Niliwakuta wanae yeye alikua ameenda kwenye biashara zake,,,tukasalimiana nikaenda chumba ambacho mara nyingi nikiendaga hua ndo nalala...nikajilaza kitandani nikitafakari niliyoyafanya...hapo sisikii maumivu wala nini nipo kawaida tuu na dam zilikua zinatoka kidogo....nilikaa kwa dada pale wiki nzima na damu zilitoka haswa zile za mimba kutoka ikafika hatua nikivaa pedi nikisima imejaa tena na inapenya pembeni muda huohuo nikienda chooni nikichuchumaa yanashuka tu mabonge ya damu puu yaani ilitoka dam acheni tu hapo dada akiondoka alfajiri kurudi usiku saa nne na akifika ni kula kulala hana mambo mengi yaani alikua anachoka sanaa ko muda mwingi nilikua nalala tu ndani na choo kilikua cha ndani maji muda wote yanamwagika hivyo haikunisumbua na hakuna aliyejua maana watoto wake walikua wadogo,,,wakwanza alikua la saba wa kike, wapili alikua la nne, na wa mwisho alikua chekechea na msichana wa kazi alikua si wa kunifaatilia maana alikua analala chumba tofauti na mimi,,, hapo tumbo lilianza kuniuma japo si sanaaa ila lilikua linaniuma nikaenda duka la madawa nikamwelezea akanipa flagily na zile za rangi mbili akaniambia ninywe kutwa mara tatu, zilinisaidia kupunguza maumivu,,,nilikaa kwa dada hadi nilipopata nafuu kabisaa na dam kuacha yaani nikawa kawaida nikaaga na kurudi nyumbani,, hakuna aliyenishtukia ila nilipofika nyumbani mama aliniuliza umefanya nini ulivyotoka chuo? Nikamwambia sijafanya kitu mama?? Akasema mkurugenzi kanipigia simu kasema unaujauzito walikupima wakagundua ni mjamzito...nikamwambia mama na wewe unamuamini mama? Sasa si ungenijua kama nina mimba jamani niko tayari hata sasa hivi twende ukanipime,,,hapo najua nishaitoa sina wasiwasi,, ila nikashangaa kwa mara ya kwanza mama anakua na jambo alafu amelivumilia hadi nimerudi dooh maajabu,,, akaniambia kama unamimba hapa kwangu ondoka mapemaaa sikataki mizigo na ukipata ukimwi mimi si mama yako usinitambue we endelea kuhangaika,, unaona navyohangaika kuwasomesha mwenyew baba enu hata mia hajawahi kutoa sasa tusisumbuane,,,kisha akaondoka,,,sikua na wasiwasi maana mimba ilishatoka niko fiti...
Siku zilisogea na likizo ikaisha nikarudi chuo,,nilifika hostel kama kawaida hapo mama alinikabidhi ada ya semester ya mwisho nawaza namna ya kureport chuo na kukutana na mtu mzima hovyo maana mama sikumwambia ujumbe alionitumia mkurugenzi na inavyoonekana hata alivyowasiliana na mama hakumwambia hivyo nilijipa moyo kua alikua ananitishia tu,,, Siku hiyo ilipita kulivyokucha nikajiandaa nikaenda chuo prisca alikua hajawasili chuoni bado,,,nilivyofika nikawasili kwa secretary nikalipia ada nikapewa risiti nikaondoka nikaenda darasani sikutaka kukutana na mkurugenzi na wala sikuitwa...siku zilisonga nikiwa naendelea na masomo na hofu ilishanitoka nikaona hakuna kitakachotokea,,,,lakini ghafla hiyo siku baada ya kutoka breakfast tulitangaziwa wanafunzi wote tunaitwa Holini,, kulikua na holl kubwa ambalo tunaingia wanachuo woote kama kuna mkutano au kikao hua tunafanyia huko...tulifika kila mtu alikaa sehem yake na staff nzima na uongozi wa chuo ulikuwepo...mkurugenzi akasimama akasema tutakaowaita hapa unakuja unachukua barua unatoka nnje...daah hakuna aliyetarajia hilo lakini waliitwa wanafunzi wengi na mimi nikiwemo nikapewa barua nikatoa nnje,, nikapiga hatua chache nikafungua nikaisoma,, ilikua barua ya kusimamishwa mafunzo kwaajili ya utovu wa nidhamu na malimbikizo ya ada ya hostel...nilikaa chini maana nguvu ziliniisha nikajuta kwanini nilitoa mimbaa,,,yaani natoa mimba alafu nasimamishwa chuo si bora ningeiacha tu nililia kwa uchungu jamani ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ prisca alinifata akaniambia mamie watu wanakuangalia ebu twende hostel kwanza,,,nilinyanyuka tuakaenda hostel nikampa barua akaisoma akanipa moyo kua nisikate tamaa yataisha tu ila nilijikuta nauchukia ualim kuanzia muda huo nikamwambia mamie mimi basi tena sitaki kuendelea kesho ntarudi nyumbani nakukabidhi vitu vyangu utaniuzia alafu utanitumia hela yangu...akasema usichukue maamuzi ya haraka hivyo,,,nikamwambia basi sitaki kuhangaika tena labda siyo rizki yangu....kweli kesho yake nilikabidhisha chumba nikaacha maagizo kua vitu vyangu kuna mtu atakuja kuvichukua niliondoka na kurudi morogoro hapo sikumtaarifu mama chochote na nilivyofika nyumbani nilimkuta hajarudi kutoka kazini. Nilifika nyumbani mida ya saa nane na mama anarudi sasa tisa ama kumi hivi....mama aliporudi alinikuta nimekaa sebleni na mabegi yangu hata chumbani sikuingiza alishangaa wewe vipi mbona uko hapa,, nikaanza kulia,,,ebu niambie kwanza usilie unanini? Nikamueleza kila kitu na kumkabidhi barua,, aliishiwa nguvu kabisa akasema nitaenda chuoni kuongea na uongozi waniambie wanashida gani na ww kwanini inakua hivi,,,ilibidi nimueleze mama kila kitu kuhusu mkurugenzi kunitaka lakini sikuwahi kumkubaria,, kama mzazi alinielewa na aliumia na nikamueleza hali halisi ya matatizo ya mkurugenzi nikamwambia mama mimi sitaki tena kurud asije nivizia siku akanibaka bure mimi sirudi
ITAENDELEA....
Tags:
CHOMBEZO