IN'BOBO 12 lovestory

Ilipoishia.

"Eti eeh,nashukuru mwaya......asa mbona huji ata kunikumbatia lucky wewe.....kwa nini unakuwa na roho ya hivyo....jomoniii???"Mariana aliongea huku akiwa amenipigia pozi fulani hivi matata sana.kwa mitego aliyokuwa amekwisha anza nayo Mariana aisee sikuwa na budi tena kujikaza juu ya kumtafuna nguru huyu.kama mashetani ya huba yalikwisha kunipanda toka kitambo sana sema nilivunga tu.kama mshale nilinyanyuka na kumvaa Mariana ambaye alikuwa mbele yangu kwa umbali Fulani.mikono yangu nilifikia kuizungusha kwenye kiuno cha mdada huyu mwenye uzuri wa haja,vifua vyetu vikakutana na kuanza kubadilishana joto.pasipo kumkawiza huyu manzi,nilimuomba juisi ya bamia,toto pasipo shaka likaniletea lips zake na Mimi nilichofanya ni kuudumbukiza ulimi wangu kunako mdomo wa bibie huyu,daa walaah tena huo uhondo nilioupata hausimuliki kirahisi.

*****

Alice baada ya kumaliza elimu yake ya juu alikuwa safarini kurejea nchini baada ya kupita karibu miaka mitatu na miezi kadhaa.Mara alipofika nyumbani kwao kitu cha kwanza kukifanya ni kuitafuta namba ya mtu wake wa muhimu kisha kumpigia.kwa bahati mbaya hakufanikiwa,simu haikuweza kupatikanika.alijisikia unyonge sana,alitegemea kuwasiliana na mtuwe huyo kabla ya kufanya chochote,lakini ikawa ndo hivyo tena,hakuwa amefanikiwa.

"Alice mama.....nadhani masomo yako tayari umekwisha hitimu,na najua wazi kwamba ushajitayarisha kunipokea kazi zangu kwani umri wangu we'mwenyewe unauona ulivyo......,natakiwa kupumzika sasa"mzee lemega,baba yake alice alikuwa amekaa kitako na bintiye Alice wakizungumza mambo kadhaa.

"Ni kweli daddy"

"Bhasi naomba ujiweke tayari kuyaanza majukumu yako.....lakini kabla ya hapo kuna kitu nilitaka ukifahamu na ukitekeleze kabla ya kuyaanza hayo majukumu yako mapya."mzee lemega aliongea kisha akaweka kituo,ishara ya kutaka bintiye aweke umakini kumsikiliza,kisha akaendelea....

"Ushakuwa sasa,unatakiwa kuwa na mwenzio.ninajua wazi kwamba kwa umri huu ulionao kivyovyote huwezi kukosa mpenzi,ninaomba kama uko katika mahusiano na mtu,hebu mlete nyumbani tumfahamu,ratiba zingine ndipo zitafuata...."mzee lemega aliongea kauli ambayo ilimshangaza Alice kwa kiasi kikubwa.

"Daaad...ddy........" Alice aliita lakini akashindwa kuendelea kwa sababu alikosa cha kuongea.

"Nadhani utakuwa umenielewa,ninakupa mwezi mmoja wa kulifanikisha hilo......"mzee lemega baada ya kuongea hivyo hakuwa na la ziada alijinyanyua kutoka kwenye sofa,kisha huuuyoo akatokomea chumbani kwake.huku nyuma alimuacha alice katika wakati mgumu sana.kwani alijikuta katika tafakari nzito kiasi ambacho kichwa chake kilijikuta kikishindwa kubeba mzigo wa tafakari zote kwa muda huo.

"Baba amefikiria nini kuniambia hivi.......alafu mie huyo mtu nitampata wapi,ilhali sina jamani.... Mbona baba ameniweka pahala pagumu hivi......"Alice aliwaza baada ya baba yake kuondoka mahala walipokuwa wakizungumzia.hakika alikuwa katika wakati ambao hakujua afanye nini kwani kiukweli binti huyu hakuwahi kuwa na mwanaume kimahusiano,na hasa ndicho kilicho kuwa kikimsumbua,katu hakujua ni mwanaume gani angeweza kumpata na kufaa mbele ya macho ya baba yake.ndani ya siku kadhaa alikuwa akiwaza ni vipi atafanikisha kile alichoombwa kukifanya.katika hali ya kutokutegemea,alimkumbuka mwanaume lucky,kijana waliyeuanzisha urafiki kupitia simu,siku Fulani alipokosea kutuma pesa.

