IN'BOBO 13 lovestory

Ilipoishia.

"Nina nywele ndefu,nimezibana kwa nyuma,nimevaa shati nyeusi nyuma ya mgongo imeandikwa 'u are my number one',nimeshika begi la kuvuta"Alice alinipa maelekezo namna ambavyo alikuwa akionekanika.nilipoangaza angaza pale kituoni,kweli bhana nikamuona mdada mmoja mweupe akiwa amezibana vyema nywele zake ndefu na nyeusi tii.kwa hatua za taratibu nikaanza kumsogelea.kutokana na kuwa huyu Alice hakuwa akifahamu upande ambao ningeweza kutokea,yeye alikuwa makini mbele yake pasipo kufahamu kuwa nilikuwa nimekwisha muona na nilikuwa namfuata kutokea nyuma yake.

"Hey"niliongea huku nikimgusa binti huyu begani.

Endelea.

yule binti ambaye nilikuwa na uhakika kuwa ndiye Alice,aligeuka baada ya mimi kumgusa begani.

"Bila shaka wewe ndiye Alice......."niliongea katika hali ya kuuliza.kwanza Alice alinizawadia tabasamu murua,nadhani nae alishajua kuwa Mimi ndiye lucky,yule niliyekuwa nawasaliana nae katika simu.

"Yaaas,Mimi ndiye Alice,wewe ni lucky eeh"Alice alijibu kisha akaniuliza swali juu kwa juu.

"Hujakosea,ndiye mimi"

Hapo nikashuhudia tabasamu la Alice likikua na kuwa kicheko kabisa,dhahiri kuonana na Mimi kulimfurahisha mno huyu bibie kiasi cha kumfanya muda wote asiishiwe na furaha.bhasi nikampokea lile begi alilokuwa nalo,tukaingia kwenye daladala nyingine ambayo ilitufikisha mahali nilipokuwa nimejenga kajumba kangu ka uongo na kweli.kwa bahati nzuri asubuhi ya leo marry ndo alitoka na kwenda kwao kwa hiyo uhuru wa kumkaribisha Alice ndani kwangu nilikuwa nao wa kutosha.

"karibu Alice,hapa ndipo kwangu,huwa ninajisitiri kwenye hiki kijibanda changu"

"Mmmnh lucky acha kuidharau nyumba yako bhana,wengine hawana hata hii,usiposhukuru kwa kidogo hata ukipatiwa kikubwa bado hautoshukuru"

"ni sahihi kabisa,wala sikupingi"

"Eti eeh,sawa asante kwa kunikaribisha"alice alinijibu.Mpaka sasa Muda ulikuwa umeyoyoma sana kwani kiza tayari kilikuwa kinaitawala nuru kwa spidi mno.saa katika simu yangu ilikuwa ikionesha kwamba muda huu ilikuwa ikielekea saa moja za usiku.bhasi baada ya kumkaribisha Alice,nikamuomba radhi kwa muda kwani nilitaka kutoka chapu then ningerejea.ndani ya dakika kadhaa baada ya kuondoka kwangu tayari nilikuwa nimekwisha rudi,ukweli nilitoka kwenda kununua kilo moja ya nyama kwa ajili ya mgeni wangu,siunajua tena mgeni anavyopatiwaga heshima,bhasi ilikuwa hivyo,hii nyama kilo moja niliyoinunua ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya huyu kigori.tukiwa tunapiga stori mbili tatu Mimi na alice,niliendelea kufanya maandalizi ya chakula kwa kutumia jiko langu la gesi.yapata saa tatu kasoro tayari diko lilikuwa tayari.bila kuchelewa nikaliweka diko kunako Meza tayari kwa kuliwa.

"Karibu chakula Alice.... ila usinikosoe kama nitakuwa nimekosea kupika manake Mimi ni mwanaume,mapishi yangu kivyovyote hayafanani na ya mwanamke"

"Mbona unajihami sana lucky wewe......"

"Lazima nijihami,unajua siku zote mapishi ya wanaume huwa hayakosi kasoro..."bado niliendelea kujihami kwa kauli zangu za kudhihirisha kwamba nisingependa kukosolewa katika upishi wangu.alafu kingine ata kwa mtazamo niliouona kwa Alice ni kwamba hakuwa binti anayetokea katika familia yenye dhiki,hivyo hata vyakula ambavyo siku zote anatumiaga bhasi visingefanana na hiki nilichokiandaa mimi.

"Kuwa na amani,usiwe na hofu.ninajua wazi chakula chako kitakuwa kitamu tu,naaa ....leo ndio itakuwa Mara yangu ya kwanza kula chakula nilichoandaliwa na mwanaume."bhasi wote tukacheka kuisindikiza ile kauli aliyoiongea Alice muda punde.baada ya hapo tulinawa kisha tukaanza kula mdogo mdogo hadi pale tuliposhiba vyema ndipo tuliacha na kunawa.

