IN'BOBO 14 lovestory

Ilipoishia.

"Ni miaka miwili na miezi kadhaa sasa niko katika mahusiano na mwanadada mmoja anaitwa marry,na katika muda wote huo,tumeshatengana zaidi ya Mara tatu,kutokana na wivu juu yangu.licha ya hivyo,mwanzo kipindi tunayaanza mapenzi yetu,huyu marry alikuwa mtiifu sana kwangu,na aliishi kwa kufuata kile nilichokuwa nakitaka.siku kadri zilivyokuwa zikienda ule utiifu ulianza kumtoka,akawa hanisikilizi tena.ndipo nikaamua kuwa na msichana mwingine pembeni,lakini alipokuja kufahamu alifanya vile alivyokuwa akifahamu hadi mahusiano yangu na ya yule binti wa kando yakavunjika.....,yani huyu binti amekuwa mkorofi mno sipatii picha akikukuta itakuwaje manake hataki niwe na urafiki na wanawake kabisa.....kwa hiyo apa naumiza kichwa nitamjibu nini kama akija ghafla....hapo ndo sielewi."

Endelea.

Alice alikaa kimya kwa muda,alionekana kuingia katika tafakari kubwa,na sijui alikuwa akiwaza nini,ila nilimuona akitazama juu ishara ya kuonekana kuwa alikuwa akikitafakari kitu Fulani.

"lucky wewe ni mwanaume,utatishikaje na mwanamke?,kwanza kwa nini unamruhusu huyo binti akuendeshe badala ya wewe umuendeshe.......acha kumpa nafasi ya kukutawala.simama kama mwanaume,mwanaume siku zote huwa hakubali kuongozwa,iweje wewe uwe mlaini kiasi hicho,unaniangusha lucky"Alice aliongea kwa huzuni sana,alionekana alihuzunishwa na kile nilichomwambia.

"Alice mi sinaga moyo wa kuendekeza ugomvi.inapotokeaga mizozo kati yangu na mwenzangu ni mara chache sana huwa nakoroma lakini mara zote huwa nanyamaza kuepusha shari"

"usijishushe kwa mwanamke lucky,hata kama umekosea tafuta namna ya kusawazisha na sio kujishusha....,ukifanya hivyo utamzoeza mwanamke wako vibaya,kwani kila siku atakuwa anapenda ujishushage wewe tu hata inapotokea yeye kukosea....."Alice aliongea.sio siri niliushangaa uwezo wa binti huyu katika kutoa hoja zilizo sahihi tofauti na vile nilivyokuwa namchukulia.ni mambo mengi sana Alice alinishauri kiasi kwamba nikajisikia hadi wivu.....ndio wivu,unashangaa nini.kiukweli nilimuonea wivu mwanaume ambaye angeweza kumuoa Alice kwani angepata mwanamke bora na sio bora mwanamke kama ambavyo wengi huoa.moyoni nikajisemea 'endapo alice nisingekuwa na urafiki nae,hakyamungu nisingeweza kukubali anipite pasipo kumvisha pete ya ndoa',ila nilipokuja kuufikiria urafiki wetu daa nilijua hicho ninachokiwaza kilikuwa ni ndoto ya mchana.tulizungumza mengi sana.lakini katika mazungumzo yote sikumsikia Alice akiyaongelea mahusiano yake,na mimi sikutaka kumuhoji kitu,nikakaa kimya.

katika usiku mmoja wakati nikiwa nimelala kwenye sofa,nilihisi kuitwa,nilipokuja kufumbua macho nikakutana na alice akiwa ndani ya gauni ya kulalia ambalo kwa kiasi chake lilimbana kimtindo.nikafikicha macho yangu kuweka macho yangu katika hali ya kutazama vyema,kisha nikakaa kitako ili niweze kusikia ni kipi kilimfanya alice aje kuniamsha katikati ya usiku mnene.

"kuna tatizo Alice?mbona umeamka usiku kuna nini"nilimuuliza 

"Ndiyo nina tatizo"

"Eenhe tatizo gani"nilimhoji tena Alice ambaye badala ya kunijibu alirudi tena chumbani,lakini muda kidogo akarejea huku mkononi akiwa amebeba kitu Fulani ambacho sikuwa nimekijua kwa uharaka,labda ni kutokana na macho kutokuzoea kuona vyema nyakati za usiku,ijapokuwa taa ilikuwa imewashwa.Alice alifikia kuketi katika sofa nililokuwa nimeketi mie kisha kwa sauti ya upole akaanza kuniambia.....

