IN'BOBO 15 lovestory

Ilipoishia.

"baby amka ukaoge,tunywe chai tayari nishaandaa"nilipokelewa kihivyo mara tu nilipofumbua macho yangu.bhasi nikajinyanyua na kuvaa malapa yangu hadi bafuni,nikaoga chapu kabla ya kurudi ndani na kujiweka sawa kimavazi.nilipokuwa sawa nikaenda mahala ilipokuwa imeandaliwa chai,hapo nikakaa na kuanza kunywa nikiwa sambamba na Alice mpenzi wangu mpya.tukiwa tunaendelea kunywa chai mara ghafla paaap.......

Endelea.

...simu yangu niliyokuwa nimeiweka kwenye sofa ikaanza kuita.Alice kwa Sababu alikuwa amekaa nayo jirani,akaichukua na kuangalia mpigaji alikuwa ni nani,baada ya kumjua niliona akinitizama kwa jicho fulani hivi utafikiri alikuwa akiniuliza 'vipi nipokee?',kwa sababu tayari nilikwisha isoma lugha ya macho kutoka kwa Alice,nikaamua kumwambia aipokee tu hiyo simu.

"Eeh hellow,mimi ni mke wa lucky naongea.........,ni huyo huyo tunda na ndo lucky pia.......,nisikilize dada naomba kuanzia leo usimpigie mume wangu simu tena ukome kabisa,mikelele yako isiyo na maana isije ikanikondeshea mwanaume wangu bure......,eeee anti jiheshimu usijibinafsishe mwanaume upo nyonyo........,sa'ndo nimekwambia huyo tunda unayemsemea asaivi ana mke.....,unataka kunijua zaidi ili iweje,ebu fanya yanayokuhusu.kama tunda ndo alikuwa bwana'ako ni enzi hizo,asaivi yuko kwenye mapenzi mapya......,mi ndo nishasema sasa fanya yanayokuhusu,niachie Mume wangu.......,wakati unamchezea ulijua hana thamani eeh,kwa taarifa yako tupo tunaomuona wa thamani.......,mpotezeee kwanza haiji kutokea ata siku akutafute,usinipotezee muda wangu kwa heri......"duu Alice alikuwa amemaliza kumchamba huyo aliyekuwa amepiga.kivyovyote nilijua ni marry ndiye aliyepiga kutokana na vile ambavyo alice alikuwa akijibizana nae.

"Ni nani huyo"niliuliza tena ili kupata hukakika kwa kile nilichokuwa nakidhania.

"si ni kimwanamke chako ki marry.......,yani kimenikelaaa heeee bahati yake sikijui,yani ningekafuata nikakitufue tufue mijingumi mpaka kingenikoma kipumbavu sana......"

"Wewe huyooo,una nguvu gani za kumtufua tufua mtu"niliingiza utani ili kuimaliza ile mada ya marry,siunajua tena nilishaamua kuwa na huyu bibie,kwa hiyo sikutaka kuendelea na hawa wengine niliokuwa nao mwanzo.

"Hee lucky unanichukulia mi mlaini sana si ndio.....nina nguvu onhooo we siku uje unichokoze ndo utaniona makali yangu"

"Akhaa nikuchokoze ili nigundue nini,kupigwa nani anataka kwani"

"lione vile kumbe unaogopa kudundwa hilooo"alice alisema kisha kwa pamoja tukacheka.Bhasi mada ya marry ikawa imeshaisha kihivyo.siku hii tulishinda nyumbani mpaka baada ya kula chakula cha mchana ndipo tulitoka na kwenda kuzuga kidogo mtaani hadi jioni kabisa ndo tulikuwa tunarudi.nyumbani alice aliandaa diko la nguvu,lilipokuwa tayari liliwekwa mezani kisha tukalifanyia haki kwa kulitupia katika matumbo yetu.

••••••

"Lucky......."alice aliniita,katika usiku fulani tulipokuwa tumelala.

"niambie mpenzi....."nilimuitikia.hapo Alice alijiweka sawa katika kifua changu ili aweze kuzungumza vizuri.

"Ni kweli huna wazazi?"aliniuliza swali ambalo nakumbuka nilishawahi kumjibu siku za nyuma,japo ni muda sana ulishapita.