"lucky........ni kweli lucky ananifaa....."alijiongelea alice huku akigusa gusa simu yake kuitafuta namba ya lucky,alipoipata akaipiga.kwa bahati mbaya alipokelewa na sauti tamu kutoka kwa mwanamke ikimjulisha kuwa namba hiyo haikuwa hewani kwa muda huo,hivyo ajaribu tena baadae.katika siku hii sio siri alijitahidi kupiga namba ya lucky Mara kwa Mara lakini mafanikio hayakupatikanika,namba iliendelea kuwa haipatikani.

******

Nikiwa niko nyumbani kwangu,katika kijinyumba nilichokijenga kutokana na faida yangu katika biashara yangu,nilikuwa najiandaa kuelekea kazini kwangu.lakini nyuma nilimuacha marry akiwa amelala,siku hizi tuliishi kama mke na mume kwani ilikuwa ikitokea akija bhasi alikaa ata wiki nzima akiwa kwangu ndipo hurudi kwao.na ndivyo ilivyokuwa ata siku hii.tayari marry alikuwa na siku tatu mfululizo akiwa kwangu.kusema za ukweli biashara yangu kuna wakati ilikaa vibaya sana,kiasi cha kunirudisha nyuma kwa kiasi kikubwa,lakini kama isingekuwa hivyo nadhani ndani ya miaka hii mitatu iliyopita ningekuwa mbali kimaendeleo..ila sio mbaya nilichokuwa nakiombea kwangu ni kila siku niweze kuamka nikiwa mzima na mwenye afya iliyo thabiti.

Majira fulani katika jioni ya siku fulani simu yangu ilipokea missed call ambazo ilionekanika kuna mtu alinipigia muda ambao simu yangu ilikuwa imezimika.kwa hiyo kwangu zilifika missed call kunijulisha kuwa hiyo namba ilinitafuta muda Fulani.nilistaajabu baada ya kuiangalia namba iliyonitafuta leo,sikuamini kuiona namba ya alice,binti ambaye kwa mara ya mwisho nakumbuka nilizungumza nae usiku fulani,miaka kama mitatu iliyopita.licha ya kutokuwepo mawasiliano kati yetu sikuwa nimeifuta namba yake.kwa sababu ya umuhimu wake juu yangu,nilitia vocha fasta kisha nikamtafuta.nilipopiga,simu iliita lakini haikupokelewa,Nikarudia kupiga tena mambo yalikuwa vile vile kama mwanzo.nilisikitika kuikosa simu ya huyu Bibie,sambamba na kutokupokelewa kwa simu yangu.

*****

"Baba kesho nina safari,kuna mahala naenda"

"Unataka kusafiri kabla hujatekeleza suala nililokuambia......,kwa nini usingoje tumfahamu mwenzio kisha ndo utaenda hiyo safari yako?"

"Safari yangu ni muhimu sana daddy,nataka nitangulie kwenda kabla ya kulifanya lile uliloniambia.....samahani kwa hilo"

"Sawa,ni muda gani utautumia huko"

"Siwezi kukadilia muda nitakao kaa huko,ila nakuahidi sint'omaliza siku nyingi"

Hayo yalikuwa ni mazungumzo ya Alice na baba yake,ni wazi Alice alikuwa na safari yake ambayo hakukuwa na mtu ambaye angeweza kufahamu ni wapi alikuwa akielekea.safari yake alitaka kuifanya kuwa siri yake na mungu wake.aliyoyaongea Alice usiku uliopita hayakuwa na uongo,kwani asubuhi kulipokucha alijiandaa vyema kisha akachukua begi lake tayari alikuwa akiianza safari kuelekea kituo cha mabasi.masaa kadhaa,alice alikuwako ndani ya basi,safari ilikuwa imekwishaanza mapema sana.ni safari ambayo alice alitegemea ingekuwa njema na angefanikiwa kwa hili alilokuwa akilifuata huko alikokuwa akienda.kuna dhamira ambayo ilikuwa ndani ya moyo wa mwanamke huyu.ukweli ni kwamba moyo wake ulimpenda mtu Fulani ambaye aliifahamu sauti yake tu,ni dhahiri hata safari hii ilikuwa ni kumfuata na kumtafuta huyo mtu kwa kutegemea mawasiliano ya simu.uhakika wake ulikuwa ni kwamba atakapofika huko aendako atawasiliana moja kwa moja na mlengwa wake,na atamjulisha uwepo wake.

