SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA; 18

Miezi ilosonga, niliongea na mama kuhusu ujio wa francy na mama akaridhia na kufurahi,,maana hilo ndio tamanio la kila mzazi kuona binti yake anapata starah na si kuangaika na waanaume,,,Alifanya taratibu zote akatoa barua na ikapangwa siku ya kutoa mahari na mungu alisaidia akatoa mahari yoote tukabaki tunajipanga na kufunga ndoa,, wakati huo bado tunaishi hapohapo nilipomkuta hatukuhama kama alivyoniahidi nami sikumlazimisha sana maana kipato chake hakikua kikubwa sanaa alafu majukumu yaliongezeka na ukizingatia kwao ni mtoto wa kwanza hivyo familia nzima inamtazama yeye kwa kila kitu, na kama unavyojua kazi za wahindi zilivyo, na frida alihama pale kwa aibu na sikujua alipoamia na sikua na mawasiliano nae tena, ile kazi niliyokua nafanya mwenye duka alifunga hivyo kazi ikaishia hapo, francy alikua anafanya kwenye kampuni ya muhindi,,,yaani kazi nyingi mshahara mdogo,,ila hilo halikunisumbua maana tulipendana sanaa hivyo tuliishi kwa kuvumiliana,, na hasa wanawake tukipenda hua tunakua wavumilivu sanaaa,, miezi saba ya mwanzo niliishi kwa raha sana,,alikua anajua majukumu yake yaani ndani chakula hakikosekani,,,na alikua akipata mshahara alikua ananipa nipange matumizi ya kununua ndani yeye alikua anachukua elf 50 tu kilinda mfuko,maana kazini kwako walikua na stuff bus inawapeleka na kuwarudisha hivyo alikua hatumii nauli labda mara mojamoja akilichelewa bus la offisi,, wazazi wake walikua wanaishi songea ila dar esaalama alikua ana mjomba ake alikua anaishi tabata segerea,,,huyo ndo alikua kama mzazi wake kwa dar esaalam maana wazazi wake walikua mbali,,hivyo akipata shidah wakanza ni mjomba kuja kutuangalia na wao ndo walisimamia hadi kupeleka mahari nyumbani,Mjomba ake alikua dereva kwenye office za bachkresa, alikua ni mwenye upendo sanaa na alijaaliwa watoto watatu tu wa uzeeni yaan shangazi uzazi ulimsumbua alichelewa sana kupata watoto,, mjomba alikua mtu poa sana mungu ampumzishe kwa amani, ila shangazi uwiiiii alikua kichefuchefu jamani,,alikua na maneno ya shombo sipati kusimulia yaani hakuwai kunipenda ile kutoka moyoni nahisi alikua anazuga tu, alinifanya kipoozea cha stress zake,,,, pia francy alikua na mdogo wake wa kike ila ni binamu yake nae alikua ameolewa,,alikua hakai mbali sana na sisi walikua wanakaa tabata matumbi,, hivyo tulikua tukitembeleana,,mwanzo tulishirikiana sana na wifi yangu ila mbele alikua ni mwiba kwenye maisha yangu na kaka yake😭😭😭.
    Maisha yalianza kua magumu baada ya kukaa muda mrefu bila kushika ujauzito 😭😭😭😭😭 nilitekesa mimi jamaniiii uwiii sitaki kukumbuka,,mwanaume hakuwahi niongelea vibaya kuhusu kutoshika mimba na hata wakwe zangu yaani wazazi wake songea,,walikua bega kwa bega na mimi kunitumia dawa za kila aina ili nishike ujauzito,,walinipenda sanaaa nisiwe mnafki yaani wakijua naenda wanaona kama sifiki,,,sikuwahi kua na maringo,shamba tulienda kulima, kama n msimu wa kuvuna nilienda kuwasaidia mpaka kumaliza kuvuna kisha narudi dar esaalam,, walinipenda sanaaaaa hasa baba mkwe jamani mungu akupe maisha marefuu,,, tulihangaika dawa kila sehemu ili nishike mimba lakini sikufanikiwa, kwa doctor mwaka mpaka nilijaza makopo ya dawa zake salfet tatu ila wapi,,nilikunywa dawa hadi nikazichoka,,,siku moja francy aliniuliza,,mkewangu kwani hujawahi shika ujauzito hapo nyuma??? Alinikumbusha kidonda ambacho mpaka leo hakijapona,, nikamwambia nilishawahi ila ilitoka,,sikutaka kumwambia ilivyokua maana wanaume hawatabiriki,, basi usijali mkewangu muda tunao tutapata mtoto wetu tu nawe utaitwa mama,,,kiukweli francy alinipenda sanaaa yaani sanaaa ila sasa upendo wake kwangu ukawa kilio maana alijua kuniumiza kichwa sasa sijajua ndo design yake ya kupenda au vipi sijajua hadi leo,,,
   Kwanza alikua anapenda kufanya jamani yaani hakuna siku ananipumzisha labda nikiwa period tu yaani kila siku ni kunipanda tuuu,,,akishinda nyumbani jumapili nikikaa hovyo tu napandwa, usiku kabla ya kulala ni lazima tena kila siku,,asubuhi alfajili kabla ya kwenda kazin lazima afanye na alikua haelewi yaani ukimkatalia atakusumbua hutalala usiku,ukitaka kulala bora uumpe tu hivi hivi hutalala,,hali hiyo ilinichosha sanaa nilijihisi kama nimekua mtumwa wa mapenzi😭😭 maana mwanzo nilijua labda kwasababu mapenzi yanaanza hajanizoea akinizoea atapunguza lakini wapi hali ilikua ni hiyohiyo,,,nilikua nakula lakini mwili umekaukiana hauna nuru jamani 🍆🍆 hii kitu inafubaisha sanaaa....sina mtu wa kumuuliza kama ndoa ndo zilivyo, sikuaa na rafiki kabisaaa toka nilivyoachana na frida sikuaga na urafiki kabisaaa na mtu yoyote nilikua najifungia tu ndani mpaka akija francy ndo napata wa kuongea nae, kuhusu kazi aliniambia nivumilie atanifungulia biashara hakutaka niajiliwe sijajua kwanini,,,siku hiyo nikaona acha nimpigie dada yangu nimuulize kuhusu namna ya kuishi na mume maana yeye aliolewa muda mrefu na ni mtu mzima,, nilimpigia simu nikamuuliza, dada angu sijawahi kukwambia chochote kuhusu maisha yangu ila naomba unisaidie.
ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post