"naweza sema hivyo kwa sababu sikuwahi kuwaona.......na mimi tangu nimepata kujitambua nimejikuta kwenye kituo cha kulelea watoto yatima,ni hivyo.mi siwajui wazazi wangu kabisa,siwezi kukuongopea"

"Mmnnnh pole mume wangu,kwa hiyo ata ndugu....labda mjomba au shangazi pia nao huwafahamu"

"Ni kweli siwafahamu,na kama ningewafahamu naamini ningeweza kufahamu pia walipo wazazi wangu"

"I'm sorry,dhahiri umepitia maisha magumu sana lucky,ila ninaamini mwisho wa yote umefika.nataka usahau maisha yote magumu uliyopitia.nitahitaji ufungue ukurasa mpya wa maisha ukiwa na mimi.nikuahidi kitu lucky wangu......,kamwe sintokutupa,sintokuacha uwe mwenyewe kama ambavyo ulikuwa kabla hatujakutana.nitakuwa faraja yako,nitakubembeleza kila utakapokuwa na huzuni,mimi nimeumbwa kwa ajili yako peke yako,hakuna mwingine....."Alice akanyamaza kwa sekunde kadhaa,akanipa kiss la ujazo kabla ya kuendelea....

"........namshukuru sana mungu kwa kunikutanisha na wewe.kwako ndiyo sehemu salama ya kuyahifadhi mapenzi yangu.oooh sijui nikwambie ni kiasi gani najisikia raha kuwa na wewe......ila ngoja nisiongee sana,tuombe uzima lucky"

Huyu Alice kiukweli alikuwa anajua sana kuzungumza maneno matamu,ilifikia muda nikajiona mimi ni kama mfalme katika kasri ya moyo wa kiumbe huyu.nikajifananisha na tajiri niliyeweza kuununua moyo wa mrembo Alice pasipo kuwepo mwingine wa kunipandia dau.

"Leo nina ombi kwako mume wangu"Alice aliongea tena.

"Nakusikiliza malikia wangu,"

"sijakua bado,naomba usiku wa leo unikuze,kutapokucha kesho nisiwe alice wa sasa,nataka kuwa Alice mpya"alice alinena lakini katika lugha ya kiutu uzima.

"Alice,Mimi na wewe tumeamua kuwa pamoja,tusiliharakishe suala kama hilo.ninajua kuwa hujawahi kuguswa na mwanaume,lakini hiyo hainifanyi niwe na tamaa ya kutaka kufanya hicho unachokitaka.nipo tayari kukungoja mpaka nitakapo kuoa,hata kama sijui nitakuoa lini ila nakuahidi nitakusubiri mpenzi wangu,nataka siku nitakayo kuoa ndio iwe siku ya kwanza kuyajua maungo yako"niliongea.alice alinitazama kwa umakini,sijui ni kwa sababu gani.

"nilimuomba mungu aje anipatie mume bora kama wewe,na kweli amenipa.asante kwa kuuthamini mwili wangu,nakupenda sana lucky"aliongea alice kisha tukaanza kubadilishana mate.

****

Wiki tatu tayari zilikuwa zimekwisha nikiwa naishi na Alice nyumbani kwangu.tuliishi kama mume na mke kabisa japo kulikuwako changamoto mbali mbali.kwani kuna siku marry alikuja kwangu na kuanzisha timbwili la kufa mtu,lakini kiubishi nikapambana nae hadi nikafanikiwa kumuondoa.katika kipindi chote hicho nilichokaa na Alice,sikuwa nimeendelea na kazi yangu,kwani Alice aliniomba kutokuendelea nayo na kuniambia kwamba,ningoje yeye atanianzishia biashara nyingineyo nzuri zaidi kuliko ata hii niliyokuwa naifanya.bhasi kweli nikaacha kwa sababu nilimuamini sana mwanamke wangu.

"Honey,kesho kutwa nataka kurudi nyumbani........."Alice aliniambia muda fulani nilipokuwa namsaidia kumtana nywele zake.kauli yake hiyo ikanifanya ni stop ata kufanya kile nilichokuwa nafanya.unajua nilishamzoea sana,kitendo cha kuisikia sauti yake ikiniambia kuwa alitaka kurudi kwao aisee kiliniondolea furaha.alice aligundua kuwa kauli yake ilinivuruga kwa kiasi Fulani.akaanza kujaribu kuniweka sawa....

"mbona umepoa ghafla my...."

"Kwa ulichokiongea unadhani nitakuwa sawa kweli?,mi nishakuzoea tayari unafikiri itakuaje unavyoniambia unataka kurudi kwenu......"

"Jamani sa'sibado naendelea kuongea,subiri nimalize bhasi mpenzi....."

"Sawa nakusikiliza,ila nishajua tu kwamba pointi yako ni unataka kurudi kwenu bhasi....."

"ndio kesho kutwa nataka kurudi nyumbani kweli,lakini sintorudi peke yangu......"

"Mmmnh!!,sawa.una mtu unaeenda nae huko kwenu?"

"yaas,kuna mtu nitaenda nae"

"haya sawa bhana.....,enhee utarudi lini sasa au ndo una kwenda jumla na hutorudi tena"

"No usiseme nitarudi lini,sema tutarudi lini,kwa sababu mtu ninayekwenda nae ni wewe baby,siwezi kukuacha peke yako mume wangu."

