KIBUTI 05💃

1st yr ikaisha, 2nd yr wakarudi kuendeleza gurudumu. Frank akawa anajilazimisha kuwa na Rebecca ingawa akimuoma Nurat huwa anaishiwa nguvu kabisa. 2nd yr ikikaribia kuisha, Frank akaanza kuzoea kuwa Nurat hamtaki na anatakiwa anendelee na maisha na aache kumtesa Rebecca.

likizo ya 2nd yr wakaondoka wote chuo, coz wanaishi Dar wote. Wakapanda zao Abood bus, wakaenda zao mjini likizo. ofcoz walipokuwa likizo walikuwa pamoja muda mwingi, ilifanya bond yao kuwa strong zaidi. Frank akaanza kumpenda Rebecca ile serious taratiiiibu. likizo ikaisha.

3rd yr(sio 3th bana), wakarudi chuo wakiwa wapenzi kamili. Sasa kulala hostel kukawa mara chache sana, wao ni lodge na hotels tu wanakula kuku(si wote wakishua, pesa ipo). sem2 Rebecca akapata ujauzito, bahati nzuri hadi anamaliza 3rd yr haikumsumbua na akafanya UE fresh kabisa.

Rebecca akagraduate huku Frank akiendelea na shule. Rebecca akapata kazi Dar, ila kila weekend yuko Moro anamletea utamu wake Frank. Frank hakutegemea kama Rebecca ni smart, loving, caring, supportive woman kiasi kile. Kwa asilimia kubwa Rebecca alikuwa anamsupport Frank.

@hadithikali 

Post a Comment

Previous Post Next Post