SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA: 14

Nilimkatalia mama kurudi chuo,alinifokea sana kua nimempotezea pesa zake lakini nilisimamia msimamo wangu nilikata tamaa kabisaaa,,,nikamwambia mama nikilazimisha litanikuta jambo pesa si kitu ila thamani na utu wangu ndo vitu vya muhim, na kumbe mama siku hiyo alikua kavurugwa,,alisimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi kuna pesa nyingi zilipotea offisin kwao na yeye ndo alikua akikaa na funguo, alikaa kimya hakusema kitu ni kama maneno yalimuingia,lakini kwa macho nilimuona hayuko sawa kabisa ila niliogopa kumuuliza maana haingiliki kizembezembe....aliingia chumbani kwake,,,ila baada ya siku kadhaa alituambia kilichomsibu offisin maana alikua haendi kazini, alisema kasimamishwa kwa muda uchunguzi ukikamilika kama atakua hajahusika atarudi kazini hivyo alikua tu nyumbani muda wote.
   Siku zilisonga miezi ikakatika nipo tu nyumbani, niliona shidah maana kukaa na mama yangu mda mrefu ni mtihani, kubanwa mwanzo nwisho,, umri umeenda ila alikua ananiona bado sanaa yaani kama nina miaka kumi hivi,,,ukikosea kidogo unakombezwa kama mtoto mdogo tena mbele ya watu hata wasiohusika, unatolewa maneno makali mpaka unahisi kufa tu,,nikaona hapa sitapaweza acha nitafute pa kwenda angalau akili ikafanye kazi,,,sehem ya kwanza niliwaza kwenda dar esaalam maana huko mishemishe zilikua nyingi,,,nikawaza pa kufikia, nikakumbuka kuna rafiki yangu tulisomaga wote A-level anaishi dar esaalam nikaona nimpigie maana no zake nilikuaga nazo sema sikua na mazoea nae sanaa ya kuongea nae,,,nikampigia na uzuri alipatikana akapokea,,,hello,,,hello mambo frida,,,poa tu mzima ww? Nikamjibu mi mzima dar wanasemaje? Akaniuliza, hivi unajua sijui naongea na nani maana nilibadiri sim na imekuja no tu,,nikamwambia mimi winie,,nikamkumbusha kua tulisoma wote,,,,,okay winie dear habari za siku? Uko wapi sasa hivi? Nikamjibu, za siku nzuri mamie,nipo moro sasa hivi ila nataka kuja dar esaalam sijui pa kuanzia je naweza pata chumba huko cha bei nafuuu maana nataka kuja kuanza kujitegemea ila sina pesa ya kutosha,,,,akaniambia vyumba vipo vingi tuu sema vya bei nafuu mazingira hayaridhishi sanaaa na navyokujua sijui kama utaviweza,ila unaweza kuja kufikia kwangu ukakaa kwa muda ukijichanga ukapata hela ya kutosha utatafuta sehem nzuri...nikamwambia asante dear basi ngoja niweke mambo sawa nakuja wiki hii hii akasema poa,,nikakata simu,,,,hapo nina hela ya vitu vilivyouzwa nilivyokua natumia dodoma,nilikua kama nina laki nne hivi, nyingine nilishatumia tumia....nikasema nitaenda kuanzia hii hii si mbaya mungu ataniongoza...nikapanga namna ya kumuaga mama hadi aniruhusu nikapata jibu. Kwa muda huo alikua chumbani kwake nilimfata nikaanza kuongea nae,,,mama samahani naomba ruhusa yako,kuna kazi imepatikana dar esaalam naomba niende kujaribu bahati yangu,,,alinijibu, ni kazi gani utaenda kufanya wakati vyeti vyako vya shule vipo chuo,,,subiri mambo yangu kazini yaishe nipate hela twende kufatilia vyeti vyako ndo ujue unaanzia wapi? Nikamwambia mama usijali sana huko kuna rafiki yangu kanifanyia mpango offisin kwao na hakuna haja ya vyeti maana mwajiri ni kaka yake naomba niende mama nikikuta hapaeleweki nitarudi,,,okay na utaenda kufikia wapi? Aliniuliza,,,,nikamjibu nitaenda kufikia kwako kwa muda nikipata hela nitatafuta sehem yangu ya kukaa,,,ilibidi anikubarie tu maana hakua na la kufanya na hali kidogo ilianza kua tete nyumbani maana woote tulikua tunamtegemea yeye na yeye yupo kwa uchunguzi....
   Nilipanga mambo yangu yakakaa sawa, nikawasiliana na frida nikaenda dar esaalam,,alinipokea ubungo tukaenda hadi kwake tabata kimanga, alikua anakaa chumba na sebule,,,alikua amejitahidi kiukwel hadi nilimuonea wivu nikaona kama nilikua najichelewesha tu...alikua anafanya kazi kilimanjaro hotel yuko mapokezi...kiufupi alikua anajiweza vizuri tu.....nilikaa kwa frida bila shida yoyote japo alikua na mapungufu yake lakini sikuyafatilia sana maana nilijua nakaa kwa muda tuu,,,na aliniahidi ikipatikana chance kazini kwako atanifanyia mpango na mimi nilikua nahangaika akitoka asubuhi nami natoka nazunguka zunguka viwandani kutafuta kazi maana kukaa tu kwa mtu bila kazi ni mtihani,,,mama hapo nilimdanganya kua nimepata kazi ili asinisumbue kurudi nyumbani,,,,nilikaa kwa frida karibia miezi minne hapo kiakiba changu kilishaisha na sijafanikiwa kupata kazi maana nilikua nasaidia kununua mahitaji yaliyokua yakihitajika pale,,,hapo ndo nilijua tam na chungu ya dar esaalam
ITAENDELEA.............. 

Post a Comment

Previous Post Next Post