"Mimi niende na wewe kwenu aah wapi,siwezi"

"Kwa nini usiweze bhana.....utaweza tu,jiamini"

"Nijiamini?kwa hivi nilivyo nitajiamini vipi"

"we jiamini tu,usiogope chochote,"

sikutaka kubisha sana,makubaliano yetu ya mwisho kati yangu na Alice ni kwamba Alice ataongozana na mimi kuelekea huko kwao.siku kamili ilipowadia Mimi na Alice mida ya saa nne asubuhi,tulikuwa ndani ya bhasi,tayari safari kuelekea kwao Alice ilikwisha kuanza.kutokana na urefu wa safari ilifikia kipindi nilijikuta nalala,kuna muda niliamka na kupiga stori mbili tatu na Alice,wakati mwingine niliangalia luninga iliyokuwamo mule ndani ya basi,bhasi tu ilimladi nilikuwa najihangaisha.

kwenye majira ya saa tatu unusu hivi,ndipo tulikuwa tunafika stendi ya mabasi moshi.uzuri tuliposhuka Alice alilipia taxi,kisha tukapanda moja kwa moja kwenda sehemu ambayo sikuifahamu.ile taxi tuliyoipanda ilikwenda kupaki nje ya jengo fulani zuri sana,ambalo kwa nje,katika geti la kuingilia paliandikwa the dreamz Lodge.sikujua neno hilo lilikuwa na maana gani,kwa sababu kiingereza kwangu ilikuwa ni sawa na kiza kinene,kiufupi sikuwa nakijua kingereza zaidi ya kusikia watu waliosoma wakikizungumza.bhasi bhana tukashuka pale kwenye hiyo the dreamz lodge,moja kwa zote tukazama hadi ndani kabisa ya mjengo.huko tukafikia sehemu ya mapokezi,kivyovyote hapa nilipagundua kuwa palikuwa ni sehemu ya kulala wageni,manake nyumba ya kawaida isingeweza kuwa na mahala pa mapokezi,Alice akadai alikuwa akihitaji chumba,baada ya kupatiwa ufunguo tukaenda hadi kilipo chumba,tukajitoma ndani.

"mpenzi wewe utalala hapa,lakini Mimi nakwenda nyumbani.kesho mapema sana nitadamka kuja"

"hapana bhana tulale wote,kesho tutadamka pamoja"nililipinga suala la alice kuniacha mwenyewe room alafu yeye aende kwao kwa madai atakuja mapema asubuhi ya siku iliyokuwa ikifuata.

"No baby,tayari nilishamwambia baba kuwa nimeshafika na niko njiani kwenda nyumbani,hatonielewa Kama sintofika....wacha niende vile nilivyosema nitadamka kesho,bhasi niamini nitadamka kweli"

"Ooopfuuuu.....sawa nenda mama,sina neno tena"

Bhasi alice akanipiga kiss la shavu kabla ya kufungua mlango na kutoka,lakini huku nyuma akiwa ameniachia hela ya kula,siunajua tena ndo tulifika muda mfupi,na njiani hatukuwa tumekula vitu vya maana zaidi ya kutafuna tafuna baadhi ya vitu vya kitoto toto tu.kwa hiyo hapa nilipo njaa ilikuwa inanisumbua atari.kwa sababu hiyo nikatoka nje ya ile lodge,kwenda kutafuta chochote kitu cha kuliweka sawa tumbo langu.kwa bahati nzuri pembeni kidogo,hatua kama kumi au kumi na tano kutoka ilipo fensi ya lodge niliyokuwa nimepata chumba,kulikuwa na banda la kukaanga viepe.nikaenda pale na kuagiza kiepe changu cha yai,baada ya kuwa tayari nilikichukua kisha nikarudi zangu room,mkononi nikiwa na soda yangu ya take away.chumbani nilikifakamia kile kiepe kwa pupa ndani ya muda mchache nilikuwa nimekwisha kimaliza.sikuwa na lingine la ziada nikapanda kitandani na kulala kabla ya kupotelea kunako usingizi wa pono,yani hata kuoga sikukumbuka kabisa...hahahaha,uchovu wa safari ulinichosha sio siri eti.

Asubuhi mapema sana kama ambavyo alisema Alice,tayari alikuwa amekwisha fika room kwangu.akaniambia kuwa baba yake alitaka kuniona mapema sana kabla ya kutwa ya leo kuisha.

"Kwani umemwambia umekuja na Mimi"nilihoji.

