SI KILA MAHUSIANO YAKUVUMILIA. 9

 Nilifika hostel moja kwa moja kwenye chumba changu, niliingia nikakaa chini nikafungua bahasha nijue kuna nini nikakuta hela na barua..mmmh hela nikaweka pembeni nikafungua barua nakuta ni barua ya kunitambulisha katika shule nayotakiwa kwenda kufanya field woiiii niliruka kwa furaha sikuamini nikasema asante mungu,, na barua ilitakiwa niripoti kesho yake maana ndo tarehe iliyoandikwa ya kuwasili nilimshukuru mungu haraka haraka nikampigia madam sim nikamwambia,,,madam kesho naenda kureport nimepewa barua ya kwenda field...madam cha kwanza aliniuliza,,,imekuaje mbona amekupa ghafla hakuna kilichotokea? Ikabidi nimdanganye, hapana madam hakuna kilichotokea ameniambia niende baada ya kumuomba sana na akasema nikirudi pesa zake apatiwe...madam aliitikia ila hakuonyesha kuridhika na majibu yangu akaniambia kua makini kisha akakata simu...nikajisemea madam usijali huyu hapati kitu ntacheza na akili yake tu...nikarudi kwenye hela nikahesabu nikakuta ni laki mbili na nusu,, nikaiweka pembeni nikamtumia msg mkurugenzi maana no nilikua nayo baada ya kunipigia nikasema asante sana mungu akubariki...akajibu usijali mpnz hapo ni mwanzo tuu mazuri yanakuja...sikumjibu kitu na msg nikaifuta maana niliona kinyaa sanaa....nikakumbuka sylivester hajanitafuta toka nitoke dar ngoja nimpigie,,,hee no haipatikari, woiii ni nini hiki mbona majanga haipatikani tena,,,nikapiga tena na tena bado haipatikani ikabidi nimpigie mdogo ake ikaita sana bila kupokelewa baadae akapoke halooo mambo...nikamjibu poa wifi mbona kaka yako hapatikani kunashida gani? Akajibu mmmh sijajua labda simu yake imeisha charg, nikamuuliza kwani yuko wapi akajibu ametoka toka subuhi hajarudi akirudi nitamwambia ulimtafuta...nikasema sawa nashukuru,nikakata sim nikaachana nae nikamtafuta prisca maana shule aliyokuwepo ndo niliyopangiwa kwenda nikamjulisha alifurahi sana akaniambia njoo dear nakusubiri na hongera sana...nikamwambia asante mamie nikakata sim...yaani nilikua nafuraha nusu huzuni maana nilikua nawaza kwanini sylivester hapokei sim na hapatikani wakati haikuwa kawaida lakini sikuendelea kumuwaza nikaamka nikaenda kuagiza chakula nnje nikarudi hostel maana nilikua sijala,,,
  Siku ilipita bila kumpata sylivester na mdogo ake nikipiga nae sim ikawa haipatikani,, asubuhi nilijiandaa nikaanza safari ya kwenda kituo nilichopangiwa hapakua mbali sana nilifika na nikamkuta prisca alinipokea. nashindwa kuwatajia jina la shule maana niliokua nao field wapo kwenye group hili na prisca si jina lake halisi..basi shule ilikua nzuri nilifurahi hapo mkurugenzi sasa muda wote sim mpaka nikawa naogopa prisca asije kujua kinachoendelea,, alikua akipiga naongea kwa kujishtukia sana na mara nyingi nilikua namuomba tuchart...mama nilimtaarifu kua mkurugenzi kanikubaria na nimeshaenda field hivyo hana haja ya kuja akaniuliza ilikuaje nikamwambia walijichanganya mama...akasema kama alijichanganya mbona simu yangu alikua hapokei nikamwambia iliibiwa...akaniuliza we umejuaje nikamwambia nilimwambia ulikua unamtafuta hapokei ndo akasema simu yake alipoteza.. Akasema sawa kua makini mwanangu kitu gani kinahitajika huko nikamwambia hakuna mama ondoa shaka nikihitaji nitakwambia...akasema sawa...sikutaka kumueleza mama ilivyokua maana ingekua balaa na mama alikua mkali sana nikahisi huenda angenigeuzia kibao yaani alikua hatabiriki...na sikutaka anitumie hela maana nilikua nayo hivyo sikutaka kumpa shidah...japo nilichelewa lakini haikua shida kwangu, ualim ulikua damuni hivyo hakuna kitu kilikua kinanishinda...niliifanya vizuri na siku ya kukaguliwa nilipata maks nzuri sanaa maana mkaguzi tulimpata mzuri hakuwa na shidah baada ya kumaliza alitutajia kila mtu alama zake...field iliisha tulirudi hoasteli,,hapo mkurugenzi simu kila siku anataka tukutane lakini nilikua namkwepa yaani nilikua najua kujieleza na kujibebisha akawa ananielewa na kwasababu alikua anatoka na wengi pale chuo ko hakunisumbua sana alikua akiona namzingua nahisi alikua anamtafuta mwingine aliekua nae anaenda kufanya anachotaka...ila nilikua najibebisha hivyo hakujua kama namchezea akili..nilikua najisikia vibaya lakini sikua na namna nilitaka kutimiza malengo yangu...na niliishi kwa raha sana yaani nikiwa na shida ya aina yoyote fasta anaitatua hela ndo usiseme,, chumba changu kikapendeza kama nafanya kazi vile kumbe mwanafunzi,, mama akituma ada inajazwa lakini baadae mkurugenzi ananiita offisin ananirudishia mwendo ndo ulikua huo,,,sylivester sikuwahi kumpata tena wala mdogo wake sikumpata yaani no zilikuwa hazipatikani....akili ikaanza kunicheza nikasema isije ikawa nimeambukizwa ugonjwa em ngoja nikachek mbona ghafla huyu mtu amechange....nilishikwa na woga moyo ukawa unanienda mbio...nikajiandaa nikaenda laboratory ilikuwepo karibu na chuo...nikamuelezea docta kua nataka kupima mimba na ukimwi.....
ITAENDELEA 

Post a Comment

Previous Post Next Post