Adelina 07

.................
niliinuka na kwenda kwenye beseni la vyombo na kuchukua kisu na kukificha nyuma "adelaaaaaaaaaaa niliita kwa hasira

"Abeeee dada aliitikia"uku akiingia ndani ,alipoingia tu niinuka kwa haraka na kufunga mlango na kutoa kisu mahala nilipokificha uku nikitetemeka

Adela alipokiona kile kisu alibaki akitetemeka "naomba unijibu maswali yangu sasa ivi ,kabla sikuchoma iki kisu na Mimi kujiua 

"Simu umepata wapi,nakuuliza "
"Alinipa akaniambia ,atatusaidia kutupa ela ,ya kula na ya kutumia"
"Hapa unakosa pesa ya kula"
"Hapana dada ,sijawai kukosa"
"Ni tamaa au nikitu gani sasa ,mdogo wangu unakosa"
"Nisamehe dada ,"aliongea uku akitetemeka
"Aisee maisha yetu unayajua,na kila kitu unakifahamu ,haina haja ya kukuelekeza tena"nilichukua simu yake na kumpigia yule mtu"mwanangu achana na wanafunzi ,kama unashida na wanawake ongea na mimi dada ake achana na siketi za shule,ikijirudia tena swala hili tutafikishana mbele"kabla sijamaliza kuongea na simu alinikatia simu ,sikuacha kumsema adela na kumuelekeza maisha yalivyo japo tumepitia wote haya.
****************************************
Baada miezi kadhaa adela alifanya mtiani wa taifa na majibu yalivyotoka yalitoka mazuri alikuwa mtu wa pili katika watu waliofanya vizuri nilijisikia faraja sana kwa kuona mdogo wangu kafaulu kama nilivyotaka,hakika alinisikiliza kama vile nilivyomuagiza na Mungu alituongoza mpaka kufikia hapa 

"Umechaguliwa shule gani adela"nilimuuliza
"Ndanda ipo tabora uko"
"Mmmmh ndanda tena ,sa itakuaje maswala ya nauli,maana biashara saivi inasumbua na nilikuwa naweka akiba niache biashara hii lakini mipango sio matumizi"nilimwambia
"Kwaiyo tunafanyaje dada"
"Nakusikiliza wewe boss,ila utapoenda ndanda nitakumisi sana"
"Hahaha" alicheka 
"Khaa! mbona unacheka sasa
"Bwana nimechaguliwa jangwani tamisemi wanajua wanachokifanya
"Hahaha kumbe apo tu,basi sawa ngoja tupambane"nilimwambia
"Hahaha nakutegemea adelina"
 Siku zilienda adela nilimkamilishia kila kitu cha shule na rasmi akaanza kidato cha kwanza japo ilikuwa kwa shida ,lakini nashukuru Mungu mambo yalizidi kutuendea vizuri

Jioni mmoja adela alirudi kutoka shule ,uku akiwa na furaha sikujua ,furaha ile aliitoa wapi

"Vipi sio kwa furaha hiyo,umeshinda ile michezo ya bahati na sibu nini"
"Hapana leo ,mitiani nimeongoza tena,kumbe sekondari ni rahisi sana"

"Ukisoma sio ufanye uzembe utegemee utafaulu hiyo haipo,ata kama nimeishia darasa la saba"

"Wewe tena na ilo deli la barafu linakazi gani sasa"

"Ilo deli kuna biashara ya maji na juice nataka kesho nianze kuuza maana nishapata msingi wa kuanzia "

"Waooh,ni habari njema kwa upande wetu,ila kuna wazo limenijia "adela aliniambia

"Wazo ,wazo la kufanya nini"nilimuuliza

"Unaonaje ukaenda nyumbani,kuangalia nyumba yetu usikute baba anaweza akawa amerudi na anatutafuta"

"Ni wazo zuri umetoa kesho nitaacha hii kazi nitaelekea huko ,kuangalia yanayojiri ,maana ni mwaka sasa 

"Sawa dada ,kuna kazi ya shule naifanya kwaiyo baadae kidogo tutaongea "

Hahahaha haya msomi soma utuokoe wakubwa zako.

Nakumbuka kesho yake asubuhi ,nilitembea mpaka tandale mtogole nilipanda gari la ubungo msasani ,nakuanza safari ya kuelekea masaki kwa ajiri ya kuona kilichojiri baada ya mwaka mmoja 

 " Sijui mama mdogo nitamfanya nini nikimkuta na uyo diva sasa cha ujeuri ,aisee walitutesa sana acha nione watasemaje nitapoenda "niliendelea kujiongelesha peke yangu

Niliendelea kujifaidia uzuri wa dar es salaam dah! kumbe sisi tulikuwa tunakaa sehemu nzuri kuliko wengine

"Baharesa"konda alisema 
"Shusha nilitoka katika lindi la mawazo na kushuka zangu pale baharesa na kuanza kuitafuta nyumba yetu nilivuka barabara na kuanza kuesabu nyumba ,mpaka nyumba iliyobandikwa kibao namba 07 

nilijikuta tu natetemeka ,mazingira yalikuwa tofauti kidogo na nilivyoyaacha "kwani natetemeka nini? nilijiuliza ,naomba Mungu afungue baba geti na sio mama mdogo"

Nilibisha hodi ,baada ya dakika kadhaa mlango ulifunguliwa nilijikuta natoa macho

"Who are you,sorry unashida gani rafiki"aliniuliza mzungu mmoja ambae kwa muda huo ndio aliyefungua geti

"Na mtaka mwenye nyumba tafadhali"nilimwambia

"Mwenye nyumba ni Mimi,au unasema before mimi"aliuliza

"Ndio I mean yule mama nilimwambia "
"Ooooooh alishaama yule ,aliniuziaga takribani mwaka sasa"alisema yule mzungu

"Ok sawa kwa heri,"nilimuaga

Geti lilifungwa ,nilibaki nalia "dah mali zetu ndo zimeisha Yale magari matatu matatu ,na maduka yote yale ya baba na mama,inaamana tunakufa masikini,ila Mungu yupo tutapata zetu "niliondoka kwa huzuni uku machozi hayakuacha kunitoka.

Jioni akati nimetulia nyumbani uku nikiwa na mawazo kuhusiana na swala la asubuhi gafra! aliingia adela

"Dada shikamoo,mbona ivo utakiwi kuwa na huzuni "aliniambia

"Nilitabasamu kidogo,uku nikimuangalia"

"Eeeee kumbe unaweza kufurai sasa leo Nina surprise"aliniambia

"Ipi hiyo na wewe "

Gafra! alifungua mlango , na kuucha wazi uku akiniangalia usoni

"Nilijikuta natoa macho kwa nilichokiona.............itaendelea like 180 naleta kingine unaposoma hakikisha una like 

Post a Comment

Previous Post Next Post