••••••

"Unasemaaa?......ee...eebuu subiri kwanza Alice,uuuuumeeesema umekuuuu.....uuuja dodoma eeh,uuumekuja liniii mmbbb....ona huuukuuuniambia"nilizungumza kwa kitetemeshi cha mshangao wa kushangaa kile alichokuwa ameniambia Alice ya kwamba muda huu ninapozungumza nae eti yuko hapa hapa mjini.

"Nimeingia muda huu huu lucky,na sina mwenyeji hapa mkoani,kama kuna uwezekano naomba uje unichukue"Alice alinipa maelezo.

"Ndo umeshashuka kumbe.....?,"

"Yes lucky, nimeshuka hapa kituoni na sijui nielekee wapi"

"sawa Alice,sasa kwa sababu umeshashuka,na mimi Niko mbali kidogo......panda daladala ya kuja sabasaba,utanikuta hapo"nilimwambia hivyo Alice. ambaye baada ya Maelezo hayo alikata simu yake.unajua kwa haraka haraka,sikuamini kama kweli Alice alikuwa amefika mjini,nilihisi ni kama mzaha lakini ukweli ulikuwa ndio huo,Alice alikuwako ndani ya jiji kwa muda huu.sikulaza damu niliwahi chapu chapu sabasaba ambako daladala nyingi zilikuwa zikipaki hapo kutoka sehemu mbalimbali za jiji.kwa sababu nilikuwa ofisini kwangu,hakukuwa na umbali mrefu kutoka hapa sokoni hadi sabasaba,ulikuwa ni mwendo wa dakika kadhaa tu.Dakika kumi na tano tayari nilikuwa nimeshafika kituo cha daladala,nikimngoja Bibie Alice.kwa muda huo nilianza kuchati nae huyu mwanamke,ili kujua alikuwa amefika wapi kwa muda huu..

"Nasikia konda anasema emaus one,nadhani hapa tulipo ni emaus ya kwanza"Alice alinijibu hivyo baada ya kumuuliza amefika sehemu gani.

"Sawa hapo napafahamu vyema, bhasi utanikuta kituoni"baada ya hapo nilikaa kimya kwa muda kadhaa kabla ya kumuuliza tena ni wapi daladala aliyokuwamo ilikuwa imefika,jibu alilonipa Alice ni kwamba walikuwa maeneo ya bunge alafu kwa mashariki kidogo,bhasi moja kwa moja nikafahamu kuwa walikuwa wamefika kwenye majengo ya CBE,ambayo yamepakana na bunge.ni jirani kabisa na kilipo kituo cha sabasaba,sema gari hupita kushoto,pembezoni mwa ukuta wa chuo cha cbe,kutoka upande wa mashariki kama unatokea morogoro.

Nikiwa makini kutizama daladala zilizokuwa zikiingia na kutoka kituoni hapa mara nikapata ujumbe kunako simu yangu.ni ujumbe uliotumwa na Alice,alidai tayari alikuwa ameshuka hapa kituoni,alichokuwa akikitaka ni Mimi kumfuata mahala alipokuwa amesimama.

"Nina nywele ndefu,nimezibana kwa nyuma,nimevaa shati nyeusi nyuma ya mgongo imeandikwa 'u are my number one',nimeshika begi la kuvuta"Alice alinipa maelekezo namna ambavyo alikuwa akionekanika.nilipoangaza angaza pale kituoni,kweli bhana nikamuona mdada mmoja mweupe akiwa amezibana vyema nywele zake ndefu na nyeusi tii.kwa hatua za taratibu nikaanza kumsogelea.kutokana na kuwa huyu Alice hakuwa akifahamu upande ambao ningeweza kutokea,yeye alikuwa makini kutizama mbele yake pasipo kufahamu kuwa nilikuwa nimekwisha muona na nilikuwa namfuata kutokea nyuma yake.

"Hey"niliongea huku nikimgusa binti huyu begani.

Itaendelea. 

Post a Comment

Previous Post Next Post