UNO LA MASIKINI 20 🔞 final


Tulipoishia
Tina alipomuona Tino alishtuka maana, hakujua kama pia Tino ana ukaribu na mzee

“Huyu ni kijana wangu mwingine tena ambaye ninamkubali sana katika harakati” alisema waziri

Kichefuchefu kilizidi kumsumbua binti akainuka na kwenda chooni kwa uoga akatapika huku akilalamika
“Huyu Tino ni nani?” alijiuliza……

Sepa nayo

Jane ilibidi amfuate Tina chooni akamkuta akiwa ameduwaa anajiangalia kwenye kioo

“Tina” alisema binti Jane

“abee” alisema

“usifadhaike ni jambo la kawaida mbona nilijua mda kwamba waziri ni mkuu wake turudi kule tukamalizie sherehe bwana “ Jane aliongea

“mwanaume muongo sana yule” alisema binti

“twende kwanza uongo wake nini bwana we twende” alisema Jane

Basi wote walitoka chooni wakiwa wameshikana mikono, wakarudi ukumbini na kuketi
“Christina vipi unaumwa” aliuliza mheshimiwa

“hapana siumwi” alisema binti

“haya tuendelee kutambulishana “huyu kijana wangu anaitwa Agustino Benjamin Clement yaani ABC kwa kifupi, ni msaidizi wa kazi zangu namkubali sana” alisema waziri

Tino aliponyanyua uso na kumtazama binti alikuta binti anamuangalia kwa macho yanayomkanya asimzoee lakini Tino alisikitika kidogo na kuinamisha kichwa tena

Shamra shamra za sherehe ziliendelea mpaka muda wa saa tisa usiku ambapo waligana lakini waziri alibaki pale na binti kwa ajili ya kutimiza ahadi yao kwamba wangelala usiku kucha ili kutafuta mtoto

Tino alipofika nje alisimama nje ya gari huku akitafakari sana namna ambavyo mpenzi wake anaenda kutandikwa na muheshimiwa, nafsi ilimuuma sana akaendelea kufikiria akisikitika

“mwanangu Tino tusepe mzee” Tonny alisema

“nendeni nyie mimi nakuja ngoja kwanza nipate moja mbili hapa” alisema mtaalamu na kuingia ndani ya ukumbi ule akaona binti anaeleka chumbani na waziri, roho ilimuuma, binti naye aligeuka akamuona Tino akiwa amesimama pale kwenye ukumbi macho yakiwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu kama nyanya alionekana alikuwa na mapenzi ya dhati sana kwa binti

Alimfanyia kwa ishara kwamba wakimbie lakini binti alizidi kuingia hadi chumbani na waziri

Tino aliwafuatilia nyuma akaenda kusimama nje ya chumba kile huku mabodiguard wote wakiwa nje ya ukumbi kama waziri alivyowaamuru
Tino kutokana na stress aljikuta amesimama kwenye mlango wa chumba kile akiwa na mawazo sana.

Baada ya dakika tano alishangaa binti ametoka, Tino alishtuka
“Tina” aliita kwa mshangao maana binti alishika viatu na pochi mkononi

“shshshhshh” binti alimuambia jamaa kwamba atulie na kumshika mkono akaanza kumvuta kuelekea sehemu ambayo hata hawazijui, walipita mlango mwingine wakaingia barabara nyembamba ya lami na kuanza kukimbia

“Tina tunaenda wapi?” aliuliza mshikaji 

“mimi mwenyewe hata sielewi Tino we twende tukimbie” alisema binti kwa hisia sana

“daaah waziri umemuambia unaenda wapi” aliuliza huku wakizidi kukimbia 

“nimemdanganya naenda kuongea na Jane nakuonea aibu Tino siwezi nikakusaliti ukiwa unaona, bora nikose hela mpenzi”

Walikmbia wakafika mahali binti akachoka na kuanza kutapika

“sasa itakuwaje mbona unatapika” alisema mtaalam

Mara ghafla zilitokea pikipiki mbili zikikimbizwa hasa na walizipaki watu wawili wakiwa wakiwa wameshikilia bastola kubwa za maana na kuwapiga kichwani Tina n Tino wote wakapoteza fahamu

******
Mida ya asubuhi Tina alishtuka akiwa amefungwa na kamba kwenye jumba moja asilojua liko wapi
Alipoangalia pembeni alikuta pia Tino amefungwa pembeni ila bado alikuwa amepoteza fahamu,

