No title

Nikiwa nimekaa nje niliwasikia wakitoka chumbani na kuja kukaa sittingroom, sikuwafatilia sana maana niliwaona wapumbavu tuu....
   Siku zilisogea na sikukata tamaa maana sikutaka kurudi nyumbani nilijua ipo siku kila kitu kitakua poa,,lakini nilifanikiwa kupata kazi ya kuuza duka la nguo hapohapo kimanga, nilikua nalipwa elf 80 ni ndogo ila ni bora kuliko kukaa bure na kukosa kabisa, ghafla jirani yetu mkaka jina tumuite francy maana dada yake yupo kwa group siwezi taja jina lake halisi,,,francy alianza kunizoea ghafla tu,,akitoka kazini lazima aniite anisalimie,au anipe zawadi yoyote tu,,nami nilikua napokea na alikua ananipa kampan maana fridah alikua akija na watu wake mi naishia kukaa nnje,hivyo francy alikua anatoka tunakaa nnje tunapiga story wakiondoka anaingia kwake nami naingia ndani,,,alinieleza mengi niliyokua siyajui kuhusu frida lakini sikutaka kumfatilia maana pale nipo kwake na sikua na muelekeo wakati huo....kipindi chote nipo dar esaalam sikuwahi mtafuta sylivester wala sikutaka kwenda anapoishi maana niliona haina haja ya kua nae tena....urafiki wetu na francy ulizidi mwisho wa siku tukawa wapenzi,,,francy alikua mtanashati,na asiependa makuuu alafu alikua mkimya sana,,,nilivutiwa kua nae maana alionekana anajitambua na sikuwahi kuona mwanamke anaingia kwake labda kama walikua wanakutana nnje ya pale maana mwanaume hashindwi,,,mahusiano yetu yalikua yasiri sana sikutaka frida ajue na hatukuwahi kukutana kimwili,, Siku moja wakati nikiwa njiani narudi nyumbani msg ikaingia kwenye simu yangu,,kufungua ni frida, ametuma ujumbe akisema,shoga ushapata kazi sasa tafuta kwako mimi leo mchumba wangu anakuja na kesho nahama nahamia kwake nitaamisha vitu vyote hivyo naomba uhame maana sitaweza kwenda na wewe,,,,dooh niliishiwa nguvu😪😪😪 machozi yalinilengalenga nikawaza nafanyaje sasa niende morogoro, nikaona hapana lakini nitakaa wapi na kazi ndo kwanza nimeanza hata mshahara sijapokea,,,sikumjibu chochote ila cha kwanza nilimpigia francy nikamuomba tuonane, akanuuliza uko wapi nikamuelekeza, akaniambia nikae sehem nimsubiri anakuja, nilitafuta sehem nikakaa nikaagiza maji nikawa nakunywa,,,hakukawia sana alifika,,,baada ya salamu nikamweleza moja kwa moja wala sikupindisha,,,,francy nimetumiwa ujumbe na fridah kasema kesho anahama na sijui nafanyaje na kurudi morogoro sasa hivi sitaki,,,,francy akaguna kwanza kisha akasema pole sana mamie ila usijali mi nina wazo kama utaliafiki nitafurahi,,,nikamwambia niambie tu nakusikiliza usijali,,,akanyamaza kidogo kisha akasema naomba tuishi wote,, 😳😳😳 we francy unasema??? Naomba tuishi wote winie mimi nakupenda sana na nimeona unafaa kua mke wangu nakuomba mama unikubarie,nilitamani kukwambia muda ila nilihisi bado mapema ila kwa sasa hakuna namna labda mungu amepanga iwe hivyo nakuomba,,,,nikamwangalia kwa mda kisha nikamjibu,,francy hunijui nami sikujui vizuri unawezaje kutamani kuishi na mimi ghafla hivyo,,,siyo ghafla nilitamani muda mrefu sana sema sikujua naanzia wapi kukwambia,nipo tayari kwenda kwenu kujitambulisha nataka nikuoe kabisaa winie naomba unielewe....alinibembeleza sana na ukizingatia sikua na pa kwenda kwa wakati huo nikaona isiwe shida ngoja nijaribu labda hili ni fungu langu,,nikamwambia, nimekubari ila kwa mashart mawili,, sema chochote mama nipo tayari,,,nikamwambia kwanza naomba tukapime afya, alafu ukikaa sawa naomba pale uhame maana sitakua na uhuru sana nikikaa nawe pale,,,hilo halina shida mama twende hata sasa hivi tukapime, na kuhusu kuhama hilo halina shida nitahama,,nikamwambia sawa twende,,,tukatoka tukatafuta usafiri tukaenda dispensary tukapima na majibu yakatoka safi wote tuko wazima, nilishukuru mungu sikutaka kurudia mistake niliyoifanya kwa sylivester,,,,tulipotoka dispensary tukapitia sehem tukala tukarudi nyumbani ila tulikubariana niende kwanza kwa frida nikikuta yupo na mtu wake kama alivyosema ndo niende kwake,,,,tulipofika nyumbani nilipitiliza kwa frida ila kila nikifungua mlango umefungwa na nasikia watu wanaongea ndani ila kwa sauti ya chini,,,nikagonga kama mara tatu kimya,,nikampigia ili anifungulie simu haikupokelewa,hapo francy anashuhudia kila kitu,,,akanishika mkono akaniambia mamie muache njoo ulale huku,,,nikaondoka kinyonge tukaingia kwa francy, ndo mara ya kwanza naingia ndani kwake sikuwahi kuingia hata nilipokua na mahusiano nae.....
ITAENDELEA......... 

Post a Comment

Previous Post Next Post