"muda umekwenda sana Alice,karibia ndani ukajipumzishe"niliongea nikimkaribisha Alice chumbani kwangu ili aende akalale.

"Asante......,vipi kuhusu wewe"Alice alihoji kutaka kujua itakuwaje kwa upande wangu,kwani kama chumba changu,yeye Alice ndiyo alikuwa akienda kulala,kwa hiyo Mimi sikuwa na sehemu ya kulala.

"Hahahaha usijali kuhusu mimi,kwanza lazima mgeni wangu upate sehemu ya kujipumzisha ndipo nami nitaangalia ni wapi nitajistiri"

"Niambie tu.......au unakwenda kulala guest?"

"hapana,sebleni patatosha Mbona pako vizuri tu....."nilimuondoa wasiwasi Alice ambaye nilimuona akitikisa kichwa chake kushoto na kulia,sijajua kama alikuwa akisikitikia kitu Fulani ama la,sikufahamu kwa haraka.Hatukuendelea tena na maongezi,Alice alijinyanyua na kwenda kulala huku akiniacha kwa kunitakia usiku mwema,nami sikuchukua muda nikajilaza katika sofa langu na kupotelea kunako usingizi fofofo.usiku huo ukapita hivyo.

mapema asubuhi kulipopambazuka nilikuwa nimekwisha amka muda mrefu sana,kwa sasa nilikuwa nje nikifagia uwanja wangu,siunaelewa usafi ni muhimu,yeees ndo hivyo nilikuwa nafagia fagia uwanja wangu kuuweka katika hali ya kupendeza.hata Alice alipoamka alikuta tayari nimeshafanya usafi kwa asilimia kubwa.kiujumla nyumba ilikuwa safi na inapendeza.

"Lucky unafanya kazi utadhania binti eeh.mi ningezaliwaga mwanaume,ningekuoa aisee....."Alice alinitania,baada ya yeye kuamka na kunikuta tayari mazingira nimeshayarekebisha vyema na yanapendeza,sikusema kitu baada ya kauli hii ya alice,niliishia kucheka tu na kutikisa kichwa ishara ya kufurahi na kusikitika kwa wakati mmoja.kwa heshima yangu juu ya huyu bibie,zamani sana nilikuwa nimeshamchemshia maji ya kuoga.bhasi nikamuandalia pale na kumwambia Alice aende kuoga.

Hii siku niliiondoa katika siku zangu za kazi,kwani uwezekano wa kwenda kazini sikuwa nao,katu nisingeweza kumuacha Alice akiwa mwenyewe hapa nyumbani.nilipenda sana Leo niitumie siku hii kwa ajili ya kumtembeza mgeni wangu angalau alifahamu jiji vyema.Alice alikwenda kubadili mavazi baada ya kutoka kuoga,akajiweka vizuri kwa ajili ya mtoko.nami vile vile nikaenda kuoga chapu kisha nikajiweka vyema kwa ajili ya matembezi.Mimi na Alice tukatoka na kuanza kutembea tembea sehemu kadhaa za jiji,lakini hatimae tuliingia kunako daladala mpaka majengo sokoni.lengo langu la kumpeleka Alice sokoni,nilitamani sana afahamu pale ninapofanyia kazi.kwa urembo wa huyu alice Mara baada ya kuingia nae mule sokoni,nikasikia miluzi ikipigwa na baadhi ya washikaji zangu,ni ile hali ya umbea ilikuwa ikiwasumbua.ndani ya lisaa tayari nilikuwa nimemaliza kumtembeza huyu kimwana ambaye ni rafiki yangu wa dhati kweli kweli.tulipo hapa sokoni tukaendelea kupiga misele miwili mitatu katika maeneo mengine nje ya hapa sokoni.

katika pita pita zetu tukaingia square ya pale nyerere.Alice alipoona makamera man akaomba tupige japo picha ya ukumbusho.dakika thelathini picha ilikuwa mikononi mwetu,kwani wapiga picha wa hapa walikuwa ni shapu mno.yani ukipiga picha wanakwenda kuisafisha ndani ya muda mfupi wanakuletea.

*****

"lucky unajua uko tofauti na nilivyokuwa nadhania......yani uko kawaida sana kiasi cha kuniaminisha kuwa we ni mwanaume mmoja wa kuigwa na wanaume....wengine."alice aliongea mi nikaishia kutabasamu na nishindwe kuongea chochote.

"Japo mi sijakaa na wewe kwa muda mrefu,lakini tayari nimekwisha kufahamu vizuri lucky,ni una upendo sana na watu,manake hata kule ofisini kwako nimeliona hilo......,"Alice akasita kiasi kisha akaendelea....

"sidhani kama huwa inatokea unagombana na watu lucky,nimegundua we ni mtaratibu sana.nimependa ulivyo"alice alijazia kile alichokuwa akikiongea,huu ulikuwa ni usiku mara tulipotoka matembezini. 