"ni muda mrefu kiasi umeshapita tangu niingie katika mahusiano na mwanaume fulani ambaye nilikutana nae katika mazingira ya kutatanisha kiasi.kipindi hicho naanza mahusiano nae nilikuwa na miaka kumi na tisa.nilitokea kumpenda sana tangu siku ya kwanza nafahamiana nae.nayakumbuka maneno yake ya faraja kwangu kila nilipokuwa na huzuni,huyu mwanaume alikuwa mshauri mzuri kwangu na bado ataendelea kuwa mshauri wangu daima......"Alice aliongea,kitu ambacho kilinifanya nizidi kumuonea wivu  huyo mtu anayezungumziwa na Alice.kiukweli nilitamani kama ningekuwa Mimi lakini ndo hivo bahati ilikuwa kwa mwingine,istoshe nimefahamiana nae muda mchache sana,kwa hiyo mambo yake mengine nisingekuwa na uwezo wa kutayamani kwa sababu yalishakuwa ni ya siku nyingi kabla ya urafiki wetu.kipindi Alice anaongea yote hayo goodlucky mie nilikuwa nimejituliza tuliii,naendelea kuufaidi utamu wa kisa ambacho alice alikuwa amekwishaanza kunisimulia.

".....huzuni ilinikumba katika siku Fulani nilipoagana nae kwa Mara ya mwisho,siku hiyo nilikuwa nakwenda masomoni.nililia Sana kutokana na kujua kuwa ninakwenda kukaa mbali na kipenzi cha roho yangu.kila nilipokuwa nazikumbuka kauli zake nilijikuta nikipata nguvu ya kusoma hata baada ya kufika chuoni.kwa kipindi kirefu kidogo nilikaa chuoni lakini hadi narudi mapenzi yangu hayakuwa yamepungua ata punje.ninachosikitika ni kwamba mimi ndiye mwenye mapenzi nae,sina uhakika kama napendwa na yeye......"hapo nikamkatisha Alice na kutaka kufafanuliwa kidogo.

"Nikukatishe kidogo Alice......umenambia ulikuwa katika mahusiano nae huyo mwanaume,iweje usijue kama ana mapenzi na wewe?vipi ulivyorudi ulikuta amebadilika kitabia ama la"

"hapana hajabadilika chochote,yuko kama mwanzo"

"Sasa utashindwaje kujua kama ana mapenzi na wewe"

"nashindwa kujua kama ana mapenzi na mimi kwa sababu mapenzi yetu hatukuwahi kuwekana wazi,istoshe mimi ndiye nilitangulia kumpenda yeye,na hata siku sikuwahi kumwambia kama ninampenda"

"Alice ebu acha kuongea mambo ya kitoto..........yani wewe ulimpenda pasipo kumwambia kuwa umempenda,alafu asaivi unadai alikuwa mpenzi wako,yani kivipi sasa mbona unanichanganya....."

"Lucky, ukishampenda mtu hata usipomwambia kuwa unampenda,tayari ndani ya moyo unakuwa umeshaanzisha mahusiano nae.na ndio maana nimekwambia.....ni muda mrefu umepita niko kwenye mahusiano,nilikuwa na maana kwamba moyo wangu ulishampenda mtu huyo tangu siku nyingi,nimeishi nikimpenda zaidi ya miaka mitatu,na bado nampenda,na naweza nikasema ni mpenzi wangu kwa sababu natembea na mapenzi yake moyoni tangu muda mrefu"

"Sawa nimekuelewa.kwa hiyo una maana kwamba umeishi ukimpenda huyo mwanaume,lakini hujawahi kumuweka wazi hisia zako juu yake...eeh"

"Ni kweli,lakini nahisi kushindwa kuendelea kuishi katika mapenzi bubu kati yangu na yake,nataka kumuweka wazi ajue kuwa ninampenda"

"hapo umesomeka,umejipangaje kumuweka wazi katika hilo"

"Sina namna lucky,natakiwa kumwambia tu,siwezi tena kumficha......"alice aliniambia hivyo.hapo Mimi nikakaa kimya sikuwa na cha kuongeza.

"Shika hii"Alice alinipa Maelezo huku akinipatia kile kitu ambacho alikuwa amekishika mkononi mwake tangu mwanzo.ilikuwa ni bahasha ambayo ilionekanika ndani yake kuwemo barua ama picha kwani hata nilivyoigusa nililigundua hilo.

"Humo ndani Kuna picha ya huyo mwanaume,najua ukiitizama picha utamfahamu vizuri mtu ninayemuongelea,pengine inawezekana unafahamiana nae au ulishawahi kumuona"bila kungoja kuambiwa nifungue ile bahasha,mi nikaifungua na kuitoa hiyo picha ambayo Alice aliiongelea.nilishikwa na kigugumizi baada ya kukuta picha yenyewe aliyokuwa  akiiongelea alice ni picha yangu,nikiwa nae,ni ile ambayo tuliipiga siku kadhaa nyuma.kwa mshangao niliendelea kubaki na kigugumizi kiasi kwamba nilishindwa ata kuzungumza chochote.