“Tino, wee Tino” binti aliita kwa sauti ya chini ili kama kuna adui pale asisikie

Tino naye alishtuka akatazama na kuanza kukumbuka tukio lilivyokuwa

“Tina” aliita baada ya kumuona Tina pembeni yake “tuko wapi hapa?” aliuliza

“sijui Tino, wewe ndiyo chanzo cha yote haya kwanini usiniambie ukweli toka mwanzo” aliuliza binti

“nisamehe Tina mimi nilishindwa kusema ukweli kwa sababu nilitumwa kukuchunguza wewe maana tulihisi unajihusisha na madawa ya kulevya” alisema Tino

“kwa hiyo wewe ni nani hasa” aliuliza Tina

“mimi ni usalama wa taifa Tina” alisema mtaalam

“kwa hiyo yale maisha yote uliniigizia Tino lakini” alisema binti huku machozi yakimtiririka

“naomba unisamehe Tina, ndiyo kazi yangu ilivyohitaji kwa kipindi chote cha maisha lakini mapenzi yangu kwako yalifanya nishindwe kutimiza kiapo changu kwa serikali”

Mara aliingia mmoja wa mabodigadi wa muheshimimiwa “shsssshit kumbe mmeshafufuka” alisema na kurudi nje akasimama huku akiwa anasubiri wenzake waje

Baada ya dakika kumi ilitokea gari kali na kupaki pale akashuka muheshimiwa lakini dereva akabaki ndani huku akiwa ameshika bastola

“wako wapi?” muheshimiwa aliuliza

“huku ndani mkuu” alisema na kupiga saluti halafu muheshimiwa akazama ndani

Kitendo cha kufika ndani alishangaa kukuta ni peupe ni kamba tu zimebaki kwenye viti pale walipowafungia

“Godfreyyyyy” Waziri aliita kwa hasira na kutoa bastola yake huku akimuita yule mlinzi wake

Mlinzi aliingia naye akapigwa na butwaa haoni watu pale alipowaacha “Muheshimiwa” alisema mtaalam kwa uoga maana alijua lazima wachezee paipu

“Tino na Tina wako wapi?” leo aliyataja majina kwa kifupi huku akimnyooshea bastola

“muheshimiwa walikuwa hapo sijui wametoroka saa ngapi”

“umewatorosha wewe halafu uniletea mambo mengi mimi...hujui mimi nwanajeshi ee?” aliuliza kwa hasira mpaka akajikuta amemshuti yule jamaa akafia pale pale na muheshimiwa akatoka na kwenda kwenye gari akampigia Tonny

“Naomba mumtafute Tino sasa hivi umlete akiwa mzima yeye na Tina” aliongea

“sawa muheshimiwa” Tonny alijibu

Kumbe wakati huo huo Tonny na Dullah ndiyo walikuwa na Tino na ndiyo wamemtorosha kutoka kule alipokuwa ametekwa, na walikuwa maeneo ya Bunju B wakikata tiketi ya mabasi ya Nairobi

“Tino mwanangu tumeambiwa tukukamate sasa shikeni hizi tiketi pandeni gari la kuelekea Nairobi mkatafute maisha yenu” alisema Tonny

“Tina achana na lile lizee lina wanawake kibao, na hawezi kuwa na malengo na wewe” waliongea pale kwa bahati nzuri basi la Nairobi likafika pale pale wakapanda

Tina alichoweza kufanya ni kumpa ufunguo Tonny tu
“Naomba vitu vyangu uviuze unitumie hela yake please shemeji” alisema binti

“sawa shemeji kwaherini”

“poa jamani” alisema gari nayo ikapigwa moto hao wakapotea kuelekea Nairobi wakasake maisha yao.

**
Baadaye Tonny na Dullah walirudi kwa waziri wakamuambia kwamba hawajampata lakini watamfuatilia mpaka pale watakapopata taarifa kwamba wameenda wapi

“Pumbavuuuu” mzee alipiga ngumi kwenye meza akiwa na hasira kali sana

***
Ni muda ulipita sana na maisha ya Tina na Tino yaliendelea vyema huko jijini Nairobi bila kifuatiliwa na mtu yeyote.
Asanteni kwa kuwa na mimi mwanzo hadi mwisho

MWISHO 

Post a Comment

Previous Post Next Post