"Hata wewe Alice uko kawaida sana,na inapendeza sana uendelee hivyo.unajua wanawake wa aina yako huwa wana maringo sana kiasi cha kujiona wao ni bora kuliko wengine....lakini kwako sijaona hicho"

"asante.........,hivi kesho utakwenda kazini eeh"

"Yaa kwa kesho nalazimika kwenda kwa sababu mzigo wangu ukikaa sana utaharibika"

"Sawa naomba kesho twende pamoja,napenda kukaa jirani yako nijue huwa unaiendeshaje biashara yako......"

"Alice hujihurumii kukaa juani....."

"Kwa hiyo unataka kuniambia utofauti wangu na wako uko wapi lucky,mbona we unaweza kukaa juani mi nishindwe nina nini.....we naomba kesho tuende wote."alice aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka siku ya kesho kutapopambazuka bhasi niende nae sokoni eti akatizame nawezaje kufanya kazi yangu.sikumkatalia kwani alipenda yeye.kwa hiyo siku iliyofuata nilikuwa na Alice kule sokoni.sio siri Alice alionesha kujituma sambamba na Mimi,kwani alikuwa akihudumia wateja kwa ubora na kauli za kuvutia kiasi kwamba nilifurahi kuwa nae hapa kazini leo.jioni Alice alionekana kuchoka sana,kwani hakuonekana kuzoea ile mikiki mikiki ya sokoni,lakini kwa kiasi chake alijitahidi sana.uzuri wake ulisababisha niuze sana bidhaa yangu,kwani wengi walikuwa wakija kununua kwangu ili tu wamtazame vyema wapate kufaidi kuuona uzuri wa huyu Alice lemega.ujinga wao wa kuja kumuangalia Alice,ulifanya Leo nikamaliza mzigo wangu,hivyo siku iliyokuwa ikifuata kwa nilivyoiona nisingekuwa na kazi yoyote zaidi ya kupumzika tu.

Tangu ujio wa Alice,zilishakata siku nne mfulilizo hadi sasa.kiukweli maisha tuliyokuwa tukiishi tuliyafurahia mno.hatukuwa wapenzi lakini mara nyingi kuna watu njiani wakati tulipokuwa tunatembea walituambia kuwa tunaendana sana,na tunaonekana tunapendana.hatukuwa na maneno ya kuwajibu zaidi tuliishia kutabasamu tu.urafiki wangu na Alice kiukweli ulipendeza sana.muda mwingi nilipendelea tuwe wote.

Siku fulani nikiwa nimekaa katika sofa langu,ghafla nikajikuta nikizama katika wimbi la mawazo,nilianza kufikiri hivi kama marry akitokea muda wowote na kumkuta alice,ningejibu nini hicho hasa ndo kilinipa mawazo,kwani kivyovyote kama kweli marry angekuja ni dhahiri angemkuta Alice,alafu kingezuka kisangasanga,manake nilikuwa naujua mziki wa huyu demu vilivyo.ile hali ya kuwaza ilinifanya niwe m'kimya kitu ambacho Alice alikijua kwa haraka kwani siku zote nilikuwa muongeaji hakuna mfano.Alice alinistua kutoka katika dimbwi la mawazo baada ya kuuona ukimya wangu.

"Lucky una tatizo gani,mbona umebadilika ghafla tofauti na nilivyokuzoea jamani......"

"amna Alice mi niko poa tu."

"Unataka kuniambia kuwa mi sikufahamu si ndio......niambie unasumbuliwa na nini lucky mi sipendi kukuona hivyo bhana"

"Alice,kuna kitu nataka ukijue.sipendi niendelee kukaa kimya mwisho nikaja kuumbuka......,wewe ni rafiki yangu wa dhati sana siwezi nikashindwa kukuambia hiki......"hapo nikavuta pumzi kiasi kutafuta gepu la kuongea kile nilichotaka kukiongea.....nae Alice aliweka umakini kunisikiliza.

"Ni miaka miwili na miezi kadhaa sasa niko katika mahusiano na mwanadada mmoja anaitwa marry,na katika muda wote huo,tumeshatengana zaidi ya Mara tatu,kutokana na wivu juu yangu.licha ya hivyo,mwanzo kipindi tunayaanza mapenzi yetu,huyu marry alikuwa mtiifu sana kwangu,na aliishi kwa kufuata kile nilichokuwa nakitaka.siku kadri zilivyokuwa zikienda ule utiifu ulianza kumtoka,akawa hanisikilizi tena.ndipo nikaamua kuwa na msichana mwingine pembeni,lakini alipokuja kufahamu alifanya vile alivyokuwa akifahamu hadi mahusiano yangu na ya yule binti wa kando yakavunjika.....,yani huyu binti amekuwa mkorofi mno sipatii picha akikukuta itakuwaje manake hataki niwe na urafiki na wanawake kabisa.....kwa hiyo apa naumiza kichwa nitamjibu nini kama akija ghafla....hapo ndo sielewi."

Itaendelea. 

Post a Comment

Previous Post Next Post