kushindwa kumjibu hapo awali.

"Yaa umependeza,uko vizuri"

"Kweli my?"

"ndio"

"Mmnhh asante,manake nilijua tu utaniambia sijapendeza"

"Umependeza sana tu"

"Eti eeh,nashukuru mwaya......asa mbona huji ata kunikumbatia lucky wewe.....kwa nini unakuwa na roho ya hivyo....jomoniii???"Mariana aliongea huku akiwa amenipigia pozi fulani hivi matata sana.kwa mitego aliyokuwa amekwisha anza nayo Mariana aisee sikuwa na budi tena kujikaza juu ya kumtafuna nguru huyu.kama mashetani ya huba yalikwisha kunipanda toka kitambo sana sema nilivunga tu.kama mshale nilinyanyuka na kumvaa Mariana ambaye alikuwa mbele yangu kwa umbali Fulani.mikono yangu nilifikia kuizungusha kwenye kiuno cha mdada huyu mwenye uzuri wa haja,vifua vyetu vikakutana na kuanza kubadilishana joto.pasipo kumkawiza huyu manzi,nilimuomba juisi ya bamia,toto pasipo shaka likaniletea lips zake na Mimi nilichofanya ni kuudumbukiza ulimi wangu kunako mdomo wa bibie huyu,daa walaah tena huo uhondo nilioupata hausimuliki kirahisi.

Itaendelea. 

Post a Comment

Previous Post Next Post