SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA. 8

 Nilivurugwa baada ya kupokea simu ya mkurugenzi nikajiuliza mbona madam hajaniambia kama mkurugenzi amefika chuo??? Niliwaza nikaona nimpigie madam alipokea hello,,hello madam shikamoo, samahani mkurugenzi amerudi? Akajibu marhaba, hapana hajarudi nami nipo chuo sasa hivi kwani vipi? Nikamwambia amenipigia amesema kesho nije offisin kwake,,,madam akanijibu labda yupo njiani anarudi au ameshafika labda yupo kwake ila hapa chuo sijamuona huenda kesho ndo atakuja offisin...nikamwambia asante madam nikakata sim hapo muda huo sylivester alikua ameenda kwao mara moja nilikua mwenyew tu gheto...nikaona nimpigie arudi kuna jambo tuongee, haikuchukua muda alifika,,,vipi mama mbona unanishtua kuna nini? Aliingia na swali nam nikamjibu, mama kanipigia simu kesho anaenda dodoma hivyo atapitia hostel kunisalimia na hajui kama nipo huku,,,sasa itakuaje aliniuliza,,,inabidi niondoke kesho yaani ingekua mapema ningeondoka leo hii hii maana asiponikuta itakua shida akasema ngoja kuna rafiki yangu hua anagari ya mizigo anapelekaga dodoma na anaendaga usiku alfajiri anakua amefika dom ngoja nimuulize kama leo anaenda,,,aisee nilishukuru nikamwambia em mpigie...akampigia na baada ya kupokea sim alimuueleza kua shm wako anatakiwa kesho alfajiri awe dodoma kuna dhalura vipi leo unaenda dom,,,akamjibu hapa tupo tegeta tunapakia mzigo usiku tunaondoka hivyo kama ataweza tumkute mbezi mwisho tutampitia maana tuna mzigo tutapakia pale pia...akamjibu poa nampeleka mtatukuta hapo...akakata sim na kunieleza kila kitu yaani sikulemba nikajiandaa haraka haraka na kwasababu sikua na mizigo ni pochi tu ilikua haraka na pesa nilikua nayo naye aliniongezea elf 30 akaniambia imekua ghafla ukifika nitakutumia nikamwambia usijali tukaondoka hadi kituoni tukapanda gari safari mbezi mwisho na muda huo ilikua saa kumi jioni....
    Mbezi tulifika saa kumi na mbili kasoro tulitafuta sehem tutakaa tukimsuburi hapo naomba mungu tu asije kugairi safari...tulikaa mpaka saa mbili kasoro usiku ndio walifika alipiga simu akatuelekeza alipopaki tukaenda nikapanda tukaagana safari ikaanza ya kwenda dodoma....nilimshukuru mungu sana niliomba atutangulie tufike salama...njiani hatukua na story nyingi maana ni usiku umakini ni muhim na hakua muongeaji sanaa muda mwingi nilikua nalala tu...ilipofika saa kumi usiku tulifika dodoma akaniambia sasa nitakufikisha hostel maana hapa ukisema uende mwenyew utapata shida nikamwambia sawa ntashukuru...kweli alinipeleka hadi hosteli nilishuka nikagonga mlinzi alifungua nikaingia nae akaondoka, nilisalimiana na mlinzi akaniuliza vipi kwema? Mbona muda huu? Nikamwambia usijali tutaongea kesho ngoja nikapumzike,, mlinzi alikua mtu poa tu hakuaga na mambo meengi alikua mwelewa sanaaa,, moja kwa moja hadi chumbani kwangu nikavua nguo nikaenda bafuni nikajimwagia maji nikarudi kulala nilimshukuru mungu sana kufika salama nikampigia sylivester sim kumtaarifu kua nimefika hakupokea mmmh nilishtuka maana si kawaida, nikapiga kama mara tatu haikupokelewa nikajua atakua amelala amepitiwa na usingizi nikamtumia tu msg love nimefika salama...kisha nikalala asubuhi mapema nilikurupushwa na sim ya madam kuniambia mkurugenzi amefika chuo nikamwambia nakuja madam,, heee wewe kwani kwani usharudi dodoma? Nikamwambia ndio nipo dodoma, akasema sawa,,, nikaamka nikaoga haraka nikajiandaa safari chuo moja kwa moja nikafika nikamwambia secretary nataka kuonana na mkurugenzi akaniambia ingia yupo...nikaingia namkuta kajaaa kwanye kiti hana hata wasiwasi,,,karibu mrembo...mmm mrembo tena,,,nikakaa kwenye kiti nikamsalimia shikamoo akaitikia marhaba, kwa mara ya kwanza tangu aache kuitukia salam yangu...akaniambia najua unataka kujua kwanini hujaenda field ni kwasababubu unadaiwa,,,nikamwambia lakini mimi mbona sidaiwi akasema hudaiwi ada ila unadaiwa hela ya hostel...😳😳😳😳 hostel IPI wakati mimi sikai hostel ya chuo? Akaniambia mimi natambua ww upo hostel ya chuo hiyo uliyopo ww mimi sihitambui hivyo utailipia lakini unaweza kufanya mambo yawe marahisi tu kama tutakubariana,,,😳😳😳 kukubariana nini mkurugenzi? Niliuliza kwa mshangao,,, akanijibu mimi nakuhitaji nahitaji uwe mwanamke wangu kama utaridhia hakuna atakae kusumbua na utaishi kwa amani sana hapa na hata ada akituma mama yako utakua unachukua mwenyew wala sitakua naihitaji....aiseee nililegea mwili mzima nikawaza hapa sasa nafanyaje na ukiangalia field imebaki mwezi na nusu iishe nikamjibu sawa nimekubari,,,nilijua nitakachokifanya lengo ilikua niende kwanza field...alitoa tabasam kisha akanishika mkono akanipa bahasha akaniambia hiyo zawadi yako kaifungulie hostel ukifika...nikaipokea kwa woga ila sikutaka kukataa nikamuaga nikaondoka....nafika nnje nakutana na madam ananiuliza vipi mmeelewana nikamwambia madam nitakupigia baadae nitakueleezea akasema sawa...nikaondoka speed kueleekea getho nijue kwenye bahasha kuna nini
  ITAENDELEA.............. 

Post a Comment

Previous Post Next Post