"najua umestuka sana lucky,lakini ukweli ndio huo.hapo nyuma kabla ya kukufahamu sikuwa nimewahi kuingia katika mapenzi.siku ya kwanza kuzungumza na wewe ndio siku yangu ya kwanza ambayo moyo wangu uliniambia kitu juu yako.nilivutiwa sana na wewe japo sikuwa nakujua kwa sura.nilianza kukukaribisha moyoni mwangu taratibu taratibu,hadi uliponikaa vyema.nikajiapiza kuwa ipo siku nitaonana na wewe na nitakueleza kile moyo wangu unahisi.Goodlucky,una bahati sana kupendwa na moyo wangu,naomba unipokee,ruhusu moyo wako unipende,wewe ndio nataka uwe  mwanaume wangu wa kwanza kupendwa na moyo wangu,na pia uwe wa mwisho.sitaki kuhangaikia wanaume wengine.lucky wewe unanifaa,kila sifa unayo please naomba unikubali,haijalishi nimefahamu kuwa uko katika mahusiano na mwanamke mwingine.tizama lucky......moyo wangu ulikupenda kabla ata haujakutia machoni,ni dhahiri ninakupenda kuliko huyo mwanamke uliyenaye......nitaumia sana endapo nitakosa nafasi moyoni mwako,nionee huruma lucky,nimetoka mbali kukufuata wewe,hapa mkoani sina nilichokifuata zaidi yako nihuuuu........"weee  sikutaka niendelee kusikia vile ambavyo Alice alikuwa akiongea,ghafla nilijikuta nimemkumbatia tu aisee,kwa maana daaa sio siri maneno yake yalinichoma sana.vyote alivyokuwa ameviongea Alice vilidhihirisha hisia zake kwangu,hivyo na mimi sikutaka kumuacha aendelee kuteseka juu yangu huyu kimwana.niliyaona mapenzi yake kwangu,nami sikuwa na sababu nyingine ya kushindwa kumkubalia.

Huwezi amini alice alikuwa akilia machozi kusindikiza ujumbe wake,ni kweli moyo wake ulikuwa na mahaba mazito juu yangu.kumkumbatia nilikomkumbatia kulimzidishia kilio,nadhani furaha yake ilipita kawaida.nisikufiche tuling'ang'aniana kama gundi.kwa mbali nikaanza kulifaidi joto la kifua kibichi cha mrembo huyu matata.ngoja nikudadavulie sifa za huyu Bibie.kwanza kabisa ni mzuri wa sura,weupe wa ngozi yake sambamba na macho yake ya kusinzia viliupamba vyema uso wake.achilia mbali pua na lips zake,chuchu zake dede zilizosimama kama embe sindano pia viliongeza urembo wake kwa kiasi kikubwa.mtoto kiuno kilikuwa kimebonyea ka'kiuno cha nyigu asikwambie mtu,sasa huko nyuma aisee Alice alikuwa amefungasha sio masikhara eti,sio siri mungu alimbarikia sana kumuumba.hata mademu zangu wote niliokwisha kupita nao kiukweli hakuna ata mmoja aliyekuwa akiunusa uzuri wa huyu Alice,labda kwenye wowowo kidooogo Mariana alikuwa akimkaribia,lakini vitu vingine aah wapi hakuwa akifua dafu kabisa.

"Goodlucky,nakupenda sana....."alice aliendelea kuniambia hivyo huku tukiwa tumekumbatiana.

"Nakupenda pia alice"

Baada ya hapo tulitizamana kwa muda kabla ya kuanza kupeana sharubati za utamu wa mate yetu.Alice alionekana kupenda kunyonywa sana ulimi,kwani alidhihirisha hilo kwa sauti za miguno yake maridhawa.tulinyonyana denda kwa muda kabla ya kuacha na kukumbatiana tena.muda punde Mimi na alice tulijikuta tukiwa kitandani,tena tukiwa tumenatana vilivyo,sio kwamba tulikuwa tukifanya mapenzi 'hapana',tulikuwa tunabadilishana tu majoto ya miili yetu.sema kuna muda nilihisi kushindwa kuendelea kukitizama chakula ilihali nilikuwa na njaa,ila tu nilijikaza kwa kuamini kwamba nikifanya papara ya kutaka kumgegeda huyu binti,bhasi ningeonekanika ni mroho wa ngono,kwa hiyo nikajitia upofu wa kutohitaji mchezo wa kikubwa.usiku huu tuliumalizia kwa raha sana kwani mapenzi yetu yalikuwa yameanza katika usiku huu huu mnene.yani hata namna kulivyopambazuka sikuweza kuelewa,nilikuja kustuka nikitikiswa na alice....

"baby amka ukaoge,tunywe chai tayari nishaandaa"nilipokelewa kihivyo mara tu nilipofumbua macho yangu.bhasi nikajinyanyua na kuvaa malapa yangu hadi bafuni,nikaoga chapu kabla ya kurudi ndani na kujiweka sawa kimavazi.nilipokuwa sawa nikaenda mahala ilipokuwa imeandaliwa chai,hapo nikakaa na kuanza kunywa nikiwa sambamba na Alice mpenzi wangu mpya.tukiwa tunaendelea kunywa chai mara ghafla paaap.......

itaendelea.

Duu nini kinataka kutokea hapo sasa,mbona kuna dalili mbaya.

TUSIKOSE SEHEMU IJAYO ITATUPA JIBU.

Post a Comment

Previous Post Next Post