SIMULIZI FUPI. HUKUMU KWA BABA MKWE MWISHOO

Ndipo nikaamua kwenda katika kituo cha Afya kilichokuwa jilani kwenda kucheki Afya yangu. Baada ya majibu kutoka nilishtuka sana nilivyoambiwa ninaujauzito na hapo hapo nilipatwa mshtuko mkubwa zaidi nilipoambiwa pia ninamaambukizi ya virusi vya UKIMWI. Nililia sana pale nilipokumbuka baba mkwe ndo chanzo cha matatizo haya.

Niliporudi nyumbani nikiwa ninauchungu na mtu mwenye kukata tamaa na maisha, Nilishangazwa sana kumkuta baba mkwe na watu kadhaa pale nyumbani, sikujua kitu gani kinaendelea, kwakua nilikuwa ninahasira nilimvamia baba mkwe na kuanza kumrushia makofi kwa hasira nilizokuwa nazo. "Wewe ndo umesababisha maisha yangu yamekuwa magumu lazima nikuuwe leo". Watu kadhaa waliokuwa hapo waliweza kunikamata ili nisiendelee kuleta vurugu. "Wewe binti unajua kwanini tupo hapa". Aliuliza mmoja wa vijana waliokuwa pale.
Kabla sijatoa jibu ghafla walitokea askari kadhaa na kumuweka chini ya ulinzi baba mkwe.
Nikawauliza askari kunanini, majibu walionipa yalinishtua sana na hapo nikadondoka chini na kupoteza fahamu.

Baada ya muda fahamu zilinijia nikiwa kitandani katika chumba changu. "Joyce hivi nikweli mume wangu Patrick amefariki". Nilimuuliza binti mmoja ambaye alikuwa amekaa pembeni yangu mwa kitanda. "Rahma ki ukweli uliyoyasikia ndo hivyo, Patrick alikuwa anajihusiha na uuzaji wa madawa ya kulevya yeye na baba yako. Kwahiyo Patrick alikufa baada ya madawa ambayo alikuwa ameyameza tumboni mwake kwaajili ya kuyasafirisha yaliweza kupasuka tumboni na umauti kumfika, hapa tunavyoongea baba mkwe wako amekutwa na hatia ya kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya na vilevile kusababisha kifo kwa mume wako". Sikuona umuhimu wa kuishi ndipo nikamuomba Joyce aweze kunipisha chumbani niweze kupumzika na alivyoondoka ndipo nikaamua kuandika barua hii ili iweze kuwafika baba wakwe wenye tabia kama hizi.
Sina haja yakuishi ni bora nikakutane na mume wangu huko alipo ili anaieleze kwanini aliamua kufanya biashara hiyo na hapo niweze kumsubiri baba mkwe na afike huku ili niweze kumpa hukumu takatifu kama itawezekana kumuua mara ya pili kwa kitendo alichonifanyia najua mume wangu Patrick atanisamehe kwakua kitendo cha baba yake kunifanyia unyama ule 
_ MWSHO_ 

Post a Comment

Previous Post Next Post