SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA. 11

Akawasha gari mbio dispensary....kufika akaita msaada wakatoka manesi nawasikia kila kitu wanachoongea ila nilijifanya nimezimia,,,wakaniweka kwenye machela hadi kwa doctor, nikalazwa kitandani, doctor akamwambia nipishe kidogo nitakuita,,,hapo nilivyosikia anatoka nikaanza kufungua macho taratibu kama ndo nazinduka doctor akawa ananitingisha hello,hello unajisikiaje? Nikamuangalia tu doctor sikutaka kukurupuka,,,akachukua cha kupimia presha akanipima kisha akasema presha yako iko juu sanaaa,,,,akanitazama kisha akaniuliza we mjamzito eeh,,,nikatikisa kichwa maana huezi mdanganya doctor akasema sawa ndo maana uliishiwa nguvu,,ulipata kitu cha kukushtua? Nikamjibu hapana,,,sikutaka kueleza sana,,,kumbe najua nimeponea chupuchupu kupewa vijidudu, akaniuliza unajisikiaje sasa hivi kuna sehem unasikia kuumwa? Nikamwambia niko sawa niliishiwa tu nguvu ghafla ila niko sawa,,,akasema okay ila inabidi upumzike kwanza tukutulize hiyo presha alafu utaondoka baadae sawa,,,nikamjibu sawa,,,akachukua karatasi kaandika maelezo yake pale akatoka nje sikujua nini kinaendelea ila nilimuona nesi anakuja akaniwekea drip hapo hapo kwa doctor kisha akatoka nikamuona mkurugenzi anaingia amekunja sura kama ameona kinyesi,,,,unajisikiaje,,nikamjibu vizuri, akanitazama kisha akatingisha kichwa akaniambia nipo nje nakusubiria,,,dooh nikajua huyu kashaambiwa na doctor kua nina mimba na nilisahau kumuomba doctor afanye siri nikajua hili mama litamfikia tu...nikakumbuka mama pamoja na ukali wake wote ila alikua ananiamini sana nikajua si rahisi kumuamini mkurugenzi lazima angetaka kujirudhisha kwa kunipima mwenyew nikasema hapa nikitoka nitatafuta cha kufanya....
   Presha ilikaa sawa baada ya muda nikaruhusiwa hapo mkurugenzi alikua ananisubiri mda wote nnje alivyoona natoka alinishika mkono huku sura ameikunja,,alishalipa gharama za matibabu tukapanda kwenye gari akawasha tukaondoka hapo nawaza sijui narudishwa hotel au naenda hostel,hanisemeshi kitu hapo yupo kimya tu,,,akanipeleka hadi hostel nilishukuru kimoyomoyo,,,tulivyofika akapaki akaniambia,,,hivi we binti una akili kweli??? Yaani unakula hela zangu, nakuhudumia kumbe una vibwana vyako huko eeh,, alafu wamekupachika li mimba hilo alafu umekaa kimya ulitaka unibambikie au??? Nikacheka kimoyomoyo nikasema hili vipi nikubambie hiyo vipi kwani ulijua ntakupa au? Sikumjibu kitu niliinama tu kimya,, akasema, si naingea na ww au hunisikii?? Nikamjibu dear nisamehe mi hata sielew imeingiaje,,,,akaja juu kwa hasira hujui imeingiaje we mjinga nini unaniona mimi mtoto mdogo sasa shuka kwenye gari na usinipigie na popote ukiniona pita mbali ntajua la kufanya shuka haraka mpuuzi wewe....nilishuka hapo nawaza nikajua akifika cha kwanza atampigia mama...ila sikua nawasi sana nilijua cha kufanya,nikashuka nikaenda hostel nilivyofika nikampigia prisca nikamuomba aje hostel nilimwambia najisikia vibaya,,bila hiyana alikuja akaniuliza nini shida nikamwambia nina malaria,akasema umeenda hospitali nikamwambia ndio nimeenda akasema pole dear pole Sana utapona,,hapo bado siku mbili twende likizo,,,prisca alinihudumia alikua anakuja kila siku asubuhi jioni anarudi chuo maana hawaruhusiwi kulala nje,,,,chuo kilipofungwa alikuja kwangu akakaa nami siku mbili akaondoka kwenda kwao yeye alikua anakaa dodoma hukohuko,,,,mama nnilimwambia kua naenda likizo lakini aliongea nami kwa kuchangamka tu nikajua mkurugenzi hajamwambia,,,na mkurugenzi hakuwahi nipigia tena sim wala kunitext tangu tulipoachana,,, nami nilijiandaa nikarudi nyumbani likizo hapo nilijua nikifika tu cha kwanza ni kutoa mimba ili nisimkwaze mama maana na chuo hatukuruhusiwa mjamzito kuendelea na masomo,,,,laiti ningekuja ya mbeleni ningeacha tu nizae 😭😭😭😭😭😭 
 ITAENDELEA......... 

Post a Comment

Previous Post Next Post