SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA: 12

Kuanzia kipande hiki ndio lengo la story hii inaanza na nitaomba mwisho wa story mnisaidie ushauri wapendwa wangu....
  Tuendelee,,,,Nilifika nyumbani mama yangu alinipokea vizuri na nilikua kanipikia pilau na ndizi mama yangu ni muhaya anapenda sana ndizi,, nikafikia kula kisha nikaingia chumbani kuvuta pumzi kwanza hapo nawaza wapi nianzie kutoa mimba,,,mtaani sikuwahi kua na rafiki wa kumshirikisha mambo yangu kiufupi mimi sikuwa mtu wa mashoga kulingana na jinsi tulivyolelewa nilishajizoelea kua peke yangu, rafiki yangu mkubwa alikua dada angu mtoto wa mama mdogo ambae tulikua tunaishi nae alikua akisomeshwa na mama huyo niliweza kumwambia mambo yangu japo si yote ila kwa hili nilidhamiria kumshirikisha,, nilifika chumbani nikajitupa kama mzigo najua mnajua usingizi wa mimba changa ulivyo,,na uzuri sikuwahi kutapika wala kubagua chakula yaani kila kitu nilikua na kula na sikuwahi kutapika wala kwa bahati mbaya tangu nijigundue,,ila nilikua nikilala utanisahau naeza amka kesho...basi nilijitupa kitandani nikiwa na nguo zangu na usingizi ukanichukua nakuja kushtuka saa nne usiku tena naamshwa na mama,,,akitaka niamke nibadiri nguo nilimuitikia kua naamka lakini sikuamka nilikuja kuamka siku inayofata mwili umechoka hatari najisikia mchovuu tu natamani kulala tu...nikajikongoja nikaamka nikaenda kuoga nikakuta nyumba nzima walishaamka kitambo hapo nasikilizia kama mama ataniuliza chochote lakini hajaniuliza...nikamsalimia mama nikaenda mezani nikamimina chai nikanywa kisha nikakaa sittingroom na wengine tukawa tunaangalia movie,,,ghafla msg iliingia kwenye sim yangu kuangalia mkurugenzi,,,nikafungua haraka haraka nikakuta ameandika,,,umwambie mwenyew mama yako ujinga ulioufanya kabla sijamwambia nakupa siku mbili,,,na ukirudi urudi na hela ya hostel ya semester hii la sivyo nakusimamisha chuo...uwiii yameanza upyaaa nikajikuta nimesema kwanguvu...manini hayo mama akaniuliza? Nikashtuka nikasema hamna mama kuna rafiki yangu hapa nachart nae,,,nilinyanyuka nikaenda chumbani nikamkonyeza dada angu aje yeye anaitwa suzy,,, fasta alikuja chumbani nikamuelekeza kila kitu na nikamwambia nataka kuitoa hii mimba sihitaji ushauri kwa hilo,,,akaniambia lakini ni hatari si unajua nikamwambia hapana shida najua ila sina namna,,naomba unisaidie kwa hili nataka kununua dawa ila sijui naanzia wapi,,,akaniambia ngoja kuna rafiki yangu nitaongea nae anazijua dawa alafu nitakujulisha lakini mama si atagundua nikamwambia nitaenda kwa dada Anna nitakaa huko hadi nijisikie vizuri kisha nitarudi nitasema naenda kumsalimia, okay sawa basi ngoja nikamcheki alafu nitakupa jibu nikasema sawa,,huyo rafiki yake tulikua tunakaa nae mtaa mmoja,,,,nilijua kwa dada yangu tuliezaliwa tumbo moja sitajulikana maana yeye yupo busy sana mda wa kukaa nyumbani hana hivyo nisingekundulika...punde suzy alirudi akaniambia ameniambia dawa zipo zinauzwa elf 25000 kama ipo nipe nikampe akanichukulie,,,aisee sikufikiria mara mbili nikampa hela maana nilikua nina kiakiba changu na suzy akatoka akaenda, nikasema ngoja nikamchek mama kwanza nafika sittingroom hayupo nikamuuliza kaka angu akaniambia ameenda chumbani nikamfata, niligonga akanikaribisha nikaingia nikamwambia mama samahani kesho naomba niende kwa dada kumsalimia,,,jamani umefika hata ujapumzika unataka kuanza kuzulura,,,nikamwambia nataka niende nikae siku chache ili nikirudi niwe busy nataka kujisomea maana tukirudi tunajiandaa na mtihani wa mwisho...akasema sawa ila usiende kukawia nikamwambia sawa...nikarudi chumbani nikakaa kumsubiri suzy arudi nikashikilia tumba langu nikajikuta machozi yananitoka 😭😭😭 mwanangu nisamehe najua natenda kosa ila sina njia nyingine nakutoa huku roho inaniuma,,,nilipiga magoti nikasali na kutubu,,,nilimlilia mungu asikie maombi yangu na asije niadhibu kwa namna yoyote ile kwa dhambi nayoenda kuitenda, niliomba mda mrefu huku nikilia na kujutia ujinga nilioufanya,,,ghafla suzy aliingia,,,vipi mbona unalia kuna shida??? Nikamwambia,,,suzy dada angu moyo unaniuma sana kwa hiki nachomifanya ila mama yangu unamjua alivyo mkali ataniua mimi,,,suzy akanibembeleza akaniambia kama moyo wako unasita basi acha usiitoe,,,nikamwambia hapana lazima niitoe,,nikafuta machozi nikakaa kitandani vipi umepata dawa? Akaniambia ndio nimepata hii hapa akaitoa akaniambia amesema kimoja uweke chini ya ulimi kingine kwa bibi nikamwambia sawa nitafanya hivyo usiku maana kesho asubuhi naenda kwa dada,,,mama umeshamwambia aliniuliza,, nikamwambia ndio na amekubari akasema poa....
    Usiku ulipofika nilifanya kama nilivyoelekezwa nikavaa pedi nikalala...asubuhi niliamka nikaona vitone tu kidogo vya dam nikajua hii tayari,,,baada ya chai nilijiandaa safari kwa dada kumbukeni hapo sijatumia dawa yoyote ya kutuliza maumivu na sikujua kama kuna dawa nyingine zaidi ya hiyo... Nilifika kwa dada baada ya lisaa, alikua anakaa morogoro hapohapo maeneo ya mafisa...niliwakuta wanae yeye alikua kwenye biashara zake........
ITAENDELEA........... 

Post a Comment

Previous Post Next Post