"Yees,anaujua uwepo wako"

"Daah Alice mama unanipa mtihani aisee,kwa hivi nilivyo kweli baba yako atanikubali niwe mkwewe?,nahisi kuumbuka lucky mie"nilijiongelea mwenyewe huku nikionesha uoga waziwazi.

"Acha uoga bhana lucky,mbona unakuwa kama mtoto wa kike vile"

"Alice hujui tu kwa nini nakuwa hivi.......kinachoniogopesha mimi hadhi yangu haiendani na wewe.je baba yako atakubali bintiye uolewe na mlala hoi,fikiria kuhusu hilo"niliongea nikionekana kuwa bado niko na mashaka rohoni.

"Bhana goodlucky niamini,hakuna baya litakalokupata ukiwa na mimi.ikitokea baba akakukataa bhasi jua kuwa na mimi atakuwa amenikataa vile vile.kwani ukiondoka wewe,mimi sibakii nyumbani nakufuata."alice aliniondoa wasiwasi.kidume nikalainika.nilichofanya nilijiandaa kisha tukatoka na kukabidhi chumba.tulipotoka nje ya fensi nilishangaa alice akiniambia tuingie ndani ya gari fulani lilikuwa limepaki pembezoni mwa barabara ambalo alidai ni lake,amekuja nalo yeye.daa asikwambie mtu gari lilikuwa zuri mpaka niliogopa kulipanda,lakini kwa sababu nilikuwa na Alice sikuona tabu.nikafungua mlango wa mbele nikaingia na kuufunga kwa kuuvuta na kuubamiza kwa nguvu.Alice akautekenya ufunguo uliokuwa pembeni mwa usukani,hapo gari ikaonekana kupokea moto na kukubali kuwaka.nikiwa namtazama namna Alice alivyokuwa akifanya,nikaona akikivuta kirungu Fulani hadi kwenye herufi 'R',ghafla gari ikaanza kurudi nyuma,hee nikashangaa,nikajisemea 'duuu kumbe herufi 'r' maana yake unaruhusu gari itembee kwa kurudi nyuma',aisee nikacheka kishikaji kisha nikatikisa kichwa ishara ya kushangaa namna ambayo dereva wangu Alice alikuwa akifanya kuliongoza gari.bhasi gari iliporudi nyuma kwa kiasi cha hatua kadhaa,Alice akaiweka vyema gari,katika usawa wa barabara,sijui akafanyeje fanyeje mara gari hiiiiloooo likaanza kwenda mbele.hapo nikaangua kicheko cha nguvu kitendo ambacho Alice ilimbidi aniulize kinachonichekesha.

"Hawa wazungu ni washenzi sana....."niliongea 

"Kwa nini"

"wanafanya vitu vingine vya ajabu ajabu sana,mfano hili gari.......halina akili lakini kila utacholiamuru linafuata.mwanzo umewasha limewaka,umeliamuru lirudi nyuma limerudi.asaivi limeanza kwenda mbele tena mmmnhhh hawa washenzi wana akili sana"kwa pamoja Mimi na alice tukaangua kicheko.ni wazi nae alifurahishwa na vijimaneno vyangu visivyo na msingi.

mwendo wa dakika sita au saba tangu tumetoka pale nilipolala,gari ikakunja kulia ikasonga kwa umbali Fulani kisha ikakunja kushoto kufuata lami ya barabara hizi ndogo za mtaani,tukavuka nyumba moja,ya pili nikamuona Alice akipiga honi,nikajua eeenhee ndo tumefika sasa,na sijui huko ndani itakuwaje manake jamba jamba iliyokuwa imenishika sio ya mchezo mchezo.geti lilipofunguliwa gari ikaingizwa ndani na kwenda kusimamishwa katika sehemu ya maegesho,ambako nako pia kulikuwako na magari mengine kama manne hivi.kuucheki vizuri mjengo wa akina'alice nikajikuta nikijuta ata kuja na huyu mwanamke.moyoni nilijua yale nitakayokwenda kuambiwa huko ndani sintotamani kurudi tena siku nyingine.nisiwafiche,kwao na Alice kiukweli walikuwa wako vizuri ni balaa.ukianza na mjengo wenyewe,magari,mazingira na vyote nilivyovikuta mule ndani ya fensi,hakuna ata kimoja kilichokuwa cha kimasikini.

"Hubby karibu nyumbani"Alice alinikaribisha,nikasema hee huyu nae kaniita jina gani tena.mi naitwa goodlucky,yeye ananiita hubby,ndo jina gani aisee.ila kwa kupotezea nikajibu...

"aaaa....aasannntee"

Itaendelea.

Mkali ndo huyo keshazama mjengoni,itakuaje akionana na baba wa alice.

kuyajua yote,namba 16 itatupa majibu. 

Post a Comment

Previous Post Next Post